NAMNA YA KUONGEZA IMANI UNAPOKUWA KWENYE JARIBU

Na: Patrick Sanga

1

 

Mpenzi msomaji Shalom,

Naomba sana radhi kwa Mungu na kwako pia kwa kuchelewa kuweka masomo tangu mwaka huu uanze. Kuna baadhi ya majukumu yalinibana sana, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuyamaliza vema na sasa nitaendelea kuweka masomo kama kawaida. Katika mwezi huu wa Januari nimeona ni vema tuanze na ujumbe huu wa imani ambao naamini utafanyika msaada kwenye maisha yako.

Biblia katika kitabu cha Mathayo 17:18 inasema‘..Ni kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana amini nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Hii ni habari ya yule kijana aliyekuwa na pepo bubu na kiziwi, mzazi wake akamleta kwa wanafunzi wa Yesu wamwombee. Biblia inatueleza kwamba wanafunzi walijaribu kumtoa yule pepo wasiweze, wakati huo Yesu alikuwa amepanda Mlimani kwenda kuomba.

Yesu aliporudi alielezwa kilichotokea, akawakemea wanafunzi wake na kisha akamuombea yule kijana akapona. Baadaye wanafunzi wa Yesu wakamuuliza, kwa nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo. Ndipo Yesu akawajibu akasema ‘Ni kwa sababu ya upungufu wa imani yenu… Neno upungufu lina ya isiyo – tosheleza, yaani imani yao ilikuwa ina upungufu na kwa hiyo wasingeweza kumtoa yule pepo. Jambo ninalotaka tuliangalie ni kwamba kwa kuwa tatizo lilikuwa ni upungufu wa imani yao, ina maana walitakiwa kuongeza imani yao wakati wanaendelea kukemea. Sasa swali muhimu ni je wangeongezaje imani yao wakati wako kwenye jaribu/vitani?.

Naam licha ya swali hili kuna maswali mengine ambayo ni muhimu kuyatafakari ili tuweze kuwa na ufahamu mzuri wa imani. Je upungufu huu wa imani kwa wanafunzi walikuwa nao kabla hawajaanza kukemea yule pepo au ulikuja wakati wanaendelea kuomba. Naam Yesu anatuonyesha kwamba kosa la hawa wandugu wenzetu lilikuwa upungufu wa imani yao?

2

 Ni kwa namna gani walikuwa na upungufu wa imani?

Biblia katika Waebrania 11:1 inaeleza kwamba ‘imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana’. Kwa hiyo endapo Yesu alisema ni kwa sababu ya upungufu wa imani yao ina maana ndani yao walipungukiwa uhakika wa kile walichokitarajia, ambacho ni kufunguliwa/kuponywa kwa kijana mwenye pepo. Naam upungufu wao wa imani ulitokana na  mashaka juu ya uhakika wa yule kijana kufunguliwa.

Nini kilipelekea wao kuingiza hofu/mashaka?

 • Kukosekana kwa dalili za kijana kufunguliwa – Ni imani yangu kwamba wanafunzi walipoanza kukemea walikuwa na uhakika kwamba Yule kijana atafunguliwa. Naam kadri walivyoendelea kuomba na kuona kwamba hakuna mabadiliko ya aina yoyote kwa mgonjwa yule ndipo hofu/mashaka yakawaingia mioyoni mwao.   
 • Maneno ya kusikia – Ikumbukwe kwamba chanzo cha imani yoyote ni kusikia (Warumi 10:17)?  Kumbuka wakati wanendelea kuomba kulikuwa kuna kundi kubwa la watu ambao walikuwa wanamsubiri Yesu pamoja nao. Hivyo huenda wakati wanafunzi wanaaendelea kuomba walisikia watu wakisema, wanafunzi wa Yohana wenyewe walishindwa kumuombea, wao wataweza, wamejaribu watumishi wa kila aina wameshindwa, huyu hawezekani anasubiri kifo, naam haya yote yakapunguza uhakika ndani yao kwamba kwa jina la Yesu yule kijana anaweza kupona.
 • Maneno yao wenyewe – Biblia haituelezi namna/approach waliyoitumia kuomba/kukemea. Huenda walianza kuomba mmoja mmoja/ au waliomba wachache na mwishowe ndipo wakaomba kama kundi. Kwenye kundi lolote kuna mengi, huenda walipokemea kwa muda kadhaa na bila kijana kuonyesha dalili za kupona baadhi ya wanafunzi wakaingiwa na hofu na wakawaambukiza na wengine na hivyo kushindwa kumtoa pepo. Hebu jaribu kufikiri mtu kama Yuda Iskariote alikuwa anafanya nini wakati wenzake wanakemea?

