NAMNA YA KUMTUMIA ROHO MTAKATIFU KAMA MSAIDIZI KUPITIA KAZI ZAKE

Na:Patrick Sanga

2

Yohana 14:16-18 … Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni, wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu”.

Katika somo hili nataka kuandika juu ya kazi za Roho Mtakatifu na kukuonyesha namna unavyoweza kumtumia Roho Mtakataifu kama Msaidizi kupitia kazi zake. Labda niseme kwa lugha hii, kama unataka kuona msaada wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yako, ni lazima kwanza uzijue kazi zake, maana kazi zake ndizo zinazotuonyuesha maeneo ya msaada wake, kazi zake ndizo zinazofafanua kwa namna gani Roho Mtakatifu ni Msaidizi.

Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye anayo nafsi na ameamua kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu. Kusudi kubwa la ujio wake ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu kwenye ulimwengu huu wa mwili, ili kumsaidia kuishi katika mapenzi ya Mungu.

Roho Mtakatifu amemamua kuishi ndani ya mwili wa mtu kwa sababu, Mungu hana namna ya  kutawala kwenye ulimwengu wa kimwili bila kuwa na mwili wa damu na nyama, kwa kuwa yeye ni Roho (Yohana 4:24). Hivyo hana budi kuingia kwenye mwili wa mtu na kufanya makao yake hapo, ili kutawala na kumuongoza mwanadamu katika mapenzi yake. (Yohana 14:23, Yohana 14:18, Ufunuo 3:20, 1Wakorinto 3:16-17, 6:19).

Kinachotusaidia kujua kwamba Roho Mtakatifu ana nafsi, ni tabia zake, maana kwenye kila nafsi kuna hisia, nia, kumbukumbu, akili nk. Baadhi ya sifa na tabia za Roho Mtakatifu ni; anapatikana kila mahali (Omnipresence), Zaburi 139:7, ana maarifa/anajua yote (Omniscient, Intelligence), 1 Wakorinto 2:10-11, ni mwenye nguvu zote/wa umilele (Omnipotent), Mwanzo 1:2, ni Mtakatifu, Luka 11:13, ana hisia (Waefeso 4:30, Mwanzo 6:3) – Wala msimuhuzunishe Roho wa Mungu…, Roho yangu haitashindana na Mwanadamu milele, ana nia (will), 1Wakorinto 12:11 – Hutenda kazi kama apendavyo.

 Kazi za Roho Mtakatifu

 • Kufundisha, Mwalimu (Yohana 14:26) … Atawafundisha yote…
 • Kuongoza, Kiongozi (Warumi 8:14, Yohana 16:13) – Atawaongoza awatie kwenye kweli yote, wote wanaoongozwa na Roho hao ndio … Mfano (Matendo ya Mitume 13:4, Acts 8:29)
 • Ni mfunuaji wa mambo/mafumbo/siri za Mungu (1Wakorinto 2:10) – Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote. Usipoteze muda kumtaka Mungu akufunulie siri zake, wewe mwambi Roho Mtakatifu hiyo ndiyo kazi yake.
 • Muombezi (Warumi 8:26) – Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
 • Mtoa/mpasha habari za mambo yajayo (Yohana 16:13f) – Na mambo yajayo atawapasha habari yake.
 • Ni msemaji wa mambo ya Mungu/Yesu (Yohana 15:26, 2 Petro 1:21) – Yeye atanishuhudia (he will speak about me), Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
 • Ni mtetezi/msemaji wa mambo yetu (Marko 13:11) – Kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.
 • Ni mkumbushaji wa yale uliyojifunza au uliyoagizwa na Mungu (Yohana 14:26)… Atawakumbusha yote niliyowaambia.
 • Kutia/kuwapa nguvu watu wake nguvu/uwezo (Matendo1:8) – Lakini mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu…
 • Kuuhakikisha (convict, make aware, sadikisha) ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8) e.g unajuaje kwamba kuna hukumu? Warumi 8:16

Naam kazi hizi za Roho Mtakatifu zinatufikisha mahali pa kujua kwamba jukumu lake kubwa ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu. Kufanyika msaada wa mwanadamu katika mambo hayo hapo juu pale mwanadamu atakapohitaji msaada huo.  Hivyo ni jukumu lako kumpa nafasi kwa kuboresha mahusiano yako na yeye ili akusaidie. Hata hivyo Roho Mtakatifu kuitwa Msaidizi haina maana kwamba ndio umvunjie heshima, bali fahamu kwamba, Roho Mtakatifu ni Msaidizi kwa namna ambayo bila yeye mimi na wewe hatuwezi kutenda neno lolote.

