Maombezi

Maombi na maombezi kwa njia ya mtandao

KARIBU KATIKA KONA HII AMBAYO WEWE MSOMAJI UNAWEZA KUTUMA MAHITAJI YAKO AMBAYO UNGEPENDA TUWEZE KUOMBA KWA PAMOJA.

kitabu cha 1Yohana 5:14-15 Biblia inasema “Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15 Na tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba .

Mstari huu ndio  ambao utakuwa mstari wetu wa msingi katika Maombezi yetu kwa njia hii ya mtandao. Mzee Yohana anatutia Moyo kwa neno hili kwamba  lolote tumuombalo Mungu haijalishi ni kubwa au dogo maadam tukaomba sawasawa na mapenzi ya Mungu basi tuwe  na  uhakika  anatusikia.

Nimeona Mungu akijibu wengi, akifungua waliofungwa na kuponya wengi kupitia huduma hii . Nawe amini tu, Bwana atafanya njia kwa ajili yako pia. Kuna namna mbili za kutushirikisha mahitaji ya maombi yako, mosi ni kutuma kwenye ’email’ yetu maalum ya huduma na hapa ina maana huhitaji hitaji lako lionekane kwa wasomaji wote wa blog hii. Namna ya pili  ni kuandika hitaji lako kwenye eneo la ‘comment’ ambapo ina maana utakuwa umeridhia hitaji lako kuonekana kwa kila msomaji wa blogu hii.

Sasa kama unataka tuweze kuomba pamoja na wewe katika hitaji/ haja yoyote uliyonayo iwe  ndoa, masomo, familia, wazazi, huduma, kanisa, uongozi, biashara, kazi, watoto, afya yako,nk. tumia njia mojawapo kati ya hizo mbili , kwa upande wa email tumia email hii;  paxifari@gmail.com 

Mara utakapotuma, waombaji wa huduma hii pamoja na wasomaji wa blog hii , wataendelea kuomba pamoja na wewe juu ya hitaji lako ukikumbuka hakuna lisilowezekana kwa Mungu wetu. Katika Yeremia 32:27  imeandikwa “Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili;je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza? Naam, Hakuna jambo gumu la Kumshinda BWANA.

MUNGU AKUBARIKI, UWE NA IMANI KWAMBA ATAFANYA, MAANA KILA AMWENDEAYE MUNGU LAZIMA  AAMINI KWAMBA YUPO NA KWAMBA HUWAPA THAWABU WAMTAFUTAO

390 Comments »

 1. 1
  Leva Says:

  Naomba mniombee nipate kazi na ningependa nipate kazi nimtolee Mungu zaka na niweze kujimdu ki maisha. Naamini baada ya maombi yenu nitajibiwa maana nimetuma barua za maombi.

  • 2
   Josephine Julius Macha Says:

   Bwana Yesu asifiwe.

   Mimi naitwa Josephine. Nina shida kubwa amani ndani ya nyumba yangu ni ndogo. Mtoto wangu ni mmoja wa kiume yuko form five. nimepewa taarifa ya kuwa hapo shuleni ameanza kunywa pombe, kuvuta sigara na bangi. Shule yenyewe ni green acres high school ambayo iko mbezi beach naomba ikiwezekana muiweke katika maombi. Nina madeni mengi hata wanaonidai wameanza kufika nyumbani kwangu hivyo mume wangu ananichukia kwa sababu ya haya yote. Nimeahidiwa kupewa mkopo na benki moja hapa mjini dar na wameahidi kunipatia lakini wanachukua muda. Hivyo naomba maombi ya haraka ili kupatiwa mkopo huo ili niweze kukamilisha ada ya mtoto pamoja na mtoto wa marehemu mdogo wangu ambae ninaishi nae, pamoja na kumaliza madeni yanayosumbua akili yangu Naomba maombi ya haraka kwani nimechoka sana. Namba msaada kuhusu mtoto wangu mpendwa.
   Mungu akubariki sana.

   • 3
    sanga Says:

    Amina, Josephine tunakuombea Bwana akufanikishe katika mambo yote kupitia jina la Yesu. Je ungependa maombi haya ni publish yaweze kusomwa na waombaji wengine pia?

   • 4
    Rehema Mwangi Says:

    Mpendwa Josephine, naakuombea amani ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe juu yako na familia yako, nimesikitika kusoma mahitaji yako karibu mwaka baada ya wewe kuyatuma, kiri ya kuwa “mimi na nyumba yangu tunamtumikia Bwana” usiangalie mtoto wako anaelekea wapi au amejiingiza wapi wewe amini kwa kukiri kile unachotaka kukiona kwa kuwa “tunatembea kwa imani na sio kwa kuona…” kwa kuwa “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana….” kiri kwa kinywwa chako kila saa kila wakati, tafuta na mistari mingine katika Biblia ukiri juu ya watoto wako, mahitaji yako ya kifedha, mume wako nk.
    Josephine madeni yamekuwa mengi kwako mpaka wadeni wako wanakuja nyumbani kwako, ukaamua kutafuta mkopo bank?? madeni ya kawaida yamekuwa shida kwako kulipa, je hilo la bank lenye na riba juu utaliweza? huo mkopo sio suluhisho, ulitumia njia ya mkato, kwa Mungu hamna kuchelewa wala kuwahi maana muda wake sio muda wa mwanadamu, kwa kusoma barua yako nimehisi huishi kufuatana na uwezo wa kipato chako, unasomesha mtoto shule ya gharama kubwa kwa kutegemea mikopo, pili ni kama vile mumeo hausiki na gharama za shule za watoto?
    Ushauri wangu kwako ni kutafuta mshahuri wa mambo ya fedha na uchumi ” financial conselor” huku ukidumu katika maombi uombe hekima, busara na ufahamu kutoka kwa Mungu, akupe neema ya Roho Mtakatifu katika maamuzi yako.
    Nakuombea ufahamu, ufunguliwe kiuchumi na amani na upendo katika ndoa yako, watoto wako wakaishi kuwa mifano ya kuigwa, wakawe viongozi, wakawe na hofu ya Mungu, wakafanikiwe na zaidi wakaishi na kukua wakimfurahisha Mungu na hata wanadamu. MUNGU AKUBARIKI SANA

   • 5
    sanga Says:

    Dada Rehema Mungu akubariki sana kwa ushauri wako muhimu kwa Josephine, Mungu akubariki sana pia.

   • 6

    dada yangu baba ashaku sikia usilie maana ajaku wacha yeye anaye sababu zake ya kukuweka hapa dunia bibilia inasema yote unayoitaji kabla yaku mwambia ashajua unatakiwa kumwamini na moyo moja usikuwe mwenye imani dogo bila imani uwezi ISAIYA:54 YOTE

   • 7
    Ev.Aminiel Tillya Says:

    BWANA WETU YESU KRISTO AKUFANYIE NJIA WAKATI HUU BILA HATA KUKOPA MKOPO MWINGINE KWA AJILI YA KULIPIA MIKOPO MINGINE.BARIKIWA SANA JOSEPHINE

   • 8
    zebadiah Says:

    Mungu anasema nenda mbele zake mhojiane usipuuze jambo hili ukaanza kutafuta watu wa kukuombea wao watahojiana na nini kukuhusu wewe. KUHUSU HABARI ZA MTOTO WAKO KUFUNGULIWA KWAKE KUNAKUTEGEMEA WEWE HAPO.UKIFUNGUKA NA YEYE ATAFUNGULIWA. AMEN.ZEBA

  • 9
   mwalami Says:

   mimi mwalami naomba muniombee kazi sina.ninamatatizo nadaiwa kodi ya nyumba natafuta mke mwema. mimi fundi ujenzi nisaidieni kuniombeaa.nadai hera sijapewa hadi reo.

 2. 10
  Sarah John Says:

  Naomba mniombee ili niweze kudumu kwenye wokovu.na niweze kuombea wengine.

 3. 11
  josephine Says:

  NAOMBA MNIOMBEE MIMI NINAHITAJI AMANI NA KWELI YA KIRSTO IKAE NAMI NA MWANANGU ANAVUTA BANGI NA ANAZINI SANA NINAOMBA MAOMBI YENU, NAISHI ZURICH SUISS.MIIMI NIMEOKOKA NA NAMPENDA YESU NA NAOMBA USHAURI WENU NIFANYE NINI JUU YA HUYU MTOTO KIMEKUWA KITANZI KWANGU KATIKA WOKOVU WANGU.

  • 12
   loyce kulwa Says:

   Watumishi wa Mungu, mimi ni mjane nina watoto wawili, naomba mniombee niendelee kuwa mwaminifu katika ujane wangu, mwaka kesho uwe wa mafanikio kwangu, ninaujenzi wa nyumba ya wanangu lakini vifaa vya kumalizia sina, mabati, mbao, misumari hela ya fundi, rangi madirisha cement Mungu afungue njia niweze kumalizia.

 4. 13
  Juliana Says:

  Ninashukuru mie binafsi kwa kuwa Bwana amewaonyesha kilicho chema maana ni wengi vijana sasa hivi wanaitamani njia hii iliyo salama kwakuwa shetani amejiinua kila kona na kimbilio ni kwa bwana, naomba bwana awatie nguvu na muendelee kutusaidia tunaohitaji msaada wenu mtuombee na kutushauri njia iliyo salama ili tusije jutia mwisho wa maisha yetu. Mbarikiwe sana

  • 14
   PATRICK MKANE Says:

   Bwana yesu asifiwe mimi naitwa patrick naomba uniombee mtumishi wa mungu nipate kazi yenye kibali machoni pake na mke mwema

 5. 15

  Niombeeni. shetani anataka kuangamiza familia yangu. nimeibiwa shilingi millioni moja na nusu . na nina kesi ya kubabikizwa ya million 28. kwa maombi mungu ataniokoa nishirikisheni katika maombi yenu.

 6. 16
  George M. Simon Says:

  naomba tushirikiane kuomba juu ya maisha yangu.

 7. 17
  George M. Simon Says:

  naomba tushirikiane kuomba juu ya maisha yangu.

 8. 18
  George M. Simon Says:

  naomba munitumie masomo pamoja na mistari katika bibilia yahusuyo maombi kweye mail yangu george.simon85@yahoo.com

 9. 19
  Evarest(belgium) Says:

  Bwana Yesu asifiwe
  Ninamzigo juu ya watoto yatima,nimeanza kukusanya kikumi changu kwa ajili ya kusomesha hao yatima na mwaka jana niliweza kuwasomesha yatima wapatao 14 ,ninaomba mnisaidie ktk maombi ili Mungu afungue milango ya baraka nipate sponsors kwani lengo langu ni kuja kufungua centre kwa ajili ya watoto hao ambao baba yao ni Mungu pekee.nachojua ni kwamba fedha na dhahabu ni vya Bwana aliye juu.
  Mungu awabariki Ameni
  Niko hapa Belgium

  • 20
   NEEMA OR MRS GEORGE Says:

   Mungu akubariki Mtumishi wa Mungu Evarest kwa hatua iliyofikia hata kwa wazo kusaidia watoto Yatima hakika Mungu atakufanikisha kwa njia saba usizotarajia Kumbuka Mungu ni Baba wa yatima sidhani kama ataacha watoto wake walale njaa, wasisome, hakika Evarest ongea na Mungu mkumbushe dai funga roho za yule mwovu hakika huna hata haja ya Sponsor Maana Mungu ndie sponsor mwombe yeye hakika utaona amini unachoomba. Hongera pia kwa kuamini kwamba fedha na dhahabu ni mali ya Bwana sasa unataka Sponsor wa nini Mkuu simamia maombi yako funga omba jinyenyekeze hakika utamwona Mungu akishuka. Ubarikiwe tuko pamoja katika maombi

 10. 21
  Daniel J Seni Says:

  Bwana apewe sifa sana!
  Namshukuru Mungu wa neema kwa ajili ya kunipa muda wa kuandika machache. Nataka kuwasaidia vijana kuishi maisha ya kiroho na maisha ya ushindi ndani ya Yesu Kristo! Lakini vijana jamani tusiwe wabishi sana tunapokuwa katika kujifunza neno la Mungu.
  nataka kupata vijana wa kusaidia kiroho (disciple them) je mko tayari? kwa walio tayari nijulisheni kwa anuani ya P.BOX 32807 DAR ES SALAAM
  Asanteni kwa watakaopokea wito wangu huu!

 11. 22
  Amani paulo Says:

  Namshukuru mungu kwa kunipa mda huu napenda kuwashirikisha katika maombi naomba mungu anipe nguvu za kusali make sina ujasili niongezea alafu naomba mungu alinde familia yangu atupe amani na upendo naomba mungu anipe kazi ili niweze kusaidia familia yangu na ninaomba baraka za bwana katika mwaka huu ni badilike mungu akubariki sana

 12. 23
  Faith George Says:

  Shallom!

  Ninaomba tushirikiane katika maombi yangu kwani hua naota ndoto ambazo shetani anaziiba, saa nyingine sikumbuki na pia napenda sana kuomba tena sana ila wakati mwingine hasa ninaponia kuomba sana najikuta nasikia kuchoka sana, hata nikitaka kusoma neno nasikia uvivu naomba mnisaidie ili nimtumikie mungu kwa moyo wangu wote na akili zangu zote. Mungu aniondolee vikwazo hivyo.

 13. 24
  zebadiah Says:

  salamu katika jina la Yesu Kristo. Mimi napenda kuwashirikisha hitaji nililo nalo katika mji ninaoishii. Naishi katika mji mdogo unaitwa korogwe. Tumwombe Mungu afungue fahami za watu wamfahamu Mungu wa kweli katka maisha yao. Maeneo mengi katika mji wetu na viijiji vyake hawajamkubali Mungu wa ISRAEL. Wanatemegea sana waganga wa kienyei. Ombea kua Mungu ainue wainjilist na Wahubiri watu wengi wa vijijini na mji wetu wafikiwe na neno la Yesu Kristo , Asante

 14. 25
  zebadiah Says:

  asante na barikiwa na BWANA YESU

 15. 26
  osward Says:

  bwana yesu asifiwe,.nami naomba maombi yenu nikue kiimani niweze kuwasaidia ktk matatizo yao ili kuwaombea na wapone.Mungu awabariki.