Nini cha kufanya?

Hofu/mashaka ni silaha kubwa sana ambayo Shetani huitumia kuwafanya watu washindwe kupata majibu ya maombi/miujiza yao kutoka kwa Mungu. Shetani anafahamu kwamba imeandikwa ‘Mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye akisstasita roho yangu haina furaha naye’ (Wabrania 10:38). Hivyo ili kuharibu/kuondoa imani ya mtu kwa Mungu, silaha anayotumia ni kuingiza mashaka moyoni mwake dhidi ya ahadi za Mungu/neno la Mungu kwenye maisha yake. Yesu aliwaambia hivi wanafunzi wake ‘… amini nawaambia yeyote atakayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake’ (Marko 11:22).  

Mpenzi msomaji kamwe usimruhusu Shetani kwa kutumia silaha hii ya mashaka azuie baraka zako na wale wanaokuhusu maishani mwako. Haijalishi jaribu limesimama mbele yako kwa kiwango gani usiondoe imani yako juu ya kile ambacho Yesu amekisema kwenye neno lake juu yako. Naam Mungu wetu si mtu hata aseme uongo, ahadi zake ni amina na kweli.   Naam katikati ya jaribu/changamoto wewe ongeza imani yako kwa kupambana na roho ya mashaka/hofu, naam tumia Biblia ili ikuongoze kukupa mistari ambayo itakuongezea uhakika wa kufanikiwa katika lile ulifanyalo.

Zaidi kuwa makini na maneno ya kusikia kwa habari ya imani yako. Wanafunzi wa Yesu walipaswa kutokujali maneno ya kusikia kutoka kwa watu, au kwa wenzao walioingia mashaka, naam walipswa kudumu kuamini kwamba kijana atapona naam ingekuwa hivyo. Je si unakumbuka habari za Petro alivyoambiwa na Yesu atembee juu ya maji. Awali alianza vema na akatembea hatua kadhaa juu ya maji.    Biblia inasema dhoruba ilipompiga akaona shaka na kuanza kuzama. Kwa nini alizama? si kwa sababu Yesu hakuwepo, bali ni kwa sababu aliona shaka.

3

Naam kitu kilichopungua kwenye imani ya wanafunzi, ni uhakika kwamba yule kijana atapona. Na kilichopelekea upungufu wao wa imani, si   kutokumwamini/kumjua Yesu, bali ni kuruhusu hofu ichukue nafasi ya imani/uhakika waliokuwa nao kwamba yule mgonjwa atapona. Naam kwa mara nyingine tena ‘usirihusu hofu iharibu muujiza/future yako’.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nawe daima.

Advertisements

104 Comments »

 1. 1
  nico lukoya Says:

  Somo hili la ”namna ya kuongeza imani unapokuwa kwenye jaribu” limenifungua sana, na nimebarikiwa sana. Ni ukweli usiopingika kuwa hofu ndio adui mkubwa wa mwanadamu. Kwa hofu tu, humfanya mtu akapooza, kuugua, n.k hivyo somo hili ni ufunguo kwa mwaka huu mpya wa 2013, Mungu akubariki sana.

 2. 6
  nico lukoya Says:

  Lakini ni ombi langu kuwa sehemu iliyobaki ungeweza kuimalizia mapema iwezekanavyo ili niwe na somo kamili.

  • 7
   sanga Says:

   Ahsante kwa ushauri, lakini sikuwa nimekusudia kuliendeleza somo hili kwa kuwa tayari nimeandika masomo kadhaa kwenye blog hii kuhusu imani, hata hivyo nitaendelea kuandika masomo mengi juu ya imani kwa kadri ninavyojifunza na kuletewa ndani yangu. Pia chini ya somo wewe msomaji una fursa ya kuandika au kuongeza kile ambacho unafikiri ni muhimu pia wasomaji wengine wakakijua kutokana na ujumbe husika nilioandika. Barikiwa sana.

