Shuhuda

Wapendwa wasomaji wa blogu hii ninawasalimu katika jina la Yesu aliye hai. Nachukua fursa hii kumshukuru Mungu kwa neema kubwa aliyonijalia inayonifanikisha kuendelea kufanya kazi yake maadam ni mchana.

Zaidi namshukuru Mungu kwa ajili yenu maana naamini mnaniombea na kuombea huduma/blogu hii, pia kwa comment zenu na mawazo yenu ili kuzidi kuboresha kazi hii. Kimsingi bila ninyi wasomaji wa blogu kusingekuwa na maana ya kuandika tunayoyaandika.

Imefika wakati nimeona ni vema kuanzisha kurasa maalumu kwa ajili ya wale ambao wanataka kutoa shuhuda zao kwa sababu ya yale ambayo Mungu amewatendea kupita mafundisho na maombezi ambayo tunafanya katika blogu hii.

Nimeona baadhi ya watu wamefanya hivyo kwenye “kurasa/category” nyingine ndani ya blogu hii na wengine wao kunijulisha moja kwa moja wakimshukuru Mungu wao. Kwa hiyo nimeona vema kuanzisha kurasa maalumu kwa ajili ya shuhuda pekee.

Hivyo kama una ushuhuda wowote ambao Mungu amekufanyia kupitia maombezi au mafundisho tunayotoa kupitia blogu hii basi ninaomba andika ushuhuda wako huo kwenye eneo la “comments hapo chini” ili na wasomaji wengine waweze kuusoma wamtukuze na kumshukuru Mungu pamoja nawe.

Kitu cha muhimu kumbuka shuhuda zinajenga, zinatia moyo na kuimarisha wengine wanaosikia au kusoma. Hivyo nakusihi usiache kushuhudia endapo kuna jambo lolote ambalo Bwana Mungu amekutendea kupitia huduma hii.

Mungu wangu akubariki.

“Glory to Jesus the redeemer who lives”.

Advertisements

71 comments

 1. Haleluya!ndg Mungu awabariki sana kwa blog hii ninabarikiwa na huduma yenu. Kweli kwa njia hii panapo nguvu ya Mungu na upako wa pekee kwa blog hii watu kupona ni lazima ktk jina la Yesu.TUZIDI KUJITOA ZAIDI KAMA AGIZO LA BWANA LILIVYO ILI WATU WAFUNGULIWE 1YOH 3:16,wana wa Mungu tuzidi kumwomba, blog zake km hii aipe upako.

  Like

 2. Ndg,umenibariki sana kwani karibu masomo mengi uliyofundisha,
  Mungu amekuwa akinifundisha na nimekuwa nikiwamegea
  vijana ambao kwa kweli wako katika harakati za kutaka kuoa
  na kuolewa.Wengi wanafikiri kuoa na kuolewa tu LAKINI
  Wanasahau Nafasi ZAO NA WITO WAO waliopewa na Mungu,
  Na hili ni kosa kubwa sana maaana ukivurunda hapo
  utakiona cha moto mbele ya safari.

  Like

 3. Mimi ni mwinjilisti mnyarwanda na nimebalikiwa sana na mafundisho yenu. Kwa bahati nimeiona website yenu na ninataka tuwe na ushirikiano
  ili niwe mwanafunzi wenu katika neno la Mungu. Uso wenu unajaa upako wa Mungu na ninawatakia kuendelea na upako huo ili mpate kuponya mioyo iliyopotea.

  wako Seneza.

  Like

 4. Napenda kuwasalimu ninyi nyote kwa jina la Yesu, kaka Sanga nimesoma sana mafundisho yako yamenibadilisha mambo mengi. Naomba Mungu azidi kukutia nguvu ili uzidi kufundisha kondoo wa Bwana. Pia ningeitaji unitumie mistari ya kunifundisha kupitia e.mail yangu asante sana kaka sanga.

  Like

 5. Mungu ni Mwenye Upendo na Anaweza yote,amenisaidia mambo mengi sana hadi hapa nilipo,Nashukukru Mungu kwa majibu yake ya kunipatia kazi,Majibu yake ya kunisaidia kufaulu vema chuo,na mengine mengi sana.Ahsante yesu.

  Like

 6. Martha Shalua,
  namshukuru Mungu kwa matendo yake makuu alionitendea mimi mpaka leo ni mzima wa afya njema na leo 27/10/1985 natimiza miaka 26,najua si kwamba mimi nimemtendea mema Mungu kuliko wengeni la hasha ni neema tu “AHSANTE SANA YESU”

  (Nawatakia kazi njema Mungu awatangulie Shetani asije akawa vuruga maana anatafuta sana walokole kuliko watu wengine. Tuzidi kuombeana kufike safari yetu salama.

  Like

 7. Bwana Sanga, sina la kusema lakini Mungu akubariki kwa wito aliokuitia chni ya jua. Namuomba Roho Mtakatifu aliye mwalimu mkuu azidi kukufundisha na kukufunulia SIRI ZA UFLME WA MBINGUNI ambazo hakuna anayeweza kuzijua pasipo kujishusha chini ya Mkono(Roho) ili zipate kuwa wazi kwake.From Mtumishi wilfred w. Tarimo

  Like

 8. Kaka Sanga mimi ndo kwanza leo tarehe 11/1/2013 nimebahatika kuona hii blog yako naomba kuwa na wewe kwa ukaribu sana maana kuna vitu vinanitatiza nahitaji kupata majibu yake kutoka kwa mtumishi wa Mungu mimi ni msichana nina umri wa miaka 28 na ni muda mrefu sana nimekuwa nikiomba Mungu anipe mume mwema lakin naona nimeshaanza kukata tamaa kiasi kwamba naanza kuwaza mambo tafauti na mpango wa Mungu nisaidie hapo nifanyeje?? By msomaji wako nisaidie pleaz!!

  Like

  • Uwe na amani Jane, Mungu wetu ni mwaminifu binafsi nina hakika kabisa kwamba Mungu alishakujibu, maana Mungu hawezi kunyamaza kwenye issue sensitive kama hii, ili hali anajua kunyamaza kwake kutakupoteza. Wasiliana nami kwa email hii paxifari@gmail.com. Weekend hii nami nitakuandikia mambo kadhaa ya kukusaidia, barikiwa.

   Like

 9. Barkiwa sana kaka kwa mafundisho yako. Mungu azd kukutumia zaid ktk huduma yako.izid kutenda kazi.mimi n kijana nna miaka 21 tangu nlipokuwa shule ya msing nlipenda kumtumikia Mungu na huduma yangu iilionekana kwa wazi. Namshukuru Mungu aliye nipa huduma ya ualimu na uinjiListi nk.sku moja nlipokuwa naomba Mungu alisema nami kuwa yanipasa watu wajue kweli kwa maana watu weng wanakosa kuijua kweli na ndio maana shetan anawanasa na kuwaangamiza ukiijua kwel huwa inaweka huru kama neno linavyo sema yohana 8:32. hosea 6:4a. Hivyo nahtaj maombi yako na ushauri zaid ktk huduma. ili itende kazi zaid ya hapo nna hamu watu waijue kwel ya Kristo ili wawe huru ktk vifungo vya shetani maana shetan amewafunga watu wasijue kweli ya Mungu ingawa wanajuhud ktk Mungu lakini s ktk maarifa.
  Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu baba yetu na kwa Bwana wetu yesu kristo.

  Like

  • Amen, ahsante sana Mtumishi Lusajo kwa kunitia moyo katika huduma hii na kuona kwamba unaweza kujifunza kitu cha kuendelea kukuimarisha katika huduma yako kupitia blog hii na kwangu pia. Naam kwa hakika aliyesema nawe ni Mungu kwa kuwa anataka watu wake waijue kweli, ni jukumu letu kuijua kweli vema na kuwafundisha wengine tokana na vile Mungu ametuita na kutufanya.

   Naam bado kuna kazi kubwa sana ya kufanya na ni lazima tufanye kazi kwa pamoja na kama viungo ili kuona mafanikio katika mwili wa Kristo. Kwa sababu hii tunahitaji kuombeana sana na kuendelea kuimarishana sisi kwa sisi. Mawasiliano yangu ni 0755816800 na email yangu ni paxifari@gmail.com naamini tutashirikiana vema kwa utukufu wa Mungu.

   Like

 10. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi wa Mungu, mimi nimeifahamu site juzi tu na nimebarikiwa sana sana na naamini nitazidi kujifunza mengi hapa ndani, MUNGU azidi kukufunulia mengi zaidi na zaidi

  Like

 11. Asante sana kwa masomo yako mtumishi wa Bwana mr Sanga.kuna somo lako nimesoma ndilo limenifanya nikuandike haya nikuombe ushauri, mimi nimeolewa na nina mtoto mmoja, wa miaka mitatu na miezi nane , nimeokoka nina hamu sana na shauku ya kutaka kuzidi sana kumjua Mungu zaidi na zaidi . lakini mume wangu hajampokea Bwana, nimekuwa nikiombea hili kwa muda mrefu, lakini hata hivyo bado ninaendelea kutamka kuwa mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana, tatizo linakuja pale ninapokuwa nimeweka nyimbo za kuhabudu, tunaabudu na mtoto , tunakuwa na wakakti mzuri sana, pindi tunapomaliza kuhabudu nikitoka kwenda kufanya kazi zingine baba yake naye anaweka miziki ya duniani wanaanza kuimba miziki , ktk hili unanishaurije? pia tatizo lingine limetokea pale mume wangu aliponiashauri kuwa sasa wewe unavyosoma biblia kila siku na kila wakati, kwa nini usipumzike kwa muda wa miezi mitatu alafu ukija kuisoma utapata kitu kipya?ktk hili unanishaurije ? kwa habari ya kuimba miziki ya duniani na mtoto sijasema neno lolote. lakini kwa habari ya kuniambia nipumzike kusoma neno la Mungu, nilimwambia kuwa hilo haliwezekani maana kusoma kwangu neno ndiko kuishi kwangu,nilimwambia kuwa nikiacha kusoma neno hata kwa muda wa siku moja maisha yangu yatakuwa hayana maana yoyote , maana nitakuwa mtu wa tofauti sana, kwa kuwa amani , furaha, upendo , ulinzi na kila kitu ninakipata kupitia neno la Mungu ninalosoma , neno ndilo kiongozi cha maisha yangu, na linanifundisha jinsi ya kuishi kwa kufuata Mungu analosema kupitia neno lake. Hakusema neno lolote wala hajawahi kunishauri tena ktk hili. hanikatazi kusoma neno na matokeo yanaonekana , maana Mungu ametuvusha milima na mabonde mengi sana , sasa unasemaje mtumishi wa Mungu ktk hili? je majibu niliyompa kwa habari ya kupumzika kusoma neno la Mungu yanafaa? , na kwa habari ya mtoto na miziki ya duniani nifanyeje ktk hili pasipo kumukwaza mwenzangu? Asante.

  Like

  • Hello Mama K, Mungu akubariki sana kwa kuwa mama/mke mwenye kujua nafasi yake kwa Mungu wako na familia yako pia. Pole kwa changamoto, maana inapotokea kwenye ndoa, mmoja kaokoka na mwingine bado linakuwa jaribu kubwa sana hasa kwa yule aliyeokoka. Glory to God kwamba mumeo hakuzuii kusoma neno, na huo ndio ushindi na mafanikio yako na nyumba yako. Ukikosea ukazembea na kuacha kusoma neno ujue taratibu utakuwa unampa Ibilisi nafasi ya kuharibu ‘future’ yenu zaidi. Kuhusu suala la ‘Muziki’, jambo la msingi ni wewe kukazana kumfundisha mwanao juu ya kipi ni sahihi kufuata, kipi ni safi na kipi sio safi maana Mtume Paulo anasema ‘vitu vyote ni halali lakini si vyote vifaavyo na vijengavyo. Naam msisitize apende zaidi kusikiliza nyimbo zenye kumsifu/kumletea Mungu utukufu na si hizo za kidunia na katika hili tumia hekima pia kumfundisha maana ukisema nyimbo anazosikiliza baba yako ni za kishetani na mtoto akalifikisha hivyo, litaleta shida zaidi. Naam usiache kuendelea kuomba BWANA atamfungua mumeo na kukushindia kwenye hilo pia, nasi tutaendelea kuomba kwa ajili yako. Pili kwa habari ya majibu uliyoyatoa juu ya kusoma Biblia, ni sahihi kabisa na uwe na amani. Ila labda pia uwe makini na muda unaotumia kusoma Biblia na pia kazi nyingine za kijamii/kifamilia hapo kwako. Isije kuwa sehemu kubwa ya muda unaokuwa na mumeo unatumia kusoma Biblia kiasi kwamba mambo mengine hayaendi vizuri. Kama wewe ni mama wa nyumbani, tumia muda wa mumeo kuwa kazini kusoma Neno, kama wote mnafanya kazi basi hakikisha mambo yote ambayo unatakiwa kuandaa kwa ajili ya mumeo yanakaa sawa, ndipo uanze kusoma neno, ili asije akaona kuokoka kunamfanya mtu akose kuwajibika katika mambo ya msingi ya kifamilia.

   Like

   • Asante sana mtumishi wa Mungu, imeandikwa mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru, Yohana 8:32. Asante kwa kunifahamisha kweli, maana sasa nimekuwa huru kabisa, na asante sana kwa ushauri ulionipa kuhusu mtoto na jinsi ya kumfundisha, namshukru sana Mungu kwa kuendelea kunipigania, na hata kabla sijampa majibu niliyompa mume wangu kuhusu alivyonishauri kupumzika kusoma neno kwa miezi mitatu, Roho Mtakatifu alinipa neno la matendo 5:29, kuwa imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu, hii haimaanishi kuwa simtii mume wangu ninamtii sana sana, imeandikwa wake tuwatii waume zetu, hii ninaifuata sana, na kila wakati ninamuomba Mungu anitie nguvu ktk hili,lakini anaponipa ushauri nje ya neno la Mungu inabidi nisimame na analosema Mungu, maana na mume wangu ni binadamu kama mimi, ndiyo sababu nilimwambia ninampenda sana lakini kwa kuacha kusoma neno siwezi, pia namshukru sana Mungu maana ninaona anavyotembea wazi ktk hili kwa kuwa mume wangu hanikatazi kusoma neno, nikishamaliza kumuudumia na kufanya yanayopasa niitendendee familia yangu kama na wewe ulivyosema, yeye anaenda kuangalia luninga na mimi ninaenda kusoma neno, pia nilishafanya utaratibu nikitoka kazini simu ya mkononi huwa ninaiacha kabisa kwenye gari maana ninataka niwe na muda wa kuudumia familia yangu kuwa karibu na mume wangu na mtoto, hawa ni muhimu sana sana ktk maisha yangu,pia uongozi huu nilipewa na Roh mtakatifu . kwa hili sina tatizo kabisa maana ingekuwa tatizo angenizuia kabisa kusoma neno, sifa na utukufu ni kwa Bwana atupaye kushinda siku zote ktk Kristo Yesu Bwana wetu 1 wakolintho 15:57.

