NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE (Sehemu ya 4b)

Na: Patrick Sanga

Photo 1

Nafasi ya tano – Mwanamke kama Mjenzi

Katika sehemu ya 4a tulianza kwa kuangalia nafasi ya tano hata hivyo kutokana na urefu wake nikaona vema kuigawanya nafasi hii ya tano katika kipengelea a na b. Ili kusoma sehemu ya 4a bonyeza link ifuatayo https://sanga.wordpress.com/2013/02/07/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia-nafasi-zake-kubadilisha-maisha-ya-ndoa-yake-sehemu-ya-4a/ . Katika sehemu ya 4b tutangalia ni kwa namna gani mwanamke atapata hekima ya kumsaidia kujenga ndoa yake. Karibu sasa tuendelee…

Hebu tuanze kwa kuangalia mstari wa ajabu sana katika Muhubiri 7: 12 unasema ‘Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi, na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliyonayo’. Hekima ndio nguzo kuu ya ujenzi wa ndoa yako, naam ukiwa nayo ni dhahiri kwamba italeta uponyaji kwenye ndoa yako pia. Mwanamke kama mjenzi anahitaji kuwa na hekima ili kulinda ndoa yake akijua kwamba ki – nafasi yeye ni Mlinzi wa mumewe. Kumbuka kwamba andiko letu la msingi katika sehemu hii ya nne ni Mithali 14:1 unaosema “Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa  kwa mikono yake mwenyewe”

Je, utapataje hekima ya kuijenga ndoa yako?

Zifuatazo ni njia ambazo zitakusaidia kupata hekima ya ki – Mungu ili kujenga, kuhifadhi na hivyo kuiponya ndoa yako:

a)    Kwa kuomba

Biblia katika Yakobo 1:5 inasema ‘Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa’. Je ni hekima ya namna gani hii? Yakobo anaendelea akifafanua kuwa ‘Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki’ (Yakobo 3:17). Kisha kwenye ule mstari wa 13 anauliza ‘N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima’ (Yakobo 3:13).

Photo 2

Je mama umeona jinsi mistari hii inavyozungumzia hekima kwa upekee wake? Ni dhahiri kwamba hekima ya namna hii ikiwa ndani yako kwa vyovyote vile ndoa yako itajengwa kwenye msingi imara, naam unahitaji kuomba kwa Mungu akupe hekima safi ambayo ndani yake itajenga msingi wa amani, upole na kudhihirisha matunda mema. Naam kwa hekima utaonyesha mwenendo wako mzuri katika nyumba yako.

Naam Yesu alisema ‘aombaye hupewa…’ (Matahyo 7:7), omba ukiamini Mungu atakupa hekima hii, si tu kwa ajili ya uponyaji wa ndoa yako, bali kwa ajili ya kusudi lake kupitia ndoa yako pia. Maana kadri ndoa yako inavyokuwa na amani ndivyo na kusudi la Mungu kupitia ndoa yako litakavyofanikiwa.

b)   Kwa kusoma neno la Mungu

Katika Mithali 4:5,7 Biblia inasema ‘Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam kwa mapato yako yote jipatie ufahamu’.

Ni muhimu sana kwako Mwanandoa ukaweka utaratibu wa kujifunza neno la Mungu kila iitwapo leo kwa kuwa ndani ya neno kuna hekima na ufahamu wakukusaidia. Biblia inasema ‘apendaye mafundisho upenda maarifa’ (Mitahli 12:1) tena katika Mithali 19:2a inasema ‘si vema nafsi ya mtu ikakosa maarifa…

Photo 3

Ni vizuri ukafahamu kwamba ‘mlinzi yeyote katika ulimwengu wa roho lazima awe na taarifa za kutosha kuhusu lindo lake na kwa jinsi hiyo hiyo mwanamke kama mlinzi lazima awe na ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu ili limuongoze katika kumpa hekima ya kiulinzi wa ndoa/nyumba yake. Naam ni LAZIMA ujijengee mazoea na nidhamu ya wewe binafsi kusoma neno la Mungu kila leo.

c)    Kwa kujifunza kwa waliotangulia

Katika kitabu cha Tito 2:3-5 Biblia inasema ‘ vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe na usingiziaji; wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao na kuwapenda watoto wao na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe’.

