NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE

Na: Patrick Sanga

Mithali 14: 1 ‘Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’.

Mchungaji mmoja rafiki yangu aliniambia asilimia hamsini mpaka sabini ya changamoto au matatizo anayoshughulika nayo mara kwa mara katika kanisa lake ni ya wanandoa. Kwa lugha nyepesi asilimia 50 – 70 ni matatizo yatokanayo au yanayohusiana na ndoa. Binafsi pia kwa upande wangu kupitia nafasi yangu katika mwili wa Kristo, email za wasomaji ninazopata na pia baadhi ya semina za ndoa ambazo nimefanya kuhusu eneo hili nimegundua kwa hakika ndoa nyingi za wana wa Mungu zina shida na wao hawajajua kwamba vita hii inatoka kwa Shetani, maana anajua ndoa zikitengamaa ni faida kwa ufalme wa Mungu na ni uharibifu kwenye ufalme wake wa giza. Naam anapigana usiku na mchana ili kuhakikisha ndoa hazitengamai kwa kuleta fujo za kila aina.

Kila siku katika ndoa kuna changamoto zinazaliwa mpaka imefika mahala baadhi ya wanandoa wanawaza kwa nini walikubali kuoa au kuolewa. Kwa hakika laiti Biblia ingetoa mwanya kwa wanandoa kuachana basi kuna baadhi ya wanandoa wangehakikisha wanaitumia hiyo nafasi vizuri kwa kuwa ndoa zimegeuka ndoano. Matarajio ambayo kila mmoja alikuwa nayo kwenye ndoa anaona hayatimii. Kinachosumbua watu wengi ni kwamba kabla hawajaonana hawakujua nini kinakuja kupitia ndoa, hawakuweza kuona uhalisia wa maisha ya ndoa utakuwaje? Bali kila mmoja alikuwa na mtazamo/fikra na matarajio yake binafsi juu ya ndoa yake.

Naam zipo sababu nyingi sana zinazopelekea matatizo au changamoto kwa wanandoa. Katika somo hili nitaandika zaidi zile zinazotokana na upinzani kutoka kwa Shetani ili kuathiri kusudi la Mungu. Lengo la ujumbe huu ni kukufundisha wewe mama (Mwanandoa) namna ya kuzitumia ‘nafasi’ ambazo Mungu amekupa Kibiblia ili kuiponya ndoa yako au kubadilisha hali ya sasa ya ndoa yako endapo unaona si ile ambayo Mungu amekusudia.

Kwa nini Mwanamke?

Pengine utaniuliza kwa nini mwanamke ndiye awajibike katika kuponya au kubadilisha maisha ya ndoa yake? Binafsi katika kuisoma Biblia nimegundua kwamba kwa kuzingatia nafasi ambazo mwanamke amepewa kibiblia ni ishara ya kwamba kwa habari ya  ndoa, Mwanamke ana nafasi kubwa ya kuijenga au kuibomoa ndoa yake na hivyo nyumba yake kwa ujumla. Mara kwa mara Mungu ananifundisha masuala ya wanawake, suala la wanawake kuwa kwenye ‘nafasi zao’ husisitizwa sana.

Kwa nini nafasi?

Sijui kama unafahamu maana ya nafasi ambayo Mungu anampa mtu katika ulimwengu wa roho. Hizi ni nafasi ambazo Mungu amekupa wewe mawanamke katika ulimwengu wa roho ili uzitumie kufanikisha kusudi lake kupitia ndoa yako. Nafasi (position) ni eneo ambalo mtu anapaswa kuwepo kwa kuhusianisha na vitu au watu wengine, naam ni wadhifa ambao mtu anakuwa nao kwa kuhusianisha na mtu au watu wengine.