Kazi hizi zinatupa kujua kwamba Roho Mtakatifu yupo tayari kutusaidia katika kila eneo la maisha yetu. Ni jukumu letu kumpa  nafasi hiyo na kutambua kwamba bila msaada wake sisi hatuwezi lolote. Watu wengi leo hawaoni msaada wa Mungu kwao kwa sababu ya kutokumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kuwasaidia katika maisha yao na pia kwa kutokujua maeneo ya kumtumia Roho Mtakatifu kama Msaidizi.

Je, unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu eneo gani la maisha yako?, ni ndoa, kazi, madeni, huduma, kanisa, utawala nk mpe nafasi akusaidie, akufundishe na kukuongoza katika kweli yote. Kumbuka yeye ni Mungu ambaye ni Mwalimu na Kiongozi pasina yeye mimi na wewe hatuwezi neno lolote. Unataka kumjua Mungu, kuwa na maombi yenye matokeo mazuri na kufanikiwa katika maisha yako kiroho na kimwili pia mwambie Roho Mtakatifu akusaidie.

Msaada wa Roho Mtakatifu hauna mipaka maadam unahitaji msaada katika yale ambayo ni mapenzi ya Mungu. Hivyo haijalishi unapita katika jambo gani mpe nafasi Roho Mtakatifu akusaidie. Na ili uweze kuthamini msaada wa Roho Mtakatifu jifunze siku zote kufikiri kwa dhana kwamba bila msaada wake wewe huwezi lolote, na kwa sababu hiyo utaona umuhimu wa yeye kukusaidia katika maisha yako.

Usisubiri mambo yako yaharibike au usiachague mambo unayofikiri magumu ndio umshirikishe akusaidie, yeye anataka kuwa Bwana wa maisha yako, akusaidie kwa kila kitu hata mambo madogo kabisa kwenye maisha yako. Kina-muumiza Mungu kuona watoto wake chini ya jua wanahangaika katika maisha yao, wakati yeye amemleta Roho Mtakatifu ili awasaidie katika maisha hayo. Tumia vizuri fursa ya Roho Mtakatifu sasa maadam anapatikana, kuna wakati hatapatikana.

 Neema ya Kristo iwe nawe

Advertisements

71 comments

 1. Nimeupata ukurasa huu kwa mujiza. Baada yakusoma somo la hapo juu nimeburudika sana,mimi ni mtumishi wa Mungu wa mbinguni,nalichunga kanisa hapa Tarime.kemakorere&nyamongo.kwa ujula nimetiwa nguvu yakumtumia zaidi ktk huduma yangu.AMANI TELE IKUFUNIKE.

  Like

 2. Mungu akubariki, Roho Mtakatifu azidi kukupa mafunuo zaidi maana tunahitaji zaidi sana kutembea na Roho Mtakatifu katika maisha yetu nimebarikiwa sana, Mungu akulinde sana.

  Like

 3. MTUMISHI KAZI YAKO NI NJEMA SONGA MBELE NIMELIPENDA SOMO LAKO NI LA TOFAUTI SANA.
  AM SURE THROUGH UR LESSON IAM EXPECTING OTHER LEVEL

  Like

 4. Kwa kwel mpaka hapo nimejifunza kitu naitaji maombi ili niweze kutambua when the Holy sprit speaks to me and when not.Mungu akubariki mtumishi

  Like

 5. AMINA MTUMISHI WA MUNGU SIKUJUA MAMBO MAKUBWA KAMA HAYA MUNGU ALIYOKUFUNULIA KUFUNDISHA NYAKATI ZA MWISHO KAMA HIZI. NINATAMANI SANA WATU KAMA NYINYI MUONGOZEKE KATIKA KAZI HII NZURI. MTUMISHI NINA NENO KUNA WATU WANATAMANI MAFUNDISHO KAMA HAYA LAKINI WAMEKOSA INTERNET WAZO LANGU UNAONAJE TUKATOA NAKARA TUKAZIPELEKA HUKO KIJIJINI MIMI NIPO MBEYA.

