Wokovu

Biblia katika Yohana 3:16 imeandikwa “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”. Mpenzi msomaji, ikiwa bado hujaokoka na umejifunza neno la Mungu au kusikia habari za Yesu na sasa umeamua kuokoka basi ukurasa huu ni maalum kwa ajili ya kukuongoza katika maamuzi hayo muhimu kabisa kwa maisha yako ya sasa na ya baadaye.
Kuokoka ni kumkaribisha YESU katika maisha yako kwa njia ya imani  ili kumruhusu achukue nafasi ya  utawala/uongozi wa maisha yako. Katika Warumi 10:9 imeandikwa “Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chacko ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka’. Jambo muhimu ni kwamba, unatambua kwamba wewe ni mwenye dhambi na unahitaji msaada wa Mungu kutoka dhambini kupitia kifo na kufufuka kwake ili kukuongoza kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi. Fahamu kwamba kuokoka siyo kuchanganyikiwa, kupotea, ujinga au kufeli katika maisha, bali ni kumpa Mungu;

  • Nafasi ya kwanza kuongoza na kutawala maisha yako kwa ujumla (Zaburi 32:8)
  • Kukuongoza kuishi sawasawa na mapenzi (kusudi) yake uwapo duniani (Warumi 8:28)
  • Kukuongoza katika njia yake ili uweze kuurithi uzima wa milele, kwa sababu baada ya mtu kufa katika mwili ndipo anaanza kuishi maisha ya umilele katika roho (nafsi).

Sasa baada ya haya naamini unaelewa aina ya maamuzi unayotaka kufanya. Kama uko tayari kuokoka sema maneno yafuatayo kwa imani “Bwana Yesu,  nipo  mbele mbele zako, ninakiri ya kuwa mimi ni mwenye dhambi, ninaamini kwamba ulikufa na kufufuka ili nipate wokovu, hivyo nakukaribisha moyoni mwangu uwe Bwana na mwokozi wa maisha yangu, naomba ulifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu ya watenda dhambi na uliandikie jina langu kwenye kitabu cha uzima, kuanzia sasa nayakabidhi maisha yangu kwako uyatawale na kuyaongoza katika mapenzi yako, kwa jina la Yesu Kristo, Ameni”. 

Baada ya sala hiyo, nakupongeza kwa kuwa umefanya maamuzi bora zaidi maishani mwako na sasa nakuomba uzingatie mambo machache yafuatayo: (a) Tafuta mtu yeyote unayejua ameokoka halafu mjulishe uamuzi (b) Kama huna kanisa unalosali, tafuta kanisa lolote linaloamini katika wokovu, kisha waambie juu ya uamuzi wako na (c) jenga mazoea ya kusoma neno la Mungu kila siku na kuomba pia.

Mungu wakubariki sana, amini kwamba Yesu yu ndani yako sasa.

74 comments

  1. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu Mungu akubariki kwa makala yako nzuri ambayo inatufunza mengi hasa katiika kukulia ktk wokovu. Mimi binafsi naweza kusema kwamba bado ni mchanga katika wokovu so that nahitaji maombi yako ili niweze kusimama katika imani yangu na kukulia katika wokovu mpaka pale Yesu atakaporudi kunichukua.
    Mungu akubariki.

    Like

  2. Bwana Yesu asifiwe sana. Ubarikiwe sana mtumishi kwa somo lako zuri. Ubarikiwe sana mtumishi wa Bwana. Mimi ni mchanga sana ndani ya wokovu. Naomba mtumishi uniombee, niweze kukua kiroho. Pia naomba unitumie masomo mbalimbali yatakayonisaidia kwenye kukomaa kiroho. KWENYE MAIL YANGU mlukindo@yahoo.com

    Like

  3. Mtumishi? bado ni mchanga kiroho!
    na mchumba tumetimiza mwaka 1 sasa. mwenzangu anasema amempokea yesu! ila ndani ya huu mwaka tumeshafanya nae mapenzi mara nyingi ! japo tulikubaliana tutubu! lakini tunatubu nakuendelea tena tunaanguka tena! sasa amekuwa aeleweki tena na mwambia tuache lakini naona kama aemenogewa! sababu anaishi mbali na Dar(mkoani) napata shaka sana anaweza hakawa anaendelea kufanya na wengine, sababu nilisha mkamata na sms toka kwa mwanaume! swali je niendelee kutegemea atakuwa mke wangu au niache tu! maana kwa mtindo huu kufika mbinguni itakuwa NGUMU!