 16. 27
  ELIREHEMA NYARI Says:

  NAOMBA MAOMBI YAKO KWA KUSOMA UJUMBE HUU JUU YA MAOMBI NINAKUWA CHANGA MOTO KWAMBWA UKINIOMBEA MAHITAJI YANGU YATAJIBIWA HARAKA TENA SANA

 17. 29
  Evarest Says:

  Bwana Yesu asifiwe
  Ninahitaji kuoa mwaka huu ninahitaji maombi yenu ili Mungu afanikishe mipango yetu ya ndoa kwani kumetokea vipingamizi vingi sana ,ila najua kuwa Mungu aliyeanza atamaliza.
  Tuna^pomuomba yeye anajibu.
  Evarest

 18. 30
  VERONICA Says:

  Bwana yesu asifiwe,mungu wa rehema awe pamoja nanyi.
  Mimi naomba niwashirikishe maombi ya kumuombea mtoto wangu Lorine aliumwa degedege mpaka leo hajaweza kukaa wala kutembea an umri wa mwaka mmoja na miezi sita, tumuombee kwani ni malaika wa bwana. Amen

  Mungu awe nanyi daima

  • 31
   Aunty Nyamizi Says:

   Bwana Yesu atamponya kwa jina lake takatifu. Amen

  • 32
   Petro Bundwa Says:

   Bwana ni mwaminifu na wa haki wakati wote,ambaye hakumuacha Nuhu apatwe na mabaya,bali alimuokoa na gharika,tambua hata kwako na vizazi vyako atafanya hivyo,Endelea kuomba na kuweka imani mbele.

 19. 33
  Joyce Jonas Says:

  WAPENDWA KATIKA BWANA NAOMBA MNISAIDIE KUOMBA, MAMA YANGU IRENE SALLY ANAINGIA KATIKA CHUMBA CHA OPERATION SAA ZA TANZANIA SAA 2 USIKU (18/5/2009) NA YEYE YUKO MAREKANI KULE ITAKUWA SAA 7 MCHANA. OPERATION YA MATITI KWA AJILI YA KANSA, WAPENDWA MUNGU ALITUAHIDI TUKINUIA MAMOJA TUTASHINDA NAWAOMBA SANA TUMSIHI MUNGU AMPONYE. BWANA AWATANGULIE NA ASIKIE KUOMBA KWETU. AMIN

  • 34
   CRAIN Says:

   Wapendwa katika bwana naomba tushirikiane katika maombi yakumuombea

   mtoto wa mdogo wangu ana miezi kumi anatalajia kufanyiwa operation ya koo siku ya jumatatu naomba maombi yenu.Na namuomba mungu amponye katika jina la yesu naamini atatenda.AMINA

 20. 35
  NEEMA OR MRS GEORGE Says:

  Nashukuru kusoma massage za vijana wenzangu zinatia moyo na inaonyesha ni jinsi gani vijana sasa tuko mstari wa mbele na Yesu wetu hakika mimi pia nahitaji maombi yenu haswaa niweze kusimama imara ktk wokovu huu mwaka uwe wa tofauti ktk maisha yangu baraka zimiminwe katka familia amen naimani Mungu anajibu . Amen

 21. 36
  B.J.KAMINYOGE Says:

  NAOMBA MAOMBI YENU,ILI NIWEZE KUWA JIRANI NA MUNGU NA KUWEZA KUITUMIKIA JAMII KWA MAMBO YALIYO MEMA NA KUMPENDEZA MWENYEZI MUNGU.

 22. 37
  B.J.KAMINYOGE Says:

  NAOMBA MAOMBI YENU,ILI NIWE JIRANI NA MUNGU NA KUNIWEZESHA KUITUMIKIA JAMII VYEMA, KWA UWEZO WA MWENYEZI MUNGU-AHSANTE.

 23. 38
  NEEMA OR MRS GEORGE Says:

  Bwana Yesu asifiwe wapendwa mimi ningependa niwatie moyo kwa mstari utakao katika kitabu cha Mathayo 18:19 – “Amin, nawaambieni yoyote mtakayofunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni, na yoyote mtakauyofungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni mstari wa 19 ” tena nawaambia ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na baba yangu aliye mbinguni”.Ndugu zangu wapendwa katika Kristo je ni kitu gani basi kitashindikana kwa Mungu wetu mimi naimani kabisa hata Ukimwi kwa Yesu una surrender Yesu si mchezo jamani kinachotakiwa tusimame Yesu alikuwa achukui muda katika kuomba sana sana alikuwa anahamrisha magonjwa yatoke na kuwacha watu wazima Amen!!!Sisi inatupasa kuomba kwasababu tunamhitaji Yesu atusaidie ashuke yeye alikuwa anamfufua mtu kwa kumwambia amka naye anaamka jamani kwa Yesu kuna raha sana maana tumepewa mamlaka na ili tuweze kutumia hiyo mamlaka ipasavyo hatuna budi kusoma neno lake, maombi kila kuitwapo leo kufunga ni njia za kumkaribisha Yesu ktk maisha yetu na kujinyenyekeza ili atutumie kama apendavyo si kama tupendavyo. Nina shuhuda nyingi wapenzi lakini kwa leo naomba niishie hapo naomba maombi yenu maana niko katika vita kali sana wapendwa niombeeni nisimame.Amen

  • 39
   sanga Says:

   Mungu akubariki sana Neema or Mrs. George kwa comment yako nzuri na yenye kubariki kwa wasomaji wote na hasa watu wenye mahitaji mbalimbali mbele za Mungu. Imeandikwa “*ombeni bila kukata tamaa”,* nami natoa wito kwenu wasomaji na waombaji wa blogu hii kuwa tusikate tamaa mpaka tuone mahitaji ya watu mbalimbali yanajibiwa. *Glory to Jesus.*

   • 40
    Mwanandoa Says:

    jamani naomba maombi yenu wakati nikiwa kazini watoto wanakuwa shule,
    wakati watoto wanarudi wanamkuta baba na mwanamke ndani kitandani.

 24. 41
  Dorah Says:

  naomba maombi yenu ili Mungu aniongoze katika safari hii ndefu ya maisha. Aiibariki kazi yangu, familia yangu. Pia naomba mniombee mwaka huu nipate kufunga ndoa na mchumba wangu.

 25. 42
  Terence Says:

  Bwana asifiwe.
  Hitaji langu ni kuomba msaada wa maombi ili Mungu anisimamishe imara katika imani. Nimeingilia na udhaifu wa kiroho, na niombapo mara nyingine najikuta na usingizi mzito. Nataka nguvu za Roho mtakatifu kutawala maisha yangu na kuniwezesha kupenda Mungu zaidi na apate kutawala maisha yangu yote. Mahitaji ya maisha ya hapa chini ya jua ninayo, ila ninaamini kama hayo yote nitapewa na kuzidishiwa kama nikitafuta kwanza ufalme wa Mbingu kama Mwokozi alivyosema.
  Mungu wetu awabariki na kuwawezesha kwa huduma yenu katika Jina la Yesu Kristo. AMEN.

  • 43
   sanga Says:

   Ndg, wapendwa wasomaji wa blog hii na hasa angle hii ya maombezi kwa mahitaji wa watu. Naomba kutoa wito kwamba utembeleapo blog hii na ukaona kuna watu wameandika mahitaji yao na wakataka tuwaombee basi maanisha kuwaombea, na njia rahisi ni kuanza kwa kuomba wakati unasoma hitaji lake, kumbuka Mungu anaumba maneno ya vinywa vyetu. So utakapotamka/kuandika neno ambalo ni positive kwa hitaji lake, Bwana Mungu saa ile atafanya jambo hilo kwa ajili ya mtu huyo. So ndugu yetu Terence katika jina la Yesu aliye hai tunakufungua kutoka katika nguvu za giza na udhaifu wa kiroho. Bwana Mungu na akupe nguvu mpya ya kukushindia katika vita iliyokukabili.

 26. 44
  sofia Says:

  Nomba Mungu ashukuriwe kwa kila jambo analolifanya kwake ni sawa, sasa mimi nomba nipate mume wa heri na mwenye upendo na amani. Maana ninavyosema hivi hapa nilipo nimeshafiwa na mume na kuniachia watoto 3. ambao hawana mapendo na familiya ya mume.

 27. 46

  Shalom,
  Naomba maombi mama yangu anasumbuliwa na kichwa na kila akipimwa hospitali hawaoni kitu, na bado anaumwa naomba wapendwa tusaidiane maombi, hizi ni hila za mwovu shetani zishindwe kabisa katika Jina La Yesu na mama yangu awe mzima.

 28. 47
  Brenda Says:

  Bwana Yesu Asifiwe wapendwa. Naomba mniombee baba yangu aweze kuacha pombe, UJEURI na kuishi maisha Yesu anayotaka. PIli naomba mniombee Bwana Yesu akuze imani yangu ili niweze kuomba kwa muda mrefu na niweze kusoma bibilia na kutafakari neno na kulifanyia kazikwani mara ninapotaka kuomba huwa naomba kwa kifupi. Pia naomba mumuombee mume wangu aweze kurudi nyumbani na kufanikiwa katika shughuli zake

 29. 48
  Isaac Mtwale Says:

  Kindly pray for me i need fees for MBA and ACCA

 30. 49
  johnson Says:

  mimi naomba niombewe ili niweze kumjua mungu zaidi

 31. 50
  johnson Says:

  crazyjohnston@yahoo.com 0756316499 mimi ni mwanafunzi ambae nini marafiki wengi kutoka nchi za nje wenye uwezo lakini ninapo jaribu kuomba msaada huwa mawasiliano yanakata naomba maombi kenye jambo hili mungu anisaidie.pia ni mmoja wa watumishi kwenye huduma ya maombi inayotolewa na mtumishi john arusha musono thank.

 32. 51
  ANNA PETRO JOHO Says:

  BWANA APEWE SIFA

  MIMI NINA KISUKARI NAOMBA MAOMBI YENU NA PIA NIOMBEWE ILI NIMJUE MUNGU ZAIDI

 33. 52
  nellys Says:

  Shalom wapendwa?
  Nataka kuwatia wote moyo kwamba Mungu wetu ni mwema,na hakika lazima utapata sawa na hitaji lako.

  Ninachowaomba nyote, ni IMANI zenu, na mziinue kwake Yesu, hakika hakuna jambo lolote gumu, lazima utapokea tu,

  Kwa Jina la YESU KRISTO, kila aliye leta ombi lake kwenye blog hii akapokee,tangu sasa.

  Tafadhali kumubuka kumshukuru BWANA MUNGU na kutoa Ushuhuda.

  BWANA YESU AKUBARIKI BILA KUMSAHAU MTUMISHI WA MUNGU SANGA.

  MCH NYS

 34. 53
  Esta Says:

  Naomba maombezi. Nami namuamini Mungu
  naomba niombeeni kazini kwangu kuna mhindi kihelehele sana wa kuwachongea wenzake uongo leo hii ameshanisemea uongo juu yangu
  naomba maombi ya kumtuliza mdomo na kihelehele.
  Niombeeni nipate amani Kazini.

  NAPENDA KUFANYA KAZI MAOMBI YASIMAME JUU YANGU HUYO MHINDI IKIBIDI AONDOKE KWANI ANANINYIMA RAHA MTOTO WA MUNGU BINTI WA YESU.

 35. 54
  SHUKRAN Says:

  NAOMBA MAOMBEZI YENU NIPATE MCHUMBA

 36. 55
  Esta Says:

  Chonde chonde waombaji tafadhali, nashindwa hata nisemeje,

  mume wangu alinifukuza, nikarudi kwetu nikaendelea kuomba bila kukoma, leo Mungu amenipa kazi, chakula na mahitaji, naendeleza ujenzi sasa wa nyumba yangu.

  nilichokosa ni wanangu, HOPENICE NA HOPELILY yeye aliyenifanikisha katika mambo yote hashindwi na kitu.

  nisaidieni maombezi tafadhali.

  mimi Esther.

 37. 57
  Vivian Says:

  Shalom naomba maombi yenu kwa ajili ya kupata kazi katika kampuni moja mkoani Tabora mshahara ni mzuri na mkubwa naona kuna vipingamizi naomba mnisaidie katika maombi maana ile kazi ni yangu ktk jina la Yesu.

 38. 58
  mary budili Says:

  Bwana Yesu apewe sifa wapendwa. Nahitaji maombi yenu, Mungu anisamehe madhambi yangu. Pia aniepushe na hatari zote. Anipe ulinzi wa Damu ya Yesu kwangu na kwa watoto wangu THERESA GRACE na BLANDINA LEAH.
  muwaombee pia watoto wangu hao. Mungu awape kufanikiwa katika masomo yao. pia awaepushe na kuwaponya na maradhi yote na nguvu zozote za mapepo, zikashindwe juu yao kwa Jina la Yesu. wawe na afya njema. awatie hofu yake ndani yao. awaongoze kwenye kila jambo.

 39. 59
  Charles Daniel Laiser Says:

  Shalom, Atukuzwe Mungu aliye juu nashukuru sana kwa neema hii ya kushirikishana katika maombi. Tuwe na Imani japo chembe ya Haradali kwani yote yawezekana kwake yeye . Mungu wetu ni Mwema na Ahadi zake ni za kweli daima .

