Huduma

KUCHANGIA HUDUMA

Ninamshukuru sana Mungu aliyeniita ningali kijana na kunipa neema hii ya ajabu ya kuweza kumtumikia ili KUIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI. Naamini kwa namna moja au nyingine hata wewe msomaji wangu utakuwa umebarikiwa kupitia huduma hii kwa ujumla wake.

Katika kufanikisha kazi yake, Mungu huwa anazungumza na watu  na kuwaagiza/kuwataka waweze kuchangia gharama zinazohitajika katika huduma mbalimbali. Maana katika kitabu cha Warumi 10:15 Biblia inasema “Tena wahubirije wasipopelekwa? …“ Si rahisi injili ikahubiriwa au masomo yakafundishwa kama hakuna watu watakaolipia gharama ambazo wahubiri, walimu, wachungaji n.k wanazihitaji katika huduma zao na kutekeleza wito walioitiwa. 

Katika huduma hii kuna gharama mbalimbali ambazo zinahitaji kugharimiwa ikiwa ni pamoja na;

 • Gharama za uandishi na uchapishaji wa masomo     
 • Gharama za uandishi na uchapishaji wa vitabu  
 • Gharama za uandishi na uchapishaji majarida ya kiroho
 • Gharama za uchapishaji wa makala  kupitia magazeti.

Haya ndiyo ambayo Bwana ameweka moyoni mwangu nipate kuyafanya kwa sasa. Hivyo naomba simama pamoja nami kwa sadaka yako ili kugharamia gharama hizi ukijua rohoni kwamba unafanya kazi ya Mungu na si ya mwanadamu.

Kwa sadaka yako kazi ya Mungu itasonga mbele, maana kila mwezi nathibitisha mamia ya watu wakiponya, kubarikiwa na kupata maarifa ya kuwasaidia kupitia huduma hii ndani na nje ya Tanzania. Ni imani  yangu huduma hii itaendelea kupanuka na kuwafikia mamilioni ya watu katika Jina la Yesu aliye hai. 

Hivyo basi ikiwa uko tayari na unataka kuchangia sehemu ya gharama hizi kifedha au kwa kutuma kitu chochote ambacho unajua kwa namna moja au nyingine kitafanikisha huduma hii na hasa zoezi zima la uandishi na uchapishaji wa masomo, majarida na vitabu, tafadhali wasiliana nami kwa simu au e-mail. Ili kupata mawasilianao yangu tafadhali bonyeza link hii https://sanga.wordpress.com/about/

Wagalatia 6:9-10“Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho, kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.”  

Ubarikiwe na Bwana Yesu

 

 

18 Comments »

 1. 1

  Mungu wangu akubariki kwa huduma uifanyayo
  (0714 07 11 39)

 2. 2

  Mkonowa Mungu usikuache katika huduma hii.

 3. 4
  SHUKRAN Says:

  MUNGU akubariiki kwa huduma uliyo nayo

 4. 5
  SHUKRAN Says:

  Bwana akupe nguvu na usikate tamaa katika huduma uliyo nayo .

 5. 6
  mary budili Says:

  Bwana Yesu azidi kuwa nawe katika huduma hii. Ubarikiwe sana mtumishi.

 6. 7
  Efrem Mbossa Says:

  Mungu akubariki sana mtumishi kwa huduma nzuri na bora utupatiayo!.

 7. 9
  elia Says:

  Dah, ubarikiwe sana. Yani nafurahi kwakua….. nadhani ni mipango ya Mungu. Mimi nafanya huduma kama wewe. Nina blog inaitwa huduma.blog.com na pia worldpress. tuwasiliane 0658662210

  • 10
   sanga Says:

   Amina na pia nashukuru sana ndg. Elia kwa comment yako, nimepitia blogu yako, ubarikiwe kwa huduma uifanyayo na Bwana azidi kuikuza kwa kadri ya mapenzi yake.
   Nafurahi kukufahamu naamini tutashirikiana kwa pamoja katika kuujenga mwili wa Kristo.

 8. 11
  Njiru Says:

  Bwana akubariki sana mtumishi

 9. 12
  lusajo Says:

  Mungu azidi kukutia nguvu ktk huduma yako itende kazi kazi sawa sawa na mapenzi yake. Ukizidi kuinena siri ya Kristo watu waijue kweli ya kristo

 10. 14
  Flano Says:

  Bwana Yesu apewe sifa Mtumishi wa Mungu Patrick Sanga, nimefurahi kutembelea huduma yako kupitia mtandao. mimi nahitaji kuwasiliana nawe maana nimejaribu kuangalia sijaona mahali popote pana contacts zako. email yangu ni flein47@yahoo.com na simu yangu 0754 991 279. ubarikiwe na Bwana Yesu

  • 15
   sanga Says:

   Amina ndg. Flano, mawasiliano yangu yanapatikana kwenye page ya ‘Patrick’ kwenye blog yangu juu kabisa kushoto, bonyeza link hii kuingia link husika https://sanga.wordpress.com/about/. Muda mzuri kwangu kuwasiliana kwa simu ni kuanzia Saa moja usiku na kwa email ni wakati wowote, Karibu.

 11. 16
  Godbless msuya Says:

  Nimebarikiwa na kujifunza kupitia huduma yako Mungu akubariki

 12. 17
  Elia Says:

  Salama kaka, tupo pamoja na ubarikiwe kwa kazi ya Mungu

 13. 18
  suma Says:

  Bwana Yesu asifiwe….Naomba mniweke katika maombi ili niweze kufaulu katika mitihan ya CPA ambayo nimeifanya mwezi november 2015


RSS Feed for this entry

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: