JIHADHARI USIANGUKE TENA ILI USITENGWE NA MUNGU

Na: Patrick & Bernada Sanga

1

Shalom, neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. Kwa mwanangu Bernada Sanga ambaye BWANA alipokuwa akinifundisha ujumbe huu alimtumia binti huyu na ndio maana ninatambua ushiriki wake katika kukamilisha ujumbe huu, naam fuatana nami tuendelee…

Katika waraka huu wa mwezi Septemba 2016 imenilazimu kuandika ujumbe huu muhimu ambao lengo lake ni (a) kuwasaidia viongozi kutimiza majukumu ya nafasi zao ipasavyo ili wasipatwe na anguko (kutengwa) na Mungu (b) kuwapa ufahamu wa kweli hii viongozi ili wasije wakarudia au kufanya makosa yatakayopelekea anguko lao kutokana na nafasi zao kwenye ulimwengu wa roho na mwili pia.

Katika ujumbe huu anguko lina maana ya kutengwa na kusudi la Mungu kunakosababishwa na mwanadamu kukosa utiifu. Naam, anayehusika kutenga ni Mungu mwenyewe kwa sababu ya uasi au kukosa utii kwa mwanadamu na hivyo kupelekea Mungu kuamua KUTOENDELEA tena na mtu huyo katika kulitekeleza kusudi lake hapa duniani.

Hebu na tuangalie mifano kadhaa kutoka kwenye Biblia kuhusu jambo hili:

 • Anguko la Adam (Mwanzo 3:9-24), mstari wa 23 unasema kwa hiyo Bwana Mungu AKAMTOA katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Kutoa hapa lina maana ya kumfukuza kutoka kwenye eneo ambalo kimsingi alikusudiwa kuwepo.
 • Anguko la Musa (Hesabu 20:2-12), ule mstari wa 12 unasema ‘Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, HAMTAWAINGIZA kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa’. Naam si tu kina Musa walitengwa na kusudi husika, bali pia walipoteza heshima ya kuwa sehemu ya utekelezaji wa kusudi la Mungu kamili.
 • Anguko la Sauli (1 Samweli 15:10-26, 16:1), naam ule mstari wa 26 unasema, Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la Bwana, BWANA NAYE AMEKUKATAA WEWE, USIWE MFALME WA ISRAELI. Na kisha Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi NIMEMKATAA asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe (1Samweli 16:1).
 • Anguko la familia ya Eli (1 Samweli 2:27-33), ule mstari wa 30 unasema ‘Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, JAMBO HILI NA LIWE MBALI NAMI; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu’.

3

MAMBO MUHIMU KUJUA YATAKAYOKUSAIDIA USIANGUKE NA HIVYO KUTENGWA NA KUSUDI LA MUNGU KAMA WALIOTUTANGULIA

 • Maelekezo mahususi (specific instrunctions) kutoka kwa Mungu ndiyo msingi wa mafanikio au anguko kwa mwamini (kiongozi). Maelekezo hayo hutolewa kwa kuzingatia nafasi aliyo nayo mtu katika ulimwengu wa roho na mwili pia. Na kwa maana hiyo anguko nalo linategemea nafasi aliyo nayo mtu katika ulimwengu wa roho na wa mwili pia.
 • Maagizo mahususi yamefungwa kwenye muda wa kila kusudi, hivyo kukosa utiifu ni kuchelewesha au kukwamisha kusudi hilo kwa muda ulioamriwa.
 • Maelekezo mahususi yameunganishwa na heshima au utukufu kwa Mungu. Yanapotekelezwa ipasavyo jina la Mungu linatukuzwa, yasipotekelewa ipasavyo yanatoa fursa kwa adui za Mungu kukufuru na jina lake kuchafuliwa (Hesabu 20:12, 1 Samweli 2:17, 29-30).
 • Hivyo Jifunze kuwa makini na maelekezo unayopewa na Mungu kwa kuzingatia nafasi yako na muda wa maelekezo hayo kutekelezwa.
 • Kutoka kwenye nafasi yako, jihadari usije ukafanya maamuzi au kuruhusu mazingira yatakayopelekea dharau kwenye jina la BWANA.

Kumbuka kwamba ishara mojawapo ya anguko ni kifo, naam kifo hapa ni kwa namna mbili, kifo cha kiroho ambacho kinazuia ufunuo wa Mungu uliokuwa ukileta maelekezo mahususi juu yako (1Samweli 3:1) na pili ni kifo cha kibinadamu kabisa  (1Samweli 2:34, 2Samweli 3:33).

3

Anguko lako si tu litakugharimu wewe binafsi bali zaidi huduma yako, familia yako na vizazi vijavyo, hivyo kuwa makini na maelekezo mahsusi yanayoendana na wito na nafasi yako, naam jihadhiri usianguke kwa kukosa utiifu ili usitengwe na Mungu na kupoteza heshima ambayo amekupa kupitia nafasi ulizonazo, heshima ya jina lake kutukuzwa hapa duniani kupitia wewe.

‘… Utaiinua misingi ya vizazi vingi’.

Utukufu na heshima vina wewe Yesu wastahili Bwana wangu.

 

Advertisements

6 comments

 1. Asante sana Mwl. Patrick kwa somo hili muhimu sana kwangu ambalo limenifikia kwa wakati. Naamini Mungu ameachilia ujumbe huu kwa watoto wake wote maana karibu kila mtoto wa Mungu ni kiongozi mahali alipo: kwenye familia, kazini, shuleni na mahali pengine popote anapohangaikia kupata maisha kwa namna yoyote ile iliyo halali mbele za Mungu. Ninaamini kila mtoto wa Mungu ana walau mtu mmoja kama si watu kadhaa ama kundi kubwa la watu la kuwaongoza ili waweze kuishi na kuenenda kwa namna ambayo kusudi la Mungu litafikiwa katikati yao. Mungu akubariki sana Mtumishi wa Mungu, azidi sana kukupaka mafuta yake ili uzidi kutupa maarifa yatakayotusaidia ili adui yetu shetani asituangamize.

  Watoto wa Mungu tunyenyekee kwa Roho Mtakatifu ili atusaidie pia kutii kwani wengi tunaangamizwa si kwa kuwa hatuna maarifa bali hata yale tunayoyapata kidogo kidogo kila iitwapo leo hatutii. Wakati mwingine watoto wa Mungu tumekuwa tunaogopa kuingia gharama ndogo ndogo za kutii na tumekuwa tayari aidha kwa kujua au kutokujua kupoteza faida kubwa ya kutii kile Mungu alichotuagiza kisha tena kutukumbusha kupitia watumishi wake. Somo hili lituamshe watoto wa Mungu, tuache kuenenda kwa ulegevu na mazoea bali sasa tuenende katika viwango vya Mungu. Mungu anatufundisha ili tupate faida hivyo tukatae hasara na tuchague faida kwa kuyafanyia kazi ipasavyo mafundisho haya.

  Like

 2. MUNGU wa Mbingu na nchi akubariki sana kwa ujumbe huu, it has transformed my thinking and my doing in general, it has brought cautious in my life. glorified be the Holy spirit who reveals this truth in you.
  I love you my Chairperson

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s