 40. 60
  upendo/ma sunday Says:

  naomba mniombee nipate mtoto, pia Yesu aniokoe na roho ya kukataliwa na kunipa amani.

 41. 62
  anna karata Says:

  naomba mniombee afya yangu siyo nzuri

 42. 64
  mat Says:

  Bwana Yesu Asifiwe! Naomba mniombee nimekuwa nikinenwa mabaya kila baya ni mimi nimefanya naambiwa nimeathirika natembea na waume za watu kitu ambacho si chakweli kila anaenipenda akiambiwa anavunja mawasiliano nisaidie naamini Mungu anauwezo wa kuvunja hii roho.

  • 65
   sanga Says:

   Naamini kila msomaji anayesoma ujumbe huu anakuombea pamoja nasi, hata hivyo hata wakinena wewe yafute hayo maneno kwa Damu ya Yesu na kujitamkia yale ambayo ni positive kwako na kwa future yako. Soma Biblia itakuongoza katika kupata ahadi nyingi ambazo ni positive kwako. Kumbuka Isaya 54:17 inasema Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako, utauhukumu kuwa mkosa. Kwa hiyo usiogope na usibakie kuhuzunika yafute hayo maneno mabaya halafu jitamkie/jiumbie maneno mazuri sambamba na ahadi za Mungu kwako.

   Ubarikiwe, kumbuka laana isiyo na sababu haimpati mwenye haki, Daudi anasema ‘nalikuwa kijana nami sasa ni mzee lakini sijamwona mwenye haki ameachwa’. Our redeemer lives, just have faith on him.

  • 66
   Tausi Says:

   Mungu atakufanya uwe kama dhahabu safi mbele ya macho ya kila akuonaye mbaya!!!

 43. 67
  mama G Says:

  Naomba mungu anifungue na amtoe huyu shetani wa uvivu wa kusali ndani yangu kwani naamini kwa Mungu hakuna linaloshindikana, pia namwomba Mungu amuepushe mume wangu na tamaa za wanawake wa nje na pia azidishe amani na upendo kwenye familia yake.

 44. 68
  BEGGER NZAGI MARABI Says:

  ninahitaji maombi yatawale suala langu la kupata kazi kwani mimi ni kijana niliyesaidiwa na Mungu kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu kama engineer lkn sijapata kazi at least ya kuniwezesha kulipa vyumba hata vitatu kwa mwezi na chakula pia

 45. 69
  wema Says:

  Bwana Yesu asifiwe sana. Namshukuru sana Mungu kwa neema hii ya kushirikishana maombi. Naomba mniombee Mungu anisaidie nipate mtoto, pia naomba maombi yenu kwa ajili ya mume wangu anakunywa sana pombe yani kupita kawaida mpaka maisha yake yamekuwa hayaeleweki. Mungu amsaidie aweze kuacha pombe na aokoke.

  Mungu awabariki katika huduma hii.

 46. 72

  naomba mniombee namatatizo kazini. mungu aniteee ili niweze kuishi kwa amani hapa kazini.

 47. 75
  Tausi Says:

  Jamani Bwana Yesu Asifiwe!!
  Naombeni mniombee nina kesi ya kudhulumiwa haki yangu na bado kesi iko mahakamani kwa muda wa mwaka na miezi kadhaa sasa lkn haijawahi kusikilizwa kila wakati wananipa tarehe. Na tarehe nyingine iliyopangwa ni 7/12/ 2010 naomba tuombe pamoja niyapite hayo kwani sipendi kuingia mahakamani watenda kazi wa kule wananikwaza sana maana hawafati sheria.
  Mungu awabariki!!!!

  • 76
   sanga Says:

   Hello Tausi, Mungu akubariki kwa maombi yako juu ya watu wengine wewnye mahitaji mbalimbali, nasi tunaomba kwa ajili yako katika jina la Yesu aliye hai, kwamba akushindie katika kesi yako na haki itendeke, na yote uliyodhulumiwa Bwana akurejeshee, hata hivyo, mimi binafsi najua kudhulimiwa lakini inapobidi kusamehe, samehe.

   • 77
    Tausi Says:

    Ahsante kaka yangu Sanga…Mungu anipe nguvu lkn sipendi kudhulumiwa na wenye kiburi cha pesa..Ila mungu nipe nguvu ya kuyashinda haya.

 48. 78
  pius w.m Says:

  Bwana YESU asifiwe..!
  Naomba mniombee mimi nizid kuimarika ktk IMANI yangu,
  Pia naomba nipate MKE mwema tutakae ishi na kujenga familia ya Mungu.

  • 79
   Tausi Says:

   Mungu akupe kaka Pius kama ulivyonena.
   Ila mwombe Roho Mtakatifu akuongoze kupata mke mwema.
   Ubarikiwe!!

 49. 80
  florence Says:

  Naomba mniombee nipate mume mwema, nina miaka 38 na mwezi ujao Mungu akipenda nitakuwa na miaka 39, nimechoka na maisha ya upweke nahitaji mwenza.

 50. 82
  Edson Clemence Says:

  HALELUYA!KILA AMWENDEAYE BWANA NI LAZIMA AAMINI KWAMBA BWANA YUPO NA UWAJIBU WAO WAMWOMBAO,TUWE NA IMANI DHABITI,KUUONA WEMA WA BWANA NI LAZIMA.Tuzidi kuomba kwa ajili ya wana wa Mungu wazidi kumtafuta sana BWANA na huo utakatifu ambao bila kuwa nao hakuna kumwona Mungu.Pia tuombe kwa ajili ya watumishi wa Mungu waliojitoa kumtumikia Bwana ktk roho na kweli ili wasilewe na tamaa ya ulimwengu huu wakasahau kazi ya Mwajiri wao,maana adhabu itakuwa ni kubwa mno.

 51. 83
  rose Says:

  bwana yesu asifiwe.Ninaomba mniombee nipate mume mwema na pia nifanikiwe katika maisha.

 52. 84

  Naomba maombezi yaweze kuniponya kiroho na mwili. Mungu awabariki sana

  • 85
   sanga Says:

   Soma Kutoka 15:26…’Mimi ndmi Bwana nikuponyaye’. Uwe na imani Bwana ni mwaminifu aweza kukuponya, tunakuombea.

   • 86
    dorothy Says:

    Namshukuru Mungu Kwa ajili watoto ambao Mungu amenijalia, naomba mistari ya biblia inayohusu kuwaombea watoto hawa wamtambue Mungu zaidi, waiishi imani ya kikristu kadri ya Mapenzi yake Mungu, wawe watoto waadilifu na mfano kwa wengine, wawe na afya njema, na wajaliwe kufaulu vizuri mitihani yao na hata kupata elimu nzuri itakayowawezesha kujikimu maisha yao.

 53. 87
  Joyce Says:

  Bwana Yesu asifiwe, wapendwa naomba mniombee nipate mume kutoka kwa Bwana.

 54. 88
  Christina Says:

  MUNGU AWABARIKI WATUMISHI WA MUNGU KWA KAZI KUBWA MNAYOIFANYA YA KUFUNGUA WATU NA KUWAWEKA HURU SAWASAWA NA NENO LA MUNGU WETU, GOD BLESS U ALL.

 55. 89
  PETER Says:

  Bwana Yesu asifiwe nimeokoka nampenda Sana Yesu,naomba mniombee ni vuke hatua niliyo nayo kiroho sasa, naona kama sikui kiroho pia naandamwa na malaria na typhod kila wakati,madeni ndio usiseme yanaongezeka kila kukicha, pia mmuombee rafiki yangu ninaye fanya naye kazi naye aokoke na pia sasa hivi tuko ktk hali ya huzuni mama yake ameibiwa kisha nyumba imechomwa moto kila kitu kimeteketea tuombeeni wapendwa ni tuke hii hatua mbarikiwe sana

 56. 90
  peter Says:

  Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika bwana naomba sana mniombee ninaendelea kukabiliwa na madeni pia nakuwa mvivu wa kusoma neno la mungu

  • 91
   sanga Says:

   Tunakuombea Peter, Lakini pia kuhusu madeni ni lazima uweke lengo la kukusudia kulipa na kumaliza na zaidi kujizuia kuendelea kukopa. Na suala la kusoma neno la Mungu hakikisha unatenga muda kila siku wa kutulia kusoma na kutafakari. Ni lazima ujifunze kuwa na nidhamu ya kuwa na muda wa kusoma neno na pia kuomba. Bila kuwa na muda na pia kuamua kufuata ratiba yako hutaweza. Zaidi mruhusu Roho Mtakatifu ayatawale na kuongoza maisha yako. Ubarikiwe Peter, na Bwana akusaidie utoke katika utumwa wa madeni kwa jina la Yesu.

 57. 92
  Agnes Says:

  habari zenu,naomba mniombee nipate kazi jamani,nina degree ya Telecommunication Engineering,nipo kazini mwaka wa 4 sasa ila maslahi ni madogo sn,nimeshaandika sn barua kuhusu kuongezwa mshahara ila naona hakuna mafanikio,
  kwa sasa mimi na mume wangu tunachomlilia Mungu kuwa afanye ni kupata kibali mbele zake kwanza,then anipatie kazi nzuri tu.na nilipwe mshahara kutokana na qualification zangu

 58. 93
  Emmanuel Says:

  Naomba mniweke kwenye maombi. Kuna jambo nilitendewa na mjomba wangu nikiwa mdogo kati ya miaka 8-12. Miaaka yote ilopita sikulikumbuka. Lakini mwaka huu nakaribia kuoa ndipo ile kumbukumbu imerudi.Sasa nina miaka 31. Ninakosa amani kabisaa.Najua huu ni mpango wa ibilisi tu. Naomba mnikumbuke katika maobi hii hali iondoke na nisahau kabisa.

 59. 94
  Hossiana Says:

  Bwana Yesu asifiwe wapendwa!
  naombeni unisaidie kwa maombi kwani nasumbuliwa na tumbo sipati period na nahitaji kuwa na ndoa lakini kwa tatizo hili nahisi km sitopata mtoto naomba jamani maombi yenu na Mungu awabariki sana.

  • 95
   sanga Says:

   Tunakuombea Hossiana Bwana Yesu alete uponyaji katika tumbo sasa, tunakemea kwa jina la Yesu kila maumivu na shida ya tumbo, uwe mzima na majira yako yawe sawasawa, mwamini Mungu. Isaya 53:5

 60. 96
  sanga Says:

  Wapendwa wasomaji wa blog hii na hasa ukurasa huu wa maombi, napenda kuwakumbusha tena kwamba punde upitapo katika ukurasa huu na kusoma mahitaji ya wana wa Mungu ambao kwa ridhaa yao wameona vema wayaweke wazi kupitia ukurasa huu.
  Tafadhali usiondoke katika ukurasa huu bila kusema neno kwa maana ya kuombea mahitaji ya watu hawa, Bwana ni mwaminifu amekuwa akijibu mahitaji ya watoto wake kwa kadri ya mapenzi yake, utukufu na heshima vina yeye tu.

 61. 97
  Amfaress Says:

  Wapendwa Bwana Yesu apewe sifa.Namshukuru Mungu kwa ajili ya uaminifu wake kwa kila amwaminiye. Nilimuomba sana Mungu anipe mtoto, na kwa uaminifu wake sasa nina ujauzito wa miezi tisa, Hivyo naombeni wapendwa tushirikiane katika maombi Mungu anisaidie saa na wakati wake ukifike nijifungue salama na mimim na mtoto wangu tukawe salama.Amina

 62. 99
  joyce Says:

  Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika Bwana.

  Nimefurahi kuona huduma hi ikiendelea kwa ajili ya kutiana moyo na kujengana katika imani yetu , Ninaamini HAKUNA GUMU LA KUMSHINDA MUNGU ndio maana nachukua nafasi hii kuwashirkisha kuwa tuungane kumuombea mtoto CECILIA anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

  Mungu anzo spea za aina zote za mwili wa binadamu kwa sababu ndiye aliye muumba hivyo kwa njia ya maombi Cecilia anaweza kupokea uponyaji wake

  Bwana apewe sifa kwa ukuu wake chini ya jua

  • 100
   sanga Says:

   Amina Joyce, ni kweli Bwana anazidi kutusaidia, nasi tunaomba kwa jina la Yesu aliye hai nguvu za Mungu zishuke juu ya mtoto Cecilia na kuachilia uponyaji katika moyo wake. Tunaendelea kuomba kwa ajili yake. Kama upo jirani na huyo mtoto jifunze kumpa mistari yenye ahadi za Uponyaji ili awe anajitamkia kila siku. Mfano Kwa kupigwa kwake sisi tumepona nk.

   • 101
    osward Says:

    Osward
    Tunamuomba sana Mungu aweze kutupatia watoto,nina miaka minne ya ndoa sijabahatika kuwa na familia,naamini Mungu kupitia Yesu na maombi ya watu woe wenye mapenzi mema ili nasi tubarikiwe ,amina

   • 102
    sanga Says:

    Ndg. Oswald, tumwamini Mungu kwamba atafanya jambo kwa ajili yenu, tuanendelea kuomba kwa ajili ya muujiza huu kwenu.

 63. 103
  omega Says:

  Bwana Yesu apewe sifa, nimekutana na mambo mengi ya kunitia moyo.mimi naomba mniombee kwanza kabisa mume wangu hana kazi na pia ana kesi ya muda mrefu alipokua anafanya kazi kabla hajanioa mpaka sasa haijaisha kweli hii inanipa huzuni kubwa pia mimi nilikua muombaji lakini sasa ninashindwa kuomba kabisa hii nayo inanikosesha amani sana naomba tushirikiane kuomba ahsante.

  • 104
   sanga Says:

   Hello dada Omega, tumwamini Mungu kwamba atafanya katika haya mahitaji yako, usiache kusoma neno la Mungu, kwa kuwa ndio taa ya miguu yetu.