    Lakini pia kukitokea tatizo kama anaumwa au ana tatizo lingine ananishirikisha mimi na kuniambia niombe , ninamshukru sana Mungu ktk hili pia kuona kuwa hata kama aamini lakini anajua imani niliyo nayo kwa Mungu wangu. Pia kuna kipindi alikuwa akitoka kazini anakuja nyumbani akiwa na uzuni, akawa hana amani na furaha, nilipokuwa ninamuuliza alisema boss wake alikuwa katiri na kila kitu alichokuwa akifanya, boss wake alikuwa anaona hakifahi, niliingia ktk maombi, nikaomba toba kwanza, halafu, nikamwambia Mungu kuwa mume wangu na mimi ni mwili mmoja, anaporudi nyumbani bila furaha na mimi ninakosa furaha, kilio chake ni kilio changu, na maumivu yake ni yangu, nilimwambia Mungu kuwa baba naomba unihurumie mimi, kama mume wangu ndiye mwenye tatizo moyo wa mume wangu uurekebishe akatii analoambiwa na boss wake, hili waelewane, na kama tatizo linatokana na yule boss Mungu baba ktk jina la Yesu moyo wa boss uko mikononi mwako, naomba uugeuze akawe mwema kwa mume wangu. Nilisimama ktk mithali 21:1. nikasema haja zetu umesema na zijulikane na wewe, nami ninaleta haja hii kwako nasimama ktk wafilipi 4:4-7. sitajisumbua na neno hili maana umesema tusijisumbue kwa neno lolote, bali ktk kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushuru. nikaanza kumshukru kuwa ametenda na amani itapatikana na furaha iliyopotea itarejea kwa mume wangu.
    Ilikuwa katikati ya mwezi wa kumi nilipoomba maombi haya, ilipofika mwezi kwa 11 mwanzoni mume wangu alirudi nyumbani kwa furaha na tabasamu . nikamuuliza vipi mbona leo una furaha sana ? akasema Boss wangu ametangaza leo kuwa mwezi huu ndiyo wa mwisho yeye kufanya kazi pale , anasitaafu mwisho wa mwezi huu. Haleluya, sifa kwa Bwana. Mungu alijibu na amekuwa akinijibu ktk mengi. Baada ya muda alikuja boss mwingine ambaye walielewana sana sana na mume wangu.Kwa manyoya yake anatufunika , chini ya mbawa zake tunapata kimbilio , uhaminifu wake ni ngao na kigao. Zaburi 91:4. Atukuzwe yeye atuchukuliaye mzigo siku kwa siku, Zaburi 68:19-20.Asante tena mtumishi wa Bwana.

    Like

   • Hongera sana Mama K,kwa ushindi mkuu katika familia yako, nisamehe nimeona ni vema ushuhuda huu nikauweka hewani ili kila mtu pia aweze kuusoma kwa kuwa ni wa kujenga sana na hauna madhara kwa familia yako pia ukiwa hewani. BWANA Mungu aendelee kuipigania familia yako na kuiponya.

