NAMNA UNAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI YA MLINZI KWENYE ULIMWENGU WA ROHO KUFANYA MAOMBI YENYE MATOKEO MAZURI (Sehemu ya 3)

Na: Patrick Sanga

Mada: Mambo muhimu kujua na kuzingatia kwa Mlinzi ili maombi yake yawe na mafanikio.

Katika sehemu ya pili tulijifunza jambo la kwanza ambalo ni ‘kuutunza utakatifu wako’. Ili kusoma sehemu ya kwanza bonyeza ‘link’ ifuatayo https://sanga.wordpress.com/2017/08/05/namna-unavyoweza-kutumia-nafasi-ya-mlinzi-kwenye-ulimwengu-wa-roho-kufanya-maombi-yenye-matokeo-mazuri-sehemu-ya-2/ . Naam fuatana nami tuendelee…

Jambo la pili – Jifunze kumuuliza Mungu kuhusu unachotaka kukiombea kabla hujakiombea (Isaya 26:16, Ezra 8:21)

Katika Yeremia 7:16 imeandikwa ‘Basi, wewe usiwaombee watu hawa, wala usiwapazie sauti yako, wala kuwaombea dua, wala usinisihi kwa ajili yao; kwa maana sitakusikiliza’. Pia Yeremia inasema 15:1 ‘Ndipo Bwana akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao’. Na mwisho kwenye Yohana 9:31 imeandikwa ‘Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo’.

Kabla sijafafanua nikuulize swali, je wewe kama Mlinzi unaona nini kwenye maandiko hayo hapo juu? Naam ni muhimu ufahamu:

 • Mlinzi ni lazima ajue kwamba sio kila maombi yanasikilizwa na pili si kila hitaji la watu wa eneo lake ni la kuliombea sawasawa na matakwa yao.
 • Mlinzi lazima ajue kwamba kwa kila jambo linalotokea na litakalotokea yapo mawazo au mapenzi ya Mungu juu ya jambo hilo, ambayo ni tofauti na mawazo ya waadamu na ufalme wa giza.
 • Mlinzi ni lazima ajue kwamba kila jambo (liwe zuri au baya) linalotokea, halijatokea kwa bahati mbaya, bali limekusudiwa na ipo sababu ya kutokea lilivyotokea.

Hebu taungalie mfano mmoja ndani ya Biblia wa kuhani aliyeitwa Eli pamoja na wanawe,makuhani, Hofni na Finehasi (1Samweli 2:12-29). Ukisoma fungu hilo hapo juu utaona dhambi mbaya sana ambazo zilifanywa na makuhani hawa mbele za Mungu na wala hawakuzitubia na ndipo Mungu akatoa adhabu na laana akisema … Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.

Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako HATAKUWAKO MZEE. Nawe utalitazama teso la maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hatakuwako mzee milele. Tena mtu wa kwako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa KUKUPOFUSHA MACHO, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako WATAKUFA WAPATAPO KUWA WATU WAZIMA.

Na hii ndiyo ishara itakayokuwa kwako, itakayowapata wana wako wawili, Hofni na Finehasi; WATAKUFA wote wawili katika siku moja. Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele. Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, APATE kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali unitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, NIPATE KULA kipande kidogo cha mkate’(1Samweli 2:30-36).

Je umeona maamuzi ya Mungu kufuatia uasi wa makuhani hawa? Kwa kifupi Mungu aliondoa ukuhani kwa kabila ya Lawi, pili alitamka kifo juu ya watoto wa Eli, tatu aliweka kikomo cha umri kwenye kabila yake na nne alieleza kwamba watakaosalia wataukuwa ombaomba.

Sasa fikiri hivi, wanakuja kwako watu wa uzao Eli waliosalia wanataka uwaombee juu ya changamoto walizonazo kwenye familia yao bila wewe kujua laana alizoziamuru Mungu juu ya familia hiyo? Kwa vyovyote vile utaungana katika kuwaombea yumkini hata kwa kufunga, je unafikiri maombi yako juu yao yatakuwa na matokeo lengwa? Kwa vovyote vile hapana maana huwezi kuwaombea wawe wazee kwani Mungu alishaweka mpaka, huwezi kuwaombea waendelee kuwa mahukahini wakati Mungu amewakataa nk.

Sasa changamoto za aina hii ndizo zinazopelekea kuona kwamba upo umuhimu wa kujifunza kumuuliza Mungu namna ya kuomba kabla hujaomba. Naam maombi yako hayawezi kufanikiwa juu yao kama hujauliza kwa Mungu chanzo cha hali waliyonayo? Kumbuka si kila mombi yanasikilizwa na si kila ombi ni la kuombea. Changamoto hii zinatufanya tuelewe kile ambacho Mzee Yohana alisema ‘Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia’ (1Yohana 5:14).

Kutokea kwenye mstari huo ndipo tunajifunza kwamba:

 • Mlinzi ni lazima ajifunze kufikiri kama Mlinzi kabla ya kuomba, huku fikra zake zikiongozwa na neno la Mungu. Naam ajiulize nini mawazo ya Mungu juu ya watu hawa au jambo hili kabla hajaomba (What is the mind of God on this matter).
 • Mlinzi ni lazima ajifunze kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu ili maombi yake yasikiwe. Hii ina maana kabla hujaombea jambo lolote ni lazima ujifunze kumuuliza Mungu juu ya nini uombee kuhusu jambo husika au uulize namna ya kuomba kuhusu jambo husika.
 • Mlinzi anahitaji kuwa na MUDA wa utulivu mbele za Bwana wa kuhoji kujua mapenzi ya Mungu kwenye maeneo mbalimbali anayotaka kuombea kabla hujayaombea, ndipo adumu kuomba sawasawa na ufunuo aliopokea (Ezra 8:21).

 Kufanikiwa kwa maombi ya mtu kunategemea muda ambao muombaji anautumia kuuliza kwa Mungu, mapenzi yake juu ya jambo analotaka kuliombea na si muda anaoutumia kuomba maombi ambayo ni nje ya mapenzi ya Mungu. Naam nidhamu ya kumuuliza Mungu itamfanya si tu aombe sawasawa na mapenzi ya Mungu bali zaidi awe na uhakika na kile anachokiombea maana anajua ni ufunuo alioupata kutoka kwa Mungu wake (2Samweli 12:14-19).

Ili kuomba kupata ufunuo wa nini cha kuombea au namna ya kuomba tumia maandiko yafuatayo kama mwongozo (Yeremia 33:3, 29:12-13). Mungu wetu anathamini sana MUDA mbao mtu anautenga kwa ajili yake, naam yeye ni Mungu na anajifunua kwenye utulivu, kama unataka kumuona tenga muda wa kuwa naye.

Tutaendelea na sehemu ya nne…

Utukufu na Heshima vina wewe Yesu Wastahili BWANA

Advertisements

7 comments

 1. UBARIKIWE SANA MTUMISHI WA MUNGU KWA MASOMO YAKO HAYA.

  NAMI NATAMANI NIWEZE KUFUNGUA BLOG NZURI YA NENO LA MUNGU KAMA YAKO ILA SIJAJUA TARATIBU ZA KUFUATA

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s