    Like

    • Hello Mpendwa wangu, Mungu akubariki kwanza kwa kuwa tayari kusaidiwa na Mungu. Maana kitendo cha kujieleza kwa uwazi kiasi hiki ni ishara ya kumshinda Shetani, kwani ni wengi wanaofanya hayo na kujificha wasijulikanae na wanadamu ingawa Mungu anawaona. Kimsingi mmefanya dhambi na unapaswa kutubu kwa nafsi yako. Kama kweli umeokoka na unataka Mungu awe upande wako kukuongoza katika kusudi lake na mapenzi yake basi nakushauri achana na huyo mwanamke maana kwako huyo ni kikwazo kwa wewe kukua kiroho na kumjua Mungu zaidi.

      Hivyo tulia ujielekeze katika kuukulia wokovu na kumaanisha katika kutaka kumjua Mungu kwa kuhakikisha unasoma neno la Mungu, unajali ibada na kufanya maombi kila iitwapo leo. Usijaribu kujiamini kwamba utaweza kuendelea kuishi naye kwa mipaka, suala ni kuachana naye in the first place ili uwe na muda wa kutafakari ya Mungu zaidi. Nitaendelea kukuombea na kuwa karibu na wewe.

      Mungu akubariki, si kwa kukutenda dhambi bali kwa kuwa tayari kutengeneza na Mungu wako, hii ni saa ya uponyaji kwako. Nitumie namba yakio ya simu kupitia simu hii 0755 – 816800 au 0715 – 816800.

      Like

      • Mungu akubariki Sana kwa Mafundisho Mazuri Na nakuomba unisaidie mafundisho mengi zaidi kuhusu Ndoa maana mimi ni kijana ambaye Bado sijaoa na Sina Mchumba, email:mashalamachiya@gmail.com

        Like

    • asante mtumishi kwa kuwa muwazi, inabidi utambue kuwa huo sio uchumba tena bali ninyi ni kama mke na mme maana mumeanza tendo la ndoa kabla ya wakati na hivyo mnadhini na hiyo ni dhambi mbele za mungu na inapasa kutubu kabisa kama huyo mtu wako anasababisha kuendelea kutenda uzinifu , basi chukua hatua waone watumishi wa mungu watakusaidia nawe utakuwa na amani moyoni mwako, hakiaka nakwambia ni lazima uchukue hatua kwa usalama wa maisha yako na imani yako

      Like

  4. Mchungaji, mimi nimekuwa nashida nyingi ikiwa pamoja na kusumbuliwa na magonjwa ni mara chache sana kulala bila kumeza hata dawa, mchungaji nisaidie kuna vitu vinanitatiza, Je kama ninaishi na mwanamke ambayesijafunganaye ndoa, je ninaweza kuokoka na Mungu akasikia maombi yangu au mpaka nimuache japokuwa nimeishi nae mwaka mmoja sasa? halafu ndio nifanye process upya?

    pili je Mtu aliyeokoka anaweza kutumia dawa za mitishamba? (siyo matibabu ya ramli}

    Like

  5. Mtumishi wa mungu ubarikiwe sana kwa huduma hii…nimesoma na kurudia-kurudia ni nikapata mambo mengi fulani ambayo nilikua siyafahamu na nikawa ninaoona la kumbe hata niko mbali na neno na mungu…lakini mungu ashukuriwe kwa maana nimepata kujua ukweli nao unaniweka huru…tafadhali ningetaka kupata mafundisho zaidi ya nini maana ya KUMUHUSISHA mungu au bwana kwa kila jambo….na mungu anataka roho yake…jinsi ya kumpata mungu roho yake….na baadae ni yapi yanafuata….mtu awe vipi…naamini unanielewa natamani kuja haya kwa undani…maana sitaki nikose mbingu….AMANI

    Like

    • Amina dada Rachel, ahsante pia kwa kutembelea na kujifunza mengi kupitia blog hii. Nafanyia kazi maombi yako ya mafundisho, kisha nitatuma kwenye email yako. Barikiwa.

