About Us

Patrick Sanga ni Mwalimu wa neno la Mungu na mwandishi wa vitabu na masomo mbalimbali ya Biblia. Mungu amemtia mafuta ili ‘kuinua misingi ya vizazi vingi… (Isaya 58:12) ’ kwa njia ya maombezi na mafundisho ya kweli ya Neno la Mungu.

Kwa zaidi ya miaka kumi na tano (15), Patrick amekuwa akitumika na kufanya huduma katika taasisi mbalimbali za vyuo, makanisa, vikundi vya kiroho nk. Huduma hii ya kuandaa masomo na kuweka kwenye mtandao ameanza rasmi Septemba 2006 na mpaka sasa ameshaandaa zaidi ya masomo mia moja na hamsini (150) ambayo yamekuwa yakifanyika baraka, majibu na uponyaji kwa makundi mbalimbali ya watu ndani na nje ya nchi pia.

Patrick alifunga ndoa na Bi. Flora Mwakalago, Desemba 06, 2009 katika kanisa la EAG (T) Sinza Dar es Salaam, Mungu amewabariki na sasa wana watoto wawili.

Karibu uweze kujifunza mengi kupitia blogu hii, ushauri, maoni na maombi yako ni muhimu sana juu yake na huduma hii pia. Kwa kadri uwezavyo wape na wengine anuani ya blogu hii ili waweze kujifunza na kupokea majibu yao toka kwa Bwana Yesu na pia kupata maarifa yatakayowasaidia katika maisha yao, maana imeandikwa “apendaye mafundisho hupenda maarifa”.

Unaweza kuwasiliana naye kwa njia zifuatazo;

Patrick S. Sanga

Email: paxifari@gmail.com

Blog: www.sanga.wordpress.com

 

Utukufu na heshima vina wewe Yesu, Unastahili Bwana.

          

 

 

103 comments

  1. Man of God,
    Mungu aliyekuita atasimama na wewe mpaka kusudi lake litimie, no one will come in between.
    Mimi nakuombea kila la mafanikio katika kazi Bwana aliyokupa.

    Ubarikiwe sana!

    Like

  2. I`m Blessed with ur ministry may the Lord Jesus bless u man of God. Continue with that spirit of making other know God.

    Like

  3. Patrick!!!!! siwezi kusema kwamba siamini ila naamini kataika Bwana aliyekuinua!Mungu akutie nguvu my young brother!unafanya kitu cha maana sana!!lazima uje kuwa Mwakasege wa kesho!
    its me M.Mayeye,unakumbuka wakati tunaishi Lugoda-mufindi? sikutegemea kama leo ungekuwa hivi!aiseee stay blessed Patrick.

    Like

    • Atukuzwe Mungu dadangu yeye ambaye alitujua tungali katika matumbo ya mama zetu na kutuwekea kusudi lake katika maisha haya. Nimebarikiwa pia kupata comment yako, hakika nakumbuka namna tulivyoishi kule Iringa – Lugoda. Maombi yako ni muhimu sana katika huduma hii.

      Like

  4. nimebarikiwa sana na unachofanyanya mtumishi wa MUNGU,,BWANA AZIDI KUINUA MAONO YAKO HADI KUFIKIA UTIMILIFU WA HUDUMA YAKO,,,KUMBUKA KITU KIMOJA USIKATE TAMAA KWA HALI YEYOTE ITAKAYOTOKEA MBELE YAKO SABABU MUNGU ANAKUPELEKA UMBALI MREFU SANA KATIKA UTUMISHI WAKO,AMEN

    Like

  5. Hosanna! Really you are much Blessed, and Isaiah 58 is my favorite, browsing through your prayer section I came across Jeremiah 32: 27….. has been my standing pillar for all my prayers … that our God is really big and creator of all, there is nothing impossible to Him, and it is being shown by many blogs I came across being solely for glorifying Him alone. Its my first time to come here, I saw it while browsing through StrictlyGospel. Stay blessed and keep it up.

    Like

  6. Thanks ,nimepata mafunzo mazuri kupitia hii glob,hopping nitaendelea kujifunza kwa kupitia hii glob.BWANA AWALINDE

    Like

  7. Bwana Yesu asifiwe kaka Patrick,
    Mungu akubariki sana kwa mchango wako mkubwa sana kwa vijana kwa hii website yako iliyojaa mafundisho mazuri yenye kutia moyo na kuponya.
    Mungu akutie nguvu uzidi kuendelea mbele na hii huduma kwa njia hii ya mtandao.

