VITA VYA KIROHO (Sehemu ya mwisho)

 Na:Patrick Sanga

Ili kusoma sehemu ya nne bonyeza link ifuatayo https://sanga.wordpress.com/2010/11/01/vita-vya-kiroho-part-4/

Mpendwa msomaji katika sehemu hii ya mwisho nimeandika dondoo kadhaa za msingi kama ‘summary’ ya somo hili la vita vya kiroho. Ili uweze kulielewa kwa undani, ni vizuri ukasoma somo lote kuanzia sehemu ya kwanza.  

Dondoo za msingi kukumbuka na  kujua kuhusu vita vya kiroho;

 • Vita vya kiroho ni vita ya matakwa kati ya ufalme wa Mungu na ule wa Shetani kwa kumtumia mtu aliyeko katika ulimwengu wa mwili.
 • Mwanadamu ataendelea kuwa katika mapambano na ufalme wa Shetani mpaka Bwana Yesu  atakapolichukua kanisa lake.
 • Ushindi wako katika vita vya kiroho utategemea ufahamu wako juu ya Mungu na namna unavyosimama kwenye nafasi yako (Luka 10:19).
 • Jambo lolote unaloliona kwenye ulimwengu wa mwili lilianzia kwenye ulimwengu wa roho.
 • Ulimwengu wa roho ni halisi kama ulivyo ulimwengu wa mwili. Ndani yake kuna ufalme wa nuru na ufalme wa giza. Mungu ni mtawala wa ufalme wa nuru na Shetani ni mtawala wa ufalme wa giza. Naam ulimwengu huu ni makazi ya viumbe wasio na mwili wa damu na nyama.
 • Siku zote vita huanzia katika ulimwengu wa roho kwa mfumo wa mawazo, naam ni kwa kila ufalme kupanda wazo lake kwenye nafsi ya mtu.
 • Shetani hapigani vita mpaka aone kwanza Mungu ameachilia wazo gani kwa watu(mtu) wake kwenye ulimwengu wa roho, ndipo naye analeta la kwake ili kupinga la Mungu.
 • Mawazo au fikra ni nguzo kubwa ambayo inatumiwa na wafalme hawa katika ulimwengu wa roho.
 • Mungu/Shetani kila mmoja anapotaka kufanya jambo kwenye ulimwengu wa mwili wanatafuta mtu wamtumie kwa kuwa wao ni roho.
 • Mtu akishinda vita kwenye ulimwengu wa roho, atashinda pia kwenye ulimwengu wa kimwili. Naam akishindwa katika ulimwengu wa roho na kwenye ulimwengu wa mwili atashindwa pia.
 • Maamuzi ya nini unataka kitokee kwenye ulimwengu wa mwili yanapaswa kufanyika kwanza katika ulimwengu wa roho.
 • Mapambano yetu katika ulimwengu wa roho ni dhidi ya  Shetani na ndiyo maana   Yesu aliwapa mamlaka wanafunzi wake dhidi ya roho chafu, mapepo nk Marko 16:15, Mathayo 10: 1, 6-8, Luka 9:1
 • Kumbuka siku zote Bwana ni mtu wa vita na siku zote yeye ni mshindi. Zaidi Malaika wa Bwana wapo upande wetu kutushindia na kutusaidia katika vita vya kiroho (Zaburi 34:7, 91:11).
 • Katika vita yoyote ya kiroho, mtu uliyeokoka hupaswi kuwa wa kushindwa kwani tayari Yesu alishamshinda Shetani kwa niaba yako, jukumu lako ni kujua namna ya kushirikiana na huyu Yesu akuongoze jinsi ya kushinda kama alivyo shinda.
 • Katika ulimwengu wa roho kila mtoto wa Mungu ana nafasi yake anayotakiwa kusimama na kutekeleza wajibu wake.
 • Mtu mwenye kuijua na kusimama vizuri kwenye nafasi yake katika ulimwengu wa roho ni pigo na tishio kubwa kwa Shetani.
 • Unaweza kuwa na cheo kikubwa kwenye ulimwengu wa mwili, lakini kwenye ulimwengu wa roho cheo chako kisitambulike.
 • Cheo chako cha ulimwengu wa mwili hakiamui nafasi yako kwenye ulimwengu wa roho. Bali namna unavyosimama na kuwajibika vema kwenye nafasi yako  katika ulimwengu wa mwili hata kwenye ulimwengu wa roho ndivyo unavyokuwa na nguvu za kiutawala.

Ni imani yangu kwamba mfululizo wa masomo haya utakuwa umekusaidia na kukuongezea ufahamu wa kutosha juu ya vita vya kiroho.

‘Nakutakia ushindi katika kuvipiga vita hivi vya kiroho’

 

 

Advertisements

3 comments

 1. Mungu akubariki sana kwa somo zuri.
  Nahitaji maombi yako ili Mungu anijalie ratiba nzuri ya kusoma Neno la Mungu ili nimjue Bwana wangu kwa undani zaidi.

  Like

 2. napenda sana mambo kama haya au mafundisho ya kiroho. Na nimefurahi kukuona ukitoa mafundisho yaliyo jaa uwepo wa Mungu. Ila mi nikija nahitaji mafundisho pia ya ujana maana na shetani naye anaupenda ujana. Thanks

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s