MAMBO YA KUTAFAKARI KATIKA KIPINDI HIKI CHA CHRISTMAS

Patrick na Flora Sanga

Heri ya Christmas mpenzi msomaji!

Mathayo 1:21 ‘Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina Yesu, maana, yeye ndiye atayewaokoa watu wake na dhambi zao’.

Hakika hii ni sherehe ya ajabu na ya kipekee sana maishani kwetu. Kila mwaka ifikapo Desemba 25, Wakristo duniani kote huadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Naam kuna mambo mengi ambayo hufanyika katika siku hii au katika kipindi cha maadhimisho ya siku kuu hii. Wapo wanaojua maana ya siku hii na wapo ambao wameigeuza siku hii kuwa chukizo mbele za Mungu kutokana  na matendo yao.

Hivyo tunapoadhimisha sherehe hii katika mwaka huu, yafuatayo ni mambo ambayo tumeona ni vema tukakumbushana nayo ni;

 • Mwokozi amezaliwa

Mstari wa 21 wa kitabu cha Mathayo unatueleza kusudi la kuja kwake Bwana wetu kuwa ni kuwaokoa watu wake na dhambi zao. Naam ni upendo wa pekee sana kwa Bwana Yesu kuacha heshima na utukufu mbinguni na aje azaliwe, afe na kufufuka ili tupate waokovu. Kwa sababu hiyo kama bado hujaokoka ni vema ukafanya maamuzi ya kuokoka. Haukuwa uamuzi rahisi kwa Yesu kuacha heshima na enzi mbinguni aje kwa ajili yetu. Na wewe uliyeokoka usiendelee kuishi maisha ya dhambi kama asiyemjua Mungu.

 • Boresha uhusiano wako na Roho Mtakatifu

Biblia inasema ‘Kuzaliwa kwake Yesu kulikuwa hivi, Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu’ (Matahyo 1:17)

Mimba ya Bwana wetu ndani ya Mariamu ilikuwa ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Nasi tunajua ya kwamba, Roho Mtakatifu ni Mungu, na kwa sasa yeye ndiye ambaye yupo duniani analiandaa kanisa la Bwana na kuhakikisha kusudi la Mungu kupitia ‘mtu’ linafanikiwa. Naam ni muhimu sana kila aliye wa Kristo kuhakikisha kwamba mahusiano yake na Roho Mtakatifu yanakuwa mazuri daima. Naam tumia kipindi hiki kumshukuru Mungu kwa siku hii na kujenga msingi mzuri wa mahusiano na Roho Mtakatifu kuanzia sasa na kuendelea.

 • ‘Christmas’ siyo siku ya kufanya uovu

Ni vema watu wote wakatambua kwamba siku hii siyo siku ya kufanya kila namna ya uchafu na dhambi ambazo wanadamu wamezoea kufanya katika siku hii. Ni vema siku hii ikaheshimika sana, maana ndiyo siku ambayo dunia ilipokea mwokozi wa ulimwengu. Naam siku ambayo ufumbuzi wa dhambi ulikuja kwa wanadamu duniani. Shetani amekuwa akijaribu kuharibu sifa/ picha (image) ya siku hii, kwa kuwafanya wanadamu wapange kufanya kila namna ya machikizo mbele za Mungu wetu. Ole kwao wafanyao hayo, naam tulio wa Kristo Yesu tunajua maana ya siku hii na tunaona fahari kwa ajili ya siku hii, utukuzwe Baba kumtoa mwanao, utukuzwe mwana kwa kukubali kuja ili tupate kuwa warithi wa ufalme wako tungali dunani na kisha uzima wa milele.

 • Fanya tathmini ya wokovu wako

Kwa kawaida wanadamu hufanya tathimini ya mambo mbalimbali katika maisha yao. Ni wachache sana ambao hufanya tathmini juu ya maisha yao ya wokovu ndani ya Kristo. Katika mwaka 2011, je umekuwa Balozi wa kweli wa Kristo katika nyumba, ofisi, mji au Taifa lako na kwa wale wanaokuzunguka kila siku? vipi kuhusu uaminifu, je umekuwa muaminifu kwa kiasi gani mbele za Mungu, je unaweza kusema umeishi maisha ya ushuhuda katika Kristo Yesu nk.

Vipi kuhusu mahusiano yako na wenzako, je kuna amani, vipi kuhusu zaka na dhabihu? Kwa kifupi katika vigezo vyote vya wokovu alama zako zikoje, ingekuwa unajiwekea alama katika mia moja ungejiwekea ngapi? na Bwana naye angekuwekea ngapi? Naam pale unapoona hukufanya vema, omba toba na kuomba nguvu mpya ya kukusaidia kipindi kinachofuata baada ya siku hii na mwaka ujao wa 2012.