    Ruth Peter

    Like

  8. Praise Jesus Patrick and Flora. God has given you this inspiration to serve the world through his name.
    I have had been seeing your work since we were at the collage.May my almighty God bless you abundantly.

    Say hi to your wife flora.
    Am still looking to God to give ma wife. Your teachings has moved me several steps foward.

    ephraem P

    Like

    • It is nice and a blessing to hear from you brother, we are doing fine by God’s grace. It is our prayer that our redeemer who lives will be with you in this journey of seeking your partner and wife.

      Like

      • Thanx bro for your concern. It is my prayer that the ministry you have should be kept in moving foward. We all believe that its God’s purpose to utilize u in these focuses.

        Like

  9. Bwana Yesu apewe sifa, hongera sana kwa glob nzuri sana, Mungu akubariki, ni kazi nzuri na kubwa sana lakini kwa nguvu za Mungu umeifanikisha kwa kiwango kikubwa sana. Mungu akubariki sana. Azidi kukubariki katika kazi hii nzuri, nimebarikiwa sana.

    Like

  10. Nimebarikiwa na hiyo mana. kwa kuipata blog yako najua hakika Mungu ana makusudi na maisha yangu niombee niweze kufika

    Like

  11. Hongera bwana Patrick kwa kuanzisha huduma hii ambayo ni wachache wamesubutu kuifanya kwa manufaa ya waliowengi. Tunakula na kunywa toka mezani pako. Keep the momentum.

    Like

  12. Shaloom Mtumishi, Hongera sana kwa kazi ya Mungu unayoifanya, nakumbuka ulivyokuwa ukituongoza katika fellowship ya CBE Dar. Mungu akubariki kwa Blog hii na kazi mbalimbali uzifanyazo.

    Like

    • Thanks Victor, nimefurahi zaidi kujua kwamba na wewe unarun blog ya Hosanna Inc, namtukuza Mungu kwa kile ambacho anakifanya kupitia wewe pia, big up, don’t give give up. Glory to God.

      Like

  13. Mpendwa mtumishi wa Mungu kazi yako ni njema. Songa mbele ng’ang’ana na upako huo ili uendelee kupokea kutoka kwa Bwana kila breaking news za mbingu ili tupone.

    Like

  14. Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu Kazi unayoifanya sio bure ipo siku utalipwa.Mungu akuwezeshe

    Like

  15. Bwn YESU asifiwe mtumishi.. Tar 13 jan 2007 nilinunua kitabu chako cha njia kumi za kibiblia zitakazo kusaidia kumjua na kumpata mwenzi wako katika maisha, wakati ule nilikuwa na umri wa miaka 30 cha ajabu sikukifuatilia na wala sikuwa na haja na mwenza. But miezi michache iliyopita nimekuwa na kiu ya kuwa na mwenzi wa maisha,na leo nimekipitia kitabu hiki kwakweli nimeelewa sana,najilaumu kwanini sikuchukua hatua mapema. Nimeelewa kuwa kwa Mungu kila jambo lina wakati wake, na wakati wa mimi kuwa na mwenza umefika na MUNGU ataniwezesha,but hofu ni kuwa nimechelewa na tayari nina mtoto wa kiume wa miaka 2 na nusu nampenda sana sitaki kutenganishwa naye kwa namna yoyote ile. Nimeokoka na jinsia yangu ni ke.

    Like

  16. Ninasema ahsante, kaka yangu Patrick kwa huduma hii. Leo hii nimeelimisha wengi kupitia blog hii. Nimekuwa ninaprinti masomo na kuwapatia wengine ambao naamini kuwa wakisoma wataelewa zaidi kuliko kuwaelezea. Kaka yangu endelea kutulisha neno la Mungu. Ubarikiwe sana, tunakufunika kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nzarethi aliye HAI. Siku zote za maisha yako katika huduma hii.

    mariam.

    Like

    • Hello dada Mariam ahsante sana kunitia moyo katika huduma hii, nami kwa neema ya Mungu sitaacha kwa kuwa uandishi ni kitu Mungu mwenyewe ameweka ndani yangu. Ubarikiwe sana kwa huduma uifanyayo ya ku print masomo haya na kuwapa wengine yawasaidie, huduma yako ni njema, Bwana Mungu akukumbuke katika mahitaji yako.