      Like

  6. Jina la Bwana lipewe sifa Mungu awe nawe daima na akujibu kama alivyomjibu Yabesi Katika 1nyakati 4:10 nimefurahishwa na huduma uifanyayo. Naomba unisaidie kujibu hili swali maombi ya rehema yapoje ukweli nimeulizwa nimeshindwa kujibu.Barikiwa na endelelea kua baraka kwa sisi wengine.

    Like

  7. Hellow Pastor, nafarijika sana na masomo yako.Mungu akubariki na akuongezee miaka ili uendelee kufundisha kweli yake vizazi na vizazi pia naomba uwe unanitumia masomo mbali mbali kwenye email yangu annynatai@yahoo.com.

    Like

    • Hello Annette Mungu akubariki kwa kutenga muda wa kujifunza neno kupitia mtandao, utukufu kwa Mungu ikiwa unapata kitu cha kukusaidia. Nitajitahidi kufanya hivyo, tuzidi kuombeana.

      Like

  8. Asante kwa kuchanganua habari hii ya wokovu,ambayo kwa sasa ni wakati muafaka sana wokovu kuwa unafafanuliwa sana,maana inataka kuwa kama mazoea,na wahubiri wengi wa injili hawahubiri na kuuelezea wokovu kwa watu ila mambo ya miujiza tu ambayo hata miujiza mingine bado inatuchanganya.Ombi langu kwako ni utufafanulie pia uhusiano wa Roho mtakatifu na kunena kwa lugha habari ambayo ilijadiliwa lakini bado hatukufikia muafaka kuelewa lipi ni lipi.ASANTE

    Like

    • Amina ndg. Noel utukufu kwa Mungu. Nimepata ujumbe wako naomba hekima na uongozi wa Mungu nitaandaa somo juu ya jambo ili kuongeza ufahamu juu ya uhusiano wa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha.

      Like

  9. Mimi napenda sana kuokoka lakn mazingira niliyomo ndo mabaya kwa sasa naishi Bukoba vijijin Mkoani Kagera ambapo hakuna kanisa hata moja la wokovu je nifanyeje? Na mim niweze kuwa na makanisa walokole asanteni.

    Like

    • Hello Happy Shalom, hongera sana kwa kufikiria na kupenda kuokoka, naam nakushauri amua kuokoka kabisa, kwa kuwa ni maamuzi bora kuliko yote hapa duniani. Wokovu siyo kanisa au wokovu wa mtu hautegemei uwepo wa kanisa au dhehebu eneo ulilopo. Wokovu ni kwa habari ya mahusiano yako binafsi na BWANA Yesu. Maana yangu ni hii, kutokuwepo kwa kanisa la wokovu kusiwe kikwazo kwako kuokoka, kwani mwanzo wa kanisa ni mtu kuokoka. Najua changamoto yako ni namna ya kukua kiroho kwa kuwa imeandikwa ‘tusiache kukusanyika kama ilivyo desturi ya wengine’. Hili lisikusumbue kwa kuwa hata sasa duniani wapo watu wengi ambao wameokoka na wapo maeneo ambayo hata kuabudu wanakatazwa, naam lakini bado wanadumu katika wokovu. Kwa ajili yako pia ndio maana kuna mtandao, kuna vitabu na zaidi ya yote kuna Roho Mtakatifu. Kwa hiyo nakushauri uokoke kabisa na kisha Roho Mtakatifu atakuongoza namna ya kuukulia wokovu (Zaburi 32:8). Ni imani yangu hata huko kuna watu waliokoka, wengine wapo kwenye makanisa ambayo kwa tafisiri yako huenda siyo ya wokovu, ninachojua BWANA ataku – connect na watu watakaokusaidia kuukulia waokovu dada yangu. Kama uko tayari kuokoka basi fanya sala ya toba hapo juu. Mungu akubariki simu yangu ni 0755 – 816800 nitafute nitakueleza mambo mengi zaidi.

