ONGEZA UFAHAMU WAKO KUHUSU NYAKATI ILI ZIKUSAIDIE KUFIKIRI KI-MUDA (Sehemu ya mwisho)

3 

Na: Patrick Sanga 

Waraka wa Januari 2014

Mada: Namna mtu anavyoweza kushirikiana na nyakati ambazo Mungu ameziweka mbele yake.

Katka sehemu ya pili ya ujumbe huu nilieleza jambo muhimu ambalo ni ‘kwa namna gani mwanadamu anapaswa kufikiri ki muda na matokeo yake’. Ili kusoma sehemu hii ya pili bonyeza hapa https://sanga.wordpress.com/2012/10/27/ongeza-ufahamu-wako-kuhusu-nyakati-ili-zikusaidie-kufikiri-ki-muda-sehemu-ya-pili/

Katika sehemu hii ya mwisho tutaangalia ni kwa namna mtu anavyoweza kushirikiana na nyakati ambazo Mungu anazileta kwenye maisha yake ili zimsaidie kufikiri na kutenda kila jambo kwa muda uliokubalika, maana imeandikwa “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu” (Muhubiri 3:1).

Naam kumbuka lengo la ujumbe huu ni kukusaidia kuongeza ufahamu wako kuhusu nyakati ili zikusaidie kufikiri na kutenda ki – muda.  Biblia katika Mwanzo 18:14 inasema “Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume”.

Je umeshawahi kufikiri kwa nini ilibidi Mungu aweke wazi muda wa Sara kumzalia Ibrahimu mtoto? Mungu alitaka Ibrahimu atumie taarifa aliyopewa si tu kuifunga/kuiweka imani yake kwenye ahadi aliyopewa bali zaidi kupata alichokitarajia ndani ya muda maalum aliosema Mungu juu yao. Hivyo ni muhimu ujifunze kukishikilia kwa imani na mombi kile ambacho Mungu amekusudia kukitenda juu yako kwa nyakati husika.

Ukisoma msatri huu wa Mwanzo 18:14 katika toleo la ESV la kiingereza unasema “Is anything too hard for the LORD? At the appointed time I will return to you, about this time next year, and Sarah shall have a son.” Umeona neno hili “appointed time” naam ni lazima ujue kwamba kwenye kila jambo linalopaswa kufanyika kufuatana na kusudi lako hapa duniani kuna ‘appointed time”.

Kumbuka appointed time yako katika mambo mbalimbali ni tofauti kabisa na ile ya watu wengine. Hivyo kadri unavyokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu nyakati na kushirikiana nazo ndivyo unavyoweka mazingira ya kuhakikisha appointed time yako inakuwa halisi kwa kuzaa kilichotarajiwa.  Hivyo ni muhimu sana si tu uwe na ufahamu wa kutosha wa nyakati bali zaidi sana ujue namna ya kushirikiana na hizo nyakati maishani mwako.

Tujifunze kutoka kwa Lea mkewe Yakobo

Katika Mwanzo 29:31 Biblia inasema ‘Lea akapata mimba, akazaa mwana, akampa jina lake Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona teso langu; sasa Mungu wangu atanipenda’

Wewe kama ni msomaji wa Biblia utagundua kwamba haikuwa mapenzi ya Yakobo kumuoa Lea bali Raheli. Na kwa sababu hiyo upendo wa Yakobo kwa Lea haukuwa mkubwa sana (Mwanzo 29:30). Maandiko yanasema BWANA Mwenyewe akaona kwamba Lea hakupendwa ndipo akalifungua tumbo la Lea akaanza kuzaa watoto.

Naam Lea alijua na alimaanisha kwamba hata kama mume wangu alikuwa na sababu ya kutonipenda, kitendo cha Mungu kufungua tumbo langu na kuzaliwa kwa Reubeni ni appointed time ya kwangu ambayo inazaa upendo wa mume wangu kwangu. Naam jambo la msingi ilikuwa si kuzaliwa Reubeni bali ilikuwa ni kile ambacho Ruebeni anakileta yaani kuzaliwa kwa upendo kwenye ndoa ya Lea na Yakobo.

Tujifunze kutoka kwa wana wa Israeli

Hesabu 9:22 – 23 inasema ‘Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka wana wa Israeli walikaa katika kambi yao wasisafiri’. Bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; wakayalinda malinzi ya BWANA, kwa mkono wa Musa’. Naam andiko hili linatuonyesha kwamba BWANA ndiye aliyekuwa akiamua muda wa kila jambo juu ya wana wa Israeli naam muda wa kusafiri na muda wa kutulia maskani kwa ishara ya wingu. Ndiyo kwa kila muda kulikuwa kuna vitu ambavyo Mungu alikuwa anavifanya kwa watu wake.

Katika Zaburi 32:8 Biblia inasema “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu, likikutazama’. Maandiko haya mawili yanatupa kujua kwamba ili nyakati zilizoamriwa na Mungu juu yako ziweze kuzaa/kuachilia/kufunua kile kilichofichwa/kilichobebwa/kilichohifadhiwa ndani yake sharti mwanadamu ajifunze kumtumia Roho Mtakatifu kama kiongozi wa maisha yake hapa duniani.  

Tujifunze kutoka kwenye ufuno wa Yohana kuhusu Ibilisi

1

Biblia katika Ufunuo wa Yohana 12:13 inasema ‘… Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye gadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu’.  Tafakari hivi, endapo Ibilisi anajua kwamba ana muda mchche tu, uwe na uhakika amejipanga kuutumia vizuri ili kuhakikisha malengo yake yanatimizwa kwa asilimia mia moja ndani ya muda mchache uliosalia.

Naam ili malengo yake yasifanikiwe juu yako, kwenye familia yako, kanisa lako, nchi yako nk. ni muhimu sana wana wa Mungu si tu wakajua nini mapenzi ya Mungu wao kwa nyakati alizoweka juu yao bali zaidi sana wadumu katika kuyatenda. Naam jambo hili limesisitizwa pia na Mzee wetu Petro aliposema ‘Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani”         (1Petro 4:2)

Tujifunze kupitia Yezebeli

Ufunuo 2: 21“Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake’. Je umeona jambo hili, hapa Yesu alikuwa akisema na Kanisa la Thiatira kuhusu kujiepusha na Yezebeli mwanamke ambaye alikuwa analiharibu kanisa hilo. Licha ya makosa yake Mungu akatoa muda wa Yezebeli kutubu wala hakutaka kutubia uovu wake. Na ni muhimu utambue kwamba muda aliopewa Yezebeli kutubu ulikuwa na kikomo.

Hata leo bado Mungu anatoa muda na fursa nyingi sana za watu wake kutubu na kutengeneza njia zao. Ile kwamba mwenzi wako, watoto wako, ndugu zako wanaendelea kuishi hata kama ni watenda maovu haina maana kwamba Mungu anafurahia uovu wao au haoni. Fahamu kwamba kimya chake ni muda ambao anautoa kwa wanadamu kutubu na kumrudia kwa kuwa yeye hafurahii kifo cha mwenye dhambi. Naam muda aliouweka juu yako, nyumba yako nk kutubu ukipita na walengwa wakakataa mabaya zaidi yatatokea kama ilivyokuwa kwa Yezebeli, miji ya Sodoma na Gomora nk.

Hivyo kwa kuwa wewe umepata ufahamu huu ni vema ukajifunza kushirikiana na muda wa kutubu ambao Mungu ameachilia juu yako, familia yako, kanisa lako, taifa lako nk, ili kwa njia ya maombi yako uiponye nyumba yako na Taifa lako pia.

Tujifunze kupitia Paulo na Timotheo

Biblia katika 2Timotheo4:2 inasema ‘Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usikokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho’. Katika maneno haya tunajifunza kwamba kumbe kwa kila jambo kuna wakati unaofaa na usiofaa.  

Jambo muhimu kwako ni kuwa tayari kuyatenda mapenzi ya Mungu kwa kila kipindi uanchopitia maishani mwako ili ndani ya vipindi husika yatimie yale yaliyokusudiwa na Mungu kutimia. Na hii ni kutokana na ukweli kwamba nyakati zimeamriwa na Mungu, kutoa ushirikiano kwa mtu ambaye anazingatia maagizo ya Mungu na sheria zake.

Naam ningeweza kuendelea kukuonyesha maandiko mengine kadhaa ndani ya Biblia lakini ninapomaliza natamani kusisitiza kuhusu kuwaombea wale waliopewa kuwa na akili za kujua nyakati zinazokuhusu katika ngazi mbalimbali. Ukirejea 1Mambo ya Nyakati 12:32 Biblia inasema “Na wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao vilikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao

Kutokana na andiko hili, ni dhahiri kwamba si watu wote waliopewa akili za kujua nyakati za yale yanayokuja ili kuwaongoza wengine namna ya kuyakabili. Hata hivyo uwe na uhakika kwamba kutokana na umuhimu wa jambo hili Mungu ameweka katika kila familia, kanisa, Taasisi, Taifa nk watu ambao ndani yao kuna akili za kujua nyakati zinazohusu familia, kanisa , taasisi au taifa husika ili wawasaidie wengine kujua yawapasayo kutenda kwa kila nyakati.

Hivyo ni muhimu sana ukajifunza kuwaombea watu wa namna hiyo kwenye familia yenu, kanisa, taifa nk kwa kuwa ndani yao kuna nyakati zote ambazo unapaswa/mnapaswa kuzipitia. Naam ni muhimu sana kuwaombea ili mosi wajitambue na pili wakae kwenye nafasi zao kwa kuwa ndani yao Mungu si tu ameweka akili za kujua nyakati bali zaidi namna ya kufanya katika kila nyakati zinazokuja juu yako.

Nami nakushukuru, Baba, Mungu wa wote wenye mwili, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga

Utukufu na heshima vina wewe Yeu! Wastahili BWANA.

 

Advertisements

15 comments

  1. Asante kaka namshukuru Mungu aliyenisaidia kuingia hapa naamini lipo kusudi Mungu akulinde utokapo na uingiapo sasa na hata milele.amen

    Like

  2. NASHUKURU KWA MSAADA WAKO KWANI NIMEJUA NA KUFUNGUKA KATIKA MAMBO MENGI KUPITIA SOMO HILI. MUNGU AKUBARIKI SANA. AMEN

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s