Naam ni muhimu sana kujifunza kwa wanawake wenye hekima waliokutangulia na wenye kumjua Mungu vizuri kama Tito anavyoelekeza. Hii ni kwa sababu si tu kwamba utajifunza kutoka kwenye hekima yao bali pia kutokana na uzoefu wao binafsi wa kuwa kwenye ndoa zao. Ni dhahiri kwamba hata wao wamepitia/walipitia kwenye changamoto mbalimbali na kwa msaada wa hekima wakazijenga ndoa zao katika BWANA hata zimekuwa na ushuhuda mzuri na leo tunamshukuru Mungu na kujivunia akina mama ambao licha ya changamoto walizokutana nazo kwanza hawakutoa siri za ndoa zao, pia kwa hekima walijifunza kuvumilia, wakatafuta amani, wakasamehe waume zao na kwa jinsi hiyo jina la BWANA halikutukanwa. Naam watafute hao ujifunze kwao maana hata leo wanapatikana.

d)   Kwa kuokoka

Wanawake wengi sana ambao ni wanandoa, ndoa zao zinashida kwa sababu Yesu si BWANA kwenye ndoa zao. Ili Yesu afanyike BWANA sharti wokovu uingie kwenye nyumba yako, kwa kuamua kuokoka. Najua jambo hili linaweza likaleta shida kwa wewe ambaye umeokoka, ukajiuliza mbona nimeokoka lakini bado ndoa yangu ina shida, naam mosi angalia hizo nafasi nyingine uzifanyie kazi, lakini pili mruhusu Yesu afanyike BWANA (Mtawala, Kiongozi, Mshauri) wa ndoa yako. Endapo utaokoka na kuenenda vema katika kuukulia wokovu uwe na uhakika yeye ni Mponyaji, na uponyaji wake hauna mipaka, naam unaweza kumkaribisha akusaidie kuiponya ndoa yako.

Ukisoma Biblia katika Wakolosai 2:3 biblia inasema ‘ambaye ndani yake yeye (Yesu Kristo) hazina za hekima na maarifa zimesitirika’ Maneno ndani yake yeye ndiyo ninayotaka uyaone kwa upana katika mstari huu. Andiko hili linafanya tujue kwamba ziko hekima za namna mbalimbali kutoka kwa BWANA ambazo tunazihitaji ikiwa ni pamoja na hekima ya kujenga nyumba/ndoa yako. Naam ili hekima ipate nafasi ya kuponya ndoa yako sharti mwenye hekima si tu apate nafasi ndani yako bali afanyike BWANA na mwokozi wa maisha yako kwenye maisha yako. (Ikiwa unataka kuokoka bonyeza link hii https://sanga.wordpress.com/wokovu/ ufuatishe sala ya toba)

Hebu tuangalie mifano kadhaa:

Mfano wa Mke wa Nabali

Ukisoma Biblia katika kitabu cha 1Samweli 25:2-35 utaona habari za mtu aliyeitwa Nabali ambaye alitaka kuleta maafa na msiba mkubwa kwenye nyumba yake kwa kitendo cha kuwatukana Daudi na watu wake, licha ya Daudi kufanya kazi kubwa ya kulinda mifugo ya Nabali ilipokuwa mashambani dhidi ya Wafilisti. Kutokana na dharau ya Nabali, Daudi aliapa kwenda kumuangamiza Nabali pamoja na nyumba yake yote. Maandiko yanasema Mke wa Nabali aitwaye Abigaili alipopata taarifa ya yalitokea alifanya hima kwa hekima kumsihi Daudi amsamehe mumewe kwa upumbavu alioufanya, naam na kwa neno la Abigaili Daudi alisamehe.

Photo 6

Tunajifunza nini?

Abigaili alizijua nafasi zake vema kama mke kwa mumewe na hivyo alizitumia nafasi zake kuiponya ndoa yake. Je, umeshawahi kufikiri kwa nini Mtumishi wa Nabali alienda kumpa taarifa Abigaili ya uovu ambao mumewe amewatenda watumwa wa Daudi? Biblia inasema yule Mtumishi alimweleza hivi Abigali ‘Basi sasa ujue na kufikiri utakavyotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya Bwana wetu (Nabali), na juu ya nyumba yake yote, kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye’ (1Samweli 25:17).