    Like

 12. Asante sana mtumishi wa Bwana, ushuuda mwingine ni kwamba mimi nimezaliwa katika familia ya watu ambao duniani wanaitwa masikini, nimesoma hadi kidato cha nne tu, nyumbani tulikuwa tukishindia miwa au mapapai ya kuchemusha tulipokuwa wadogo , tulienda kanisani tulisoma neno na kuomba hasubui na kabla ya kula chakula cha jioni, wazazi wangu walijishughulisha sana na mambo ya Mungu lakini nilikuwa nikishangaa kila tulipokuwa tunatoka kanisani tulikuwa tukienda kwa jirani kuomba mchicha, wakati mwingine tulikuwa tunalala njaa , wakakti ninasoma nilikuwa nikisimamishwa masomo kila wakati sababu sikuwa na school fees, nikawa nashindwa kuelewa ni Mungu wa namna gani ambaye alikuwa hatupatii mahitaji ya kila siku?, kuna kipindi nilipokuwa kidato cha pili mama alininunulia nguo ya ndani ( chupi) nilikuwa nikiivaa hasubui jioni ninaifua hili niivae tena kesho yake, lakini baada ya miaka miwili lasitic ilichoka sana ikalegea , hiyo ilinipelekea nianze kufunga chupi na kamba, basi tulikuwa tukipiga mguu pande mguu sawa shuleni nilikuwa nikiofia pengine kamba itakatika na nguo ile ingedondoka, na ingekuwa aibu, lakini sikupata aibu aikudondoka, . baadae nilimaliza kidato cha nne niliondoka kijijini kwetu nikaenda jijini Dar , nikafanya kazi kwa wazungu , kazi za ndani, nilienda nchi mbalimbali nikisafiri nao kama nchi tano za ulimwengu lakini mambo bado hayakuwa mazuri,nilipokuwa ninarudi tena Tanzania nilikuwa nikirudi mikono mitupu bila hata kitambaa cha kupangusa jasho la Dar, baadae alikuja rafiki yangu akaniambia kuwa wewe ulivyo na bahati hivi unatembezwa nchini mbalimbali ,laiti ungemjua Mungu ingekuwa mali kweli, umeenda nchi nyingi pasipo kumjua Mungu je ungemjua Mungu si angekutendea makuu ya ajabu zaidi? kwa kweli sikutaka kusikia kabisa habari za kuokoka maana kutokana na tulivyokuwa tunaomba kila siku nyumbani lakini maisha yalikuwa machungu na magumu , sikutaka kusikia habari za kuokoka nilimpa sababu na akaniambia kuwa kule ninakotaka uende wanakufundisha neno, unaamua kulitendea kazi, au kuliacha na lile neno unalohamini ndilo linakuletea mabadiriko ktk maisha yako , neno la Mungu lina nguvu, nilikuwa nikimuheshimu nikamwambia twende, tukaenda muhubiri alihubiri kutoka Mathayo 28;18, Yesu akaja kwao akasema nao , nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani, akahubiri kweli, lile neno kuwa Yesu ana mamlaka juu yangu lilinipa nguvu kweli, nikajua kabisa kuwa umasikini, magonjwa, mikosi, na mateso hayana mamlaka juu yangu nikaokoka nikanunua bible maana sikuwa nayo, nikaanza kusoma neno na kulitamka kama lilivyoandikwa na kulihamini na kuliingiza ktk matendo, baadae maboss wangu walirudi kwao UK lakini wakaniacha kwa mtu mwingine ambaye ni Mwingereza lakini ameoa Mmarekani (mke wake) , nikafanya kazi huku nikiwa nimejipanga ktk neno , tukasafiri kwenda Swizerland likizo, na kwa mara ya kwanza nililipwa overnight, na nilinunuliwa vitu vya kurudi navyo Tanzania kama zawadi, baadae tukaenda tena South Africa, baade Canada na kila tulikoenda walikuwa wananilipa vizuri sana walisema eti wananilipa zaidi sababu ninafanya kazi nje ya mazingira yangu, Niliendelea kumtukuza Mungu, nikaendelea kumutafuta maana nilishaamini maneno ya rafiki yangu aliyenipeleka niokoke kwamba ningemjua Mungu angenitendea makuu, Baadae boss aliniambia niende driving school, akalipia kila kitu na hii kwangu ilikuwa big deal maana nyumbani kwetu hatukuwa na mkokoteni. ninakumbuka kipindi nilipokuwa ninauza nyanya kijijini nilikuwa ninabeba ndoo mbili kichwani ninatembea tangu saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tano asubuhi ninafika sokoni, kichwa kimeishawaka moto kwa ndani, acha Mungu aitwe Mungu tu, mkuu wa mashauri muweza wa mambo yote. nilimaliza masomo ya udreva mwaka 2003 mwezi wa kumi, mwezi wa kumi na mbili boss wangu akaniambia kuwa walikuwa wanakuja USA moja kwa moja akaniambia walitaka wanilete nikae nao miezi mitatu na baadae nirudi tena Tanzania, nilikuja USA lakini Mungu wa nguvu anayeliangalia neno lake akalitimiza sawa na Yeremia 1;12, nilimwambia Mungu shauri la mimi kurudi Tanzania halitasimama wala halitakuwa ktk jina la Yesu, Isaya 7:7, nilisema kwa jina la Yesu sitarudi Tanzania bila mume nitakuwa ninarudi Tanzania kutembea na kurudi tena USA. baada ya miezi mitatu boss akaniambia alitaka kuongezea VISA, alilipa pesa kwa wakili akaongezea muda, baada ya muda alilipia tena muda ukaongezewa, Haleluya, ni mda hule ambao nilikutana na ambaye ni mume wangu kwa sasa, yeye ni mzaliwa wa hapa, kwa hiyo tulikutana hapa tukapendana , tukafunga ndoa , tukaenda Tanzania akalipa mahali, kwa sasa nina green card ya mika 10 Haleluya , ninaenda nyumbani ninatembea na kurudi tena hapa USA Kweli Mungu alinipa haja ya moyo wangu. kwa sasa sijui hata idadi ya nguo za ndani nilizonazo maana ni nyingi, silali njaa wala sili mapapai ya kuchemsha, na kwetu hawatalala njaa daima, pia Mungu maenivua gunia akanivika furaha, maana baada ya kubeba nyanya ndoo mbili kichwani tangu saa kumi na mbili hadi saa tano asubuhi leo hii Mungu amenibariki kwa usafiri wangu , Bwana Yesu asifiwe, na mimi naweza kuwakumbuka walio kijijini wanaosomesha watoto kwa shida nikawabariki watoto wao wakasoma pasipo kusimamishwa masomo kama ilivyokuwa ikitokea kwangu, japo siyo wote lakini Mungu amekuwa akinikumbusha sana alikonitoa na niliyopitia na mimi kwa kukumbushwa hilo inanisaidia kusaidia wengine hili watoto wao wasipitie nilikopitia mimi, hata kama siyo wote lakini wale anaowaleta Mungu ndani yangu anawasaidia kupitia mimi, maana mimi pasipo yeye siwezi kufanya neno lolote,Yohana 15:5. Ninapomutazama mume wangu na mtoto na kila nilichonacho namushukru sana Mungu maana mkono wake ndiyo uliotenda haya yote. sawa na Isaya 62:2. Hata ninapoandika haya ndani ninashindwa jinsi ya kuelezea vizuri ukuu wa Mungu, ni baada ya kusimama ktk neno nimeweza kuona utukufu na wokovu wa Bwana , maana kumbe tulikuwa tunasoma neno kwetu bila kuliamini na kuliingiza ktk matendo, badala ya kuangalia neno la Mungu lilichokuwa linatuambia tulikuwa tunaangalia mazingira yalivyokuwa yanatuambia, baada ya kuweka imani yetu ktk nguvu za Mungu tulikuwa tukiweka imani yetu ktk dunia na kujitaabisha kujaribu kufanya mambo yatokee kwa nguvu zetu, Hila leo hakika nimejua kuwa neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi bali kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu za Mungu. 1 wakolintho 1:18. Nimemuona na ninaendelea kumuona kupitia neno lake, Halihanguki neno la Mungu wala halishindwi. Nimeandika ushuuda huu kutokana na ulivyoniandikia kutokana na ushuuda wa kwanza, nimeona niseme mengine ambayo Mungu amenitendea. na watu wajue kuwa swala siyo uko wapi au wewe ni nini , swala ni neno la Mungu liko wapi na wewe unapojijua kuwa ni nani ndani ya Yesu Kristo. neno neno neno la Mungu limebeba majibu yote. 1 Wakolintho 4:13. Lakini kwa kuwa tuna roho ileile ya imani, kama ilivyoandikwa , nalihamini na kwa sababu hiyo nalinena , sisi nasi twaamini , na kwa sababu hiyo twanena. Nani mama K nina amini neno la Mungu, pia ninahamini kuwa haya yote Mungu ndiye amenitendea na kwa sababu hiyo ninanena. Mzidi kubarikiwa wateule wa Bwana. Mama. K.