Kwa hiyo hizi ni nafasi ambazo Mungu amempa mwanamke zikihusiana na mwanaume katika kilitumika kusudi la Mungu hapa duniani. Mwanamke anapokuwa amesimama katika nafasi zake ndipo anapoweza kuruhusu mawazo ya Mungu kupitia ndoa yake kutimia naam ndivyo anavyoweza kuzuia mawazo ya Iblisi kupitia ndoa yake yasitimie. Naam nafasi ya mwanamke katika ndoa ndiyo inayoamua uzima au mauti ya ndoa yake, nafasi ndiyo inayopelekea kufanikiwa au kufeli kwa ndoa yake, nafasi ya mwanamke katika ndoa ndio inayoamua nini kingie au kitoke kwenye ndoa.

Katika kusoma kwangu Biblia nimegundua kwamba Mungu amempa nafasi zifuatazo mwanamke;

 • Mwanamke kama ‘msaidizi’ wa mumewe
 • Mwanamke kama ‘mlinzi’ wa mwanaume
 • Mwanamke kama ‘mjenzi’ wa nyumba yake
 • Mwanamke kama ‘mshauri’ wa mumewe
 • Mwanamke kama ‘mleta kibali’ kwa mumewe

Naam kutokana na changamoto zinazoendelea katika ndoa mbalimbali nimelazimika kuanza kuandaa mfululizo huu wa namna mwanamke anavyoweza kusimama kwenye nafasi zake na kuiponya ndoa yake. Jukumu langu kubwa itakuwa ni kufafanua kila nafasi ambayo mwanamke amepewa na namna anavyoweza kuitumia hiyo nafasi kubadilisha ndoa yake ambayo anaona inaangamia.

Somo litaendelea, maombi yako ni muhimu sana.

Advertisements

58 comments

 1. Mungu akubariki mtumishi wa Mungu mafundisho kama haya lazima upate msaada kutoka kwa Roho Mtakatifu, wewe peke yako huwezi, nakuonea wivu kwa neema uliyo pewa antena yako ya kiroho ielekezee huko huko unapopokea mafundisho haya, usigeuze kushoto wala kulia. Mungu aendelee kukutumia zaidi na zaidi kwani mafundisho haya yanaponya nafsi za watu wengi, huenda wewe usijue ila Roho Mtakatifu anayavuvia upako inakuwa dose tosha kwa kila aliye jeruhiwa. Pia huduma kama hizi vita vyake ni vikubwa JITIE NGUVU, SONGA MBELE, UTASHINDA.

  Like

  • Ahsante sana Ndugu Twaha kwa maneno haya ya faraja na kunitia moyo katika huduma hii. Utukufu kwa Mungu kwa yote afanyayo kupitia masomo haya, tuzidi kuombeana.

   Like

 2. Thanks a lot i like it keep it up, for all your lessons i have passed them through and i have seen are greatly amazing for this generation and the upcoming generation bye it’s me your beloved friend in christ Lugano Samson Mwafyela from Kyela Stamico Mbeya.

  Like

 3. mimi ni binti bado cjaolewa lkn kwa mafundisho hyo nimebarikiwa na nimujua nafac yngu ni ipi ktkt maisha ya ndoa.

  Like

 4. kaka sanga ni kweli tupu umezungumzia, na watu wengi kwa mtazamo wa kimwili wadhani mwanamke ni dhaifu hii si kweli kutokana na hayo uliosema, Mungu anamwamini sana mwanamke na amempa nguvu sana ktk ujenzi, usaidizi, ushauri, ulinzi n.k .namshukuru sana Mungu alinijulisha haya before kuingia ktk ndoa na nilianzan kuomba sana Mungu anisaidie kusimama ktk nafasi zote nilizopewa kama mwanamke na Mungu mwema nimeolewa na ndoa yangu inaendelea vizuri kila iitwapo leo.

  Like

 5. kwa mabinti ambao hamjaolewa, mwanamke ambae hujaokoka amua kuokoka kwanza alafu penda kusoma sana neno la Mungu ujue nafasi yako na uombe msaada wa roho mtakatifu kukusaidia kusimama, usijichanganye mwanamke kwa Yesu unataka duniani pia upo, ili kusikia sauti ya Mungu sana na msaada wa karibu lazma uwe ndani ya Yesu.

  Like

 6. Bwana Yesu Asifiwe.
  Namshukuru Mungu sana anavyokutumia katika kufikisha ujumbe kwa watu wake. Hakika ninabarikiwa sana na Masomo yako. Mungu akubariki sana na aendelee kukutumia kwa namna ya Kipekee.
  Baraka za Bwana Yesu ziambatane nawe. Amina

  Like

  • Amina, ahsante pia kwa kutenga muda wako ili kujifunza kupitia blog hii, naomba mara kwa mara uombapo usiache kuombea wajibu huu ambao BWANA mwenyewe ameweka ndani yangu kwa utukufu wake, jina lake na kusudi lake. Ubarikiwe sana.

   Like

 7. Mpendwa wangu Mungu akubariki sana haya ni mafunuo yanayopakuliwa kabisa toka madhabahu ya mbinguni ili kuziponya ndoa. Kwa sababu ndoa nyingi sasa zipo intensive care msaada wa ziada kama huu usIpopatikana zitaingia motuary si muda mrefu.

  Hakika neno hili NAFASI ni neno la muhimu sana. Najua somo hili linaendelea na ninaamini litaonyesha nafasi ya kila mmoja katika ndoa na madhara ya kutoka katika nafasi yako na kukaa katika nafasi ya mwingine yaani mwanamke kukaa katika nafasi ya mwanamme na mwamme kukaa nafasi ya mwanamke.

  Ndoa nyingi leo ziko katika matatizo makubwa kwa sababu ya kutokaa katika nafasi zetu sawasawa.

  Tunakumwomba Mungu mtumishi aendelee kukufunulia matatizo haya ya ndoa ili ndoa zetu zipone. Mungu akubariki sana.

  Like

  • Naam uwe huru waweza ku ‘download’ au kama ni zaidi ya hapo basi namba yangu ni 0755-816800. Hata hivyo somo hili lina muendelezo, na bado linaendelea. Barikiwa.

   Like

 8. Kaka Sanga nimebarikiwa sana na masomo yako yaani Mungu amekufunulia mambo mazuri ya kujenga ndoa za wana wake. Mimi Ni mwanamke ninaye pitia magumu haya kupitia mafundisho yako naamini nitashinda maana nilikuwa sielewi nafasi yangu sasa nimejitambua .

  Shetani atakipata sasa inabidi kusimama sawa sawa kwa zamu yangu ili kumuokoa na mkono wa shetani.

  BARAKA ZA BWANA YESU ZIZIDI KUKUFUNIKA UPATE MAFUNUO ZAID

  MAMA FARAJA

  Like

 9. vyombo vingi vipo kumdidimiza mwanamke,zikiwemo mila,desturi,taratibu,sheria na hata dini.yote haya hupelekea mapokeo dhaifu ama potofu kwa jamii nzima.kupitia mapokeo haya,mwanamke atajiona dhaifu,asiyeweza na kuthaminiwa na waliomzunguka,jamii nayo kupitia mapokeo hayo itamchukulia mwanamke kuwa dhaifu.kwa mapokeo haya mwanamke uponaji wake upo katika kubadili mapokeo tulio nayo.ni jukumu letu sote kushiriki kuleta mabadiliko na ukombozi wa mwanamke na kuacha malumbano na mashindano yasiyo na tija kwani taratibu,mila,sheria na vyote tumejiwekea wenyewe,NI SAWA NA KUKUBALIANA JOGOO AITWE JOGOO NA KIKOMBE KIITWE KIKOMBE