      Like

      • naomba unijibu swali hili.kuokoka ni lazima uhame kanisa? kama sivyo kwa nini watu huwatafuta waliokoka ili waabudu pamoja nao uoni kama ni kujitenga na jamii? na kuweka makund mm wa apolo mwingne mimi n wa kefa . hakika bado cjapata jibu kuhusu ilo.

        Like

      • Ndugu Jackson, kwa kifupi kuokoka si lazima uhame kanisa, kwa sababu wokovu si jengo, na kuna ambao wanaokoka hata hawako kwenye kanisa/maeneo yao hayana kanisa. Siwezi kujua sababu zote kwa nini watu hutafuta waliokoka ili waabudu nao pamoja, lakini jambo ninalojua ni hili, haikanushiki kwamba katika madhehebu mbalimbali tutlionayo si yote yenye kuwajenga vema watu juu ya namna ya kuukulia wokovu, kwa hiyo naamini huenda watu hutafuta chakula/mafundisho ya kuwasiaida kuukulia wokovu. Naam hata leo nimeona baadhi ya makanisa ambayo Roho Mtakatifu hapewi nafasi/hatambuliwi kabisa kama Msaidizi wa kanisa kwa sasa, na kwa sababu hii usitegemee watu kuukulia wokovu kwenye mazingira kama hayo.

        Ahsane Yesu kwa kuwa sasa kanisa la Mungu linaendelea kufunguka na hata madhehebu ambayo hayakuwa yanatambua vizuri juu ya wokovu sasa yanatambua na yanaruhusu uongozi na utawala wa Roho Mtakatifu katika ibada zao. Naamini jambo hili likipewa mkazo hakutakuwa na sababu ya watu wakikokoka kuhama kwa kuwa mafundisho ya kweli ya neno la Mungu yatakuwa yakinenwa mahala kote. Naam huko ndiko ambako BWANA Yesu anataka kanisa lake lifike.

        Like

  10. Mtumishi wa Mungu ubarikiwe sana kwa mafundisho mazuri katika blog hii. Nimejifunza mengi kila nilipopita na kusoma. Nahitaji pia maombi yako ili Mungu aendelee kunilinda na yule mwovu(shetani) na kuniponya na ugonjwa unaonisumbua ambao nilipopima hospitalini niliambiwa hawaoni ugonjwa unaonisumbua, lakini nahisi maumivu makali.
    Ubarikiwe!

    Like

  11. Bwana Yesu asifiwe, habari zako mtumishi wa Mungu mimi ni kijana ambaye nimebahatika kuokioka kwa muda. Kipindi ninasoma chuoni kuna wakati nilijaribu sana kumshika Mungu na nikawa hadi naenda ibadani asubuhi, jioni na usiku. Niliungana na wapendwa wenzangu hadi nikajiunga na kwaya mnamo mwaka 2009 na nikawa najifunza kupiga vyombo vya muziki. Tatizo lililokuwa likinirudisha nyuma ni ulevi wa pombe maana niliokoka chuoni na wakati huohuo nilikuwa tayari nishaanza kunywa pombe. Muda ulienda na nikaendelea kusali na kudondoka mara kwa mara mwishowe nikaona niache kabisa maana waumini wenzako watanionaje mara nipo ibadani mara nipo kwenye ulevi. Niliona nitawakatisha tamaa waumimi wengine na wataona hakuna umuhimu wa kuokoka kama walokole wenyewe wanakunywa bia na matendo mengine ya uzinzi alafu unawakuta ibadani hivyo taratibu nikajitoa kwenye kwaya kisha nikaanza kuwa mvivu wa ibada na baadae nikabaki kusali kwa mazoea kila jumapili tu.