  Like

  • Haleluya, hakika utukufu apewe Mungu mama K, huu ni ushuhuda mzuri sana na wenye kujenga sana sana, naam hakikisha unadumu katika imani na kumrudishia Mungu utukufu kwa kila atendalo kwako na jamaa yako kwa ujumla wake. Ahsante kwa kutenga muda wako na kuandika ushuhuda mrefu namna hii, naamini utawasaidia na kuwajenga watu wengine. Mungu akubariki.

   Like

  • hakika nami nimejifunza kitu kupitia ushuhuda huu,Mungu anisaidie hasira ya kiMungu niliyoipata kupitia ushuhuda huu iendelee kulipuka ndani ya moyo wangu ili niweze kutimiliza kile ninachokitamani ktk umama wangu

   Like

 13. Asante sana mtumishi wa Mungu Patrick kwa kazi unayofanya ya kumtumikia Mungu na pia nashukru sana kwa muda wako unaotumia kusoma shuuda zetu maana nyingine zinakuwa ndefu lakini unavyojibu inaonyesha unavyosoma zote. Mungu azidi kukutia nguvu mtumishi kwa kazi yake unayoifanya. hakika unajua unalolifanya ktk utumishi uliyoitiwa .Mama K.

  Like

 14. Jina la Bwana libarikiwe. Nimebarikiwa sana na ushuhuda wa Mama k hakika unajenga kiroho na kiimani pia .Mungu akubariki wewe Mtumishi wa Mungu usikate tamaa endelea kumtumikia Mungu.

