NITAMTAMBUAJE MKE AMBAYE MUNGU AMENIANDALIA?

Na:Patrick Sanga

Swali
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu Sanga.
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yenu kwa huduma mnayoitoa ambayo imekuwa msaada katika maisha yangu kama mkristo na kama mwanajamii. Mungu awabariki sana.

Pili naomba msaada wa maarifa juu ya namna ya kumtambua mke ambaye Mungu ameniandalia. Nimefanya maombi ya kumuomba Mungu mke mwema tangu septemba 2008 hadi sasa lakini bado sijapokea majibu ya maombi yangu. Ninaamini ninasumbuliwa na tatizo la upokeaji wa majibu ya maombi yangu jambo ambalo linahatarisha ustawi wangu kiroho.

Naomba kwa manufaa ya wengine pia ambao wana tatizo kama langu utupatie majibu hayo kwenye kipengele cha maswali na majibu. Ninaomba pia kwa ajili yangu na wengine ambao ninaweza kuwafikia unisaidie majibu hayo kupitia email address yangu hapo juu. Asante sana na Mungu awatimizieni haja za mioyo yenu na kuimarisha huduma yenu ili watu wengi zaidi waimarike kiroho.

 Lucas

 Majibu;

Hello Lucas, tunakusalimu kwa jina la Bwana, ahsante kutuombea, kututia moyo na kwa swali lako ambalo naamini majibu yake yatawafaa wengi kama ulivyoshauri katika swali lako.

Kaka Lucas swali lako ni pana sana na ‘it is more personal’ kimajibu, lakini namshukuru Roho Mtakatifu anayeweza kutupa majibu ya kutufaa .Katika swali lako nimegundua mambo mawili ya msingi ambayo natakiwa kuyatolea ufafanuzi, moja ni namna unavyoweza kumtambua mke ambaye Mungu amekuandalia na pili namna bora ya kuomba yenye kuleta matokeo.

Katika kujibu maswali haya mawili nitazungumzia mambo manne yafuatayo ambayo naamini baada ya kuwa umeyasoma haya utapata ufahamu wa kukusaidia katika kufanya maamuzi hayo yanayokukabili;

Jambo la kwanza; Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wa maisha yako (Isaya 55:8).

Oktoba 2006 naliandika kitabu kuhusu Njia kumi za Kibiblia zitakazokusaidia kumjua na kumpata mwenzi wako wa maisha. Katika ukursa wa nne wa kitabu hicho ndipo nilipoandika wazo hili hapo juu, kwamba, Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kumjulisha mtu mwenzi wake wa maisha.

Nimeona hata sasa nianze na msingi huu na hii ni kwa sababu vijana wengi hujaribu kuuliza wanandoa waliotangulia kwamba waliwapataje wenzi wao wa maisha kwa dhana ya uongozi wa Mungu? Kutokana na majibu ambayo vijana hao hupewa wengi humuomba Mungu na wanasubiri, Mungu aseme nao kwa njia ile aliyotumia kusema na mtu mwingine.

Kibiblia wazo hili siyo sahihi kwani, Mungu ana njia nyingi sana za kusema na watu wake katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nani atakuwa mwenzi wako wa maisha. Kwa mtu mmoja Mungu anaweza akasema naye kwa ndoto, mwingine kwa sauti yake, na mwingine kwa maono, mwingine kwa mafunuo, mwingine kwa amani ya Kristo, mwingine kwa kutumia watumishi/wachungaji nk

Jambo ninalojaribu kukuonyesha hapa ndugu Lucas ni kwamba ‘Mungu ana namna yake ya kukusaidia kumtambua mwenzi wako wa maisha, ambayo si lazima ifanane na ya mtu mwingine’. Na mara nyingi namna/njia hiyo haitofautiani sana na ile ambayo Mungu hutumia kusema nawe katika mambo mbalimbali. Hivyo tafuta kujua njia ambayo Mungu huwa anatumia kusema na wewe katika mambo mbalilmbali, naam kwa hiyo aweza kusema na wewe hata kuhusu mwenzi wako.