 64. 105
  KIFWE WILIMECK Says:

  I have been blessed with your service servent of GOD.May you be blessed!! I request you to help me know types of prayers

  • 106
   sanga Says:

   Thanks Kifwe, I’m writing a staff on prayers at large, pray for me that the Holy Ghost will make it relevant to you and the rest who requested the same staff.

 65. 107
  Victor Says:

  Bwana Yesu asifiwe naomba mniombee ninatatizo la moyo kwenda mbio na kushtuka,pia nina sumbuliwa na malari sugu ambayo huwa inanisumbua na kusababisha mwili kukosa nguvu mara kwa mara

 66. 108
  Sarah Mayanja Says:

  Niombeeni kwa Mungu wetu nipate kazi katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam. Mungu wangu anajua ninavyougua juu ya hili.

 67. 110
  tuiva Says:

  yote yawezekana kwake yeye aaminie

 68. 112
  aggy Says:

  Mimi naomba muniombee nina matatizo sana kila nikipata mchumba nakaa kama mwenzi simpendi tena, kuanzia mwezi wa 7 mwaka jana nilipata mchumba mwingine tena akaenda mpaka kwa wazazi kuanzia mwezi huu wa kwanza yametokea matatizo makubwa sana sijawahi kuona wala kusikia, kuna mtu anakuja anamwambia nimekuambia uachane na huyu Aggy, ana mpinga sana mpaka mwili wote huwa unama mikono inakufa gazi, nae kaniambia sikutaki tena ww unamatatizo, jamani naombeni msaada wa maombi kwa akili zangu ziwezi.

  • 113
   sanga Says:

   Amina Aggy tunakuombea, lakini kuna mambo ya msingi ningehitaji kujua toka kwako, nitakutumia maswali ya awali kwenye email yako. Mungu akubariki.

 69. 114
  Glady Says:

  Gladness
  Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu. Ombi langu kuu naomba uniombee kwani ninaumwa muda mrefu na tatizo langu ni mapepo naomba uniombee mtumishi wa Mungu kwani ninateseka sana, yananifanya nishindwe hata kufanya kazi zangu vizuri

  • 115
   sanga Says:

   Amina Glady tunakuombea na Bwana Yesu akuponye na kukufungua kabisa, mwishoni mwa mwezi huu nitakutumia mafundisho ya msingi ya kukusaidia.

 70. 116
  R omary Says:

  Mimi ni kijana nafanyaa kazi nje ya nchi shida yangu napata pesa lakini mambo hayaishi naomba Mungu kila siku mambo yawe mazuri lakini bado magumu,namshukuru sana Mungu kwa riziki ya kila siku.

  • 117
   sanga Says:

   Ndugu Romary, suala la pesa ni la kanuni zaidi, kuna vitabu vingi kuhusu matumizi ya fedha, naomba pata muda wa kusoma ‘staff’ mbalimbali kuhusu matumizi ya fedha na Bwana Yesu atazidi kukupa ufahamu mzuri juu ya namna ya kutumia fedha kwa utukufu wake na maendeleo yako binafsi. Nipatapo nafasi nitaandika mambo machache ya msingi kwa ajili yako.

 71. 118
  Marther Says:

  Shaloom watu wa Mungu,
  Jaman tusimame na tuwaombee watu wasio na watoto, kwani Bibilia inasema hakuna aliyetasa wala kuharibika Mimba katika nchi yako sasa kwa nini tatizo la utasa limeshamiri katikati ya vijana wengi sasa? tusimame kwa Umoja na Tuseme neno Naamini Mungu Huyu atarudisha uasili aliomuumba nao kila mmoja wetu. Amina..

 72. 119
  Emmanuel Rodrick Says:

  Mimi ninaitwa Emmanuel Rodrick ninasumbuliwa na maumivu ya mgongo,malaria sugu pamoja na vidonda vya tumbo muda mrefu, naomba watumishi wa Mungu mniombee ili shetani asijiinue katika afya yangu.

  • 120
   sanga Says:

   BWANA Yesu na akuponye na kukuondolea kila ugonjwa katika mwili wako, kukumbuka ahadi hii, kwa kupigwa kwake Yesu, sisi timepona na yeye ndiye mwenye kutuondolea ugonjwa usiwepo tena juu yetu.

 73. 121
  eddy Says:

  Bwana Yesu asifiwe naomba maombi kwa ajili ya mke wangu ajifungue salama

 74. 122
  dora Says:

  Bwana YESU asifiwe naombeni mniombee Mungu anijalie nifunge ndoa,vikwazo vinavojiinua kila wakati visipatikane na vishindwe jamani.Mungu anipe kuwa mke mwema.

  • 123
   sanga Says:

   Katika jina la Yesu, Bwana Mungu akufanikishe na kukuongoza katika kumpata mume mwema, uwe na amani tunaomba kwa ajili yako (Zaburi 32:8)

 75. 124
  Veni Says:

  Bwana Yesu asifiwe mtumishi tafadhali naomba uniombee Mungu aweze kunijalia watoto niko katika ndoa kwa muda wa miaka miwili sasa lakni bado sijafanikiwa kupata mtoto jambo hili linaniumiza sana hasa nikiona marafiki zangu ndugu zangu na watu wengine wanashika watoto wao kwa muda mfupi tu baada ya ndoa kwa kweli huwa ninaumia sana na kukosa raha na wakati mwingine linanifanya imani yangu ishuke naomba sana mniombee Mungu anisaidie `katika hili.Mungu akubariki

 76. 126
  Selewini mapunda Says:

  Bwana asifiwe sana, naomba mniombee mimi pamoja na mke wangu na mtoto wangu tunasumbuliwa na nguvu za giza kwa kiasi cha ajabu. Nimeokoka na niko kwenye maombi ya kuzuia balaa. Ndugu katika kristo

 77. 127
  Anna Says:

  Amen

 78. 128
  JANETH ABBU Says:

  Naommba mniombee juu ya mtoto wangu joseph alieanza kunywa pombe, kuvuta bangi na sigara na hapendi shule.pia nimekuwa na mikono ya chuma ulete, na madeni ni mengi. pia kuna mtumishi anataka kunirusha pesa zangu na ndoa haina amani na nina ugonjwa wa sukari na mkono wa kushoto unauma sana muda mrefu nikienda hospitali hawaoni kitu.Amen mbarikiwe sana

  • 129
   sanga Says:

   Bwana Mungu akutete na kukupigania katika mahitaji yako yote, mwamimini Mungu yeye ni Mungu wa yasiyo wezekana, nawe uwe mwaminifu kwake.

 79. 130

  BWANA YESU ASIFIWE,KWASASA NINARECORD NYIMBO ZA KUABUDU,NAOMBA MAOMBI YENU ILI KUPITIA ALBAM HII MIOYO YA WENGI IMWELEKEE MUNGU PIA IWE NI IBADA YENYE MAANA MBELE ZA MUNGU,HIVYO UTUKUFU WA MUNGU UKAFUNIKE KAZI HII.MUNGU AWABARIKI.

  • 131
   sanga Says:

   Amen, uwepo wa Bwana uende nawe katika kazi yako.

   • 132
    sanga.wordpress.com Says:

    Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu. Naitwa Elimonsia Minja nina mwanangu anaitwa John Benedicto anasoma form two lakini hataki kwenda shule. tukimpeleka shule baada ya siku tatu anatoroka. Ninaomba maombi yako mtumishi wa Mungu. Mimi pia nipo kwenye mafungo kwa ajili ya watoto wote wanaokataa kwenda shule kwani nafahamu tatizo halipo kwangu peke yangu. Ninaamini kwa uwezo wa Mungu atatenda kwani yote kwake yanawezekana

 80. 133
  Dada L Says:

  Naomba uniombee nipate mchumba mwema,msomi na mwenye kazi

 81. 135
  JANETH ABBU Says:

  Isaya 54:13
  Na watoto wako …………………………
  Mungu yu pamoja nasi atatenda kwani hata wangu anaitwa joseph ameanza kuvuta sigara pombe, bangi na wasichana. Tusaidiane kuomba Mungu ni mwaminifu Ameen

  • 136
   sanga Says:

   Amen, mwaminini Mungu ndugu zangu, atafanya njia juu ya watoto wenu. Tunaomba kwa ajili yenu, na ni imani yangu kila msomaji apitaye kwenye ukurasa huu, anafanya hivyo.

 82. 137
  UPENDO Says:

  Bwana YESU asifiwe, naomba mnisaidie kushirikiana nami katika maombi ya kumuomba MUNGU amuwezeshe mume wangu kupata uamisho wa kazi kutoka Mwanza kuja Dar es Salaam. Namuomba MUNGU atutendee muujiza na amkumbuke mume wangu ili apate uamisho kwani ameshakata tamaa ni mda mrefu sasa kuanzia mwaka 2008. Naamin MUNGU atatutendea AMEN.

 83. 138
  Leocadia Stanslaus Says:

  Bwana Yesu asifiwe. Kaka Sanga naomba maombi yenu kwani mimi nimekuwa napoteza kumbukumbu mara kwa mara, naweza nikapewa pesa nikaweka sehemu baada ya muda sikumbuki nani alinipa na nimeweka wapi, na hili tatizo limekuwa likinisababisha kukwaruzana na mume wangu naomba mnisaidie. Mungu akubariki.

  • 139
   sanga Says:

   Tunaufungua ufahamu wako kwa damu ya Yesu, BWANA akuponye na kukurejeshea kumbukumbu vema. Mwamini Mungu tunaomba kwa ajili yako.

 84. 140
  Leocadia Stanslaus Says:

  Kaka Sanga pole na kazi ya Mungu wa Yakobo,…… naomba pia nikushirikishe katika maombi ya kuomba mume wangu amjue mungu, amtumainie yeye katika kila jambo, na apate kiu ya kumjua Mungu.

  • 141
   sanga Says:

   Amina dada Leocadia, umechagua fungu jema, tunakuombea na tunamuita mumeo kwa jina na damu Yesu aje kumjua Mungu. Naam Bwana Yesu na akutendee wema.

   • 142
    Leocadia Stanslaus Says:

    Amina!! kaka Sanga Mungu akuinue juuu zaidi, akuepushe na majaribu, akutie nguvu zaidi katika kazi yake. Mume wangu sasa ameanza kufungua Biblia.Ubarikiwe.

   • 143
    sanga Says:

    Amina sifa na heshima kwa Mungu wetu, na tuendelee kuomba kwa ajili yake, Bwana azidi kumfungua macho yake na kumuonyesha neema yake.

 85. 144
  JANETH Says:

  Watu wa mungu Bwana Yesu ainuliwe juu sana.Nisaidieni kumsihi Mungu juu ya mtoto wangu Joseph alieanza kuvuta sigara,bangi,pombe na kujihusisha na ngono na sasa alikuwa fomu five lakini amefukuzwa baada ya kushikwa na mirungi shuleni. kaka Sanga nisaidieni jamani niko njia panda.

  • 145
   sanga Says:

   Hello dada Janeth, pole kwa hili, lakini lisikuvunje moyo, Shetani anajaribu kuharibu future ya mwanao, uwe na amani katika hili Shetani hatafanikiwa kwa kuwa lile alilolikusudia Mungu juu ya mwanao litafanikiwa (Rejea Isaya 46:9-11), nasi kwa Jina la Yesu tunamfungua Joseph kutoka kwenye kila namna ya nguvu za giza na kwa damu ya Yesu tunamfunika awe salama. Zaidi ukipata nafasi anza kufuatilia mfufulizo wa somo ambalo naendelea kuandaa, ili kusoma mfululizo huo bonyeza link hii https://sanga.wordpress.com/2011/11/20/ijue-na-kuitumia-nafasi-yako-ya-ulinzi-katika-ulimwengu-wa-roho/ naamini somo hili litakusaidia sana. Nimeshafika sehemu ya nne ya mfulululizo huu kwa hiyo fuatilia masomo yote mpaka part 4. Wombaji wenzangu na tuundelee kuombea mahitaji ya watu mbalimbali, Mungu awabariki kwa huduma mfanyayo.

 86. 146
  JANETH Says:

  Kaka Sanga nashukuru sana kwa maombi haya ya joseph mwanangu. huyu mtoto nilimpata nikiwa bado shule na babake ni masai ukoo wa mollel.Sikuolewa tena nae kwa hio nakaa na mtoto peke yangu baba hatoi ushirikiano wowote wala gharama zozote.niliolewa na mume mwingine na tunaishi vizuri na mtoto lakini ndo yaliyotokea hayo niliyoeleza mwanzoni. Nimegundua kuwa mizimu ya kwao ndo inamfuatilia huyu mtoto na kumletea yote hayo.Nisaidieni kumtenga na hio mizimu ya kwao. Be blessed all.

 87. 147
  Joram Yona Says:

  BWANA YESU akutunze sana.

 88. 148
  violet kaitila Says:

  Bwana Yesu Asifiwe sana,

  ni kwa neema ya MUNGU tu nimeoneshwa blog hii, nashukuru kwa huduma Mungu awabariki sana sana. blog hii indelee mbele!

  naomba mnisaidie kuomba mafanikio mema katika mwaka huu 2013 mimi pamoja na familia yangu. Nimeanzisha miradi mbalimbali naomba minisaidie pia kuomba Mungu aweke mkono wake wa baraka na mpenyo wa kifedha maana nilikopa fedha kwa ajili ya kuanzisha. Hivyo Mungu aniwezeshe biashara hii irudishe madeni na faida ya kuendeleza mradi huu nijisimamie mwenyewe nisiendelee kukopa, na Mungu aguse miradi yangu nipate wateja tele niendelee kumshukuru Mungu na kutoa shuhuda kwa wengine.

  kabla ya kuanza shughuli zangu niliwaomba wanamaombi kutoka kanisa la winners chapel – banana ukonga kuja kubariki na kuweka wakfu eneo lote na nimeendelea kuomba na kufunga kwa ajili ya baraka za Bwana mahali hapo pa biashara, Mungu afungue milango ili hata wasioamini kuwa Mungu anatenda kuwa kupitia maombi yaliyofanyika pale watu wengine nao washuhudie Mungu alivyojibu, nilianza mwaka jana mwezi wa saba, na nikaweka matangazo kuwa yatima bure. naomba Mungu andelee kunipigania maana kuna watu wananikatisha tamaa sana sana lakini mimi nasimama tu katika Bwana na kusoma zaburi ya 123.