  Like

  • Hello ndg. Ngobola ahsante kwa maombi yako na kunitia moyo katika utumishi huu. Binafsi ninarhusu uweze kutoa nakala za masomo haya kwa lengo la kuwafundisha na kuwapelekea wale ambao hawana ‘access’ na matandao na masuala ya teknolojia pia. Mungu akubariki kwa wazo lako jema. Tuzidi kuombeana.

   Like

 6. Mtumishi wa Mungu kwa wakati kama huu naomba usinyamanze kabisa wala kuchoka maana ni wakati wa Mungu kusema na kizazi hiki kupitia maneno aliyoyaweka kinywani mwako.Kumbuka tunaishi kwa Kutimiza Ratiba ya Mungu aliyotuitia duniani mimi na wewe.Naomba fanya zaidi ya hapo ulipofikia ukimshirikisha Roho Mtakatifu akufunulie siri yake Mpendwa.

  Like

 7. Haya ndo masomo muhimu kwa kanisa! Makanisa na maisha ya kikristo sasa yanaendeshwa kimazoea na kupoteza kabisa sura ya Kristo,kwa kuwa masomo haya ya Roho mt hayafundishwi tena. Siku za leo injili imeegemea upande mmoja tu wa prosperrities/mafanikio.. Nakubali Roho mt ndo kila kitu ktk ukristo na ndo UHAI wa imani yetu. Ubarikiwe mwalimu

  Like

 8. katika mambo ambayo nayaona muhimu sana ktk maisha yanguya wokovu ni kumtii Roho mt, nashukru watumishi wa MUNGU kwa kunifundisha habari hizi,MUNGU na awabariki sana,amen

  Like

 9. Ninashangazwa na baadhi y waumini wenzangu wasepo “sina roho mtakatifu” kwa kuwa sineni kwa lugha. Je biblia inatufundishaje kuhusu kunena jambo lisilofahamika?

  Like

 10. Asante kwa mafundisho mazuri uliotupatia. Nimejifunza mambo mengi na mazuri ambayo kwayo yatasaidia kuijenga imani yangu katika kristo Yesu kupitia nguvu ya Roho mtakatifu.
  Mtumishi tusaidie kutofautisha wajibu wetu kama wakristo katika Utatu wa Mungu (Mungu baba,Mungu Mwana na Roho mtakatifu) wengi tunachanganya nashukuru umeanza vizuri sana na Roho mtakatifu naomba umalizie pia kwa Mungu baba na Mungu Mwana
  Ubalikiwe na Bwana

  Like

  • Sawa, naomba muda maana nina mambo mengi sana ninayoulizwa na ninayosikia pia kuandika, kwa wakati muafaka nitalifanyia kazi, lakini jibu fupi kwa hoja yako ni kwamba Baba, Mwana na Roho lao ni moja, na kwa sasa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu ndio yupo duniani, hivyo jenga mahusiano mazuri na huyu itakusaidia

   Like

 11. Roho mtakatifu ni wasaman sana kwa maisha ya muumini hivyo bac ndugu zangu tumpe nafasi inayostaili Roho mtakatifu katika maisha yetu na kuishi maisha matakatifu iyo ndio silaa pekee ya kutembea na Roho wa Bwana. Mbarikiwe sana mtumishi wa Mungu kwa somo zuri

  Like

 12. AMEN MTUMISHI WA MUNGU MIMI NIMEFURAHI SANA KUSOMA KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NA MUNGU AKUTIE NGUVU ZAIDI KWA KUWASAIDIA UJUMBE MZURI KAMA HUU] MIMI NAITWA MTUMISHI AMINIELI NI MWEZI WA PILI SASA NIFUNGUE UKUMBI WA MAOMBI ARUSHA NA MUNGU AKUTIE NGUVU

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s