Mpenzi msomaji unapomalizia ujumbe huu hebu sema maneno yafuatayo ya shukrani;

“Bwana Yesu hongera kwa siku hii ya pekee ya kuzaliwa kwako, ambayo ulifanya maamuzi magumu sana kwa sababu ya upendo wako kwetu. Watoto wako tunajua maana ya siku hii na tunaona fahari sana kwa ajili ya siku hii, ahsante sana kwa kutuchagua na kutufanya warithi wa neema yako. Kwa imani tunaungana na jeshi lote la mbinguni katika kusherekea siku hii ya pekee, tunatamani tungekuwa na wewe kwa jinsi ya mwili ili tufurahi kwa pamoja. Nasi tunaoomba uwepo wako na furaha (tabasamu) yako vidhihirike ndani yetu, kwa namna ya pekee, maana furaha yako ndiyo nguvu zetu. 

Mpenzi msomaji, familia yangu inakutakia heri ya ‘Christmas’ na maisha yenye kumuja Mungu zaidi.

Utukufu na heshima vina wewe Yesu! Wastahili Bwana wetu.

Advertisements

12 comments

 1. Unajua kaka kuna kitu ki1 kinanisikitisha sana, wakristo hatujitambui. shetani ametushika kila leo tunahangaika na mambo ya dunia wakati walio kwake wanakimbilia kwa Yesu! ukristo jina hautatupeleka popote, kila kitu kinagharama. Asante kwa huduma yako na mimi naap date blog yangu.

  Like

  • Ubarikiwe ndg. Eliyaliya kwa ufafanuzi wako, ni kweli Wakristo wengi wanafikiri wataingia mbinguni kwa sababu wao ni Wakristo, jambo ambalo si kweli, na Shetani kafanikiwa kuwafunga watu kwenye hili kama usemavyo. Ndio maana Yuda alisukumwa kutuandikia ili kutuonya kwa habari ya kuishindania imani. Kwa hakika tunahitaji kujipanga vizuri ndani ya Kristo kwa kuyatenda mapenzi yake.

   Like

 2. Bwana Yesu Kristo apewe sifa.
  Namshukuru Mungu baba kwa Upendo wake wa ajabu kutufanya watoto wake na warithi wa Ufalme wake kwa kumtoa mwanae Yesu Kristo aje kuichukua dhambi ya Ulimwengu kwao waaminio. Wakristo na watu wote ulimwenguni nataka niwakumbushe kuwa dhambi ni mizigo na ni utumwa wa hali ya juu. Bwana Yesu amekuja kuibeba hiyo mizigo yetu tumtwisheni yeye na ndiyo maana anasema nitwisheni mimi fadhaa zenu zote au njooni kwangu ninyi msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. lakini watu bado wameng’ang’ania mizigo yao, jamani mnataka msaidiwe vipi? miili itawaponza ni ya muda mfupi tu nasema ziangalieni roho zenu zidumuzo milele, ili hiyo milele iwe uzimani na sio kwenye ziwa la moto

  Ukisoma Yoh 1:14 anasema;
  Naye Neno alifanyika mwili- Neno ni Yesu, Mwili unawakilisha udhaifu wetu yaani alijifanya mwenye dhambi kama sisi ili abebe adhabu tuliyostahili…Akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokae kwa baba. Amejaa neema na kweli

  Neema ni wokovu, ambao ndio tunapaswa kuupokea ndio kumpokea Kristo mwenyewe ili tuwe na huo uzima wa milele. Wapendwa hapo naomba niongee kidogo, Watu wengi wamekuwa wakidhani kuwa kwenda kanisani, kutoa sadaka, kuwa muombaji sana inatosha hapana ni lazima tuukiri Wokovu. Mwangalie Kornelio alivyokuwa na sifa zote nilizozitaja na zaidi ya hizo lakini alipungukiwa na kuukiri wokovu hadi Mungu akamhurumia na kumtumia Malaika ili ampe ujumbe akamwite Petro aje kumhubiria habari za Wokovu ili awe mkamilifu mbele za Mungu.

  Wapendwa WOKOVU NI LAZIMA KAMA TUNATAKA KUINGIA MBINGUNI.

  BWANA YESU AWABARIKI SANA….AMEN

  Like

  • Dr. Daniel ubarikiwe sana kwa comment yako na mafundisho hayo ya msingi, kwa hakika hakuna upendo kama huu wa Bwana Yesu kuutoa uhai wake kwa ajili yetu. Naam ni muhimu sana watu wakajua hili na kuyakabidhi maisha yao kwa Yesu kwa kumwamini maana hukumu inakuja na tena imeshakuja, Barikiwa sana.

   Like

 3. Christmas kweli ni siku ya ajabu, hasa kujua kuwa kuna mkombozi ambae alitumwa kutuweka huru. ajabu watu wengi bado wamefungwa ma vifungo vya kila mamna. christmas hii watu wafunguliwe na kupewa nguvu mpya.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s