  GOD BLESS YOU. EMEN

  • 149
   sanga Says:

   Amen hongera kwa kutambua kwamba Mungu pekee ndiye atufanikishaye, uwe na amani waombaji wengine pamoja nasi tunaendelea kuomba juu ya mahitaji haya. Ashukuriwe Yesu kwa ajili ya yote atendayo katika blog hii.

 89. 150
  julia gathonni Says:

  niombee bwana yangu na mimi tupate kazi kwani tumesoma na biashara kidogo yenye tumeanza mwaka huu iinuke.

  • 151
   sanga Says:

   Katika jina la Yesu, BWANA Mungu na awafungulie mlango wa kazi sawasawa na taaluma yenu, naam aibariki biashara yenu pia.

   • 152
    Leocadia Stanslaus Says:

    Kaka Sanga nashukuru kwa maombi, katika punguzo la wafanyakazi mimi bado naendelea kufanya kazi.Mungu akubariki sana na akuinue juu zaidi hasa katika nyakati hizi za mwisho.

   • 153
    sanga Says:

    Glory to Jesus, hakika ashukuriwe Mungu.

 90. 154
  Pendo Says:

  Bwana Ysu asifiwe wanamaombi,
  Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu wetu kwa uaminifu wake. Nasema asante kwa Yesu kwanza kwa kunifia msalabani kwa ajili ya wokovu wangu. Namshukuru Mungu kwa kujibu maombi yangu. Nimezungukwa na madeni mengi ambayo kwa namana ya kibinadamu kwakweli hayalipiki. Kwa njia ya imani naamini Bwana ameshatenda muujiza na madeni yameshalipwa kwa jina pekee la YESU KRISTO. Mungu ni mwema na mponya pia. I’m claiming the most perfect solution kwasababu Biblia inatufundisha kuwa imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Kiroho nimeshalipiwa deni zangu. Bwana atasema na wadeni wangu. Ataweka sawa maisha yangu. Amen.
  Mungu awabariki wapendwa.

 91. 155
  Mariam Says:

  Wapendwa tumsifu Yesu Krito. Ninaomba kuwashirikisha mniombee kwani nina tatizo la amani katika familia yangu. Pia watoto wangu hawana kazi ninaomba muniweke kwenye maombi ili impendeze Mungu wapate kazi kwani tumeomba kwenye ofisi mbalimbali. Mimi mwenyewe ninataka kusajili biashara yangu ya usafi wa mazingira na shughuli zinazofanana na hizo hivyo mniombee ili impendeze Mungu nipate kibali machoni pake.
  Ahsante, , Mariam.

 92. 158
  JANETH Says:

  Niombeeni juu ya mume wangu aliyeshikwa na kahaba na sasa amezaa nae.

 93. 160
  Leocadia Stanslaus Says:

  Imenigusa sana, hakuna namna zaidi ya kumtegemea Yesu Kristo aliyetufia pale msalabani kwaajili ya dhambi zetu. Funga na kumlilia Mungu mumeo ataachana tu na huyo kahaba, nami pia nakuombea mwanamke mwenzangu.Ee Yesu mwema naomba uiumbe upya ndoa ya huyu dada Janeth. Amina.

  • 161
   sanga Says:

   Mungu akubariki sana dada Leocadia kwa huduma yako, kwa hakika mwili wa Kristo kwa ujumla unahitaji maombi kutokana na changamoto unaozikabili.

 94. 162
  mama B Says:

  helo,mimi ni mama wa mtoto mmoja,nimeolewa na tuko vizuri na mume wangu,naomba maombi yenu jamani,tunaishi nyumba ya kupanga,mume wangu anakaz nzuri tu serikalini ila hatujengi na kila siku ni wimbo wangu nikimsisitiza tuanze ujenzi,yaani anasema tutaanza tutaanza,mpaka nahisi kama kuna nguvu za giza jamani ambazo zinazuia tusijenge,tumeshaenda hapo kufanya maombi ila wapi,tafadhali tuombee kama ni pepo lishindwe ktk jina la Yesu

  mama B

  • 163
   sanga Says:

   Amen BWANA Mugu awapiganie katika suala hilo la ujenzi kupitia jina la Yesu, kwa imani tunatamka mwaka huu 2013 hatua kubwa ya kuanza na kuendelea na ujenzi wa nyumba yenu ifanikiwe, naam Mkono wa Mungu uwe juu ya ndoa yako kulifanikisha hili.

 95. 164
  mama B Says:

  Amen

  Mama B

 96. 165

  Bwana Yesu asifiwe!, Mimi naitwa Kelvin napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mungu kwa wema wote alionitendea mpaka kufikia siku hii ya leo ninaishi na mwenye afya njema kabisa. Kusema kweli sikumbuki ni siku gani nimetumia dawa au kuumwa maana ni mda mrefu mno, naamini ni kwa neema na upendo wake Mungu ndiyo niko hivyo sasa, pia napenda Kumshukuru Mungu kwa kunisaidia katika masomo yangu ya chuo kikuu kwani mpaka hii leo nipo mwaka wa tatu na wa mwisho katika chuo kikuu cha Dodoma. Kanivusha vikwazo vingi mno, nasema ASANTE BWANA MUNGU KWA YOTE ULIO NITENDEA, NAOMBA UKANIFANYE VILE WEWE UPENDAVYO

 97. 166

  Wana na mabinti za baba amani na iwe kwenu, naomba mniombee kwani niko katika safari ya kutafuta mchumba au mke, kwani jambo hili linaninyima raha na linanipa changamoto sana. Niombeeni nipate mke mwema na mcha Mungu.

 98. 168
  PHINA Says:

  BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI WA MUNGU NAOMBA MAOMBI KWA AJILI YA KUPATA WATOTO MAPACHA NIMETAFUTA KUPATA MIMBA MIAKA KUMI MPAKA LEO SIJAFANIKIWA MTUMISHI NIOMBEEN NIFANIKIWE

  • 169
   sanga Says:

   Katika Jina la BWANA wetu Yesu Kristo pokea, naam BWANA na akupe sawasawa na haja ya moyo wako (2Nyakati 20:20)

 99. 170
  Mama Emma Says:

  Nimesoma kwenye blog hii shida na matatizo mbalimbali yanayowakabili wana wa Mungu aliye hai,maombi yangu ni haya; Bwana awajibu siku ya dhiki, jina la Mungu wa Yakobo liwainue,awapelekee msaada toka patakatifu pake, na kuwategemeza toka sayuni.Azikumbuke sadaka zao zote,na kuzitakabali dhabihu zao.Awajalie kwa kadri ya haja za mioyo yao na kuyatimiiza mashauri yao yote. Bwana awatimizie matakwa yao yote kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake aliotenda katika Kristo Yesu alipomfufua katika wafu na mcho ya mioyo yao yatiwe nuru wajue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo, katika jian la Yesu Kristo wa nazareth . AMEN

 100. 172
  tamaly Says:

  Bwana Yesu asifiwe naomba maombi Mungu anisaidie nipate mahitajiya chuo ada,laptop

 101. 176
  Elibariki mushi Says:

  Naomba mniombee kwa mungu hitaji langu la kupata kazi mahali panaitwa ms tcdc au denish kazi ya umeme na bomba.

 102. 178
  Edson Says:

  Bwana yesu Asifiwe SANGA
  Naomba maombi natarajia kufunga ndoa mwezi wa saba lakini naona kuna migogoro isio na kichwa wala miguu inatokea hasa kwa upande wa familia ya baba yangu mzazi kiasi cha kunipa mashaka kama kweli tutaifikia siku hiyo bila vikwazo.Pia naomba maombi kwa wale wote ambao wamehaidi kuniunga mkono mungu akawape nguvu ili wafanikishe kile walichohaidi roho ya HAPANA isipate nafasi mungu akubariki sana SANGA!!!!!!!!

 103. 179

  Naitwa Gasto Richard
  Naomba maombi juu ya familia yetu tume kuwa ni watu wa shida sana kila tunacho jaribu kufanya hakifanikiwi tukujenga nyumba zinabomoka biashara mitaji inakufa yaani ndugu tumekuwa ni watu wa ajabu mpaka majirani wanatucheka, naombeni maombi yenu jamani hali ni mbaya sana, kazi nimefukuzwa familiam inanitegemea mpaka hela ya chakula inanikosa sasa kila nacho shika hakifanikiwi naomba maombi yenu..

  Ahsanten na Mungu awabariki

  • 180
   sanga Says:

   Ooh BWANA Yesu akutetee ndugu Gastor, naamini hata waombaji wengine hawataacha kuombwa kwa ajili yako. Ila naomba huku tukiendelea kuomba zingatia yafuatayo; soma Kumbukumbu la Torati sura ya 28 yote itakusaidia na ufanyie kazi, pia angalia uhusiano wako na Mungu kwenye eneo la zaka (Malaki 3:7-10).

 104. 181
  JANETH Says:

  Bwana Yesu Kristo wa Nazaret asifiwe Sanga/wapendwa.Naomba mniombee juu ya ndoa yangu na pia mtoto wangu Joseph ambae hataki shule amenisumbua muda mrefu na sasa nimempeleka huko Kampala Uganda na bado anasumbua kutorokatoroka shule na kwenye ulimwengu wa roho alikuwa ananiambia mama mimi sitaki shule tena. Nisaidieni jamani lango la elimu la huyu mtoto linufuatiliwa muda mrefu na nafsi yake itakuwa imeshikiliwa mahali lakini hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Kuna marafiki wanamdanganya.Tumwombeeni kumtenga noa na kuwa na marafiki wazuri na wawe na hofu ya Mungu. Amen.

  • 182
   sanga Says:

   Amina dada Janeth, mwamini Mungu kwa habari ya family yako, naamini waombaji wanaopita kwenye blog hizi na kusoma mahitaji haya pamoja nasi tunaomba na tutaendelea kuomba kwa ajili yako nyumba yako.

 105. 183
  JANETH Says:

  Amen kaka Sanga nashukuru. Naamini kwani hakuna lisilowezekana kwa baba yeyu wa Mbinguni.

 106. 184
  Lugano Mwailolo Says:

  Habari zenu watumishi wa Mungu, Ni mara yangu ya kwanza kutembelea website hii. Naomba niungane nanyi, nataka mniombee niweze kuendelea na masomo yangu mwaka huu kwani nilikwama kutokana na gharama. Nina imani MUNGU atafanya

 107. 186
  JANETH Says:

  Mungu aliekuleta hapa Duniani kwa makusudi yake yatatimia usiogope.
  Endelea kumwangalia yeye peke yake

 108. 187
  Happiness Says:

  Bwana yesu asifiwe naomba mniombee natarjia kufunga ndoa mwezi wa nane tareh kumi na saba iliniweze kufanikiwa pia naomba mniombee nisiwe na hasira na niwe na heshima hasa kwa mume wangu mtarajiwa,

 109. 189
  Candida Nkobelerwqa Says:

  Bwana Yesu Asifiwe.
  Naitwa Candida Nkobelerwa ni mara ya kwanza kutembelea blog hii naomba niungane nanyi katika maombi. Naomba tuombee mtoto wangu Neema ambaye amejaza nafasi za kupata vyuo hivyo basi Mungu aweze kumchangulia chuo kizuri na aweze kupata mkopo wa masomo kwa sababu katika Bwana Mungu hakuna lisilowezekana. NINA IMANI MUNGU ATAFANYA MUUJIZA JUU YA MTOTO WANGU

 110. 191
  JANETH Says:

  Amina Candida.Mungu Atuangalie sisi sote hata mimi nina mtoto ninaemlea anaenda chuo kikuu, Mungu atusaidie sisi na wengine wote wenye watoto kama sisi wapate hio mikopo na vyuo vizuri wapate kuendelea na masomo yao ili neno la Mungu likatimie AMEN.

 111. 192
  JANETH Says:

  Happiness pokea kama ulivyoomba Mungu wetu ni mwaminifu.

 112. 193
  salome Says:

  Naomba mniombee niweze kupata mchumba mwema mwenye upendo wa dhati maana naamini Mume mwema hutoka kwa Mungu

 113. 195
  JANETH Says:

  Amen pokea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti kwa sababu Mungu anasema ombeni lolote kwa jina langu name nitawapa

 114. 196
  mariam njalambaha Says:

  Mungu awabariki wote mnaoshiriki katika BLOG. hii mimi Mariam mwanangu Rehema yuko JKT baada ya kumaliza form six naomba mumuombee amalize salama pia apate mkopo atakapo jiunga na chuo kikuu pia waombeeni sana watoto wangu hawako kwenye mazingira mazuri mdogo wake yuko kunduchi girls. Mungu awabariki na akutane na haja zenu.