 3. 8
  M.Noel Mselle junior Says:

  Asante sana mtumishi kwa neno hili la kuwajenga askari wa Kristo na wale wote wanaotegemea kupokea kutoka kwake. Maana mashaka, wasiwasi,na hofu vimekuwa vizingiti vikubwa sana katika utendaji wa imani yetu na ndiyo maana unamkuta mtu ana miaka kumi ndani ya wokovu lakini hana ujasiri wa kuitumia imani yake na hasa pale ambapo panakua na watazamaji pengine wasioamini kama sisi na wana mpango wa kuthibitisha imani ya mtu

  Ninaamini kama mwamini atajengeka kiimani na kukifahamu kile anachokifanya na kufahamu kwamba nyuma yake yuko Yesu aliyesema “kazi njema aliyoianzisha mioyoni mwetu ataimaliza” huduma yetu ndani ya Kristo ingekuwa haina mpinzani. Bwana abakie yeye peke yake kupokea utukufu.

  • 9
   sanga Says:

   Amen ndg. Mselle, Mungu akubariki sana kwa mchango na ufafanuzi mzuri ambao umeongeza juu ya suala zima za imani, hakika mara nyingi licha ya kuzikosa baraka zetu, lakini pia tumemwaibisha hata Mungu wetu kwa sababu ya upungufu wa imani au kuona mashaka juu ya ahadi za Mungu kwenye maisha yetu.

 4. 10
  Wilfred Tarimo Says:

  Mungu wangu Yesu akubariki mtumishi wa Mungu aliye hai. Yaani unanibariki sana kila ninapoingia kwenye blog hii. Nilikuwa kila wakati naingia kuangalia somo jipya uliloweka nakuta bado,ila nashukuru Mungu leo nimeingia na kukutana na kitu kipya. Mungu azidi kukuinua katika utumishi wako na kukufundisha zaidi yale ambayo ni muhimu kufahamika kwa sasa katika kanisa lake. Mtumishi hii kazi ni nzito sana hasa ya ufundishaji lakini kwa kuwa ni wito na karama tulizopewa na Mungu yatupasa kukubali kufanya katika Bwana tena kwa Uaminifu wote. Roho Mtakatifu yupo na ninaamini pasipo yeye hatuwezi Neno lolote. Nakutia Moyo songa mbele katika utumishi wako Bwana aliyokuitia. Mtumishi wilfred Tarimo

  • 11
   sanga Says:

   Amen ahsante sana Mtumishi wa Mungu Wilfred kwa maombi yako na kunitia moyo. Kwa hakika kazi hii si nyepesi, bali kwa msaada wa yeye aliyetuita katika kazi hii, tunayaweza mambo yote. Mungu akubarikie pia katika huduma yako, na tuzidi kuombeana sana.

 5. 12
  Wilfred Tarimo Says:

  Usihofu Mtumishi tupo pamoja katika Kuombeana tena sana. Kwa kuwa ninajua siri hii na ninapenda sana “huduma ya ualimu/ufundishaji” kwa kuwa naamini inahitajika sana kwa sasa katika Kanisa la leo, ili kuondoa kila aina ya Maarifa mabovu,ujinga na chuki miongoni mwa viungo vya kanisa la Tanzania na nje ili kuliponya kanisa na kuliinua. Nitasimama na wewe kukuombea Mungu anitie nguvu kwa hlo kwa kuwa kipo kitu cha tofauti kwako-kwa mwenye Macho ya rohoni amekwisha liona hilo-utukufu ni kwake Bwana. WAEFESO 4:1-16. Mungu akubariki pia.

  • 13
   sanga Says:

   Amen, amen, amen glory to Jesus.

  • 14
   says Dorice. Says:

   Bwana Yesu asifiwe sana. ni kweli kabsa mara nyingi watu wengi wameharibu miujiza yao kwa kutokuwa na imani, hii yote inatokwanna na hofu.kiu yangu tufike mahali ili tumwamini Mungu kwa klia jambo kwamba linawezekana sawa na neno laMungu linasema hakuna lisilowezekana kwa Mungu. tukiweza kutembea kwenye imani yakumwamini Mungu kwa jambo lolote pasipo mashaka na hofu tutafika mbali sna.

 6. 15
  venance Says:

  Nashukuru mtumishi kwa huduma yako, naomba nikuulize swali kuna mafungo yoyote ambayo mtu unaweza kutumia kuongeza imani?