    Kwa kweli simshauri mtu kujifunza ulevi maana kuanza ni rahisi ila kutoka ni shughuli. Nimeshajaribu mara kadhaa kuacha lakini inakuwa ngumu hasa pale napokutana na marafiki zangu, nilishajaribu kunywa dawa moja ya miti shamba ambayo imesadikika kuwasaidia wengi lakini kwangu haikufua dafu.

    Mwanzo nilijua ukinywa pombe wewe ni afadhali kuliko yule ambaye ulevi wake ni uzinzi kumbe sivyo ukiwa mlevi utakuwa mzinzi pia. Zaidi ya yote kuna siku nilisafiri kikazi kwenda mkoani singida nikawa na marafiki zangu tukinywa pombe, ilikuwa mwaka jana mwezi wa saba ghafla alikuja dada mmoja na kuomba nimnunulie kinywaji nami nikamnunulia akadai kuwa hajala nami sikusita kumnunulia chips na nyama choma. Hii siku sitaisahau katika maisha yangu kwani ni siku ambayo inanifanya niwaze kuwa hata sifai kuonekana mbele za uso wa Mungu. Yule dada alikunywa na kula na mimi pia nilikunywa na nililewa sana.
    Baada ya hapo nikajikuta tumeondoka naye hadi chumbani nilipofikia. Tukaenda kufanya mapenzi na yule dada hakuwa na kipingamizi hakunipa ushirikiano sana na baadae akataka apande juu yangu nami sikumkatalia akapanda nami nikagundua kuwa hapo ndo yeye anafurahi zaidi, kuja kushtuka kumbe yule dada amenipa sehemu ambayo Mungu hapendi na ndipo pombe ziliniisha na niliumia sana kwani sikuwahi kufikiria kufanya dhambi hii katika maisha yangu. Dhambi ya sodoma na gomora mimi nimeifanya!!! kwa kweli nilichukia na nikaamua kumtimua yule dada chumbani kwangu. Nililia kwa uchungu na taswira ya tendo lile huwa inanijia kila mara. Naona kama sistahili msamaha na naona kama siwezi kuokoka kwani nimefanya machukizo sana mbele ya Mungu wangu. Nimekuwa na roho ambayo inanisumbua na kunifuatafuata kwamba nirudie tukio lile kwani sikufaidi na roho nyingine inanikataza. Unaweza ukanikuta nimekaa kimya nawaza kwa muda mrefu.

    Jamani naomba ushauri wenu nifanye nini ili niweze samehewa na nibadilike niwe mwanakondoo wa Mungu na mfano katika jamii yetu.

    Samahani kwa wale nitaokuwa nimewakwaza lakini mambo kama haya yapo na watu wa namna hiyo wapo wengi duniani hasa wale ambao hawajamjua mungu.
    Nisaidieni katika maombi na naomba mnisaidie katika masomo niweze kubadilika.
    Mungu awe nawe.

    Like

    • Hello Erick pole sana kwa changamoto zote ulizokutana nazo kuhusu wokovu wako, nakupongeza kwa kuwa umekuwa muwazi na hii ni dalili ya kukusaudia kubadilika na kuhitaji msaada ili uweze kupona kabisa. Katika Mithali 1:10 imeandikwa “Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi wewe usikubali” na Pia katika Zaburi 1:1-3 Biblia inazungumzia kwa habari ya kuwa makini na maisha yako kwa habari ya kutoenenda katika shauri la wasio haki, kutoketi barazani pa wenye mizaha nk. Kwa upande wangu tatizo ninaloliona kwako ni makundi mabaya ya rafiki zako ambao uliamua kuendelea nayo ukijua kwamba wewe umeookoka. Ulipaswa na kuanzia sasa unapaswa kuachana na makundi mabaya ambayo unajua lengo lake ni kukushawishi utende dhambi, Paulo aliwaambia Wakorinto ‘Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”. Naam uwe na uhakika makundi mabaya na marafiki wabaya watakufanya uwe mbaya pia.