  Like

 10. Shalom, nami nimelifurahia sana somo; nilikuwa si mfuatiliaji sana lakin kwa sasa nimekuwa pindi nipatapo muda napenda kusoma sana….Mungu akuzidishie hekima yake Mtumishi wa Mungu uzidi kuponya makovu makubwa kwa wana wa Mungu yaliyojikita katika ndoa zetu…Nami ni mchanga sana ktk ndoa nina miezi 3 sasa ila naamini Mungu atazidi kunifunika na kwa kupitia masomo haya naamini nitaboreka zaidi! Shetani hana chake kwa ndoa za wana wa Mungu tukimtumaini na kumtegemea kwa yote. Ubarikiwe sana Mr. Sanga

  Like

  • Naam ahsante kwa Yesu anayeweka utayari ndani yako wa kujifunza juu ya mambo haya, naam hakikisha unaendelea kujifunza zaidi na zaidi, si tu katika blog hii na nyingine nyingi zenye mafundisho yenye msingi wa kibiblia. Ahsante kwa maombi na mchango wako kwenye hili eneo kwa wanandoa. Tuzidi kuombeana.

   Like

 11. GW:Gen 16:10 The Messenger of the LORD also said to her, “I will give you many descendants. No one will be able to count them because there will be so many.” Gen 16:11 Then the Messenger of the LORD said to her, “You are pregnant, and you will give birth to a son. You will name him Ishmael [God Hears], because the LORD has heard your cry of distress.
  Gen 16:12 He will be as free and wild as an untamed donkey. He will fight with everyone, and everyone will fight with him. He will have conflicts with all his relatives.”

  Muhubiri Kutoka Nijeria Rev Dr Chidi Tar 2/10/2005 alisema siku Ibrahim aliposikiliza sauti ya Sara Mwz 16:2 ndipo Osama alipozaliwa, ndipo magaidi ulimwenguni walipoingia. Ukisoma Gen 16:10 Ishimael alibarikiwa kama Isaka kisha Gen 16:12 Ishmael alilaaniwa. Ukweli somo lako nimelipenda nafasi ya mwanamke ni kubwa sana katika ndoa akiitumia vibaya ndoa na familia vinabomoka na kuanguka na anguko lake ni kubwa sana.

  Like

 12. Mtumishi wa Mungu, ubarikiwe saana, mimi ni mchanga sana katika ndoa lakini tumejaribu kupitia haya mafundisho ya Mungu kupitia wewe, mimi na mke wangu, tumebarikiwa saana, neno la Mungu hata ukilisoma siku nyingi always huwa ni jipya sana tu.niseme tu kwamba kupitia hili ambalo nimeliona katika ulimwengu wa roho, kulingana na fikra za mke wangu na zangu, tunayo maono ambayo Mungu amesema na mke wangu,,, umeponya ndoa nyingi saana,kupitia wewe ambapo mtu anaweza kusema ni kazi ndogo na Mungu anajaza nguvu nyingi saana, andiko hili kwa kazi ya mikono bila sauti.Tunatamani siku hiyo yukutane mbinguni tushangilie wote.tunafuraha sanaa.

  Like

 13. Mtumishi wa Mungu ,Haleluya!!!,awali ya yote tunatumia fursa hii ,kulitaja vizuri jina yote kuwa n i jema sana, tena linatulinda, na kutufariji pia na Baraka za mwilini na rohoni,Bwana yesu asifiwe saana.tunaendelea kufurahi updates zako mtumishi hasa,la ndoa na la Ijue nafasoi yako ya ulinzi katika ulimwengu wa roho.
  nasi tunaendelea sasa kujipanga na kuchukua hatamu zaidi katika wajibu wetu wakufanya, kama vile mungu anavyotutaka tufanye,kama watoto wanaosikiliza baba asemavyo. Mtumishi pia nimesoma ushuuda wako…Your testimonial expressions mtumishi Mungu akutie/ atutie nguvu ili kazi hii itendeke kwa ufasaha zaidi. ili Mungu atupandishe vyeo.Mtumishi wa Mungu katika maombi yako uombapo tamka lolote lile jema juu ya familia yetu changa na mke wangu, kile ambacho Mungu alicho kiweka ndani yangu hasa kwa mke wangu basi kitimie na kimpe utukufu aliye juu.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s