 115. 197
  Mama peter Says:

  Bwana Yesu asifiwe!, Mimi naitwa Mama Peter napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mungu kwa wema wote alionitendea Mimi na familia yangu mpaka kufikia siku hii ya leo,naamini ni kwa neema na upendo wake Mungu ndiyo niko hivyo sasa.Ningependa kuwashirikisha katika maombi ya tatizo la mtoto wangu Peter anayesumbuliwa na mafua ya muda mrefu (allergy) na pia anatatizo la kutoweza kutafuna vitu vigumu na kumeza toka alipozaliwa na sasa yupo darasa la sita.naamini Mungu wetu ni mwema na ni mponyaji atafanya kadiri tunavyoomba hata maandiko yake yanasema ombeni lolote kwa jina langu nami nitawapa.NINA AMINI MUNGU ATAFANYA KADIRI YA MAHITAJI YANGU..AMEN

 116. 199
  Joseph Pius Says:

  amen hutusikia jamani wapendwa tusilegeze imani tusonge mbele

 117. 200
  Coellastina Nangi Says:

  Naye alituokoa kutoka katika nguvu za giza akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake ( Yesu) Kol 1: 13. Ufalme wake ni wa milele

 118. 201
  Isaac Says:

  Naombea kira mutu ambaye aanashida kuhusa maisha yake, yatima na wajane Mungu awakumbuke wagonjwa pokea nguvu kwajina la Yesu. pokea kazi wewe, yatima jueni baba yenu Jesus na Mungu awa baliki.

 119. 203
  Carol Says:

  Naomba mniweke kwenye maonbi Mungu afungue njia na anipe hekima ya kuweza kumaliza madeni niliyonayo nakosa raha na sina amani lakini nina imani Mungu wetu atafungua njia. Amen

 120. 204

  Bwana Yesu asifiwe,
  Naitwa Yonas naumwa koo na kipindi cha nyuma niliumwa nilipoenda hospitali wakaniambia hakuna kitu lakini nilikua nasikia kama kuna kitu baadae nikabadilisha hospital daktari akatoa inzi wanne(imepita kama miezi 4) lakini sasa hiyo halo imerudi na naona kama hii sio hali ya kawaida…….niombeeni jamani wapendwa kama ni roho za kishirikina zishindwe…..simulation yangu ni +254715515085,+255783317316

 121. 206
  beda robert Says:

  nina matatizo katika maxomo yangu kila wakati nashindwa kufikia malengo yangu tangu niingie A-level sijawahi kufanya vizuri kabisa katika masomo yangu hivyo naamini tukishirikiana katika maombi naamini naweza kubadilika naombeni mnikumbuke katika sala zenu na YESU atawabariki Amina…

 122. 208
  happiness Says:

  TUMWAMINI MUNGU KATIKA KILA TUNALOMWOMBA KWA KUWA YEYE HAWAHI WALA HACHELEWI.MPENDWA USICHOKE KUPELEKA HITAJI LAKO KWA BWANA YESU YEYE NDIE KILA KITU NA ATATENDA,MWELEZE YEYE.

 123. 209
  JANETH Says:

  Bwana Yesu na akuwezeshe kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.
  Kaka Sanga naomba maombi juu ya motto wangu Joseph ambae nimekuwa natuma maombi kwenu ili aombewe.Joseph amekuwa kila akienda shule yoyote ile lazima afanye kosa afukuzwe.Kwa sasa yuko huko Kampala anasoma form five lakini bado anasumbua tu ndipo nilipogundua kuwa walichukua shati la motto wangu na kulizika na kunenea maneno kwamba hatasoma atakuwa ni mtu wa pombe na madawa na mengine mengi. Kwa sasa niko kwenye maombi ya kumtoa huko kuzimu walikomzika wakimtumikisha ili maisha yake yawe ya kawaida. Naombeni maombi yenu watumishi wa Mungu.

  • 210
   sanga Says:

   Amina dada Janeth, mwamini Mungu waombaji mbalimbali pamoja nasi tunaomba juu ya mwanao na mahitaji mengine, Isaya 54:17 inasisitiza kwamba kila silaha itakayofanyika juu yake haitafanikiwa.

 124. 211
  esta Says:

  Mungu ni mweza wa yote tena ni mwaminifu .plz mniombee nahitaji kibali cha Bwana maishani mwangu.

 125. 212
  BARAKA M ELIYA Says:

  naitwa Baraka naomben mniombee kwa yesu kristo nipate kazi nipate kutoa zaka niombeen wapendwa

 126. 213
  mwalami Says:

  namba muniombee mimi fundi ujenzi sipati kazi zangu za kujenga .natafuta msichana wa kuishi nae cdae tuowane nisaidieni mm mwalami

 127. 214
  Majaliwa Says:

  Naomba muungane nami kuomba kwa ajli ya Kupata Mke mwema,maana”…Mke mwema anatoka kwa BWANA”.Pia tuombee kwa ajili ya amani ya Tanzania,Vijana na Mchakato wa kupata katiba mpya.

 128. 216
  michael mwimanzi Says:

  hongera sana kwa maneno mazuri na mungu wetu akubariki

 129. 217
  michael mwimanzi Says:

  naomba mnisaidie maombi nina kaka yangu anaitwa pius ulaya anasumbuliwa na kisukari sasa ni muda wa miaka 6

 130. 219
  mwalami Says:

  mwalami naomba maombi ya nguvu nipate kazi

 131. 220
  J Says:

  Bwana yesu asifiwe
  naomba msaada wa maombi,nina umwa Tb pia naomba Mungu aniponyeshe maana natumia dawa HIV Nimeathirika na amini kama mungu anaweza yote pia yote ya wezekana kwake naamini nitapona katika jina la yesu kristo.
  Amen.

 132. 222
  tumu Says:

  am blessed…. Mungu wa mbinguni awabariki sanaa

 133. 223
  NELSON Says:

  KATIKA JINA LA YESU! NAMUOMBA MUNGU ANIPE WAZO LINALOTEKELEZEKA LITAKALONIWEZESHA KUPATA MAKAZI MAZURI YENYE AMANI FURAHA NA UPENDO

 134. 224
  rose ernest mnzava Says:

  nahitaj maombi sana naumwa tumbo

 135. 226
  Joseh hubert Says:

  Bwana Yesu Asifiwe watumishi wa Mungu,Nimefurahia masomo yenu,ningependa kujifunza masomo yenu.Naamini nitasaidiwa na Bwana yesu awabariki

 136. 228
  sillah joseph Says:

  NAOMBENI MNISAIDIE KUOMBA KWA MUNGU WETU NIPATE KUMJUA NA KUMTUMIKIA YEYE, PIA NAHITAJI AMAN NA UPENDO KTK FAMILIA YETU.BWANA AWABARIKI SANA WAPENDWA.

  • 229
   Osward.Mbwile Says:

   Mungu hutenda kulingana na nia yako ya ndani , hivyo soma sana neno lla Mungu maana ndio nuru kujua unaelekea wapi hapo utamtumikia sawasawa na unavyohitaji ubarikiwe na Bwana

 137. 231
  sillah joseph Says:

  skuamin kama ujumbe wangu ungeonekana, kiukweli napenda sana kumpokea roho mtakatifu ili awe mponyaji na mwokozi wa maisha yangu pia nipate nguvu na mamlaka ktk kukemea pepo wachafu. NISAIDIENI KUOMBA WAPENDWA MAANA HATA NAFASI YA KUFIKA KANISANI IMEKUA ISHU KUIPATA KUTOKANA NA KAZI NILIYO NAYO, NNAYATEGEMEA MAOMBI YENU WAPENDWA.

  • 232
   sanga Says:

   Hello Sillah jambo unalohitaji kuotka kwa Mungu ni pana sana na haliji kwa maombi tu, tafadhali nitafute kwa namba 0755 816 800 nitakueleza nini cha kufanya, na zaidi nipatapo nafasi nitakuandikia kwenye email yako moja kwa moja.

 138. 233
  Temihanga Says:

  Naomba Mumuombee Ndugu yangu RICHARD Myovela Kwani Anatatizo la Kulala muda mrefu anaonekana mtu aliyekata tamaa ya Maisha.Alipelekwa kwa Mganga wa Kienyeji akafukiwa kuku..akatolewa nywele na kucha.akanyweshwa damu ya njiwa Yakasomwa maneno ya kiarabu toka hapo ni matatizo naomba Maombi kuvunja mikata hiyo Katika Jina la yesu nimeamini AMINA

  • 234
   sanga Says:

   BWANA Yesu na amponye, tunakiri kufunguliwa kwake katika jina la Yesu, tunendelea kuomba kuomba kwa ajili yake

  • 235
   Osward.Mbwile Says:

   Hakuna jambo linaloshindikana kwa Mungu amini atapona, lakini kikubwa kili kwa jina la Yesu kuvunja kila maneno na mikataba ya kipepo natafuta msaada wa kiroho zaidi kwa watumishi wa maombi ya ukombozi

 139. 236

  Bwana yesu asifiwe naitwa grace naomba kuombewa ni fanikiwe katika maisha

  • 237
   sanga Says:

   Ok, Grace kufanikiwa kimaisha ni kitu kipana sana, na hakitegemei maombi peke yake bali vitu vingi ikiwa ni pamoja na kuliweka neno la Mungu kwenye matendo (Rejea Kumbukumbu la Torati Sura ya 28:1-15). Hakikisha unasoma neon la Mungu kila siku, unalitafakari na kulitenda naam utafanikiwa katika kila utendalo (Zaburi 1:1-3)

  • 238
   Osward.Mbwile Says:

   Mungu afungue milango ya mafanikio sawasawa na unavyohitaji na ishi maisha ya utakatifu pia mtegemee Mungu utafanikiwa

 140. 239
  janeth Says:

  Mungu ni mponyaji na wewe pokea uponyaji toka kwake.

 141. 240
  Osward.Mbwile Says:

  Mungu ni mwaminifu hujibu mahitaji yetu hivyo hakikisha unaamini kile anachosema ktk maneno yake msikate tamaa kuna wakati mtatokea upande wa mafanikio

 142. 241
  Vedastus Mayunga Says:

  Bwana Asifiwe
  Mimi naitwa Veda,nina matatizo katka mahusiano yangu na mchumba wangu sasa ana mimba yenye matatizo,naomba mniombee ili niweze kupata pesa ya kumpeleka hospitali kwani nin mwezi sasa nahangaika.

  Asante kwani
  Mungu ni mwema

  • 242
   sanga Says:

   Poleni sana ndugu Veda, hakika Mungu ni mwema, hata hivyo mmevuka mipaka, kwani uchumba sio ndoa, hivyo ni muhimu kuomba toba kutokana na hayo yaliyojitokeza mkingali wachumba na si wanandoa, naam BWANA Mungu awarehemu, amponye mwenzi wako na kila aina ya madhara na zaidi awasaidie katika changamoto ya fedha.

 143. 243
  Junior jaka Says:

  Hakika Mungu ni muweza hakuna kinachoshindikana kwakwe

 144. 244
  Godoni yohana Says:

  Mungu ni mwema,yeye atushindia yote.

  • 245
   CRAIN Says:

   Wapendwa katika bwana naomba tushirikiane katika maombi yakumuombea

   mtoto wa mdogo wangu ana miezi kumi anatalajia kufanyiwa operation ya koo siku ya jumatatu naomba maombi yenu.Na namuomba mungu amponye katika jina la yesu naamini atatenda.AMINA

 145. 246
  Happyness Says:

  Hakika hakika ni hakika hakuna jambo linalomshinda MUNGU.

 146. 247
  Mama peter Says:

  Bwana asifiwe,wapendwa wa bwana naomba niwashirikishe maombi ya mtoto wangu veronica anatakiwa kufanya interview muda wowote kutoka sasa.namshukuru Mungu sana hata kwa mwanangu kuwepo katika short list.BWANA AWABARIKI SANA WAPENDWA, Mungu ni mwaminifu.

 147. 248

  Bwana wetu yesu kristo asifiwe.ninaomba niwashirikishe kwenye maombi yangu ninataka kazi kwani ninahitaji kufanyakazi ya mungu kutoa zaka na sadaka pamoja na kuwasaidia maskini lakini sina kipato cha kutosha kuyafanya hayo jina la Bwana libalikiwe.AMINA

 148. 249
  BETHPALASEMA Says:

  HAKUNA LISILOWEZEKANA

 149. 250
  Mama peter Says:

  BWANA YESU ASIFIWE, NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KWA YOTE ALIYOWEZA KUNIFANYIA MWAKA JANA NA MWAKA HUU 2014,TAREHE 23 JANUARY NILITUMA MAOMBO KUWASHIRIKISHA KATIKA KUMWOMBEA BINTI YANGU VERONICA ANAFANYA INTERVIEW.WAPENDWA MUNGU NI WAAJABU HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU AMEPATA NAFASI HIYO ILIKUWA MOJA,NA KULIKUWA NA USHINDANI MKUBWA WENYE KUJAA (MEMO) ZA KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI LAKINI SISI TULIKUWA NA MEMO KUBWA AMBAYO ILIFUNIKA VI MEMO VYOTE AMBAYE NI BWANA YESU.NAPENDA KUWATIA MOYO WAPENDWA WANGU MUNGU ANAJIBU MAOMBI KWA WALE WANAOMTAFUTA NA KUMWOMBA KWA IMANI.TUZIDI KUOMBA NA KUMTEGEMEA MUNGU.

 150. 252
  Leocadia Stanslaus Says:

  Bwana Yesu asifiwe, wapendwa naomba mniombee kwani nina maumivu ya kiuno na chini ya kitovu yakiambatana na vichomi, kwasasa ni siku ya tano tangu nianze kuumwa. Kuna dose ambayo nilipewa nitumie kwa siku 14 na leo ni siku ya sita. Mbarikiwe.

 151. 254
  Leocadia Stanslaus Says:

  Nashukuru kwa maombi kaka Sanga, mimi naendelea vizuri. Ubarikiwe.

 152. 256
  Emmy komba Says:

  Naomba mniombee nibadilike nimfuate mungu niachane na yadunia. Pia nipate mchumba mwema

 153. 258
  Emmy komba Says:

  Pia mniombee familia yetu afya njema upendo na mshikamano. Pia nipate kusahau yote niliyotendwa. Ikiwa ni pamoja na kukanwa na baba mzazi

 154. 259
  Furaha Chibululu Says:

  Shalom,Naomba mniombee Kwa ajili ya kupata kibali cha kwenda kusoma pia

  kupata mume anayetoka Kwa Bwana.