      Ni kweli wokovu ni changamoto sana na kusimama kwenye wokovu unahitaji neema na uamuzi wako binafsi pia, ndio maana Biblia inasema wenye dhambi wakikushawishi wewe usikubali. Naam suala la kukubali au kukataa lipo katika uwezo wako binafsi. Naam unapaswa kudhamiria kutokumtenda Mungu dhambi tena na ndiyo maana Paulo anawaambia Waefeso msienende kama wamataifa waenendavyo kwa kuzifuata tamaa za mioyo yao. Mzee Yohana naye anatuambia Msiipende dunia na kila kitu kilichomo katika dunia yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima … Ukiangalia mistari hii yote inamtaka mtu husika kuchukua hatua ya kuwa makini na maisha yake ya wokovu, naam zingatia sana haya mpendwa wangu.

      Licha ya ukweli kwamba dhambi ulizofanya kwa jinsi ya kibinadamu na kwa Mungu pia ni chukizo kubwa, fahamu neno hili kwamba Mungu mwenyewe anasema ‘ Mimi ni Mungu niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe’ (Isaya 43:25). Nataka nikutie moyo kwamba bado neema ipo kwa ajili yako Erick, usikubaliane na hayao mawazo ya kipepo yanayokutaka urudie kutenda ile dhambi tena (USIKUBALI). Bali tambua kwamba kwa Mungu wewe ni wa muhimu sana, kitendo chako cha kuwa muwazi kiasi hiki ni ishara kwamba Mungu anakuhitaji kwa ajili ya ufalme wake, naam rudi kwake, yeye husamehe maovu yetu kabisa. Kumbuka kama Mungu angelihesabu maovu yetu tusingelikuwapo, bali BWANA ni mwingi wa rehema, naam hafurahii kifo cha mwenye dhambi.
      Hivyo nakushauri rudi kanisani na kutubu, na sina maana mbele ya kanisa, bali tafuta Mchungaji au kiongozi ambaye ni mwaminifu na msiri mweleze jambo hili ili iwe rahisi kukusaidia na kukufuatilia pia kwa habari ya maendeleao yako ya kiroho. Kama unaona ni zito kwako kulifanya nitafute kwa namba hizi (0755-816800) nitakueleza cha kufanya kwa kirefu.

      Mwisho kwa wasomaji wa blog hii, ndg yetu Erick ametambua kosa lake, sisi ni nani hata tumuhukumu, naomba tumsaidie in a positive way kwa ushauri na maombi pia, Mungu awabariki kwa huduma yenu njema pia na hasa wale waombao juu ya wale wenye mahitaji mbalimbali na kutoa ushauri wao.

      Like

      • Mtumishi namshukuru Mungu kwa ajili ya utumishi wako nimependa ulivyomwelewa na kumjibu Erick kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu Warumi 3:23, Pia naomba afarijiwe na 2Korintho 1:3-7 Mungu ametufariji nasi tuwafariji wengine. Nampongeza kwa kuwa muwazi ni hatua njema ya kupata uponyaji. Ningekuomba kama ulivyompa namba ya simu afuatiliwe kwa karibu maana si wote tuna karama kama yako ya kutoa faraja. pia apende kuanagalia na kusikiliza redio au Tv zinazotoa mafundisho ya Mungu na aifanye Biblia kua ni kitabu cha kwanza kwake na aendelee kuliitia Jina la Bwana YESU daima. Baraka za Bwana ziambatane nanyi daima. Deodata Martin

        Like

      • Ahsante Deodata naomba tuzidi kuombeana maana wajibu unachangamoto kubwa. Ubarikiwe sana pia kwa mchango wako uliotoa juu ya maendeleo yake binafsi ya kiroho, naamini Erick atayazingatia.

        Like

  12. Asanteni sana naomba tuzidi kuombeana na kushirikiana katika kumjua Mungu, Mungu awabariki sana, Nakushukuru sana kaka Sanga kwa kunitia moyo najiona mwenye amani ya Bwana.

