NAMNA YA KUSIKIA NA KUIELEWA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDIE KATIKA KUFANYA MAAMUZI (Sehemu ya 2)

Na: Patrick Sanga

1

Mada: Mambo mhumu kujua kuhusu sauti ya Mungu

Katika sehemu ya kwanza ya ujumbe huu niliandika kuhusu mambo matatu ambayo ni kujenga mahusiano na Roho Mtakatifu, kuongeza ufahamu wako kuhusu alama za mawasilano na tatu ujue namna ya kutofautisha sauti ya Mungu na isiyo ya Mungu. Ili kusoma sehemu ya kwanza bonyeza link hii  https://sanga.wordpress.com/2015/04/02/namna-ya-kusikia-na-kuielewa-sauti-ya-mungu-ili-ikusaide-katika-kufanya-maamuzi-sehemu-ya-1/ Sasa fuatana nami tuendelee na mabo mengine muhimu kujua:

 • Vifahamu vikwazo vinavyopelekea kutokusikia sauti ya Mungu

Biblia imeainisha vikwazo kadhaa vyenye kupelekea mtu kutokuisika sauti ya Mungu. Vikwazo hivyo ni pamoja na moja kutenda dhambi au kuishi maisha ya dhambi (Isaya 59: 1-2), pili kukosa uaminifu (Hesabu 12:7-8, 1 Samweli 2:35). Biblia katika Isaya 59: 1-2 inasema ‘Lakini maovu yenu, yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia’ Pia katika Hesabu 12:7-8 imeandikwa ‘Sivyo ilivyo kwa mtumshi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si mafumbo.

2

 • Ongeza ufahamu wako kuhusu njia anazotumia Mungu kuzungumza

Ni dhahiri kwamba zipo njia mbalimbali ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu. Namna Mungu anavyosema na huyu sivyo atakavyosema namtu mwingine. Tofauti hizi zipo tegemeana na mahusainao yaliyopo kati ya Mtu na Mungu na pia ngazi ya kiroho aliyonayo mtu katika ulimwengu wa roho. Hivyo ni muhimu sana kuwa na uelewa wa hizi njia mbalimbali ili kuelewa mazingira yake na hivyo kutafuta kumsika Mungu kupitia njia hizo ili kudumisha mahusiano na mawasiliano yako na Mungu. Katika sehemu ya tatu ya somo hili nitaanza kufundisha njia husika hivyo naamini ufahamu wako utaongezeka.

 • Unahitaji kufahamu umuhimu wa Mungu kuzungumza/kusema nawe

5

Zipo sababu nyingi za Mungu kuzungumza na wanadamu laikini kubwa yenye kuzibeba zote ni ile iliyoandikwa katika Zaburi 32:8 kwamba ‘Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama’. Ni muhimu ukakumbuka kwamba kwa mujibu wa Wayumi 8:28 umeitwa ili kulitumika kusudi la Mungu katika siku zako. Ili uweze kulitumika ipasavyo sharti akuongoze katika njia sahihi. Naam njia mojawapo ya kukuongoza na kukufundisha ni kwa yeye kusema na wewe.

Lengo lake katika kusema na wewe ni kukuongoza katika njia sahihi kwa kukuondoa kwenye makusudi ambayo yapo nje na mapenzi yake kwenye maisha yako maana imeandikwa ‘Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam hata mara ya pili ajapokuwa mtu hajali, ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi’ (Ayubu 33:14, 17).

 • Ongeza ufahamu wako kuhusu ulimwengu wa roho

Mambo yote yanayotokea katika ulimwengu wa mwili yameanzia katika uilimwengu wa roho, naam maamuzi ya kile ambacho hutokea katika ulimwengu wa mwili hufanyika katika ulimwengu wa roho. Zaidi hata mapambano (vita vya kiroho) yote aliyoanayo mwamini katika kulitumikia kusudi la Mungu hufanyika katika ulimwengu wa roho.

Hivyo kuwa na ufahamu wa ulimwengu wa roho hususani namna ya kuishi na  kuwasiliana katika ulimwengu huo ni muhimu sana kwa mwamini mwenye kutafuta kujua na kuisikia sauti/mawazo ya Mungu katika maisha yake kwa kuwa Mungu ni roho kama alivyo na Shetani pia. (Rejea 2 Wafalme 6:8-17 na Waefeso 6:10-12).