 155. 260
  seleman Says:

  naomba maombi sina amani kazini nataka kuacha kazi familia haitaki imekuwa ugomvi .na mimi nimepanga kujiajiri

 156. 261
  Joseph Satori Massawr Says:

  Let the world pray for me. Amen

 157. 262

  naomba mmiombee kufunguliwa kwangu nimekosa mbele za Mungu na wanadamu pia ninakosa amani kwan nimesababisha mtu mwingine kuumia kwa sababu yangu.

  • 263
   sanga Says:

   Neema ya BWANA Yesu iwe nawe, amaini Mungu wetu ni wa rehema, jambo la msingi ni kutengeneza na kutoendelea kusababisha maumivu kwa wengine

 158. 264
  gayl Says:

  bwana yesu asifiwe mimi naomba mniombee niweze kupata mtoto maana umri unazidai kwenda na sijabahatika kupata mtoto nisaidieni kwa maombi jamani

 159. 265
  Neema. Says:

  Bwana Yesu Kristo asifiwe.ninaomba mniombee haswa famila yetu tuko mabinti wa tano na hata mmoja hajaolewa na kwa hao watatu wa kwanza wote tunamiaka zaidi ya 26,tunaomba maombi ili milango hii ya unyumba ifunguke ili wote tuwe na familia wetu.

 160. 267
  amosi mbogo Says:

  maombi yangu ni biashata yangu.mungu afungue baraka tuweze kupata pesa.na tuweze kulipa kodi ya pango ambalo ni ghari sana.ninaamini bwana atafanya

 161. 268

  Maombi ya kazi, mwenyezi mungu naomba nibarikiwe,

 162. 269
  majaliwa Says:

  Nawasalimu katika jina la Yesu.Wapendwa naomba muungane nami kwenye maombi kwa ajili ya mitihani inayonikabili.Nimefanya Mara nyingi bila mafanikio.Na amini kwa MUNGU hakuna linashindikana.

 163. 271

  Baba kwa jina la yesu,naomba unibariki baba, niweze kufanikiwa ,kupata kazi, baba katika jina la yesu,,,naamini kuwa maombi yangu umeya sikia,baba,,naomba, maombi yangu yafunikwe na damu ya yesu kristo ,,,Amina

 164. 273

  Katika jina la yesu wa nazareth ,naomba unibarikh,baba nifanikiwe kujiunga na wenza ngu katika ,kiwanda changuo,nainua macho yako nikukuomba, baba nibariki

 165. 274
  selina Says:

  nai
  naomba maombi yenu juu ya familia yangu

 166. 275
  Emmanuel Belyo Says:

  Bwana Yesu asifiwe. Naomba maombi yenu ili Mungu amfungue mke wangu katika magonjwa yanayomtesa. Pia tuungane katika maombi Mungu atusamehe dhambi tulizofanya mimi na mke wangu.

 167. 276
  steven Says:

  Naomba msimamie maombi yangu ya kazi ,mungu anibariki anilinde,aniongoze,anipe mwanga,anipe ujasili wa kuepuka mabaya,asante yesu

 168. 277

  NAOMBA MNIOMBEE KTK KUCHUMBIA NI MPATE MKE MWEMA NA BWANA AWABARIKI

 169. 278
  Mussa adamu Says:

  Bwana Yesu asifiwenaitwa Mussa Adamu Mahiga, ninamtumikia Mungu katika huduma ya uinjilisti. ninaomba maombi mungu aniinue zaidi

 170. 280

  Amina

 171. 281
  lazaro Says:

  mafundisho ya biblia

 172. 282
  selina Says:

  bwa
  Bwana yesu apewe sifa ninaomba maombi kwa ajili ya mdogo wangu Loyce J. M. amefanyiwa oparesheni ya uvimbe lkn bado mshono unamsumbua na pia anasumbuliwa na kutopata usingizi na anaweweseka usiku kucha anaongea maneno mengi kama mtu mwenye mapepo.

 173. 284
  flora Says:

  Bwana yesu asifiwe. Watumishi wa Mungu naomba mniombee nipate kibali kutoka kwa Mungu cha kuendelea na masomo yangu kwan nimefika hatua nzur ila nimekwama kwa kutopata msaada wa ada. Naomba Mungu anionyeshe njia na aifanye njia kwenye elimu yangu maana yeye ndie alieanza kunipandisha mlima huu.

 174. 285
  asnath john Says:

  Shalom naomba mniombee nipate mme bora wa kunioa awe anampenda mungu

 175. 286
  Leocadia Stanslaus Says:

  Bwana Yesu asifiwe .Wapendwa naomba muungane nami kwenye maombi kwa ajili ya kumuombea mwanangu (Matilda F. Kimaro) ambaye anatarajia kufanya mitihani wiki hii tarehe 10/09/2014 na 11/9/2014 ili aweze kufaulu vizuri.

 176. 287
  mama peter Says:

  Bwana Yesu asifiwe!, Mimi naitwa Mama Peter napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mungu kwa wema wote alionitendea Mimi na familia yangu mpaka kufikia siku hii ya leo,naamini ni kwa neema na upendo wake Mungu ndiyo niko hivyo sasa.Ningependa kuwashirikisha maombi kwa ajili ya familia yetu ambayo haina maelewano,pia namwombea mdogo wangu Anitha anasumbuliwa sana ugonjwa wa akili mungu amsaidie amalize chuo.

 177. 288
  elina masewa Says:

  ningependa kushiriki maombi na nyie mungu awabariki sanaaa

 178. 292

  Mimi ni mfanyakazi wa hospitalini nimeapply kwenda.kusoma na nimepata chuo na sasa naenda kuomba ruhisa kazini…naomba kifanikisha ruhusa kwa maonbezi….

 179. 294
  lydon Says:

  please pray for me, i dont have a job

 180. 296
  Mkumbo Mkoma Says:

  thank you kaka..

 181. 297
  Monica Says:

  Tuwaombee wanafunzi/wanachuo ili waweze kufanya kile walichofuata shuleni/chuoni na si vinginevyo, ili Mungu awafanikishe katika elimu yao. Asanteni.

 182. 298
  Monica Says:

  Wapendwa katika Bwana, naomba tuwaombee wale wanaishi katika mazingira magumu watoto, vijana na watu wazima. Mungu awakomboe, awasaidie na kuwafanikisha.

 183. 299

  amina monica

 184. 300
  Godwin Says:

  Mwanangu ana tatizo la kuanguka anajiweza sana kimasomo tatizo linakuja hapo sasa, tumwombeeni kipitia nyie apone

 185. 301

  Nakuombea Bwana aweze kumponya

 186. 303
  Jofrey Sakara Says:

  Nimeipenda Huduma Hii, Nami Naandika Mahijaji Yangu Muda Si Mrefu Maana Nimepitia Mambo Mengi Ktk Internet Kuhusu Huduma Hii, Mungu Awabariki Muifanye Kazi Ya Bwana Kwa Uadilifu.

 187. 305
  JOYCE ANDREW SINGANO Says:

  Bwana Yesu asifiwe, niko karibu kujifungua naomba maombi yenu ili Mungu anifanyie wepesi wa jambo hili.

  • 306
   sanga Says:

   Mwamini Mungu, tumekuwa tukiomba kwa ajili yako, kila itahitaji linalowekwa hapa watumishi mbalimbali wanaendelea kuyaombea hata kama bado haujajibiwa kimaandishi katika ukurasa huu. Barikiwa

 188. 307
  Joel Mtangoo Says:

  bwana yesu asifiwe
  Ninayofuraha kubwa kufikia blogi hii…nimefarijika na nimejengeka sana kupitia mafundisho yaliyoandikwa na watumishi wa bwana. Namshukuru Mungu sana kwani nimeona imani yangu ikikua. Nina mahitaji ambayo nitayatuma kupitia e mail yenu.
  Mungu awabariki wote
  Mr joel

 189. 309
  Chaka sauda Says:

  Naitwa dada S. naomba niombewe kila nifanyacho hakifanikiwi nampenda Yesu

  • 310
   sanga Says:

   Hello dada S. Pole kwa changamoto unazopitia, Yeremia 29:11 inasema wazi kabisa kwamba ‘Mawazo ya Mungu juu yako ni ya amani na ya mafanikio wala si mabaya’ hivyo uwapo na Kristo huna sababu ya kutofanikiwa. Je umempokea huyu Yesu kama BWANA na mwokozi wako? na pia uko wapi? Kama upo huru kujibu haya maswali hapa nijibu, kama haupo huru nijibu kupitia email yangu farixipa@gmail.com. Mungu ni mwaminifu atafanya njia na kwako.

 190. 311
  elina masewa Says:

  Bwana Yesu asifiwe mm niko arusha napenda kushiriki nanyi ktk maombi nimechanganyikiwa naomba msaada wa maombi nina madeni makubwa na zimebaki siku tano natakiwa nipeleke naomba bwana Yesu anisaidie sina mungu mwingine wa kumtegemea ila yesu tu mungu awabariki sana

  • 312
   sanga Says:

   Neema ya Kristo ikusaidie, kila upatapo fedha kwanza kumbuka kutoa zaka, pili lazima uweke Mpango wa kulipa hilo deni na kwa hiyo kwenye kila fedha utoe pia peas ya deni mpaka utakapomaliza. BWANA Mungu akusaidie na kukupa kibali mbele za wanakudai iwe mtu binafsi au Taasisi mpaka umalizapo deni lao, wasikuchukulie hatua kali.

 191. 313
  trova Says:

  naomba mniombee niweze pata kazi, na hii kazi inisaidie niweze somesha angalau hata watoto 5 kutoka ktk kituo cha watoto yatima

 192. 314
  Samson CHIRHUZA Says:

  Naomba muniombee Mungu anitie nguvu katika huduma. Niwe mtumishi mwaminifu katika kazi yake.

 193. 315
  Japhet Gabagambi Says:

  Naomba ushirikiano ktk maombi ya kazi. Mi ni dereva na nimeokoka nampenda Yesu

 194. 316
  OMBENI MBISE Says:

  Nimeipenda sana huduma yenu.MUNGU WA MBINGUNI AWABARIKI SANA.

 195. 317

  Nashukuru kwa kazi njema ya kusambaza neno la Mungu kwenye mtandao maana watu wengi wataweza kuokolewa kupitia hayo mafundisho

  • 318
   sanga Says:

   Amen, tuzidi kuomba kwamba BWANA awape watu wengi kupenda kujifunza neon lake kupitia mtandao, maana Shetani ametumia fursa ya mtandao kuharibu maisha yao

 196. 319
  Samuel Martin Mendulo Says:

  Bwana Yesu Apewe Sifa! Ninamshukulu Mungu Kwa Ajli Ya Huduma Hii Maana Inazdi Kunionyesha Njia Mim Kama Mtumish Chipukiz Ahsante, Na Mungu Alyeumba Mbingu Na Inchi Azdi Kuwabariki Nakuwapa Maono Zaid Na Zaid Amen

 197. 321
  upendo mwatwinza Says:

  Mungu awabariki sana! Naomba mniombee kuhusu ndoa yangu izidi kuwa na amani.

 198. 323
  Julieth Says:

  Naomba nisaidiwe kuomba nipate mtoto/watoto na furaha

 199. 325
  Teddy Says:

  Tumsifu Yesu Kristo. naitwa Teddy. Ninaosumbuliwa na madeni mengi ya pesa. Ninaomba mnisaidie katika maombi niondokane na madeni na madeni hayo yote. Ninateseka sana moyoni kwani kila jinsi ninayofikiri kupunguza madeni nakabiliwa na ongezeko la mahitaji ya pesa. Pia ninaomba mnisaidie kuomba Mungu amuongezee mume wangu kipato. Kibinadamu naona ni vigumu lakini najua pia kuwa nchi na vyote vilivyomo ndani yake ni mali ya Bwana na hivyo madeni yangu sio hata nukta ya utajiri wa Mungu wetu. Pia njia za Mungu si za mwanadamu na mawazo yake si kama ya mwanadamu hivyo ugumu nauona mimi tu kwa sababu ya ubinadamu wangu na ufahamu wangu mdogo. Nimeona katika hii blog wako watu wengi wenye shida kama ya za kwangu. Ninaomba Mungu atufunulie uso wake na kuturehemu, asikie kilio chetu atupe yote tunayomwomba sawasawa na mapenzi yake kwa ajili ya sifa na utukufu wa Jina lake amina.

 200. 326

  Naomba maombi ,mimi niko mombasa, kwakweli nimejaribu kutafuta maisha ila kila ninavyo fikilia nina failed. pia ninapataga pesa nashindwa vile sinaisha bila kufanyia kitu! naitaji maombi, naamini huu ni mwisho wa matatizo yangu.

 201. 327
  Magreth Says:

  Mungu nisaidie ktk magumu ninayo pitia

 202. 328

  Napenda kumshukuru mungu kwa kila jambo hakika wema na fadhili zake zitanifuata sikuzote za maisha yangu jumapili njema watu wote

 203. 329
  faudhia Says:

  Tumuombe Mungu katika roho na kweli

 204. 330
  Judith Constantine Says:

  Naitaji maombi yenu

 205. 331

  Natafuta ada ya chuo naomba mniombee

 206. 332
  pinaelly Says:

  shallom watumishi wa Mungu naomba mniombee nategemea kujifungua karbuni ,Mungu anifanyie wepes katika hili tukio…

 207. 333
  Emanueli meela Says:

  Amani ya Bwana iwe nanyi nyoote, furaha yangu kuungana nanyi katika maombi. Bwana Yesu wakusanyikapo wawili watatu kwa jina langu mimi nitakuwepo kati yao,tena akasema mpaka sasa hamjaomba kitu bado? Ombeni chochote kwa jina langu ili furaha yenu itimizwe Mungu awabariki sana

 208. 335
  Lutengano Mwakasege Says:

  Bwana Yesu apewe sifa! Namtumainia Mungu ktk yy anitiaye nguvu. Naomba maombi juu ya Dada yangu ni mgonjwa miaka mitano sasa bado anaumwa.

