ONGEZA UFAHAMU WAKO KUHUSU NDOTO KAMA NJIA YA KUKUSAIDIA KUFANYA MAAMUZI (Sehemu ya 2)

Na: Patrick Sanga

2

Mada: Mambo muhimu ya kujua kuhusu ndoto kama njia ambayo Mungu anatumia kusema na wanadamu

Katika sehemu ya kwanza tualiangalia maandiko kadhaa yanavyozungumza kuhusu ndoto. Ili kusoma sehemu ya kwanza tafadhali bonyeza ‘link’ hii https://sanga.wordpress.com/2018/02/17/ongeza-ufahamu-wako-kuhusu-ndoto-kama-njia-ya-kukusaidia-kufanya-maamuzi-sehemu-ya-1/ Katika sehemu hii ya pili tutaangalia baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kujua kuhusu ndoto, naam karibu sasa tuendelee…

(a) Sio kila ndoto inatoka kwa Mungu – Licha ya kwamba ndoto ni njia muhimu ambayo Mungu anatumia kusema na wanadamu, si ndoto zote zinatoka kwa Mungu. Biblia inatuonyesha wastani wa vyanzo vitatu vya ndoto ambavyo ni Mungu, Shetani au Mtu mwenyewe. Katika Ayubu 33:14 imeandikwa ‘Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika NDOTO, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani’. Kupitia andiko hili tunaona kwamba Mungu ndiye chanzo.

c

Yeremia 29:8 imeandikwa Maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Manabii walio kati yenu, na wabashiri wenu, WASIWADANGANYE ninyi, wala msisikilize NDOTO ZENU, MNAZOOTESHA’. Pia Zekaria 10:2 imeandikwa Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi WAMEONA UONGO; nao wameleta habari za NDOTO ZA UONGO, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji’.

Kumbuka Shetani ndiye baba wa uongo (Yohana 8:44, 1 Yohana 4:1), ile kusema wameona uongo ina maana kuna aliyezileta hizo ndoto za uongo ni Shetani, naam wameona uongo wakaleta habari za uongo. Ndiyo maana Mungu anaagiza watu watu wake wasikubali kudanganywa na wala wasisikilize ndoto za manabii hao kwa sababu ni za uongo na kwa maana hiyo chanzo chake si Shetani. Hii ina maana kwamba mtu au watumishi wengine wanaweza wakaota na kutumia ndoto hiyo kukupoteza na kukuondoa kwenye mapenzi ya Mungu.

Muhubiri 5:3 imeandikwa Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno’. Hii ni kutonyesha kwamba mwanadamu kupitia wingi wa shughuli zake ni chanzo kingine kikubwa cha ndoto na hivyo ziko ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe.

Maandiko haya yanatufanya tujue kwamba sio ndoto zote zinazotoka kwa Mungu na hivyo uko umuhimu wa kuwa na ufahamu kuhusu masuala ya ndoto ili ujue kuzitofautisha. Hata leo tunao waamini wengi ambao wamekuwa wepesi sana kushirikisha watu au watumishi mbalimbali ndoto wanazoota bila kuongozwa na Mungu. Biblia inatutahadharisha tuwe makini katika hili, maana sio wote wanasikia kutoka kwa Mungu wa kweli.

2

Ndio, nakushauri usiwe mwepesi sana kuuliza wengine kwa habari ya ndoto ulizoota bali zaidi uwe mwepesi kuuliza kwa Mungu maana ndiye awezaye kukupa tafsiri sahihi. Sina maana hatupaswi kuwashirikisha watumishi ndoto tuotazo, la hasha, bali nakushauri shirikisha wale ambao unajua nao watauliza kwa Mungu na si kutegemea uzoefu au mazoea maana wanaweza kukupoteza kwa kukupa tafsiri tofauti na ile ambayo Mungu alikusudia anapokuletea ndoto husika.

(b) Mungu pekee ndiye mwenye kutupa tafsiri sahihi za ndoto – Mwanzo 40:8 imeandikwa ‘Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, KUFASIRI SI KAZI YA MUNGU? Tafadhalini mniambie’. Pia Danieli 2:26-28 imeandikwa ‘Mfalme akajibu, akamwambia Danielii, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake. Danielii akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu; lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi’.