  • 16
   sanga Says:

   Ahsante kwa kunitia moyo, kimsingi kwa mujibu wa Warumi 10:17 chanzo kikibwa cha imani ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo, hivyo namna kubwa ambayo mtu anaweza kutumia ili kuongeza imani ni kuongeza ufahamu wake juu ya neno la Mungu kila siku. Ukisoma Biblia utagundua hata wanafunzi wa Yesu waliomba wakasema BWANA tuongezee imani, katika kujibu swala lao aliwafundisha neno akijua kadri wanavyosikia ndivyo na imani yao itakavyoongezeka. Hivyo kufunga na kuomba ili kuongeza imani, ni namna moja wapo ya kuliweka neno kwenye matendo na uwe na uhakika katika kukujibu BWANA atakuongoza katika kulijua neno lake zaidi.

   • 17
    boaz bujuli Says:

    Mtumishi wa Mungu nimebarikiwa Sana baada ya kutembelea kurasa zako. Kazi ni nzuri Sana na inatujenga kiroho. Mungu akubariki sana

 7. 18
  kwizela Says:

  Asante kwa somo hili la kuongeza imani unapo kuwa ktk majaribu,kweli na mshukuru Mungu sana hata kuliona somo hili maana limekuja ktk mda muafaka Mungu akubariki sana tena sana,ninaa amini kwa kulitendea kazi litanitoa mahali nilipo.

 8. 20
  ANNA Says:

  ASANTE SANA MTUMISHI…MUNGU AZIDI KUKUBARIKI

 9. 22
  Flano Says:

  Haleluya Mtumishi wa Mungu, hongera kwa huduma nzuri ya ualimu wa neno la Mungu. Ni jana tu nilipata kuiona tovuti yako leo nimetembelea tena. Mungu akubariki kwa baraka zote na asante kwa somo la imani. ni kweli tuna shida sana na imani na namna ya utekelezaji wa neno yaani kusimamia neno hadi situation iwe wengi tumekuw wenye kufeli hapo, ila ahimidiwe Mungu alilyekupa kulifundisha neno lake leo na kuelezea namna ya kuisimamisha imani na kuikimbiza hofu

 10. 24
  basil Says:

  Its so nice living words that I receive, Lets God give you a lot of health so that we can still share sweetable words like these. Be blessed man of Living GOD.

 11. 26
  Lazaro Mollel Says:

  Ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu kwa somo hili la Imani

 12. 29

  Nimebarikiwa sana na somo la imani Mtumishi,Na nimekuwa mpya kabisa!Mungu aendelee kukupa Roho ya unyenyekevu ili uzidi kutumika zaid!Coz adui cko zote hutafuta pengo ili aweze kukuangusha.Na watumishi wengi wameanguka kwa kukosa unyenyekeve!Tena wengine wamelizoele neno na kuona as if ni wazoefu sana!GOD BLESS U BROTHER.

  • 30
   sanga Says:

   Ashukuriwe Mungu atendaye haya, na awezaye kugusa maisha ya watu kupitia masomo kwa namna hii, ahsante kwa maonyo muhimu, tuzidi kuombeana

 13. 31
  GEORGE S Says:

  nikwelikwamba upungufu wa imani unaweza kuzuia muujiza,lakini bado neema ya mungu inaweza kusimama badala ya imani

 14. 32
  GEORGE S Says:

  nimebarikiwa kaka Mungu akutie nguvu uendelee zaidi nazaidi

 15. 34
  ally yohana Says:

  Hakika imani yangu inazid kukua ninapo soma kweli ya MUNGU na inanipa uweza wa kutumia silaha za BWANA.

 16. 35
  jackson reuben Says:

  Hakika mm nimeona kuwa, jambo unalolitenda ni zuri sana hasa kwa sis vijana ambao tumeokoka. Ni kweli kabisa mambo ulioongea huwa yanatokea sana hata sisi tunapojaribu kumuombea mtu mwenye matatizo hayo lakini huwa tumekuwa tukikata tama mara nyingi kutokana na hofu, mashaka na wasiwasi juu ya yule tunae muombea, ila hakika leo nimepata ufumbuzi wa jambo hilo. Asante sana kaka Sanga. Jina la Bwana libarikiwe

 17. 37
  Simon Sanga Says:

  I appreciate your lessons, God bless you in advance.Be of great courage,keep it up, you benefit many.Thank you.

