KITABU, KITABU, KITABU( Ruhusu mapenzi ya Mungu yatimie kuhusu mwenzi wa maisha yako)

 

 

Patrick & Flora Sanga

 

Awali ya yote tunamshukuru sana Mungu, kwa kipawa cha Uandishi, alichotujalia. Mke wangu pamoja nami tumeamua kwamba tutahakikisha tunatumia kipawa hiki siku zote kwa utukufu wa Mungu, katika kuujenga mwili wa Kristo.

 

Katika mwaka huu wa 2010 tumeweza kuchapisha kitabu cha pili chenye kichwa kisemacho RUHUSU MAPENZI YA MUNGU YATIMIE KUHUSU MWENZI WA MAISHA YAKO’. Kitabu cha kwanza nalichapisha mwaka 2006 (kabla sijaoa), kilihusu ‘NJIA KUMI ZA KIBIBLIA ZA KUKUSAIDIA KUMJUA NA KUMPATA MWENZI WAKO WA MAISHA’.

 

Ndani ya mwaka wa 2010 tumeandika zaidi ya vitabu saba vya kiroho. Katika hivyo tumefanikiwa kuchapisha kitabu hiki kimoja, ingawa lengo letu ilikuwa ni kuchapisha vitabu viwili. Jambo la msingi kwetu ni kuzingatia uongozi wa Mungu katika kuvichapisha vitabu hivi, maana katika orodha ya vitabu saba, si jambo jepesi kuamua kwamba ni katbu kipi kianze na kipi kifuate. Tunaamini kwamba, ni mapenzi ya Mungu kitabu hiki kichapishwe katika majira haya, maana tulimwomba Bwana uongozi wake.

 

·        Yaliyomo

 

Kitabu kina jumla ya sura nne kama ifuatavyo;

 

Sura ya kwanza – Ni mpango wa Mungu uoe/kuolewa sawasawa na mapenzi yake.

Sura ya pili – Mungu ndiye anayewajibika kukupa mwenzi wa maisha, ni jukumu lako kuruhusu mapenzi yake yatimie.

Sura ya tatu – Jifunze uhalisia wa mambo  haya  kupitia Yakobo, Hosea na Samweli ndani ya Biblia.

Sura ya nne – Mwenzi wako ana nafasi kubwa sana katika kukusaidia kulitumikia kusudi la Mungu maishani mwako.

 

 Na katika ukurasa wa mwisho wa kitabu kuna sala ya toba.

 

·        Kwa nini kitabu hiki wakati huu?

Suala la mwenzi wa maisha limekuwa changamoto kubwa sana katika kizazi cha sasa. Kwani wapo wanandoa wengi, ambao leo wanajutia maamuzi yao ya kuoa au kuolewa. Naam moja ya sababu kubwa za majuto hayo kwa wanandoa wengi, ni kuoa au kuolewa nje ya mapenzi ya Mungu.

 

Hivyo Kitabu hiki kinaeleza kwa undani nafasi ya Mungu katika kumpa mtu mke/mume, sababu zinazomfanya Mungu afanye hivyo, kwa namna gani mtu anawajibika kuoa au kuolewa sawasawa na mapenzi ya Mungu, Dondoo za msingi kujua kuhusu mapenzi ya Mungu, nafasi ya mwenzi wako katika kulitumikia kusudi la Mungu na mwisho mifano kadhaa ndani ya Biblia itakayokusaidia kufanya maamuzi yako kwa kuzingatia mapenzi ya Mungu.

 

Lengo la kitabu hiki ni kukupa ufahamu na maarifa juu ya mapenzi ya Mungu katika suala zima la kumpata mwenzi wako wa maisha, ili kukusaidia uweze kulitumikia vema kusudi la Mungu, kwani, mwenzi wako wa maisha ana nafasi kubwa sana katika kulitumikia kusudi la Mungu.

 

·        Upatikanaji wa vitabu

Vitabu hivi vitaanza kupatikana kuanzia mwenzi Januari 2010 katika maduka   ya vitabu na wauzaji binafsi Mikoa mbalimbali. Kama pia unafahamu Bookshop/wauzaji ambao twaweza peleka vitabu hivi basi wasiliana nasi ili viweze kusambazwa na kuwafikia watu wengi kwa urahisi. Taarifa zaidi za kule vinakopatikana vitabu hivi tutawajulisheni.

 

·        Tamati

Ni imani yetu kwamba Mungu atagusa na kuponya maisha ya watu wengi ya sasa na ya baadaye, hasa kwa wale ambao wanatarajia kuja kuishi kwa pamoja kama wanandoa. Kwa wewe ambaye bado hujaoa au kuolewa ni vema ukapata nakala ya kitabu hiki, kwa hakika kitakuongezea ufahamu na maarifa ya kukusaidia kufanya maamuzi sahihi katika mapenzi ya Mungu.

 

Ubarikiwe, endelea kuombea kitabu hiki kifanyike baraka na uponyaji kwa kila atakayekisoma.

Advertisements

14 comments

 1. Bwana asifiwe,

  Asante sana kwa kitabu hiki (Ruhusu mapenzi ya Mungu yafanyike) nilichosoma habari zake hapo juu. Je nitaweza kupata vitabu hivi kwa ajili ya vijana wetu kanisani. Mimi ni mchungaji na niko Kenya, mkoa wa pwani mji wa Malindi.

  Like

  • Mimi naitwa sylvere na ni mwalimu wa vijana katika inchi ya Marecani ni ngependa unijulishe jisi yakupata au kununuwa vitabu vyako. kwasababu vimenibariki sana Mungu aendelee kuku bariki pamoja na mke wako. Na ningependa tuzidi kuombeana.

   Like

   • Mungu akubariki na kukufanikisha katika huduma yako kwa vijana ndg. Sylvere. Kwa habari ya namna ya kupata vitabu, nimeshajibu kwenye email yako. Barikiwa sana.

    Like

 2. Ahsante sana pastor Patric na Flora sanga Mungu akubariki sana kwa kitabu hicho!
  je kitabu hicho nitakipataje Mimi ninapatikana Mkoa wa Kigoma-Tanzania

  Like

  • Amina, kwa mkoa wa Kigoma bado vitabu hivyo havijafika, lakini naweza kukutumia kwa basi au posta. Tuawasilanae kwa namba zangu 0755816800 au 0715816800 kwa urahisi na uharaka wa mawasiliano.

   Like

 3. Ubarikiwe sana na Bwana Yesu mtumishi Sanga, ama kweli nimekuwa nikijiuliza kwenye mtandao kuna kitu chochote cha kunifaa kiroho? lakini leo (26/12/2011) nimegundua masomo yako, nami nitakuwa nayafuatilia ili kujifunza zaidi.

  Like

  • Amina, utukufu kwa Yesu endapo umepata unapata kitu cha kukufaa kupitia blog hii, naam hayo matarajio yangu kama Mwandishi, ahsante kwa kunitia moyo, niombee kuna masomo mengi yanakuja mwaka 2012, naam maombi yako ni muhimu sana.

   Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s