  Like

 15. Jina la Bwana libarikiwe. Nimebarikiwa sana na ushuhuda wa Mama k hakika unajenga kiroho na kimwili pia .Mungu akubariki.
  Mtumishi wa Mungu usikate tamaa endelea kumtumikia Mungu.Na mungu ataendelea kutenda miujiza.Amina

  Like

 16. BWANA YESU ASIFIWE, NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KWA YOTE ALIYOWEZA KUNIFANYIA MWAKA JANA NA MWAKA HUU 2014,TAREHE 23 JANUARY NILITUMA MAOMBO KUWASHIRIKISHA KATIKA KUMWOMBEA BINTI YANGU VERONICA ANAFANYA INTERVIEW.WAPENDWA MUNGU NI WAAJABU HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU AMEPATA NAFASI HIYO ILIKUWA MOJA,NA KULIKUWA NA USHINDANI MKUBWA WENYE KUJAA (MEMO) ZA KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI LAKINI SISI TULIKUWA NA MEMO KUBWA AMBAYO ILIFUNIKA VI MEMO VYOTE AMBAYE NI BWANA YESU.NAPENDA KUWATIA MOYO WAPENDWA WANGU MUNGU ANAJIBU MAOMBI KWA WALE WANAOMTAFUTA NA KUMWOMBA KWA IMANI.TUZIDI KUOMBA NA KUMTEGEMEA MUNGU.

  Like

 17. nimebarikiwa xana na maxomo ya vijana kwan yamebadilisha xana uelewa na mtazamo wangu kwa kiwango kikubwa kwa habar ya uchumba MUNGU awabariki sana

  Like

 18. amina Mungu wa mbinguni azidi kuwatia nguvu nabarikiwa sana nionapo kuwa watu wanashuhudia matendo makuu ya Mungu kama mama k Mungu aendelee kukutia nguvu

  Like

 19. Amen jina la Bwana libarikiwe leo ni mara ya kwanza kuingiakwenye Blog hii lakini nimejifunza mengi kupitia shuhuda mbalimbali .Jina la Bwana lihimidiwe

  Like

   • BWANA Yesu asifiwe wateule, Ombi langu ni tuzidi kuombea Uchaguzi mkuu wa Raisi wa Tanzania na viongozi wengine .uchaguzi utakaofanyika mwaka huu , Binafsi ninaomba kupitia neno la Kutoka 18:21. .Mungu atuinulie watu walio na uwezo , wenye kumcha Mungu,watu wa kweli wenye kuchukia mapato ya udhalimu . Unaweza pia kutafuta neno lingine la kusimamia kadri utakavyoongozwa na Roho Mtakatifu ndiye msaidizi wetu, mwalimu wetu na kiongozi wetu , pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya neno lolote . Mungu awabariki . Mama K

    Like

   • Naam hakika tunahitaji kuendelea kuomba sana juu ya jambo hili wala tusinyamaze kama waombaji/walinzi, barikiwa mama kwa kutukumbusha.

    Like

   • Shalom wateule , Napenda kumshukru sana Mungu kwa kujibu maombi tuliyoomba , kwamba atupatie Viongozi wakweli, wenye uwezo, wenye ofu ya Mungu na wasiopenda mapato ya udharimu , Kutoka 18:21.Narudi mbele zenu kwa sifa na utukufu na shukrani kwa Mungu wetu , kwa kujibu maombi yetu . Ninamuona Rais Pombe John Magufuli ktk andiko hilo la Kutoka 18:21. Utukufu na sifa kwa BWANA , kufunga na kuomba kwetu hakukuwa bure . Sifa kwa Yesu .

    Like

 20. Ndugu wapendwa Bwana Yesu asifiwe sana, namshukuru huyu Yesu ambaye ameniokoa na kuniweka huru, mbali na vifungo vya shetani. wakristo wezangu ambao mmetakaswa kwa damu ya thamani ya YESU, niwatie moyo kuwa Yesu anawapenda sana, upendo wake kwetu ni wa ajabu mno na anapenda siku moja tuishi naye pamoja mbinguni. Mungu amenionyesha mambo mengi yajayo yanayohusu ufalme wake wa mbinguni, lakini napenda nieleze matukio makubwa ambayo Mungu kanionyesha kwenye ndoto na ni vyema na ww ukafahamu kwa kuwa tupo safari moja ya kwenda kwetu mbinguni.Tukio la kwanza ambalo Mungu kanionyesha, ulikuwa usiku mmoja nilipokuwa nimeamka kuomba, nilimuomba Mungu kwa habari ya maono hasa ya mbingu, wakati nilikuwa natumia maandiko ya (YEREMIA 33:3 na YOEL 2:28). nilipomaliza maombi hayo, nilipoingia kulala namshukuru Mungu alijibu maombi yangu, Nilijikuta nipo sehemu moja nzuri sana. Gafla nikiwa sehemu ile ndipo mtu akatokea mahali pale na akaniambia nifuate ,ndipo mawazo yakanijia hapo ndipo mbinguni, wakati tunatembe

  Like

 21. Amina sana mtumishi,BWANA awe nawe pia mm jna langu naitwa ANDREW LEONARD nami nina ushuhuda juu ya habari za YESU lakini sifahamu huwa wanaandikeje kwenye sim hvyo naomba msaada wako, Amina

  Like

 22. MTUMISHI WA MUNGU SANGA NAKUOMBA SANA UNIOMBEE ILI MWAKA 2017 NIMTUMIKIE MUNGU BABA KWA NGUVU ZANGU ZOTE NA KWA AKILI ZANGU ZOTE NA KWA MALI ZANGU NAJUA BILA MUNGU SIWEZI NAHITAJI MSAADA WA MUNGU SANA PIA NAOMBA MUNGU ANIWEZESHE KURUDIA HUDUMA YANGU YA KWAYA NA HUDUMA ZANGU ZOTE ALIZOIBA ADUI ZIRUDI ZOTE NA VITU VYOTE ADUI AVYOIBA VIRUDI VYOTE KWA UWEZA WA MUNGU AMEN

  Like

 23. Mimi napenda kumshukuru Mungu kwa yale aliyonitea, nikipindi cha mwezi wa saba ndipo nilipobariki ndoa yangu, zikiwa zimebaki kama siku tatu hivi nikaota ndoto kwamba kuna mtu anataka kunichoma kisu wakati nahangaika nae nikawa nakemea mara nikashtuka, wakati nashtuka na mwenza wangu nae akawa ameshtuka anakaniambia vipi nikawa nimemsimulia akaniambia hata mi wakati nashtuka kuna kitu kimenichoma hapa kwenye kalio, basi baada ya kuniambia hivyo tukawa tumeomba mara chumba kizima kikajawa na nguvu ya Mungu kuanzia saa 10 mpaka saa mbili asubuhi kila mmoja kazama kwenye maombi, baadaye tukaendelea na maandalizi kama kawaida lakini kitu cha ajabu wakati tumetoka kanisani tupo ukumbini mara mwenzangu akashindwa kukaa akidai kalio linauma sana, basi tukawa tumetoka ukumbini tukaludi hoteli, mme wangu akiwa na khali mbaya sana ikabidi tuamkie hospitali. kucheki wakakuta ni jipu kubwa sana basi nikawa nimeuguza mpaka akawa amepona, nikamshukuru Mungu kwa hilo.
  LAKINI shetani hachoki bado ni mwezi huu mwanzon tukawa na maombi ya siku tatu kavu tena lile jipu likawa limerudi mahala pale pale nikasema Mungu ndo ananijaribu nini nikaingia kwenye maombi nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaa asubuhi nikawa nimepasua lile jipu halafu jioni yake akaja kwenye mkesha juma mosi asubuhi naenda kusafisha kidonda nikakuta kidonda hakipo yaani kimepona kabisa limebaki kovu tu. kwakweli namshuku Mungu kwa muujiza wake huo. mtanisamehe kwa maadishi mengi ila nataka tu kukujenga kuwa Mungu wetu ni mwaminifu na anajibu tukimuomba. MUNGU AWABARIKI.

  Like

 24. BWANA YESU Asifiwe
  namshukuru BWANA kwa matendo yake makuu na ya ajabu aliyonitendea maishani mwangu.
  Nakumbuka ilikuwa tarehe 14.8.2014 nilipoanza kuugua ugonjwa wa kujihisi kuchanganyikiwa na kupoteza kumbukumbu hali hii ilikuwa mbaya sana kwangu kwani ilikuwa inanfanya nijihisi kuwa niko kuzimu kabisa lakini ilitokea siku moja nilikuwa nimelala nikasikia kama vile sauti inaniita nikatazama nikaona kama uweza na nguvu za MUNGU zikishuka pale kitandani kwangu na ile sauti ikaniambia inakupasa kuchagua njia iliyo sahihi ya kumuabudu MUNGU peke yake la sivyo nitachukuliwa kuzimu kabisa lakini Mimi nilianza kulia hapo hapo hatimaye ule uwepo wa MUNGU ukatoweka pale kitandani kwangu lakini kila nikitaka kuchukua uamuzi wa kwenda kuombewa najihisi kama vile nimepona,
  Ilipofika tarehe 10.1.2015 hali ikawa mbaya sana kwani kwa wakati huo nilikuwa sitamani chochote katika hii dunia lakini nikalikumbuka neno la BWANA aliloniambia pale kitandani na pia nikakumbuka neno katika (Mathayo 11:28) ndipo nilipoamua siku hiyo ya jumamosi kwenda kanisani kuombewa, nilipoonana na Mchungaji nikamweleza shida zangu ndipo aliponipeleka madhabahuni .alipotaja tu jina la YESU mapepo hapo hapo yakalipuka nikapoteza fahamu nikawa kama mfu ila baadae BWANA akanifungua tangu hapo nikawa mzima hadi leo. Sifa, utukufu na heshima namrudishia BWANA
  AMINA..

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s