 18. 39
  FLORIAN NYONGOLE Says:

  NIMEPENDA HII, KUWA WALIKUWA NA UPUNGUFU WA UHAKIKA WA KIJANA HUYO KUFUNGULIWA NIMEIPENDA, UBARIKIWE

 19. 43

  Sifa kwa Mungu kwa kukufanya tawi lililounganizwa na mzabibu ambao ni kristo. Mungu akubariki ukazae matunda mema zaidi .

 20. 45
  Alen Anton Says:

  Ubarkiwe Sana,sana..iman Kwel Asa Ndiyo Slaha Asa Ya Kumshinda Shetan!mung Atusaidie!

 21. 46
  leonard maketa Says:

  mtumishi ubarikiwe sana

 22. 47
  benomkoma Says:

  Asante sana Mtumishi kwa Neno lenye kutuongeza Imani zetu Barikiwa sana ili uzidi kutufunza

 23. 49

  Ahsante kwa mafundisho. Lakini napenda kuwa na imani kubwa ju ya ahadi za mungu lakini mapito yamezidi yananifanya nisahau hata ahadi ya Mungu ju ya maisha ya mwanadamu.

  • 50
   sanga Says:

   Hupaswi kusahau ahadi za Mungu dadangu maana ahadi zake (neno lake) ndio ushindi wako, naam hakikisha unakuwa na nidhamu ya kuwa na muda wa kusoma na kutafakari neon la Mungu kila iitwapo leo.

 24. 51
  Meshack Kussaja Says:

  Ahsante sana mtumishi wa Mungu, somo lako kwa hakika limegeuza maisha yangu. Uzidi kubarikiwa.

 25. 52

  habari ,nazani ningependa kujuazaidi juu ya imani au niogezoeze imani

 26. 54
  saimon blaise Says:

  nakushkr sana mwalim kwa somo lako hakika umenifunua upeo katka imani.Mungu akubariki sana.

  • 55
   Aidani kahimbi Says:

   Yaani nimegundua kuwa Hakuna cha kukihofia,isipokuwa ni kuwa na imani tu,kuwa yatakuwa,hata kama kuna ugumu fulani,hako katakuwa ni kajaribu sio jaribu kwa mtu aliye kamili kibiblia,UBARIKIWE MTUMISHI.

 27. 56
  Israel Says:

  Nimebarikiwa sana na somo hili MUNGU ya Ibrahim Isaka na Israel akubariki

 28. 57
  Songana2 Says:

  Ubarikiwe sana kwa kutuwekea masomo mazuri

 29. 58
  Yeremia K. kITILA Says:

  Mungu wangu na akubariki sana.

 30. 60
  Yeremia K. kITILA Says:

  nimebarikiwa sana na somo hili kwani ndiyo msingi mkuu wa imani yenye ushindi , nimewahi fundisha mara nyingi somo somo la (imani iletayo ushindi) asante sana,

 31. 61
  SEM DEDE. Says:

  NENO la MUNGU limenijenga na kuponya maisha yangu .endeleeni kutoa neno na MUNGU awabariki zaidi kwa kuwapa mafunuo mapya.

 32. 62
  natalia Says:

  ubarikiwe ndg kwa somo hili limenifungua zaid kujua nn nguzo ya iman yangu.na kutambua hofu naashska ndio hupunguza iman ys kuponya na kuponywa.

 33. mr Jackson nimependa mafundisho yako mh mm ni mchanga katika huokofu lakini sasa nimetambuwa kuwa kunakitu ambicho nimejifunza kuhusu imani na kugoa milima

 34. 65
  jasson jaspa Says:

  kwa kweli mtumishi wa Mungu nimependa sana masomo yako maana mimi ndo mara ya kwanza kuangalia masomo yako

 35. 67
  Yohana Lukwaro Says:

  Nimepata kubarikiwa sikujua kumbe upungufu wa imani hutokea kati kati ya jaribu na hii huwa sababu ya kutopokea like unachotarajia ,,Mungu naatuongezee imani tuwe na utaratibu wa kuamini kabla ya kupokea kama maandiko yanavyohitaji…ubarikiewe mtu wa baba…..

 36. 68
  JANUARY L SHAYO Says:

  Mtumishi wa Mungu ubarikiwe .Somo lako limenibariki sana.Bwana aendelee kukufunulia zaidi juu somo la IMANI

 37. 69
  jafeti Says:

  somo hili ni zuri sana na limefanya kitu in my life. thankyou.