3

Mpenzi msomaji usiruhusu yale unayoyapitia au yale ambayo watu /mazingira yanasema juu yako yabadilishe au kuongoza maisha yako, bali tafuta kuijua na kuielewa sauti ya Mungu kwenye maisha yako. Na ndiyo maana somo hili limekuja ili kukusaidia kufika mahala ambapo utaweza kuyatenda mapenzi kamili ya Mungu kwenye maisha yako.

Baada ya kuwa tumeangalia mambo haya saba ambayo ni muhimu kujua kuhusiana na sauti ya Mungu, katika sehemu ya tatu nitaanza kuandika kuhusu njia mbalimbali ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu. Somo litaendelea….

Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.

 

Advertisements

14 comments

 1. Mtumish Mungu akubark umenikomboa roho yang nilikokuwa naenda kiroho kwasasa nadhan mungu alikuwa anaelekea kuiadhbu nafc yangu! Ahsante sana ubarikiwe!

  Like

 2. Mtumishi wa Mungu, Sanga. Mungu akubariki sana. Mwezi februari tarehe 15 2016 nilituma maombi yangu nikiomba tushiriki pamoja kuomba. Namshukuru Mungu nimemwona Mungu kupitia Jina la Yesu Kristo katika maombi ambapo pia nilishirikisha kikundi cha maombi cha kanisa la Breakthrough Boko kwa Mchungaji G. Simtomvu.Namshukuru Mungu Nimeweza kufunguliwa Kwa neno la Mungu Isaya 45: 1-7, ambalo nilipewa na Mchungaji kulisoma kila siku saa 6 usiku, nikimwomba Mungu anishike mkono, afungue mlango wa shaba na kwenda mbele yangu na kupasawazisha mahali palipoparuza, kukatakata mapingo ya chuma na vizuizi vyote vya shetani katika maisha ya familia yetu na hapo nikaweza kwenda kumchukua Jerome na sasa niko nae hapa Dar na tunashiriki maombi kanisani sana. Amefunguliwa na anaendelea vizuri sana kuelekea kupona kabisa.
  Namshukuru Mungu sana kwa hamasa niliyopata ya maombi kila siku asubuhi katika mtandao niki google huku na kule kumtafuta Mungu kupitia Yesu Kristo na kweli nimemwona Mungu kwa muda huu tangu februari 2016.
  Nakushukuru Mtumishi wa Mungu Ndugu Sanga kwa Blogi yako kwani ilinitia mwanga wa kukazana kumtafuta Mungu kupitia Maombi kipindi hiki, Ahsante sana na Mungu Kupitia Jina kuu la la mwanae Yesu Kristo na Roho Mtakatifu, Akubariki saana wewe na Neema au Mrs George, Elina Masewa na Mkumbo Mkoma.

  Leo nime google tena blogi yako kupitia neno,’UTAINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI’ ISAYA 58:12 na kupata articles nyingi na za wachungaji wengine, na ya Mwalimu Mwakasege ya njia tatu za kujiweka vizuri kama mtu hauko vizuri katika maombi, Imenibariki saana.
  Pia kuna article nyingine inayohusu jinsi Shetani anavyozuia maombi yetu yasifike kwa Mungu! mwanzo ilinitisha lakini mwishoe nikatambua kuwa vita yetu tuliookoka ni ya Mungu. Mungu anatupingania na kupitia kifo cha Mwanae Yesu Kristo tumeshinda vita hiyo (ya mauti) kwani ameshinda kuzimu na alipaa kwenda Mbinguni kwa hiyo yetu yote ni …..duniani kama mbinguni… Amen, Halleluhjah Amen.
  Ailine.

  Like

 3. Mtumishi wa Mungu Sanga,
  Ahsante pia kwa somo hili la Namna ya kusikia sauti Ya Mungu kutusaidia Kufanya maamuzi! limenipa Nuru, (limeni HULUKU! Isaya 45).
  Ubarikiwe saana, Amen

  Like

 4. Barikiwa sana mtu wa Mungu. Hili somo la namna ya kuisikia na kuielewa sauti ya Mungu ili ikusaidie katika kufanya maamuzi , linanibariki, na kunipa shauku ya kutaka kumjua Mungu zaidi. Hivyo mtumishi, naomba ikiwa wapata kibali, naomba unitumie hili somo sehemu zote, hasa ile sehemu ya kwanza ndo naitafuta siioni. Ahsante sana.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s