    Like

    • Amen, glory to Jesus, BWANA akubarki na kukulinda na kukuongoza katika njia ikupasayo kuiendea (Zaburi 32:8) kwa ajili ya jina lake na kusudi lake katika maisha yako.

      Like

    • Nipe muda, nitajitahidi kufanya hivyo, lakini njia rahisi unayoweza kufanya nikuji – subscribe kwenye blog hii ili kila ninpoweka somo lije kwenye email yako mija kwa moja.

      Like

  13. Asante Mtumishi wa Mungu, Mungu akubariki sana.
    Na mimi nimeokoka, Ombi langu ni kuwa, naomba nitumie masomo ya kunikuza kiroho!
    Mungu aibariki kazi yako.

    Like

    • Nitajitahidi kufanya hivyo, nipe muda, ila njia rahisi ji – subscribe kwenye blog hii, kila nitakapokuwa naweka somo jipya litakuja kwenye email yako moja kwa moja pia.

      Like

  14. Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu endelea kuifanya kazi ya Mungu kwa uhaminifu na Mungu atakusaidia . Na endelea kumtia moyo kaka Erick asimamie kweli ya neno la Mungu maana ndimo ulimo uzima .ENDELEA KUMTIA MOYO APATE KUSIMAMA. Amen.

    Like

  15. Shalom mtumishi hongera na kazi ya Bwana nimejifunza mengi kupitia Blog zako. Pia mimi kama mwanamke nimeboresha ndoa yangu kupitai masomo yako ya ndoa na pia nimewapa na wengine na wote tunafurahia ndoa zetu na Mungu anaonekana ubarakiwe sana

    Like

    • Hakika Tumaini, nimekuwa kimya kiasi kwamba nikajua ninamkosea Mungu kwa kimya hiki, nisamehe bure, kuna majukumu mengi na hasa la shule lilinibana sana, lakini sasa nimemaliza na utaendelea kuona masomo mapya mara kwa mara. tuzidi kuombeana, vita ni kubwa pia, Shetani hafurahii huduma hii.

      Like

  16. Leo nimefurahi sana kukutana na somo jipya sehemu ya mwisho NAMNA M.KE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFAC ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA.Kwakweli nimebarikiwa mtumishi Mungu aendelee kukutia nguvu na naamini yatakuja masomo meeengi kwa kadri RM atakavyokufundisha.

    Like

  17. Nabarikiwa sana na masomo yako. Ni maombi yangu kwa Mungu azidi kuzifunua akili zetu kuelewa maandiko na masomo haya. Na pia Mungu akubariki wewe na nyumba yako kwa utumishi wenu.

    Like

  18. Mungu akutie nguvu kwa kutupa nuru juu ya wokovu maana wengi hatujui maana yaWokovu tunajua kwenda kanisa fulani unakuwa umeokoka

    Like

  19. asante sana kwa maoni yako kaka kwan mimi ni kiziwi ambaye sisikii vizuri
    kutokana na ulemavu wangu natamani kujua zaidi biblia naomba uendelee kufundisha na mengineyo pia ili nifahamu zaid .nakumbuka biblia katika matendo ya mitume sura ya 8:37 FILIPO akasema ukiamini kwa moyo wako woteinawezekana akajibu akanena naamini ya kwamba YESU KRISTO ndiye MWANA WA MUNGU …..

    Like

    • Ahsante pia kwa kutenga muda wako na kujifunza kupitia blog hii, BWANA Mungu wetu na ayafungue masikio yako upate kusikia sawasawa. Naam sitaacha nitaendelea kuweka masomo maadam ni mchana.

      Like

  20. Shalom! Mt Naomba namba ya simu yako ili nikupigie tuzungumzee mim ni mtumishi ninaye chipukia hivyo nahitaji watu waliyotangulia kwa ajili ya kujifunza mengi. Nitashukulu kama utanipa namba mim nsmba yangu ni+255656995917 Ubarikiwe

    Like

Leave a reply to Peter aidan Cancel reply