      Like

  17. Bwana Yesu asifiwe!Namshukuru sana Roho Mtakatifu kuniongoza kwenye hii blog leo yani sikuifahamu.Nimeipenda mno na nitafuata mafundisho humu.Nimemshangaa sana Mungu jinsi anavyotuinua vijana kumtumikia.Patrick na mke wako,Mungu awabariki.Kweli Roho wa Bwana yu nanyi maana hata ufundishaji wenu ni mzuri sana.Endeleeni kumtumikia Bwana kwa njia hii ambayo ameichagua.Mimi ni mama wa watoto watatu,ni mpiga keyboard mzuri sana maana nilifundishwa na naendelea kufundishwa na Roho Mtakatifu mwenyewe.Pia kuna huduma ambayo nitaiweka wazi baada ya YEYE kuniwekea wazi zaidi nitaisema.Ila ipo inakuja.Mbarikiwe mno.Nimewapenda,mmeni-impress sana.

    Like

    • Amina, ahsante dada Margareth kwa ujembe wako wenye kututia moyo, tutaendelea bila kukata tama, hongera kwa kujua kupiga kinanda, nami pia binafsi natamani kujifunza naamini Mungu atanipa nafasi ya kujifunza pia.

      Like

  18. Bwana asifiwe mtumishio wa kristo,kwanza na mshukuru mungu kwa kukutumia kuwafikia watu wake,kwa habari ya injili,mm nilikua na omba ushuuda wako na historia yako ya maisha ya wokovu toka sikuulipo mpokea YESU KRISTO.

    Like

  19. Mara ya kwanza nilipopewa blogu hii, niliposoma mistari kadhaa na kuangalia masomo yake, hakika nilikubali kuwa ni blogu bora kabisa na mwandishi wake ameitwa kazini. Nikaisambaza haraka kwa rafiki zangu ili wanufaike na riziki hii.

    BWANA AKUBARIKI SANA

    Like

    • Ahsante kwa huduma yako njema, naam maadam ni – mchana na tuifanye kazi yake, kumbuka MAVUNO ni mengi lakini watenda kazi ni wachahce. Sharti wachache walioitwa wawe serious na kazi ya BWANA wakati wengine wanaendelea kujairiwa.

      Like

  20. mungu akubariki mtumishi kwani umefanyika baraka katika maisha yangu kama kijana! mimi ni mwanafunzi wa kidato cha sita tanga school! huwa napenda sana masomo yako natamani kuwa kama wewe kwani nimetumia masomo yako kufundishia wengne na wamekua wakifunguliwa na kupokea miujiza, hold my hands please!

    Like

    • Utukufu kwa Mungu, barikiwa pia, Moses. Naam BWANA akuongoze kuwa vile alivyokusudia yeye katika maisha yako. Tukazane kufanya kazi yake maadam ni mchana.

      Like

  21. BWANA YESU ASIFIWE HABARI YA UZIMA MTUMISHI WA MUNGU ALIE HAI POLE NA MAJUKUMU YA KULIFUNDISHA NENO LA MUNGU NINA SWALI KUHUSU UTOAJI WA ZAKA. SEHEMU GANI UNAWEZA KUTOLEA ZAKA? ubarikiwee na YESU

    Like

  22. MAFUNDISHO YAKO KUHUSU NDOA NI. MAZURI SANA HASA. KWA. WANAWAKE. SHETANI. ANAPENDA SANA KUSHAMBULIA NDOA. ZA. WAKRISTO. MAKANISA MENGI. HAYANA. TABIA ZA. KUTOA. ELIMU KWA WAUMINI. WAO

    Like

  23. (hosea 4:6) Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
    Kuangamia kwetu ni kwasababu tumekataa maarifa,Mungu atunusuru tugeuke na kuyapenda maarifa ili tusiendelee kuangamia maana siyo mpango Mungu sisi kuangamia……

    MUNGU AKUBARIKI SANA MZEE NA MLEZI WANGU…..MUNGU AZIDI KUKUTUMIA KAMA APENDAVYO

    Like

  24. Daaah sina la kusema ila yote zaidi ya yote, Mungu wangu wa mbingu na nchi na azidi kuwa nawe na kukutumia zaidi kwa ajili yetu vijana. Mungu akubariki sana

    Like

  25. Ubarikiwe Mtumishi, nimefurahia masomo yako….”Namna ya Kusikia Suti ya Mungu”…Mungu azidi kukubariki na kukufunulia zaidi kwenye mada na zile za kuwalenga Vijana maana wana changamoto nyingi kwa sasa.

    Like

Leave a comment