Hii ni kwa sababu Abigaili alikuwa Mlinzi wa Nabali na kwa kuwa alikuwa kwenye nafasi zake, taarifa za msingi juu ya lindo lake zilimtafuta. Naam mwanamke aliyesimama kwenye nafasi zake hakuna jambo litatokea au linalokuja mbeleni litatokea bila yeye kuwa na taarifa, na ndio maana Mungu anataka ujifunze mambo haya.

Baada ya Abigaili kupata taarifa husika, aliandaa chakula na kwenda kwa Daudi kuomba msamaha kwa ajili ya mumewe na  Daudi alijibu hivi … Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli ambaye amekuleta hivi leo kunilaki, na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe (1Samweli 25:32-33).

Je umeliona jambo hili lakini? naomba rudia tena kusoma maneno ya Daudi hapo juu. Naam umeshawahi kujiuliza kwa nini Daudi aanze kumhimidi Mungu kutokana na kitendo cha Abigaili? Kwa lugha rahisi Daudi alikuwa akisema ‘atukuzwe Mungu aliyempa Nabali mke mwenye Busara/hekima kiasi hiki’ (Mithali 19:11), maana kwa busara ya huyu mama nimezuiliwa nisimwage damu’. Naam Daudi hakuishia tu kumbariki Mungu bali alimbariki na Abigaili akasema ‘Na ibarikiwe busara yako naam na ubarikiwe wewe Abigaili’ kwa kuchagua kuwa mwanamke mwenye hekima nk.

Tambua kwamba, kama si Abigaili kusimama kwenye nafasi zake, siku ile si tu Nabali angekufa bali yote yaliyokuwa chini yake yangeharibiwa na kutekwa pia. Pengine Biblia ingeandika matukio yote ya Nabali ungeshuhudia namna ambayo mkewe alitumia hekima yake kuilinda na kuijenga ndoa yake. Ni imani yangu kila mumewe alipotenda kwa uovu, mkewe kwa hekima kama mjenzi alitengeneza ndoa yake kama alivyofanya na kwa Daudi, naam kwa nafasi yake Abigaili alizuia msiba usiingie katika nyumba yake.

Hata leo wapo akina mama wengi sana ambao wanamlilia Mungu aziponye ndoa zao kwa sababu zina shida kubwa. Katika hao wanaomlilia Mungu, si wote wanaojua kwamba Mungu anafanya kazi kwa taratibu na kanuni alizojiwekea. Ni matarajio ya Mungu kuona kila Mwanamke aliyeko kwenye ndoa anasimama kwenye nafasi zake, kutokea kwenye nafasi zake ndipo Mungu atasema na kumuongoza huyo mama juu ya nini cha kufanya ili kuponya ndoa yake na si vinginevyo.

Photo 4

Kumbuka kwamba ‘ni vigumu sana kwa Mungu kukusaidia/kukupigania kama hauko/haujasimama kwenye nafasi zako’. Katika kufanya kazi zake hapa duniani Mungu anaangalia nafasi ambazo amewapa watu kwenye ulimwengu wa roho. Naam wale ambao wapo kwenye nafasi zao ndio ambao Mungu anafanya nao kazi. Hivyo sio suala la kulia tu, bali ni suala la kusimama kwenye nafasi yako kama Mjenzi wa ndoa yako na utaona mabadiliko makubwa sana. Kumbuka pia na adui naye akitaka kuharibu ndoa yako sharti akuondoe kwenye nafasi zako, hii ni kuonyesha kwamba nafasi alizokupa Mungu kwenye ulimwengu wa roho zina thamani kubwa sana.

Mfano wa Stefano

“Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na wale wa kilikia na Asia wakaondoka na kujadiliana na Stefano; lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye” (Matendo ya Mitume 6: 9 -10). Naamini umeliona jambo hili wewe mama, jaribu kufikiri watu kutoka kwenye masinagogi matano tofauti walikuwa wakishindana na Stefano kwa habari za Injili aliyowashuhudia. Utamu wa habari hii ni kwamba Stefano alishinda na zaidi ya kushinda kwa sababu mosi, si tu alijazwa Roho Mtakatifu, bali kwa sababu ndani yake kulikuwa na hekima ambayo ilipita fahamu za wapinzani wake wote. Naam hivi ndivyo hekima ilivyofanyika ulinzi kwa Stefano na kwa shauri la BWANA.