 38. 71
  meshack Says:

  Amen

 39. 72
  Paschal Ernest. Says:

  Amen! Ni kweli! Na hakika kwamba HOFU ni adui wa kila kitu.Hata ktk maisha yetu ya kila siku ya namna ya utafutaji. Mungu na Azidi kukutumia Mpendwa.

 40. 73
  Abango Dalton Says:

  Jambo nina hamu ya kutumia somo nyingine ili ziendelee kuni imarisha ki ukristo.

 41. 74

  mimi ni mwinjilist ningependa jinsi ya kukusa uduma yangu nitafanya aje ndio nikuwe kiroho

 42. 76

  pia leo ni mara yakuansa kushiriki kwa mafundisho nimefurahia sana

 43. 78
  veronica Says:

  barikiwa mtumishi……nimejifunza neno hili na limenitia nguvu. Napita ktk jaribu had I nimeona kama Mungu amenisahau hofu na mashaka vimetawala. Lakini neno hili limenifungua hakika shetani ni wa kushindwa kila siku.

  • 79
   frank archie Says:

   Namshukur sana mungu kwakutumia wajumbe wake ktk kutufungua,kutok ktk hali ya vifungo vya hofu nakurudishwa ktk iman iliyosimam!
   .mungu akubarik na azid kukufunulia uzidi kupasha habar kwa mataifa. Amem

 44. 80
  John Kinyange Says:

  amina YESU KRISTO akubariki sana.

 45. 82

  ASANTE SANA MTUMISHI WA MUNGU SANGA KWA MAFUNDISHO MAZURI MUNGU AKUBARIKI SANA

 46. 84
  Loveness Piniel Says:

  Mtumishi wa Mungu ubarikiwe sana juu ya somo hili zuri kabisa la namna ya kuongeza imani hakika limenibariki na kuniongezea nguvu, ni somo umelitoa miaka kama mitatu iliyopita ila kwa mwaka huu hakika litatenda jambo kwenye maisha yangu, uwe na moyo mkuu endelea kutuma masomo kama haya na mengine mengi. Ubarikiwe saaana!!

 47. 86
  Mattimba Peter Says:

  Ubarikiwe Sana Mtumishi Wa Mungu Kwa Utumishi, Tuko Pamoja, Amen !

 48. 87
  Cornelius Namukhaywa Says:

  God Bless You And Your Family For This Brill Lessons Thank You And We Are Together

 49. 89
  Dinah weddy Says:

  Ubarikiwe Sana mtumishi Mungu azidi kukutumia

 50. 91
  jack huruma Says:

  Bwana yesu apewe sifa, somo hili limeniongezea nguvu na uakika wa kubaki imara ndani ya neno alilo lisema yesu kwa maisha yangu, hata lichelewe naamini nitatendeka. asante sana

 51. 93
  asenga Says:

  Asenga renatus asante kwa somo zuri mtumishi wa Mungu ubarikiwe

 52. 95
  Edwin Vahaye Says:

  Shalom, ni mara yangu ya kwanza kuwa katika forum hii lakini nimebarikiwa sana. Kiukweli najiona nimekosa amani moyoni mwangu hadi nimekataa tamaa baada ya kuona watu wangu wa karibu wananiombea mabaya. Niliposoma hili neno la imani, naona naanza kupata nguvu na kuona kuwa yamkini ni kwa sababu nilisahahu kuwa yupo Mungu asiyeshindwa na ambaye ni mfariji wetu wakati wote.

  Ubarikiwe sana mtumishi

 53. 97
  Israel Samson Says:

  Amina!!Mungu atupiganie tuishnde dunia hii

 54. 98
  Robert Mushi Says:

  Mtumishi wa Mungu,
  Hong era sana kwa mafundisho ya Kujenga na kuimarisha Imani. Hakka kwa somo Lako hili umeponya imani za wengi . Mungu aendelee kukutumia kwa kukujaza vipawa vyake ili tuweze kutumia silaha za Imani yetu katika Kristo vizuri. Ubarikiwe sana.
  Robert Mushi

 55. 100
  alexander kisunga Says:

  Mungu wetu aliye hai akuongezee neema na hekima Mungu akubariki sana

 56. 103
  Victor malale Says:

  Thanks a lot

 57. 104
  jenny mmary Says:

  amina mtumishi ubarikiwe Sana na Mungu kwa kazi nzuri unayofanya nimebarikiwa Sana .pia nimejifunza kwa wakati sahihi .


RSS Feed for this entry

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: