UMEJIAANDAAJE KWA TUKIO LA UNYAKUO? (Sehemu ya 7)

Na: Patrick Sanga

Mada: MAENEO YA MSINGI KATIKA KUJIANDAA

Eneo la nne – Usiipende dunia wala kuifuatisha namna ya dunia hii (Sehemu ya 2)

Katika sehemu ya sita ya somo hili tulianza kuangalia sehemu ya kwanza ya eneo la nne ambalo ni ‘Usiipende dunia wala kuifuatisha namna ya dunia hii’. Ili kusoma sehemu husika bonyeza link ifuatayo https://sanga.wordpress.com/2017/11/04/umejiaandaaje-kwa-tukio-la-unyakuo-part-6/  Katika sehemu hii ya saba nitamalizia sehemu ya pili ya eneo hili la nne. Fuatana nami tuendelee…

 Biblia katika 1 Yohana 2: 15-16 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia’.

Tamaa ya mwili – tamaa ya mwili ni roho inayofanya kazi kupitia mwili wa mtu ambapo kazi yake ni kuhakikisha matakwa au matendo ya mwili yanatimizwa na hivyo kumfanya mtu ashindwe kumpendeza Mungu kwa kuwa nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, na tena mauti (Warumi 8:6-8, Wagalatia 5:19-22). Daima Shetani hupandikiza fikra za tamaa ya mwili kutokea kwenye uhitaji wa mtu. Hizi ni fikra anazoziachilia kwenye ufahamu wa mtu kumuonyesha kwamba tatizo lako linaweza kutatuliwa kwa njia nyingine, huku yeye Shetani akijua kwa njia hiyo atakuwa amemwondoa mtu kwenye mapenzi ya Mungu (Rejea Mwanzo 3:1-6).

Tamaa ya macho – hii ni roho inayofanya kazi kwa nguvu kupitia macho ya mtu, roho hii humwonyesha mtu husika uzuri wa dunia hii, yaani kila kilichomo ndani yake na hivyo kuuvuta na kuuondoa moyo wa mtu katika kumpenda Mungu na kuuelekeza moyo wake, nguvu zake, akili zake na roho yake kuipenda dunia na si Mungu. Shetani hupitia kwenye macho ya mtu kukuonyesha uzuri wa vile alivyonavyo ambavyo ndani yake vimejaa uharibifu (2 Samweli 11:1-4).

Kiburi cha uzima – hii ni roho ambayo inaachilia ndani ya mtu mawazo ya uharibifu kwamba yeye ni kila kitu na anao uwezo wa kufanya jambo lolote kwa hoja kwamba vipo katika uwezo wake na zaidi Mungu mwenyewe anaridhia au ataridhia. Mtu mwenye kuipenda dunia, Shetani kupitia kiburi cha uzima atapandikiza fikra za uharibifu ndani ya mtu husika. Ndio adui hutanguliza sifa, kupandikiza ndani ya mtu kiburi au majivuno, pale mtu anapokuwa katika kilele cha sifa, ndipo atamletea na wazo la kumwambia ‘jitupe chini’,i.e ulipofikia ‘you can do or say anything’ maana hakuna kama wewe, even God will support you (Mwanzo 3:1-6).

Rejea ya Mathayo 24:39 inatufanya tujiulize kwa nini watu wa kipindi cha Nuhu hawakutambua hata wakamezwa na gharika?. Jibu ni kwa sababu waliipenda sana dunia na hivyo wakapuuza wito wa maandalizi waliopewa. Naam hawakujua kwamba kuipenda dunia kunampa Shetani uhalali wa kupofusha macho yao na kugeuza fahamu zao wasipokee maonyo ya Bwana wala kuelewa na kuyatenda mapenzi ya Mungu kwenye maisha yao. Mtu mwenye kupenda au kuifuatisha namna ya dunia hii anakuwa amefungua mlango au ametoa nafasi kwa roho husika kutawala na kuongoza maisha yake.

Mpenzi msomaji, kuipenda dunia kutakufanya ukose sifa za kunyakuliwa Bwana Yesu atakapokuja kulichukua kanisa lake, usisahahu imeandikwa kwamba mtu akiipenda dunia kumpenda Baba hakumo ndani na hii ni kwa sababu vilivyomo duniani vimetengenezwa kwa namna ambayo vinaharibu uhususiano wa mtu na Mungu kwa yule ambaye anavitumia au kuvipenda.

Mpenzi msomaji, tambua kwamba kadri mtu anavyoipenda na kuifuatisha namna ya dunia hii ndivyo kwa mawazo, maneno na matendo yake anavyotengeneza uadui kati yake na Mungu. Kumbuka kwamba Shetani ndiye mungu wa dunia hii, na maandiko yanathibitisha kwamba mwivi haji ila aibe, na kuchinja na kuharibu (Yohana 10:9a), hivyo uwe na uhakika chochote anachokiachilia kwenye dunia hii ndani yake kimelenga kuiba, kuchinja na kuharibu maisha ya mtu (asomaye na fahamu).

Mpenzi msomaji, jiupeshe kuipenda dunia ili usivutwe na nguvu ya uharibifu kupitia tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima ili wakati wowote Bwana Yesu ajapo tuwe tayari kwenda naye, maana dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Wito wangu kwako – Mpenzi msomaji, nimeandika kwa kirefu na ninatumia muda mwingi sana kuandaa masomo haya kwani Machi 2010, BWANA aliniuliza umejiandaaje kwa tukio la unyakuo na kisha akaniuliza umewaandaaje watu wangu kwa tukio la unyakuo? Naam licha ya mimi binafsi kujiandaa na kutunza vazi langu, swali la pili ndilo linalonifanya niandike na kuandika na kuandika masomo haya bila kuacha licha ya vikwazo vingi.

Nakusihi usipuuze jumbe za aina hii kama watu wa kipindi cha Nuhu walivyofanya na hata wengine wafanyavyo hata sasa, bali wewe, mwambie Roho Mtakatifu yakague maisha yangu na endapo ndani yangu kuna jambo lolote ambalo unajua ni kikwazo cha mimi kumuona Baba (Mungu), endapo nikifa au akija kuchukua kanisa (unyakuo) nikali hai, naomba nisaidie kutengeneza maadam ni mchana, naam wakati nuru ingalipo (asomaye na fahamu)

Hakika ipo siku nayo imekaribia ambayo Bwana Yesu atakuja kulichukua kanisa lake maana neno lake ni amina na kweli. Hivyo basi, kanisa, hatuna muda wa kulala au kujisahau kiroho, wala hatupaswi kwa namna yoyote kurudia au kufanya makosa kama ya watu wa kipindi cha Nuhu, bali tunatakiwa kujiandaa kwa ajili ya ujio wa Yesu (1Wathesalonike 5:4-11)

Kumbuka hapa duniani siyo kwetu, na tena hatujui siku wala saa, basi na tudumu kutunza vazi letu la wokovu maana imeandikwa ‘Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake’ na tena imeandikwa Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo’ (Ufunuo wa Yohana 22:14, 21:27).

Utukufu na Heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA wangu.

 

Advertisements

4 comments

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s