Jambo la pili; Jenga na kuboresha mahusiano yako na Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu ndiye aliyepewa jukumu la kuwa Msaidizi wako hapa duniani katika kufanya maamuzi mbalimbali. Watu wengi leo wanakwama au wanajikuta wamefanya maamuzi mabaya kwa kosa la kutokumshirikisha Roho Mtakatifu awasaidie. Mwambie Roho Mtakatifu nahitaji mwenzi(Mke), nisaidie kumtambua yupi ni wa kwangu, naomba uongozi wako. Roho Mtakatifu kwa hakika atakuongoza katika njia sahihi (Zaburi 32:8). Jambo la msingi ni kwa wewe kuboresha mahusiano yako na yake ili kuruhusu mawasilano mazuri kati yenu. Kumbuka mawasilano hutegemea mahusiano. Na jambo la msingi katika kuboresha mahusiano ni utakatifu na kutenga muda wa kuzungumza naye kwa njia ya maombi na neno.

 Jambo la tatu; Jifunze kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie kuhusu mwenzi wa maisha yako.

Hili ni jambo lingine la msingi kuzingatia. Endapo umeamua kufuata au kutafuta kumjua mwenzi wako kutoka kwa Bwana, basi ni vema ukaruhusu mapenzi yake juu yako yatimie. Wengi huenda mbele za Bwana wakimuuliza jambo hili lakini anapoleta wazo/jibu lake juu ya nani anafaa, wengi wakishamtazama huyo muhusika kimwili na kwa vigezo vyao humkataa na kusema si Mungu. Ni vizuri ukafahamu kwamba, kama Mungu ndiye aliyemleta mtu wa kwanza kwako na wewe kwa sababu zako binafsi ukasema huyu si wa kutoka kwa Bwana, maana yake umemzuia  Mungu asikusaidie kwenye hilo eneo, na hivyo usitegemee kusikia tena kutoka kwake, labda mpaka ujue kosa lako na kuomba toba.

Kumbuka usimuombe Mungu akujulishe mwenzi wako wa maisha wakati moyoni mwako tayari kuna mtu au watu ambao umeshadhamiria kutaka mmoja wao awe mwenzi wako, Mungu hawezi kusema hapo. Ikiwa unataka Mungu ahusike mpe asilimia mia moja hatafanya makosa kama Mwandamu.

Jambo la nne; Jifunze kuomba kimaswali

Najiribu kufikiri kwa nini umeomba tangu Septemba 2008 hadi sasa Mungu asijibu? Kwa ufahamu nilionao katika Kristo nina hakika yeye alisha-kujibu ila wewe ndiyo hukuelewa kwamba alijibu. Nina uhakika huo kwa sababu mtu amwendeaye Mungu kutaka kujua jambo, Mungu humjibu mtu huyo ili kumsaidia asipotee katika jambo hilo.

Naamini shida ipo kwako, huenda jibu ulilokuwa unataka wewe ni kuambiwa fulani ndiye mwenzi wako, kumbe kwa Mungu huenda alikuwa anasema huu si muda wake endelea kuomba maana kwa kila jambo kuna majira yake. Zaidi huenda shida iko kwenye namna unavyoomba na namna unavyopokea, au kuelewa Mungu anapoleta jibu.

Ili kuweza kupata ufumbuzi juu ya jambo hili jifunze kutumia mfumo wa maswali katika maombi yako, naamini utaona matokeo yake. Jifunze kuyatengeneza maombi yako kimaswali, omba huku ukitaka kujua/ukitafuta ufumbuzi wa lile unaloliombea kwa Mungu.

Jambo la msingi katika maombi haya ni kuwa na muda wa utulivu wa kuhojiana na kusemezana na Mungu wako. Kama vile ambavyo unaweza kuongea kwa simu na rafiki yako na mkasikilizana na kujibizana, ndivyo Mungu anavyotaka tujifunze kuwasilama naye. Unaeleza haja yako kwa swali na unampa muda na yeye akujibu. Najua kama hukuwa na mazoea ya kutumia mfumo huu, unapoanza itakusumbua, lakini endelea kufanya hivyo utona matokeo yake. Ili kupata ufahamu zaidi juu ya maombi soma link zifuatazo;https://sanga.wordpress.com/2006/10/23/mafundisho-ya-neno-la-mungu/ na pia https://sanga.wordpress.com/2009/10/29/jifunze-kuomba-kimaswali-3/

Ingawa swali  lilikuwa ni pana, naamini Roho Mtakatifu ameniongoza kujibu kwa namna ambayo kwako Lucas na  hata msomaji mwingine mwenye changamoto kama hii, mtakuwa mmepata ufahamu wa kusaidia. Kama umefuatilia kwa makini katika majibu yangu sijeleza moja kwa moja ni kwa namna gani utamjua mwenza wako, ila nimeelezea mazingira mbalimbali ambayo ukiyazingatia itakuwa ni rahisi kwako kumjua mwenzi wako wa maisha. Kupata ufahamu juu ya njia za Kibilia za kumjua na kumpata mwenzi, wasiliana nami nitakutumia kitabu bado nina nakala chache naamini kitakusaidia pia.  

