Vitabu

Mpenzi msomaji licha ya kuandaa masomo, Mungu amenijalia kipawa cha uandishi wa vitabu mbalimbali vya kiroho. Mpaka sasa nimeandika na kuchapisha vitabu viwili. Kitabu cha kwanza ni “Njia kumi za Kibiblia za kumpata mwezi wa maisha” cha mwaka 2006 na cha pili ni “Ruhusu mapenzi ya Mungu yatimie kuhusu mwenzi wa maisha” cha mwaka 2010.

Hadi sasa kwa neema ya Mungu nimeshaandika vitabu zaidi ya vitano ambavyo vinasubiri kuchapishwa baada ya kukamilisha uhariri wake vizuri. Ninamshukuru Mungu, aliyenijalia neema hii na kipawa hiki. Ni imani yangu kwamba, Bwana Yesu atafanikisha uchapishaji wa vitabu hivi kwa ratiba yake.

Hakika nimethibitisha Mungu akiponya maisha ya watu wengi hasa vijana kupitia vitabu nilivyoviandika awali kwa kushirikiana na mke wangu maana vitabu husika vimeweza kufika na kuingia mahala ambapo binafsi nisingweza kufika.

Suala la uandishi na uchapiji wa vitabu lina gharama kubwa  kimuda na kifedha pia. Hiyo kadri upatavyo nafasi shiriki pamoja nasi baraka hizi za uandishi kwa kuchangia gharama za uchapishaji wa vitabu hivi. Kama upo tayari kugharamia sehemu ya gharama hizi tafadhali wasiliana nami kwa simu na. 0755 816 800 au email: paxifari@gmail.com.

Hata sasa bado naendelea na uandishi wa vitabu vingine, changamoto kubwa ni muda wa utulivu ili kukamilisha kazi husika, hivyo ninaomba maombi yako.

Utukufu na Heshima vina wewe Yesu, Wastahili BWANA. 

Advertisements

24 comments

 1. Bwana Yesu Asifiwe!
  Ninachukuwa nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kunijalia uzima na afya.Mpendwa katika Bwana wetu Yesu Kristo pole kwa kazi ya Bwana.Mimi ni kijana ambaye nimeokoka na ninamtukia Mungu, sijapata mwenzi wa maisha, na nilipokuwa katika mtandao nimekutana na semina za aina yake zenye kunitia nguvu katika maisha yangu na zaidi katika kumtumikia Mungu.

  Kwasababu ya mafunzo haya niliyoyapata ninaomba kujua ni mikoa ipi ambako umevipeleka vitabu vyako. Moja kati ya vitabu kichonivuta ni “Njia kumi za kibiblia zitakazo kusaidia kumjua na kumpata mwenzi
  wako katika maisha yako” na “Matumizi ya damu ya Yesu katika kurejesha mahusiano yaliyoharibika.
  Mimi ninaishi mkoa wa Iringa,Wilaya ya Makete. Hivyo ninaomba kujulishwa ili niweze kuvifuata.
  Asante kwa kazi njema Mungu akubariki na akupiganie katika kazi hii ngumu unayoifanya.

  Like

 2. Nakusalimu katika jina Yesu.
  Mimi niko Kigoma Tanzania nitapataje kitabu kiitwacho MATUMIZI YA DAMU YA YESU KRISTO?Na ni bei gani?
  Nimatumaini yangu nitafanikiwa.
  Mungu akubariki
  Eford Kitwe

  Like

 3. Namshukuru Mungu kwa kazi nzuri anayoifanya na wewe. Hakika amedhamiria kufanya yaliyo mengi nawe. Kubali kwenda katika neneo lake analo kuambia. Nimefurahishwa sana na picha ya vita vya kiroho, hiyo picha niliiona mwezi huu mwanzoni, lakini zilikuwa ni flying jets. nami nilikuwa katika jet ya upande w kulia tukiilinda ya kati isishambuliwe.
  Mungu akubariki na akutie mafuta mapya uzidi kuenenda katika njia yake ukitenda yaliyo yake.

  Like

 4. Bwana Yesu asifiwe kaka sanga na dada flora,

  Nilikuwa naulizia kuhusu hivyo vitabu kwa hapa dar es salaam ,vinapatikana wapi?na ni kiasi cha pesa ningependa kusoma vitabu vyako vina nibariki sana…yani Mungu aendelee kuwatumia ili muwe watumishi wazuri kila wakati Amen!

  tafadhari nahitaji kujua

  Like

  • Tunashukuru kwa maombi yako dada Grace, kwa hapa Dar vitabu vinapatikana kwa wauzaji wa kujitegemea pale ubungo na pia kanisa la EAGT Sinza kwenye duka la nje la vitabu, waweza nitumia namba yako ya simu kupitia 0755816800 then nitakutumia namba za wauzaji wa vitabu hao.
   Bwana akubariki.

   Like

 5. Mungu awa bariki sana, nauzika sana moyoni mwangu sababu nakuwa mbali sipati mafundisho yako, nilikuwa nabarikiwa sana ikiwezekana kuwa nanitumia na mimi mafundisho kwenye mtandandao. Mungu awa bariki mpaka mushangae. Amen.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s