UMEJIAANDAJE KWA TUKIO LA UNYAKUO? (Part 1)

Na: Patrick Sanga

Nakusalimu kwa jina la Yesu!

Ili uweze kuelewa somo hili mpenzi msomaji nakushauri tafuta muda usome vizuri sura ya 24 ya kitabu cha Mathayo.

Mimi nitanukuu mistari michache  kwenye sura hii;

Mathayo 24:36-44 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala mwana, ila baba peke yake. Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adam.

 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizovyokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adam. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa mmoja aachwa, wanawake wawili watakuwa waskisaga; mmoja atwaliwa,mmoja aachwa.

 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamunu neon hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingeliacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyoidhani mwana wa Adam yuaja”.

 Nakumbuka ilikuwa tarehe 27/03/2010, majira ya saa kumi na moja za jioni, nikiwa nimekaa chumbani kwangu, naangalia mkanda kwenye Laptop na nilikuwa na mke wangu. Ghafla nikahama katika ulimwengu huu kimawazo nikaenda kwenye eneo jingine, picha ya siku ya unyakuo ikanijia, na nikaanza kuona kwa sehemu nga kidogo jinsi unyakuo utakavyokuwa, nikaona  nguvu fulani ambayo inamnyanyua mtu na kwenda naye juu.

 Kwa ujumla si rahisi kuandika vizuri jinsi nilivyoona, lakini niliona watu wakianza kunyanyuliwa na dunia ilikuwa kama imepigwa na butwaa!. Baada ya maono haya nikaanza kutafakari na moyoni mwangu nikasikia uzito kwenye moyo kana kwamba Yesu ndiyo anarudi saa ile, ndipo nikasikia sauti kwenye ufahamu wangu ikiuliza umejiandaaje kwa ajili ya unyakuo na umewaandaaje watu wangu kwa ajili ya unyakuo?

 Wakati mambo hayo yanaendelea, mke wangu alikuwa akinisemesha lakini sikumelewa ingawa nilikuwa namsikia kwa mbali, macho yangu yalielekea kwenye mkanda lakini sikuelewa kilichokuwa kinaendelea pia. Baada ya dakika kumi hivi ndipo nikarudi kwenye ufahamu wangu wa kawaida nikaanza kutafakari na nikachukua hatua ya kwenda kuomba kwanza.

 Mara nyingi jambo hili limekuwa likinijia na Bwana ameendelea kunifundisha vitu vingi juu ya suala hili. Kutokana na yale ambayo nimejifunza na ninaendelea kujifunza katika neno lake imenilazimu kuanza kuandika mfululizo wa somo hili mpaka hapo Yesu atapokuja ikiwa atatukuta tukiwa hai au hadi pale nitakapoondoka kwa njia ya kifo. Na nimeamua kufanya hivi kwani swali la pili niliulizwa umewaandaaje watu wangu kwa tukio la unyakuo?. Nitaandelea kuweka mafundisho haya kwenye blog, ili kila mtu anayetaka kuwa tayari kwa unyakuo basi ajifunze na ajue namna ya kujiandaa.     

 Mpenzi msomaji maswali haya mawili kwangu yaliniumiza sana. Unajua wakristo wengi kwa jinsi tulivyo kila mmoja ana amini kwamba Yesu akija leo ataenda mbinguni. Hakuna mtu unaweza ukamsikia anasema siku ya unyakuo nitaachwa. Unajua ni kwa nini?. Wengi si kwa sababu Roho wa Yesu ndivyo anavyowashuhudia kwamba wataenda na Bwana, bali ni kwa sababu Shetani amepanda wazo kwenye fahamu zao kwamba Mungu hawezi kuwaacha hata kama mtu hayatendi mapenzi yake.

 Nisikilize kanisa, maadam niliulizwa nimewaandaaje watu wake, nami nina ujasiri wa kuandika na kukufundisha mambo mengi ambayo najua Shetani asingependa uyasome na kuyasikia. Nami nakuomba anza sasa kufuatilia masomo nitakayokuwa naandika kuhusu unyakuo, lakini pia fuatilia masomo ya watumishi wengine juu ya unyakuo ili uweze kuwa tayari kwa tukio hili la kushangaza na kuogofya.

 Nini anachokifanya Shetani nyakati za sasa?

 Katika kipindi hiki cha dakika za mwisho Shetani anatumia hila na uongo wake kuwapumbaza watu wengi kuhusu unyakuo na habari za Yesu kwa ujumla. Anachokifanya shetani ni kuhakikisha anazuia kwa kila hali watu wasisikie habari za Yesu na hasa kuhusu matukio ya mwisho wa dunia. Na hii ni kwa sababu anajua chanzo cha imani katika Kristo ni kusikia habari za Kristo Yesu.

 Na kwa wale waliokwisha kusikia ana hakikisha hawaliweki kwenye matendo lile neno. Si hivyo tu bali, anajitahidi kuwafanya watu wasiamini kweli ya neno la Mungu. Anapofusha amri/sheria nyingi za Mungu kwenye fahamu za watu. Ananyanyua watumishi wa ufalme wa giza na kuwapa uwezo mkubwa na hao watumishi anawaagiza kutofundisha kweli yote ya neno la Mungu (kumbuka yeye hujigeuza na kujifanya malaika wa nuru). Si hivyo tu bali hata wale watumishi wa ufalme wa nuru anawapumbaza na kuwalaghai kwa hila na kuteka fahamu zao kwa njia nyingi ili wasiwafundishe wanafunzi/washirika wao kweli yote ya neno la Mungu. Shetani anawafanya watu kuwa ‘busy’ na kazi na pia mambo yasiyo ya msingi /yasiyofaa hata kama ni halali.

 Sikia kanisa, si tu kusema kwamba  umeokoka ndiyo tiketi ya kwenda mbinguni. Warumi 2:13 inasema “kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki”.

 Ndugu yangu maadam umeamua kumwamni Yesu, sharti uwe tayari kufuata sheria zinazoongoza ufalme/utawala wake, na sio tu kusema mimi ni mwanachama wa Yesu. Je, unakumbuka jinsi shetani alivyotumia hila kuwadanganya Adam na Eva pale bustanini (Mwanzo 3:1-7). Naam hata leo ndivyo anavyofanya, na kwa njia hiyo atawafanya wengi kuachwa na Bwana siku ile itakapofika.

 Je, unajua kwa nini anafanya hivyo?

 Lengo ni kuwapumbaza watu wasiwe macho kiroho/wasikeshe wakidumu kuzitenda amri za Bwana, wala kutafakari neno lake wasije wakafunguka macho yao na kugundua hila zake. Yesu alisema kama ilivyokuwa siku za Nuhu ndivyo itakavyokuwa katika kizazi hiki.

 Je kwa Nuhu ilikuwaje?

 Watu walikuwa wakiendelea na shughuri zao za kila siku kama kawaida, wakioa, wakiolewa, wakilima, kufanya biashara nk. Unisikilize ndugu hakutakuwa na matangazo kwenye vyombo vya habari kwamba watu jiandaaeni Bwana Yesu atakuja siku au mwezi fulani kulichukua Kanisa Lake. Itakuwa ni kitendo cha ghafla na bila wengi kutarajia. Ni katika saa usiyoidhani wewe ndipo Bwana atakapokuja.

 Kwa hiyo Shetani anawapumbaza watu wawe ‘busy’ na mambo mengi ili ile siku Bwana atakapokuja waachwe. Nasema usikubali, maadam umeokoka wewe si mtu wa giza, haipasi siku ile ikukute kama vile mlevi. Huu ndio wakati wa wewe kujiandaa na kuwaandaa wengine.

 Sikia ee, Kanisa, kurudi kwa Yesu kumekaribia sana. Mara nyingi kwenye ufahamu wangu wazo la unyakuo huwa linanijia na nina amini kwanza ni kwa ajili yangu kujiandaa, lakini kila likinijia huwa nafikiri na watu wengine ambao bado hawajaokoa, lakini pia na wale ambao wameokoka lakini maisha yao hayapo sawasawa na mapenzi ya Mungu tunawasaidiaje?.

 Ndugu zangu siku hiyo haisemeki, itakuwa ni siku ya aibu, huzuni isiyo na kipimo, majuto yasiyosemeka. Ni heri kama usingelizaliwa mpenzi msomaji, kuliko kuokoka halafu ukaachwa kwenye ile siku. Huruma ya Yesu itafikia mahali itakoma. Yesu anatuvumilia sana, na laiti ungelijua namna anavyokulinda usife na sababu kubwa ikiwa ni kukupa nafasi ya kutengeneza maisha yako, usingefikia mahali pa kujisifu, kuhukumu wengine, kudharau na kuishi maisha ya kienyeji kiasi hicho.

Ngoja nimalizie kwa sentensi hii, siku moja nikiwa natembea kwenda kanisani Bwana aliniambia “watu wengi ninawapigania na kuwalinda wasikutwe na mauti, maana najua wakifa kwa kuwa hawako tayari hawawezi kuja kwangu, inaniuma sana hao watu wanapotafsiri vibaya ulinzi wangu kwao, wao wanafikiri ni kwa sababu wana haki ya kuishi tokana na elimu, fedha, madaraka yao, kumbe sivyo. Na mbaya zaidi licha ya kuwatengenezea watu hao fursa nyingi za kutubu/kutengeneza njia zao, wao hawakubali kutii/kubadilika. Sina namna ya kumsaidia mtu ambaye hayuko tayari kunitii”.

 Mpendwa wangu uvumilivu wa Mungu kwako na kwangu kwanza ni ili tutengeneze njia zetu, ukiendelea kufanya shingo ngumu, huruma yake itafika mahali na kukoma. Watu wengi ambao wako kuzimu hivi sasa, ujue sehemu kubwa walipuuzia nafasi/fursa ambazo Mungu aliwapa za wao kutengeneza njia zao.

 Ujumbe huu unakuja kwa lengo la kukuonyesha mambo ya msingi unayotakiwa kufanya kama sehemu ya maandalizi tayari kwa siku ya unyakuo.

 Tutaendelea na sehemu ya pili…

Advertisements

23 comments

 1. NInakuabudu Bwana wangu ,Ninakuheshimu Mfalme wangu ,Ninakuhitaji MUngu wangu ninakuomba unitakase Roho yangu, Mawazo yangu,na nafsi yangu na mwili wangu Baba, kwani nahitaji kufika kwako kama kuna kitakachozuia Bwana wangu na Mwokozi wangu nimekukaribisha ndani ya moyo wangu, Bwana nigeuze nimekubali nimekuchagua YESU usiniache, Nakusihi nichonge upendavyo,Lengo langu ni kuishi na wewe milele,Nakupenda Yesu sana. Mtumishi SANGA nakutakia amani ya YESU WEWE NA MAMA YETU.

  Like

  • Amina ndg. Chuli, nashukuru kwa comment yako na kwa website nyingine za kiroho ambazo zinatujenga na kutufundisha zaidi. Ubarikiwe na Bwana Yesu pia na tuzidi kuombeana.

   Like

 2. Mwalimu ubarikiwe.

  Nimekuwa napata shida sana na watu ambao wamekuwa wakikashifu na kupinga ukweli kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo. Sasa naanza kupata ufahamu wa kuniwezesha kuwajibu na kuwaonyesha ukweli.

  Nisaidie zaidi katika hilo Mwalimu.

  Like

  • Ni kweli Ndg. Ndunguru, ukisoma Biblia yako vizuri utagundua sio rahisi watu wote wakamwamini Yesu kwa kiwango kile ambacho ungetegemea wafanye hivyo. Ni jukumu lako kama askari wa Bwana kuendelea kujifunza neno la Bwana na kuhakikisha linakaa kwa wingi ndani yako. Bwana atatumia neno hilo kukufanya uwafikie wengine. Hata hivyo kisikusumbue sana kama mtu hataki kumpokea Yesu uliye naye wewe, cha maana endelea kuwaombea na kuomba ufunuo zaidi kutoka kwa Bwana wa namna ya kuwafikia na kuzungumza nao taratibu, kwa maelewanao na siyo kwa kubishana. Kadri Bwana anipavyo nafasi nitaendelea kukupa miongozo ya kukusaidia kuwafikia watu kwa ajili ya Bwana.
   Is me Patrick.

   Like

 3. Bwana YESU asifiwe! Nashukuru Mungu kwa ajili yako! Nimesoma kuhusu UNYAKUO na ningependa kujua zaid kuhusu huduma yako je inapatikana wap? Na namna ninavyoweza kupata mafundisho zaid!
  Noah
  from karatu-ARs

  Like

  • Hello Noah’ Sorry for late reply, Kimsingi mimi nipo Dodoma ni mshirika wa kanisa la EAG(T) Central hapa Dodoma mjini. Mimi nimepewa tu kufundisha mwili wa Kristo duniani kwa njia ya kuandaa masomo kwa style hii lakini sina huduma kwa maana ya kanisa ninalolihudumia kama Mchungaji.

   Naomba maombi yako zaidi maana tangu nilipoanza kuandika somo hili la Unyakuo na lile la Vita vya kiroho, vita ninayokutana nayo katika kuandaa masomo haya ni kubwa sana. Ubarikiwe na Bwana.

   Like

 4. ooooh! Mungu akushike mkono mtumishi umemtingisha shetani ametoka alikokuwa ,alipoona tu umeanza kufunua jambo hilo kaona aje atishe haweziiiiiiiiiii amechelewa kwa sasa maana tazama nalikuwa nimekufa na sasa ni HAI wow atakoma na uasi wake na tunakufunika kwa damu ya Yesu wewe na mama yetu tunawapenda hawezi hawezi hawezi na hataweza maana Yesu anaishi leo na kesho anaishi hana mwanzo wala hana mwisho. Shetani hana lake tena lazima watu wamwamini Yesu waokolewe hampati hata mmoja wote wanakuja kwa Yesu.

  Like

 5. Nimesoma kwa makini ujumbe huu hakika ni ujumbe ambao Bwana Yesu amekusudia uwafikie watu wengi kwa kadri iwezekanavyo na huu ni ujumbe ni wa muhimu sana katika nyakati zetu hizi na ambao unapaswa kuzingatiwa na pia kuwekwa katika utendaji kwa gharama yoyote. Mimi binafsi ninakubalina na ukweli kuwa wakristo wengi na hata katika makanisa ya kipentekoste ufahamu umetiwa upofu na shetani kwa kuamini kuwa hali ni shwari kumbe katika uhalisia hali ni mbaya katika mahusiano yetu na Mungu wetu.

  Ubarikiwe sana na Mungu kwa wewe kufanyika njia ya kufikisha ujumbe huu

  Wako katika Kristo

  Bellington G Lyimo

  Like

 6. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu kwa huduma yako njema,nimebarikiwa na ujumbe wako.Ni kweli kanisa tumejisahau na kujikita kuangalia vinavyoonekana,na kanisa linafikiri kuwa viwango vya Mungu vya utakatifu wa Mungu vimepungua,ndiyo maana wakristo wengi wanaishi maisha wanayopenda kuishi wala si kama Mungu anavpopenda tuishi.Ndiyo maana makanisa mengi wamejikita katika kuhubiri kwa habari ya baraka NA KUSAHAU kukemea dhambi makanisa,na hivyo kufanya waamini wengi ndani ya makanisa wa uvuguvugu.
  Mtumishi wa Bwana zidi kuieleza KWELI ya Mungu tupate kuwekwa huru Fahamu zetu.
  Ningependa tuzidi kuwasiliana zaidi.

  Naitwa David
  UDSM-MLIMANI.

  Like

 7. Mara kadhaa nimekuwa naota Bwana Yesu amerudi,hata kabla sijaokoka nilikuwa naota Yesu amerudi,hii siisahau maana nilijiona waziwazi nimeachwa,na hali niliyoiona imebaki duniani,hakika huwezi kuitamani dunia,matajiri wote na mambo tunayoyatamani hakika tukiwa na macho ya kiroho hatuwezi kuyatamani,hii dunia haina thamani kabisa.Pia nimewahi kuota Yesu karudi hata baada ya kuokoka,huwa naona ni upendo wa Mungu tu unaonikumbusha nijiweke vizuri na mara nyingine inanitia moyo kwamba nami nimo safarini ndio maana nakumbushwa.Lakini kiukweli ,mambo ya dunia tunayahangaikia tu ni vile macho yetu hatujaruhusu yatiwe nuru ipasavyo,ndio maana hatufanyi kazi ya Mungu ipasavyo,hakika baada ya YESU KURUDI WATU WATAPATA HUZUNI YAKUTOSHA ,na ule usemi wa kumkebehi Yesu kwamba alisema atarudi lakini mpaka leo yuko wapi,napenda niwaonye wale watu wa Mungu waachane na maneno ya mkumbo,wasije jipatia hukumu ya bure.MBARIKIWE.

  Like

  • Mungu akubariki sana ndg. Noel Msanjila kwa mchango wako kwenye hili eneo. Naam ndio maana Paulo kwa Waefeso aliomba macho yao yatiwe nuru.. hakika laiti watu wangejua kile ambacho kinakuja wangemgeukia Mungu na kuhakikisha wanalitumikia kusudi lake huku wakiishi maisha safi. Maadam tumepata neema ya kujua haya ni jukumu letu kuwafundisha na wengine kweli yote ya neno la Mungu.

   Like

 8. Na tazama nipo pamoja nanyi hata ukamilifu wa dahari. Ukifanya kazi ya Mungu yeye amesema atakuwa nawe hata ukamilifu wa dunia Bwana akutie nguvu na akupe ufunuo zaidi wa macho ya kiroho.amina

  Like

  • Yeremia 29:11 inatoa jibu la swali lako. Kifo cha mwenye haki ni utaratibu alioweka Mungu ambao mtu akisha kulitumikia kusudi la Mungu awapo duniani kwa njia ya kifo anahamisha kutoka katika dunia hii na kuingia katika ufalme wa Mungu (mbinguni) kwenye ulimwengu wa roho ambako ataishi milele kwa furaha na BWANA Yesu. Vivyo hivyo na mtenda dhambi akifa anaenda kwenye ufalme wa giza (kuzimu) katika ulimwengu wa roho. Lakini soma kwanza andiko la Yeremia ndio linajibu swali lako la msingi haya mengine ni nyongeza tu.

   Like

   • Haya ndio masomo niyapendayo sana, MUNGU Nisaidie Nisijeachwa. Endelea Mtumishi wa MUNGU kufundisha kweli hii, hata kama ukipingwa taji yako Mbinguni ndio jambo la Msingi

    Like

   • Utukufu kwa Mungu, ahasante kwa amaombi yako na kuzidi kunitia moyo, kwa hakika sitaacha maana NAMJUA ninayemtumika na ninajua nisipoandika kweli, kuna siku nitaulizwa na kuwajibishwa pia.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s