Mungu akubariki, tuzidi kuombeana.

Advertisements

36 comments

 1. Nakushukuru sana na kukupongeza kwa kazi nzuri ya kuelemisha na kushauri watu mbalimbali na hasa vijana.
  Mimi ni kijana na nimebahatika kupata Msichana ambaye mategemeo yangu ni kuwa mke wangu na yeye alikubali. Baada ya muda amekuwa mzito sana kwenye mawasiliano yani waweza kumpigia simu asipokee na hata ukimtumia sms huwa hajibu na akijibu ni tofauti au kwa ufupi sana kitu kinachonipa wasiwasi sana. Je nifanye nini katika hili?

  Like

  • Hello ndugu Ngaiza sorry for late reply. Nashukuru kwa comment yako na kunitia moyo pia katia utumishi huu. Katika suala lako nashauri kwamba ni vema ukamtafuta huyo mdada na kuongea naye kwa ukaribu zaidi ili upate kujua kwa nini tabia yake imebadilika au yuko alivyo sasa kimawasiliano. Naamini baada ya kuongea naye utagundua mambo kadhaa. Sasa baada ya kugundua pima na kutafakari ni uamuzi sahihi wa kuchukua. Hata hivyo siku zote mahusiano ambayo yapo katika mapenzi ya Mungu Shetani huyapiga vita ili ndoa husika isifungwe maana Shetani hafurahi kuona watu wanaoana katika mapenzi ya Mungu, hivyo ni muhimu kuombeana sana.

   Like

 2. Bwana asifiwe sana Mtumishi Sanga na familia yako!

  Mbarikiwe sana kwa utumishi mwema mlionao ktk Nyumba na Familia kubwa mno ya BWANA. Tunajifunza mengi na kutiwa nguvu rohoni kupitia mafundisho yenu yaani wewe na mkeo. Napenda kukutia moyo mkuu kuwa uzidi na kusonga mbele. Bwana Yesu akutie nguvu ili uzidi kuinua misingi ya vizazi vingi zaidi.
  Nawatakia utumishi mwema. Amen.

  Wenu katika utumishi,
  Boniphace Msigwa.

  Like

 3. Swali;Mimi nimeshaoa ila swali langu ni kwa faida ya ambao bado hawajaingia ktk ndoa; Endapo kijana,akivutiwa na msichana halafu akataka ishara kuthibitisha kwa Mungu kwamba ndiye mwenzi na ishara zile zikatokea je bado shetani anaweza kuwemo ktk zile ishara tatu ili akupoteze ?

  Like

  • Binafsi nafikiri jibu laweza kuwa ndiyo au hapana, tegemeana na hali ya muomba ishara kiroho na ufahamu wake juu ya utendaji wa Mungu kupitia Ishara. Maombi ya Ishara ni maombi ambayo yanapaswa kufanywa na mtu mwenye ufahamu mzuri au wa kutosha kiroho mwenye uwezo wa kutofautisha ishara za Mungu na Shetani, kumbuka Musa alipogeuza fimbo kuwa nyoka na wachawi wa Farao waligeuza pia, kwa hiyo kuna baadhi ya ishara Shetani pia anaweza kuzifanya.

   Jambo la msingi ni kijana kumjua vizuri Mungu, kujua namna anavyozungumza, kujenga mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu ili hata akisema ujue huyu ni Mungu na siyo mungu. Binafsi sishauri vijana watumie sana maombi ya ishara katika kutafuta wenzi wao wa maisha kwani njia hii tokana na uzoefu wangu kwa vijana imegonganisha vijana wengi wa jinsia zote kwa mtu mmoja, bali kumjua Mungu vizuri ni ufunguo wa kuelewa mambo mengi hii ni pamoja na kumjua mwenzi wa maisha.

   Like

 4. Mungu akubariki kwaku tusaidia vijana.Nawezaj e kupata vitabu vyako? Ningependa kujua kama biblia imebainisha muda wa uchumba kabla ya kuwa wanandoa la,naomba ushauri wako.

  Like

  • Amina na utukufu apewe Yesu, kwa habari ya vitabu ningependa kujua uko Mkoa gani then nikueleze namna ya kuvipata. Kimsingi Biblia haijaweka bayana upi ni muda wa kuwa katika kipindi cha uchumba, ingawa kwa maana ya ushauri binafsi naona si vema kikawa kifupi sana au kirefu sana.Hata hivyo ni muhimu kujua utaratibu wa kanisa lako, maana kuna baadhi ya makanisa yanataka wachumba wake kwa muda wa miezi sita ili waweze kuwapa mafundisho maalumu kwa muda huo. Binafsi nashauri uchumba usiwe chini ya miezi mitatu na pia usizidi miezi sita.

   Like

   • Ubarikiwe kwa majibu mazuri.Kwa sasa nipo Shinyanga chuoni mpaka mwezi 5-2013 baadaye nitarudi kwetu Iringa.Ninge penda kujua vile naweza kupata vitabu vyako ktk mikoa hii miwili.

    Like

   • Utukufu kwa Mungu, kwenye hiyo Mikoa miwili sijapeleka vitabu vyangu, lakini twaweza wasiliana, halafu ukanipa anuani yako, then nikakutumia huko uliko.

    Like

 5. Mtumishi nimebarikiwa na majibu uliyoyatoa hapo juu kwami Nimeimarika.MUNGU akuinue wewe na familia yenu.Mimi nipo Moshi kwa sasa nitapataje vitabu vyako? Nijibu kupitit email yangu Mtumishi.

  Like

  • Bwana Yesu asifiwe ndugu,naitwa Albert niko arusha.nimefuatilia mada ilokuwa hewani na mtumishi Sanga.kwa kweli nimevutiwa sana kwani mi pia ni muda mrefu namwomba Mungu kwa habari ya mwenzi ila nado sijapokea majibu.ndugu yangu nishirikishe baraka ili nami nijue namna Mungu alivyokusaidia ukampata mwenzi wako.ubarikiwe sana.nasubiri kwa hamu kubwa ndugu yangu.

   Like

 6. Nashukuru kwa mafundisho yako Mtumishi Sanga, yananijenga kiroho. Ila kuna kitu sikielewi naomba unijibu make najua ww unaufaham zaid. Je ntawezaje kuomba kwa maswali? Make sijui hata njia ya kuuliza maswali kwa Mungu. Pili, inawezekana kuomba kwa Mungu kwa mahitaj zaid ya moja na Mungu akakutimizia yote au mtu anapaswa kupelekb hitaji moja moja? Naomba kama unaweza nijibu kwa email yangu. Ubarikiwe sana.

  Like

 7. hata mm moyo wangu umefarijka kwa majibu naamin bwana Yesu atanijibu kwa ufaham huu mana amesema tukiijua kweli tutakuwa huru

  Like

 8. Asanteni Sana Watumishi Wa Mungu Kwa Kuendelea Kulisukuma Gurudumu La Mungu Ipasavyo Mungu Aendelee Kuwatia Nguvu Katika Kazi Yake Hata Ienee Ulimwenguni Kote OMBI langu ni naomba milango inayohusu maonyo kwa watoto wa kikristo waliozaliwa katika ukristo wanaohisi kuwa hyo sababu itawafanya waione mbingu wengne wanjifariji kwasababu wazazi wao wameokoka wao hata wafanye dhambi wazaz wao ni dhamana nilisoma sehemu nimesahau

  Like

 9. Nakusalimu katka jina la Yesu kristo swali langu ni hili: kwan kuna umri au mtu akifikia miaka fulan ndo anatakiwa awe na mchumba?

  Like

  • Hakuna umri muafaka hasa ukizingatia historia ya Biblia, wapo walioa wakiwa na miaka kuanzia kumi na sita na kuendelea. Na hata wakati wa sasa tunashuhudia watu wakioana wengi wao hata miaka 20 hawajafika. Kimsingi mtu anayeoa au kuolewa anapaswa kuwa tayari kuoa au kuolewa kaba ya kufanya hivyo. Hii ina maana anapaswa kuwa mtu aliyekuwa na kukomaa kifikra na kimaamuzi hata kustahili kuishi na mwenza. Hili ndilo jibu ninaloweza kukupa hapa.

   Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s