IJUE NA KUITUMIA NAFASI YAKO KAMA MLINZI KWENYE ULIMWENGU WA ROHO (Part 6)

Na: Patrick Sanga

Mada: Je mwanadamu anawezaje kujua kwamba amewekwa kuwa Mlinzi wa eneo fulani katika ulimwengu wa roho?

Katika sehemu ya tano tuliangalia tafsiri ya kuwa mlinzi katika ulimwengu wa roho. Ili kusoma sehemu ya tano bonyeza link hii https://sanga.wordpress.com/2012/11/05/ijue-na-kuitumia-nafasi-yako-kama-mlinzi-kwenye-ulimwengu-wa-roho-part-5/ Katika sehemu hii ya sita tutaangalia jambo jingine nalo ni, je mwanadamu anawezaje kujua kwamba amewekwa kuwa Mlinzi wa eneo fulani katika ulimwengu wa roho? Ikumbukwe kwamba Mungu ndiye anayewaita na kuwaweka watu kwenye nafasi mbalimbali za ulinzi katika ulimwengu wa roho. Naam katika kuwaita watu kwenye nafasi husika mtu anaweza kupewa maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu au anaweza kupata maelekezo ya Mungu kupitia mtu au watu.  Ukirejea (Ezekieli 33:7) Biblia inasema ‘Basi, wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli, basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu’.   Lakini pia ukirejea (2Wafalme11:18-19) Biblia inasema (Yehoyada)…akawasimamisha walinzi malangoni pa nyumba ya Bwana’….  Licha ya kwamba walinzi wengine wanawekwa na wanadamu, lakini mwenye kumfanya mtu kuwa mlinzi ni Mungu. 

Kwa kuzingatia ukweli huu zifuatazo ni njia kadhaa zinazoweza kukusaidia kujua kwamba umewekwa kuwa Mlinzi wa eneo fulani katika ulimwengu wa roho;

Njia ya kwanzaUwepo wako binafsi kwenye eneo husika.

Kitendo cha Mungu kukuweka kwenye eneo ambalo upo sasa yaani Kijiji, Mji, Wilaya, Mkoa na Nchi nk, kiroho ina tafsiri ya kwamba umewekwa kuwa Mlinzi wa hilo eneo. Je umeshawahi kufikiri kwa nini ulizaliwa kwenye familia uliyozaliwa, kwa nini upo kwenye Shirika/Ofisi uliyopo na si pengine, kwa nini upo kwenye ukoo falani na si mwingine?nk. Naam Mungu anapokuweka kwenye eneo fulani kuna mambo anataka kuyafanya kupitia uwepo wako kwenye hilo eneo. Moja ya malengo yake ni kukufanya kuwa Mlinzi wa kusudi lake kwenye hilo eneo. Na ndio maana katika mfululizo huu nimesisitiza kwamba ni muhimu sana kwa Mlinzi kujua nini ni mapenzi ya Mungu kwenye hilo eneo lake.

Njia ya piliKupitia Wakufunzi/Viongozi/Watumishi wa kiroho (2Nyakati 23:19)

Viongozi wetu wa kiroho kwa nafasi zao mbalimbali pia ni walinzi wa kusudi la Mungu hapa duniani. Moja ya jukumu lao kubwa ni kulea, kuchunga na kuwasiaida wale wanaowaongoza kulitumikia kusudi la Mungu wakali hapa duniani. Viongozi ambao kiroho wamekaa vizuri kwenye nafasi zao, Mungu husema nao mara kwa mara kwa habari ya wale wanaowaongoza na kile ambacho Mungu amekusudia kufanya kupitia wao. Hivyo kiongozi wako wa kiroho anaweza kukusaidia kujua eneo ambalo Mungu amekupa uwe mlinzi katika ulimwengu wa roho.

Njia ya tatuRoho Mtakatifu/Msukumo wa kuomba

Mlinzi/Walinzi waliosimama kwenye nfasi zao ni viungo muhimu sana kwa Roho Mtakatifu katika kufanya kazi zake hapa duniani. Kwa uzoefu wangu binafsi nimeona namna ambavyo Roho Mtakatifu anatoa maelekezo kuhusu maeneo mbalimbali ambayo yanatakiwa kuwa na ulinzi katika ulimwengu wa roho. Kimsingi moja ya kazi zake ni kuongoza watu kwenye maeneo ambayo yanahitaji ulinzi. Naam anaweza akasema nawe moja kwa moja au akaleta mara kwa mara msukumo ndani yako wa kuomba kuhusu yale ambayo anataka kufanya kwenye eneo husika. Hivyo ni muhimu sana kwa Mlinzi kuwa na mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu kwa kuwa mara kwa mara Roho Mtakatifu husema na Mlinzi/Walinzi husika juu ya wajibu wao kwenye maeneo yao ya ulinzi.  

Njia ya nneKuletewa watu wenye uhitaji wa aina fulani mara kwa mara

Endapo mara kwa mara Mungu anawaleta watu wenye uhitaji wa aina fulani au ndani yako Mungu anakuletea kuombea watu wa aina fulani, au viongozi, au wanandoa, au watumishi, au mataifa nk katika maono au kama ni watu basi wanakuja kabisa kimwili ni ishara kwamba umeitwa kuwa Mlinzi kwenye hilo eneo. Naam Mungu ameweka walinzi wa masula ya ndoa, viongozi wa kiroho, watawala, wanasiasa, watumishi wa umma na wasio wa umma, wafanya biashara, wakulima nk.

Njia ya tanoKuwa kiongozi wa kiroho

Si viongozi wengi wa kiroho wenye kuijua siri hii. Unapowekwa na Mungu kuwa kiongozi kanisani, kwenye jumuia yoyote au kusanyiko lolote la kiroho tambua kwamba huo ni wito wa kuwa Mlinzi katika ulimwengu wa roho. Maandiko yanasema hivi ‘Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi’ (Waebrania 13:17). Naamini umeona yale maneno yanayosema maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu. Sentensi hii inatupa kujua kwamba licha ya viongozi wetu kuwajibika kutuongoza katika malengo tuliyojiwekea, lakini kiroho wao wamewekwa kuwa walinzi wa kusudi la Mungu kwetu kupitia nafasi zao.

Kumbuka kwamba lengo la Mungu kukupa nafasi ya/za ulinzi ni; kuhakikisha unalisimamia na hivyo kufanikisha kusudi lake kupitia nafasi yako/zako. Katika kuzifanya kazi zake hapa duniani Mungu amejiwekea utaraibu wa kufanikisha kusudi lake kupitia mwanandamu. Naam endapo kina Ibrahimu, Nuhu, Daudi, Yeremia, Ezekieli nk. walifanikiwa hatuna budi nasi kuwa na mafanikio zaidi kwa kuwa hili ni agano jipya ambalo Roho wa Mungu anakaa ndani yetu.  

Mungu akubariki, somo litaendelea…

Utukufu na heshima vina wewe Yesu! Wastahili Bwana.

Advertisements

5 comments

  1. mr.Sanga kazi yako si bure mbele za Mungu utalipwa kwa majira yake mungu ucpo zimia moyo.Iam so interested with ur ministry keep it up.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s