 Maandiko haya yanatufanya tujue kwamba kufasiri ndoto ni kazi ya Mungu na si ya mwanadamu. Hivyo basi pale unapomshirikisha mwanadamu iwe ni kwa lengo la yeye kukusaidia kuuliza kwa Mungu tafsiri sahihi ya hiyo ndoto na si kwenda kwake kana kwamba yeye ndiye mwenye tafsiri ya hizo ndoto, utakosea sana na ndio maana wengi leo wameishia pabaya, kwani walipewa tafsiri za ndoto ambazo si za kweli na hivyo wakapotea.

Naam usishau kwamba zipo ndoto zinazoletwa na Shetani na kwa maana hiyo zipo pia tafsiri za kipepo. Kama una mazoea ya kuuliza watu bila kumshirikisha Mungu nani wa kumuuliza, Shetani anaweza kukuletea ndoto na akakuunganisha na mtu wa ufalme wake ambaye atakupa pia tafsiri ya kipepo na hivyo kukupoteza zaidi (asomaye na afahamu).

Binafsi nimejifunza kwamba hakuna uzoefu katika kutafsiri ndoto, kwa kuwa kila ndoto inakuja na ujumbe wake unaojitegemea, hivyo ili kupata tafsiri sahihi ya ndoto mtu anahitaji kumshirikisha au kuuliza kwa Mungu. Jambo muhimu ni kwamba  ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu ndio msingi muhimu wa kumuongoza mtu kupata tafsiri sahihi za ndoto mbalimbali anazoziota au zile ambazo wengine wanaziota (Daniel 2:26-28).

(c) Lazima uombe kila baada ya kuota ndoto – Kumbuka nilikuambia kwamba si kila ndoto zinatoka kwa Mungu, lakini hata hivyo si kila ndoto mbaya inatoka kwa Shetani, kuna nyingine Mungu anazileta kwako ili kukufanya ujue ufalme wa giza una mikakati gani dhidi yako, wale wanaokuhusu au mali, mji, taifa nk.

6

Hivyo basi kwa sababu ndoto zinabeba ujumbe na kuna vitu zinaachilia ni muhimu sana kila baada ya kushtuka au kuamka uombe kwa maana ya kupinga au kukemea endapo umeota ndoto mbaya na pia kuruhusu mazuri uliyoyaona ndotoni ili yatokee au yawe dhahiri kwenye maisha yako.

(d) Jifunze kutilia maanani kila ndoto unayoota – Katika Isaya 42:20 imeandikwa Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii’. Watu wengi Mungu amekuwa askisema nao kwa njia ya ndoto, naam wao ama kwa kutokujua au kutojali wamekuwa wakshindwa kuzitilia maanani ndoto wanazoota na hivyo wanajikuta kwenye matatizo.

Jifunze kuheshimu ndoto wala usizipuuze, kwani ndoto ni sauti na maonyo ya kukusaidia kufanya maamuzi na kuishi sawaswa na mapenzi ya Mungu duniani. Mungu anapokuletea ndoto uwe na uhaika amekupa wajibu wa kufanya, nikimaanisha wajibu wa kuwa makini kufauatilia kile ulichokiona na kuuliza uliza kwake maana yake nini ili uweze kuyajua na kuyatenda mapenzi yake, naam wajibu wa kufanya ambao unahitaji muda wako wa utulivu.

3

Kwa nini utilie maanani kila ndoto? – hii ni kwa sababu ndani ya kila ndoto kutoka kwa Mungu kuna ujumbe umebebwa.  Ndio kila ndoto kutoka kwa Mungu inakupa taarifa ya nini cha kusema, kufanya au uamuzi wa kuchukua kwa maana hiyo. Mfano: Katika ndoto ukiona unaongea, unafanya jambo fulani au unachukua uamuzi fulani nk maana yake Mungu anakuonyesha nini cha kusema, kufanya au kuomba punde utakapoamka  kutoka usingizini.

 Jambo la msingi ni lazima mtu ajifunze kutafsiri ndoto anayoiota kama sauti ya Mungu kwa kuwa ndani ya ndoto kuna ujumbe. Kuwa na ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu ndio msingi muhimu wa kuelewa na kufasiri ndoto unazoota.

 Somo litaendelea …

Utukufu na heshima, vina wewe Yesu wastahili BWANA wangu.

Advertisements

2 comments

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s