 209. 336
  pauline Says:

  Mwokozi wangu ni bwana mungu wangu nami namuomba anisimamie

 210. 337
  Judy Saul Says:

  Bwana Yesu apewe sifa naomba mniombee naumwa upande mmoja wa mwili hasa kichwa na kifua upande wa kulia

 211. 338
  jimson detaramo Says:

  i need prayer from you so that through you God may bless me and give a good job

 212. 339
  Charles Mmbaga Msengi Says:

  Mungu aibariki na Ku iinua zaidi huduma hii.

 213. 340
  PATRICIA Says:

  Naomba mniombe naenda chuo kuSOma lakin ada yangu ndogo nategemea mkopo kutoka bodi ya mkopo ya elimu ya juu.naombamniombee nipate mkopo na pia chuoni nikaishi kwa aman

 214. 341
  leticia nduwimana Says:

  BWANA yesu apewe sifa , ninaugonjwa wakujikuna kwenye mwili nimeshaenda hospital awapate ugonjwa naomba msaada wamaombi watumishi wa mungu asanteni sana

 215. 342
  Simon William Says:

  thanx for this

 216. 343
  Yeriko Says:

  Bwana Yesu apewe sifa,Mimi naomba tuungane kumshukuru MUNGU kwa kuvuka salama mwaka 2015.Pili tuombe kutembea nae kwa mwaka 2016.Mipango yetu yote aisimamie yeye.

 217. 344
  Emmanuel kibaki Says:

  Naitwa Emmanuel kibaki Nasoma kidato cha nne lakini nimekuwa sina bidii kwenye masomo yangu nafeli mitihani kila mara naomba maombi yenu maana ndo mwaka wa mwixho huu na ukizingatia nina rudia tena kufanya huu mtiani maana nilixha fanya2012 nikafeli sasa nimerudia tena lakini hali niileile naomba maombi yenu jamani nateseka xana

 218. 345
  Ailine Maro Says:

  Bwana Yesu Asifiwe, Mimi naitwa Ailine, nina shida nyingi sana lakini kinachonikosesha raha ni mdogo wangu, Jerome, kuumwa huu ni karibu mwaka wa 20. tangu alipomaliza form IV mwaka 1992/3 alipigwa kichwani na akachanganyikiwa. hadi leo yuko Moshi na bado hajaweza kupona. Mtu wa kumsaidia kule hajapatikana baada ya Baba yangu kufariki agusti 2015 na Mama alikwisha fariki 1996. Naomba mumweke Jerome katima maombi maalum kwa Mungu wetu ili aweze kusikia maombi yangu. Pili, ninawaombea watoto wangu wawili wa kiume Mungu awalinde na mabaya yote na awainue katika kazi na masomo yao ili wawe na maisha mazuri. Nawaombea watoto wa ndugu zangu ninaokaa nao Mwenyezi Mungu aniwezeshe kuwasomesha na wasome na kufanikiwa katika maisha yao. Amen

 219. 346
  Rachel L. Stephano Says:

  Bwana Yesu asifiwe mtumishi, naitwa Rachel ninaomba maombi npate kaz maana nme2ma sana barua bila mafanikio wala majibu ni miaka miwil sasa tangu nihitimu. AMEN

 220. 349
  Bonny Says:

  Bwana Yesu Asifiwe. Ninaitwa Bonny na nlikua na mahitaji ya maombi Kwa Mungu. Namwomba Mungu Anisaidie nipate pesa za kumaliza research yangu ya masters mapema na kwa urahisi. Mungu Anipe kazi nzuri, mke mwema, hekima, maarifa, upendo kwa watu wote na fursa nyingi, amani na furaha pia visinipungukie. Nashukuruni kwa maombi na ninaimani Mungu Amenijibu vyote. Mungu wabariki na muishi maisha marefu.

 221. 350

  Nitwa rachel Haule naomba mniombee imani yakupenda kumtegemea mungu na si mwanadamu

 222. 352
  Rachel haule Says:

  Bwana apewe sifa naomba mniombee tamaa za kidunia zisipate nafasi katika maisha yangu,bali neno la mungu lipate nafasi

 223. 353
  juma samuel Says:

  MUNGU
  Mungu atukuzwe kwa huduma hii

 224. 354
  ailine Says:

  Ashukuriwe Mungu Mkuu kwa kuniona na kunikumbuka, kupitia blog hii ya huduma ya maombi. Naamini nimebarikiwa kwani niyaombayo ninayaona, ndugu yangu aliyekuwa anaumwa bila msaidizi kwa muda mrefu nimeweza kwenda kumchukua na niko nae na anaendelea vizuri kupitia huduma ya maombi yenu na ya kanisa la Breackthough Boko Magengeni kwa Mchungaji G. Simtomvu. Mbarikiwe wote na BWANA Mungu Amen

 225. 355

  MTUMISHI WA MUNGU SANGA MUNGU AKUBARIKI SANA KWA HUDUMA YAKO NIMEMWONA MUNGU KATIKA MAPITO YANGU NAOMBA MAOMBI KWA AJILI YA WATOTO WANGU ELIMU NA MAISHA YAO KWA UJUMLA NAOMBA MAOMBI KAZINI KWA MUME WANGU ULINZI AMANI KIBALI MAFANIKIO NA MIMI NAOMBA MAOMBI KWENYE MJI WANGU BONITE MIEMBENI NAOMBA MAOMBI KAZINI KWANGU HUDUMA YANGU AFYA YANGU NAOMBA MUNGU WANGU ANIPE KIBALI MAFANIKIO MUNGU WANGU AINUE UCHUMI WETU TUNAOMBA ULINZI WA MUNGU AMEN

 226. 356

  MTUMISHI WA MUNGU SANGA NAOMBA UNIOMBEE KWA MUNGU BABA HEKIMA BUSARA NA UFAHAMU KATIKA JINA LA YESU KRISTO PIA NAKATAA ROHO YA MADENI KWA JINA LA YESU KRISTO AMEN

 227. 357
  gelas Says:

  amen

 228. 358
  Flavian Faustine Says:

  Bwana Yesu asifiwe sana mtumishi wa Mungu. nimebarikiwa sana na ujumbe mzuri unaoutoa ili kuwainua wote wamjue Kristu na kuenenda katika wokovu. Naomba pamoja na jumuia yako ya maombi mniombee maana napata shida hasa katika kuisikia sauti ya Mungu. pamoja na namna ya Kuomba. Asante sana

  • 359
   sanga Says:

   Amina, twaomba kwa ajili yako pia

   • 360
    vicky alex Says:

    Bwana Yesu asifiwe mimi naomba mnisaidie kuomba napenda nimtumikie mungu kwa viwango vya juu zaidi, lakin nimekua kila nikijitahidi kufanya kazi ya Mungu vinatokea vikwazo mbali mbali mpaka nahisi kuchoka. pia anipatie mpenyo katika biashara yangu ya stationery.

   • 361
    sanga Says:

    BWANA Mungu akukumbuke katika mahitaji yako yote

 229. 362
  vicky alex Says:

  Bwana Yesu asifiwe hongera kwanza kwa kazi yako mtumishi wa Mungu, naomba mniombee nami napenda kuwa na Nyumba yangu, nimechoka upangaji. naamini ni kwa maombi tu kila kitu kinawezekana.

 230. 363

  naomba maombi yenu wapendwa nnashda ya ada na muda umekwisha wa kuripoti chuoni

 231. 364
  Gamaliel Shiuga Says:

  Bwana Yesu asifiwe naomba maombi mimi nimwimbaji pia nahubili naomba Mungu ainue Huduma yangu na aitambulishe ulimwenguni, Amina

 232. 366
  Beatrice Mathias Says:

  Nilivyomaliza form6 ndio dada zangu walimaza masomo yao ya degree sasa mimi ndo namaliza mwakani ila dada zangu hawajawahi kupata kazi wala hata ndoa wako wawili,kwa Mungu wetu ninaamini kila kitu ni timezone ila kwa maombi yetu timezone yao yaweza kuwa sasa,asanteni na Mungu wetu awatie nguvu kwa kila mlitendalo na haja za mioyo yenu akazitimize kwa mapenzi yake AMEN!

 233. 368

  NAOMBA MAOMBI MUNGU ANIPE NGUVU YA KUOMBA NA KUPATA MAJIBU KWA MUNGU BABA YANGU WA MBINGUNI AMEN

 234. 369

  NAOMBA MAOMBI KWA AJILI YA WANA WA MUNGU EVANS JEREMIA NA ELISHA J ZAHABU WAFANIKIWE KATIKA MAISHA YAO NA HUDUMA YAO NA FAMILIA ZAO AMEN

 235. 370

  WAPENDWA KATIKA KRISTO YESU NAWAOMBENI MNIOMBEE FAMILIA YANGU MJI WANGU AFYA YANGU MUME WANGU KAZINI KWETU MSUKUMO WA KUSOMA NENO LA MUNGU KWA BIDII AMEN

 236. 371
  OKULIANNA SALEMA Says:

  MUNGU AKUBARIKI SANA MTUMISHI WA MUNGU NILITUMA MAHITAJI YANGU MNIOMBEE NA MUNGU BABA AKANIJIBU AMEN

 237. 373

  Shalom naomba maombi sababu njia za kifedha zimefunga kabisa natafuta kwabidii lakini ibilis kajiinua kupita kiasi mwaka wa pili sasa riziki zimefunga nahitaji maombi yenu ili kwakupitia maombi yenu MUNGU anionekanie na utukufu umurudie Yeye ili pendo lake lizidi kudumu. ndani yetu kama biblia ilivyo sema tumbeane naombeni mniombee nifunguliwe niweze kua huru na hichi kifungo ili niweze kuona pia familia yangu baada yakua mbali nayo miaka miwili sasa niko mozambique MUNGU awabariki

 238. 374
  vicky alex Says:

  Bwana Yesu asifiwe wapendwa, mimi nina shida kwakweli kila ninapojaribu kufanya kazi ya Mungu ndipo mambo mengi ya kunikatisha tamaa yanainuka mpaka nashindwa tena kuhimili, kwa kweli wapendwa nashindwa sijui nifanyeje.

 239. 375
  napenda Says:

  shalom naomba mniombee mungu afungue milango niweze kulipa madeni ya anisani niliyo ahidi pia niweze kjenga nyumba ya kuishi mungu afungue milango yanu aniondolee magonjwa umasikini

 240. 376
  napenda Says:

  nashukuru mungu kwa kunisaidia kupokea maombi yangu pia nahitaji mwenza wangu wa kubadilishana naye mawazo kutoka kwa bwana

 241. 377
  JENIPHER Says:

  SHALOM WAPENDWA,
  mimi naomba mniweke kwenye maombi yenu Mungu akanipatie mtoto

 242. 379
  napenda Says:

  BWANA YESU ASIFIWE SANA WATUMISHI WA MUNGU NAOMBA MAOMBI KWA AJILI YA WATOTO WATOTO WANGU WAOKOKE KABISA WAFANIKIWE KATIKA MAISHA YAO MASOMO YAO MUNGU AWALINDE AWAEPUSHE NA MABAYA YOTE YA DUNIA HII MUNGU BABA AWAINUE KUTOKA MAVUMBINI NA KUWAKETISHA NA WAKUU AMEN

 243. 380
  napenda Says:

  WATUMISHI WA MUNGU NAOMBA SANA MNIOMBEE NINA MAPITO SANA AFYA YANGU KAZINI .MAZINGIRA NINAYOISHI MJI WANGU HUDUMA YANGU MAMA YANGU NA FAMILIA YAKE YOTE NDETEFYOSE AACHE UCHAWI KABISA MUNGU ASHUGHULIKE NA WACHAWI WASHIRIKINA WOTE MAADUI WATESI WOTE WALIO KINYUME NA FAMILIA YANGU MUNGU BABA AWASHUGHULIKIE AMEN MUNGU BABA AWABARIKI SANA KWA HUDUMA YENU NJEMA

 244. 382
  OKULIANA Says:

  NAOMBA TUOMBEE SANA VIJANA JAMANI WANAANGAMIA MUNGU AWAPONYE KATIKA JINA LA YESU TUOBEE NDOA FAMILIA TAIFA LA TANZANIA UCHUMI KAZI YA MUNGU IENDELEE MBELE AMEN

 245. 383
  OKULIANA Says:

  JAMANI WAPENDWA NAOMBA MNIOMBEE NINA MAPITO BABA MUNGU ANISHINDIE YOTE

 246. 385
  Jackline mnefi Says:

  Amen

 247. 386
  Prisca kira Says:

  Mungu ni mwema kwagu

 248. 387
  Prisca kira Says:

  Mungu ni mwema kwagu
  Hitaji langu naombeni mniombee niwe mwepese wa kusali, mwepesi wa kusoma neno la Mungu na kulitafakari vyema

  Nahitaji kuombewa ili nipate mume mwema na mwenye hofu ya Mungu. Mungu awabariki katika kazi zake za kumtumikia yeye.

 249. 388
  Bina Says:

  Bwana Yesu Asifiwe,nimebarikiwa kwa maombi yenu watumishi,Mungu wa mbinguni aendelee kututunza na kutuongezea imani,kwa kujiweka sawa kiimani ndipo milango yote inafunguka


RSS Feed for this entry

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: