USHAURI KWA WAJANE

Na:Patrick Sanga

Mpenzi msomaji katika category hii ya “maswali na majibu” huwa naandaa masomo yanayolenga kujibu maswali ya wasomaji mbalimbali wa blog hii kama yanavyoulizwa na wasomaji husika kwa njia mbalimbali. Mwezi huu nimeona ni vema nikajibu swali lililoulizwa na dada L  kuhusu wajane. Majibu yangu hayakuzuii wewe msomaji mwingine kuongezea majibu yako juu ya maswali wanayouliza wasomaji mbalimbali.

Swali; Ahsante mtumishi kwa masomo yako mazuri. Mimi nakiri kuwa yamenipa uamsho mkubwa. Naomba niulize, unatushauri nini sisi tulio wajane tena vijana? Mimi ni mjane tokea mwaka 2004. Nina miaka 39 na watoto wawili wakike, naomba uniombee sana Mtumishi. Dada L     

Jibu; Hello dada L na kwa wajane wengine, nawasalimu kwa jina la Bwana Yesu. Pole sana kwa kumpoteza mwenzi wako wa maisha tokea mwaka 2004. Bwana akuwezeshe na kukutia nguvu katika hali yako ya sasa.

Paulo alipokuwa akimfundisha Timotheo kwa habari ya makundi mbalimbali ambayo atapaswa kuyaongoza likiwemo kundi la Wajane alimwambia maneno yafuatayo katika ile 1Timotheo 5.

(3)Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli, (5)Basi yeye aliye mjane kwelikweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku, (6)Basi yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai, (11)Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa, (13) Usiwe mvivu, epuka kuwa mchongezi na mdadisi, usinene maneno yasiyokupasa, (14)Basi, napenda wajane ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani, ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu, (15)Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. Nakushauri pata muda usome kuanzia msitari wa kwanza hadi wa kumi na sita.

Mtume Paulo alipokuwa akiongea na wandugu wa Korinto kuhusu Wajane pia, aslisema hivi;

1Wakorinto 7:8-9 “Lakini nawaambia wale, wasiooa bado na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilvyo, lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”.

Baada ya kuangalia maandiko hayo hapo juu nashauri mambo yafuatayo kwako na wajane wote na hasa wale ambao bado ni vijana;

 • Weka tumaini lako kwa Mungu

Katika hali ya kawaida na kibindanamu kuna namna mwenzi wako alikuwa msaidizi mkubwa kwako juu ya mambo mbalimbali pamoja na kuangalia na kutunza familia yenu kwa ujumla. Punde mmoja wenu anapoondoka mambo mengi hubadilika tena kwa kuharibika. Hii ni kwa sababu wajane wengi huwa wanakuwa waliweka matumaini yao kwa mwenzi wake, kwa hiyo kitendo cha mwenzi wake kuondoka anafikiri huo ndio mwisho wa maisha yake mazuri na    ya furaha hapa duniani. Fikra hiyo si sahihi, wewe weka tumaini lako kwa Bwana ukijua yeye ndiye mume wa Wajane na Baba wa yatima, mtetezi aliye hai, hatashindwa kukulisha wala kuwatunza wanao.(Isaya 54:5)

 • Endelea kuishi maisha ya utakatifu

Kuondokewa na mumeo isiwe sababu ya wewe kupunguza jitihada yako katika kumtafuta na kumpendeza Bwana. Endelea kudumu katika maombi na sala mchana na usiku, jizuie nafsi yako kutenda dhambi na zaidi chunga sana matumizi ya kinywa chako. Tumia kinywa chako katika mambo yenye kuleta utukufu kwa Mungu na  sio kusengenya, kuchonganisha na mambo yanayofanana na hayo.

 • Ni vema ukaolewa kama huwezi kujizuia kutenda dhambi.

Mtume Paulo kwa Wakorinto alitoa ushauri kwamba ni vema Wajane waamue kutoolewa au kuoa tena. Lakini kwa Timotheo anamwambia, napenda wajane ambao si vijana waolewe, tena wazae watoe na wawe na madaraka ya nyumbani.

Usije ukafikiri Paulo alijichanganya, hapana. Ushauri wa Wakorinto ulitokana na namna ambavyo Paulo aliona ndoa nyingi zikisababisha watu kumokosea na kumkosa Kristo. Paulo alikutana na watu ambao walijuta kwa nini waliamua kuoa au kuolewa na ndio maana akashauri kwamba basi ni vema kuto oa au kuolewa kama mtu ataweza kujizuia asiwakwe na tamaa na kisha kuanguka dhambini.

Biblia inasema ‘Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe’ (1 Wakorintho7:2).

Hivyo kutokana na umri wako binafsi ningeshauri ni vema ukafikiri na ukachukua uamuzi wa kuolewa tena. Maana ni heri ukaolewa kuliko kushindwa kujizuia nafsi yako ukajikuta unaingia katika dhambi na fedheha. Kama unafikiri unaweza ukaishi katika hali hiyo ya sasa ni bora zaidi, lakini Kibiblia maadam mwenzi wako alifariki uko huru kuolewa tena(Warumi 7:1-3). Kama ukichukua uamuzi wa kuolewa basi usiharakishe, bali muombe Mungu akuongoze na akuunganishe na mtu ambaye atakufaa na zaidi atawapenda watoto wako.

 • Watumie wajane kwelikweli(Wazee)

Pia ni vema ukawatafuta akina mama ambao wamekutangulia katika hali hiyo ya ujane na wameshuhudiwa katika Bwana kuwa waaminifu. Watumie hao  kuomba ushauri kwao, naamini watakushauri vema pia katika Bwana.

 • Endelea kuwa mwaminifu kwa Mungu

Naam mwisho nakushauri endelea kuwa mwaminifu kwa Mungu na Mungu atakuwa mwaminifu kwako. (Zaburi 18:25-26).

 Mungu akubariki naamini ujumbe utakusaidia katika safari hii tuliyo nayo. Bwana akulinde na kukutunza na watoto wako wazuri.

 

Advertisements

4 comments

 1. Mtumishi mimi ni mwimbaji binafsi wanyimbo za injili, ambaye lengo la huduma hii ni kwakile Mungu atakacho nibariki ktk huduma yangu iwe kwa kualikwa, kuuza cd nitawawezesha waishio ktk mazingira magumu na tayari nimeshaanza kwa kuwapatia wajane 35 nguo na mchele pia mayatima 15 vifaa vya shule changamoto ni niliofanya nao mkataba wa kuisambaza cd sokoni ibilisi amezuia hazitoki nashindwa kutekeleza kusudi la huduma hii kwani fedha haipo, nifanye nini?.
  A.(0713101616/0783101616)

  Like

  • Samahani sana kuchelewa kujibu, Mungu akubariki sana kwa huduma njema unayofanya kuna mambo mawili yanaweza kuwa chanzo cha changamoto husika kwako, je unatoa zaka katika fedha unayopata licha ya sadaka husika kwa wasiojiweza? Pili licha ya kwamba unasaidia wasiojiweza unafanya hivyo kwa uongozi wa Mungu au unapeleka pale unapojisika wewe kufanya hivyo? Sihitaji unijibu maswali haya lakini nimeona nikufikirishe kutoka kwenye kona hii, hata hivyo tambua kwamba Shetani hafurahii kuona likifanikiwa hivyo atadumu kulipiga vita, hivyo usichoke kuombea huduma yako, nasi twakuombea.

   Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s