Binafsi nalipenda sana andiko hili, maana linadhihirisha uwezo wa hekima katika kutenda, kulinda, kuhifadhi, kuponya nk. Naam si tu Roho Mtakatifu alimsaidia Stefano bali pia hekima aliyokuwa nayo Stefano ilimjengea mazingira mazuri Roho Mtakatifu ya kumshindia Stefano. Hekima hii ndiyo iliyokuwa ndani ya BWANA wetu Yesu Kristo alipokuwa bustanini na wanafunzi wake, wakati wa mateso yake na hata kifo chake. Maana alisema ‘Baba uwasamehe maana hawajui walitendalo’.  Mpenzi msomaji fikiri endapo ungekuwa wewe kwenye mazingira kama ya Stefano au Yesu ungechukua uamuzi gani?

Nimeandika Mfano huu wa Stefano si kwa bahati mbaya bali kwa kusudi kamili. Najua kesi ya Stefano haikuwa ya ndoa, bali upinzani dhidi ya injili ya Kristo. Nilichotaka kukuonyesha ni uwezo wa hekima katika kulinda, kuhifadhi, kusaidia nk wakati mtu anapokutana na changamoto mbalimbali. Hekima ya Mungu ilimsaidia Stefano kutokana na mazingira yake, naam na hata kwako inaweza kukusaidia kuiponya ndoa yako. Naam hekima ni Mlinzi, hekima ni Mjenzi, hekima ni Mponyaji nk, kwa neema ya Mungu, kupitia ujumbe huu nimemtambulisha Hekima kwako mama, MTAFUTE NA KUMTUMIA ATAKUSAIDIA KUIPONYA NDOA YAKO.

Ahsante kwa kufuatilia mfululizo huu, katika sehemu ya tano (5) nitaweka sehemu ya mwisho ya ujumbe huu muhimu kwa wanadoa… naam usiache kuomba kwa ajili yangu.

Utukufu na Heshima vina wewe Yesu! Wastahili BWANA wetu.

Advertisements

40 comments

 1. Mtumishi Mungu akubariki sana kwa kutukumbusha kina mama,na kupitia ujumbe huu Mungu ataenda kuponya ndoa zetu,Mungu akubariki na kukufunulia zaidi na zaidi

  Like

 2. Bwana akubariki sana mutumishi wa Mungu nimejua mengi kupitia ujumbe huu.tuzidi kuombea wakina mama. hata nitahubiri kanisani.

  Like

 3. Nimebarikiwa sana na somo mtumishi wa MUNGU.MUNGU AKUTIE NGUVU NA AZIDI KUKUPA MASOMO MAPYA.Mimi napenda sana kutembelea blog hii bt huwa nahuzunika napokosa somo jipya.MUNGU AKUBARIKI KWA NAMNA UNAVYOTENDA KAZI YAKE.

  Like

  • Mungu akubariki sana kwa kutembelea na kujifunza katika blogu hii, naam kwa habari ya masomo mapya naomba maombi yako maana ukweli kinachonikwamisha ni ratiba na majukumu mengine niliyonayo, lakini BWANA ni mwaminifu naamini atanisaidia katika hili maana najua wengi hawafurahishwi na hili, hata BWANA Yesu mwenyewe.

   Like

 4. Ubarikiwe mtumishi kwa mafundisho yako! Naomba unisaidie mbinu za kumsaidia mwanamke asiyependa kujituma katika shughuli mbalimbali za kimaisha hasa aliyekosa ubunifu wa nini afanye aweze kujisimamia kwa kuwa na kipato.
  Ahsante.

  Like

 5. Mungu akubariki sana Mtumishi kwa mafundisho mazuri na ya kujenga. Naamini tukisimama imara na kuomba ndoa zetu zitakuwa ni msingi bora wa kanisa.

  Nakutakia utume mwema.

  Like

 6. Lucy

  Shalom,

  Mungu wa Mbinguni na abarikiwe.
  Mtumishi nimebalikiwa sana na huduma yako katika mtandao Mungu na anifunulie zaidi mafundisho kama haya. Kama Yer. 33:3 inavyosema.

  Lucy

  Like

  • Shalom, sehemu kubwa natoa mafundisho kwa njia hii, mimi ni mwajiriwa wa Serikali pia, hivyo mafundisho ya ana kwa ana nayatoa ninapokuwa kwenye semina ambazo makundi husika wanakuwa wameomba na hususani wakati wa likizo, sorry for late reply.

   Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s