VITA VYA KIROHO (Part 1)

 

Na: Patrick Sanga

 Yohana 10:10 ‘Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu…

 Waefeso 6:10-18 ‘Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake, vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani 12 kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama ; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwngu wa  roho’.

 2 Wakorinto 10: 3-5 ‘Maana ingawa tunaenenda kaitka mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili,bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome); 5 tukiangusha mawazo na kila kkitu kilichoinuka kijiinuacho kinyume cha elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo.

 Siku zote jambo lolote lile linalotokea kwenye maisha ya mtu katika ulimwengu wa kimwili ujue lilianzia kwenye ulimwengu wa kiroho. Mfano ukiona wanandoa wanatengana ujue walishatengana kwanza katika ulimwengu wa roho ndipo sasa inadhihirika kwenye ulimwengu wa kimwili.  Kwa hiyo siku zote vita kati ya Mkristo na Shetani inapigwa katika ulimwengu wa roho kwanza.   

 Mtu akimshinda shetani na mapepo yake kwenye ulimwengu wa roho ujue hata kwenye ulimwengu wa mwili atashinda. Naam ni katika ulimwengu wa roho ndipo Mungu anapotaka watoto wake tuliokoka tujue namna ya kuvipiga vita dhidi ya shetani. Naam tukishindwa kwenye ulimwengu wa roho na kwenye ulimwengu wa kimwili tutashindwa na tukishinda kwenye ulimwengu wa  roho na kwenye ule wa mwili tutashinda.

 Ukweli huu tunaupata kutoka kwenye andiko la 2Wakorinto 10:3-5, maana Biblia inasema silaha zetu si za mwili, ina maana ni za kiroho, sasa huwezi kutumia silaha za kiroho kupigana vita ya kimwili. Na kwa hiyo mapambano ni katika ulimwengu wa roho sawasawa na Waefeso 6:12.

 Watu wengi huwa wanasubiri hadi jambo litokee kwenye ulimwengu wa mwili ndipo na wao utaona wanapanga mikakati mizito ya maombi tena ya kufunga. Sio kitu kibaya lakini kibiblia ni makosa kwa sababu tunakuwa watu tunaoongozwa na matukio katika ulimwengu wa mwili wakati Mungu alikusudia tushughulike na hilo jambo tangu lilipojitokeza kama wazo katika ulimwengu wa roho. 

 Unapoona watu wanafanya maandamano katika ulimwengu wa mwili ujue tayari hayo maandamano yalishafanyika kwenye ulimwengu wa roho. Kwa hiyo kama hukutaka hayo maandamano yafanyike, ulitakiwa kuwa macho kwenye ulimwengu wa roho ili punde utakapoliona wazo la kuandamana kwenye ulizuie kule kule na kisha ungesikia hata kwenye ulimwengu wa kimwili maandamano yameahirishwa.

 Ikumbukwe kwamba chanzo cha vita/ugomvi/vurugu zozote zile kwa wanandoa, viongozi, watumishi, marafiki nk ni Shetani. Shetani ndiye anayepanda wazo la ugomvi, kusengenya ndani ya mtu nk kupitia mapepo. Mapepo ni watenda kazi wa shetani, ambao wanafanya kazi kwa amri yake. Mfano ili kuvuruga ndoa Shetani anaweza kutuma pepo la kutozaa kwa wanandoa, na vita ikaanzia hapo nk.

 Na ndiyo maana Paulo kwa kainsa hili la Efeso aliomba akisema “Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru…” (Waefeso 1:18). Hii ni kwa sababu vita yoyote ile huanzia kwenye ulimwengu wa roho tena kwa mfumo wa wazo. Shetani hutafuta nani ampatie wazo lenye kuleta uharibifu. Na akimpata ndipo huteremsha wazo hilo kwenye moyo wake. Ezekieli 38:10 inasema “Bwana Mungu asema, itakuwa katika siku hiyo mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya”.

 Vita yoyote ambayo Shetani anaipiga inalenga kuharibu maisha ya mtu. Mfano Adam na Eva (Mwanzo 3), Mfalme Daudi (2 Samwel 11). Hata siku moja shetani huwa hafanyi vita bila lengo. Kama Mungu anayo mawazo ya amani anayo kuwazia, na shetani naye anayo mawazo ya uharibifu anayokuwazia.

 Mwenye kuvileta vita hivi ni shetani. Kwa hiyo usije ukamchukia ndugu yako kama unaona anakuchukia wakati mlikuwa manapatana. Ukiona ndugu yako anakuchukia ujue siyo yeye ni wazo alilopewa kwenye ulimwengu wa roho. Sasa badala ya kulifanyia kazi huko, yeye akazembea na ndio maana hata kimwili anakuchukia.

 Tutaendelea na sehemu ya pili…

 

 

Advertisements

24 comments

 1. Mtumishi SANGA nakushukuru sana, nampa Yesu shukurani nyingi mno kwa kukutumia, hili somo limenigusa mno,hakika sina la kusema ila asante sana YESU, yote nimeyapokea na nitayafanyia kazi, Bwana wangu na Mfalme wangu.

  Like

  • Amina Vana, ubarikiwe kwa comment zako, maombi yako ni ya muhimu juu yetu waandishi wa neno la Mungu kupitia blog/websites mbalimbali maana vita ni kubwa, Shetani hapendi watu wasome na kujua kweli ya neno la Mungu. Maana imeandikwa “asomaye na afahamu…” na pia “apendaye mafundisho hupenda maarifa” Barikiwa na BwanaYesu.

   Like

 2. Asante sana kwa mafundisho haya. Maana nimeachana na mchumba wangu kwa sababu ya kutoelewana. Ila mafundisho haya yamenifundisha kuwa nisimchukie kwani najua ana tatizo la chuki na hasira, na hiyo ni mbinu ya shetani mpaka tumeachana hii leo.

  Like

 3. Kaka SANGA Mungu akubariki na azidi kuongeza mafunuo juu yako tuweze kusimamisha kusudi la MUNGU juu ya watu wake.

  Like

 4. Ndugu Mtumishi,Bwana asifiwe,

  Ninakushukuru kwa somo hili,kwani ni jana tu tarehe 24.08.2010,jirani yangu ambaye bado haja hamia kwenye nyumba yake alipokuja kwangu,mimi nikiwa kazini akaanza kufanya vurugu na kuzika vitu kwenye ukumbi wa nyumba yangu,kwa hiyo vita hivi vilianzia kwenye ulimwengu wa roho,hadi kwenye ulimwengu wa mwili,nashukuru MUNGU,jana usiku kama desturi yangu nililiita jina la bwana na tulilala bila hofu yoyote,
  Elisante

  Like

  • Naam Elisante, utukufu kwa huyu Bwana hakika kuna nguvu ya ajabu ndani ya jina la Yesu. Ni jukumu letu kweka imani yetu kwa hili jina la ajabu kila tunapoliita.

   Like

 5. Nimependa sana namna ulivyofundisha kuhusu matarajio ya Mungu hasa kwa vijana lakini nawezaje kupata kwa kirefu zaidi lakini isiwe kwa vijana iwe kwa matarajio ya Mungu kwa mwanadamu yeyote, nitashukuru endapo usema kuhusu hilo walau kwa dondoo tu nikafuatilia mwenyewe. Barikiwa

  Like

 6. mh ama kweli mtumish sanga “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”kwel kabla yakuokoka shetani hutekafahamu zawatu

  Like

 7. kaka SANGA, Mungu akubariki. kwa kweli JINA LA BWANA LIBARIKUWA, AHSANTE BWANA YESU KWA KUTUCHAGULIA HIKI CHOMBO SANGA. UBARIKIWE SANA KAKA.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s