JIFUNZE KUOMBA KIMASWALI (Part 2)

 Na: Sanga, P.S.

March, 2010

Yeremia 29:13 “Nanyi mtanitafuta na kuiniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote”.

Kumbuka nilikuambia kwamba maombi ya maswali ni maombi ambayo ndani yake yanalenga kutafuta ukweli juu ya kitu/jambo fulani. Ni maombi ya kutafuta, kuchunguza, kutaka, kupekua, kusaka nk kwa lengo la kutaka kujua ukweli au kupata taarifa ya kile unachokiomba. Kwa uelewa zaidi soma tafsiri ya KJV inasema  And ye shall seek me, and find me, when ye shall search for me with all your heart (Jeremiah 29:13)

Naandika sehemu hii ya pili ya somo hili kwani licha ya kufanya maombi haya kama nilivyoandika kwenye sehemu ya kwanza bado unaweza usione mpenyo mzuri. Zipo sababu nyingi ambazo zinaweza kusababisha mkristo asione mpenyo kwenye maombi yake, lakini katika maombi haya ya kimaswali licha ya hizo sababu nyingine iko sababu moja kubwa nayo ni maovu na dhambi za mtu husika au mwombaji na mazingira yake.

 Isaya 59:1-2 “ Tazama mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia ; lakini maovu yenu yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”.

 Pengine ni vema kwanza nikakupa tafsiri nyingine tatu tofauti za mstari huu ili ikusaidie kuona kile ninachotamani tujifunze katika somo hili;

 NLT inasema – 1 Listen! The Lord is not too weak to save you, and he is not becoming deaf. He can hear you when you call. 2 But there is a problem—your sins have cut you off from God. Because of your sin, he has turned away and will not listen anymore.

 NSRV inasema – 1 See, the Lord’s hand is not too short to save, nor his ear too dull to hear. 2 Rather, your iniquities have been barriers between you and your God, and your sins have hidden his face from you so that he does not hear. 

 RSV inasema – 1 Behold, the Lord’s hand is not shortened, that it cannot save, or his ear dull, that it cannot hear; 2 but your iniquities have made a separation between you and your God, and your sins have hid his face from you so that he does not hear.

 Tafsiri hizi zinatuonyesha kwamba katika kipindi cha nabii Isaya kuna tatizo lililojitokeza na kusababisha Mungu asiwaokoe na kuwaponya watu wake  kama kwanza. Ujumbe huu wa  Mungu ulimjia Isaya  kwa sababu kuna mtu (watu) hakuridhika na hali ya kiroho iliyokuwa kwa nyakati hizo. Na kwa sababu hiyo akaanza kuomba/kuwaza kimaswali. Akamuuliza Mungu maswali mazito au   pengine aliwaza na kujiuliza ndani yake kwanba kwa nini hali iko hivi?,  Mungu uko wapi?, kwa nini tunaendelea kuishi katika hali ya mateso na kuaibika kiasi hiki?, kwa nini hatuoni uso wako kama kwanza? Tatizo liko wapi? nk.

 Naamini pia  Katika mawazo ya huyu mwombaji alifikiri huenda uwezo wa Mungu katika kuokoa umepungua, na yumkini sikio lake limekuwa zito hata asiweze kusikia kama kwanza. Zaidi Kadri ninavyozidi kusoma neno la Mungu kila siku nimejifunza kwamba sehemu kubwa ya neno la Mungu ni majibu ya Mungu kwa kuzingatia maswali waliyokuwa nayo ndani yao, na wakayapeleka kwake kimaombi au kimawazo au kwa kujadilana wao kwa wao.

 Sasa katika kujibu maswali hayo, Mungu akaweeleza kwa nini hawasikilizi na kuonekana kwao kama kwanza. Kwa hiyo kwa lugha nyepesi tunaweza kusema Isaya 59 ni matokeo ya maswali ambayo mwombaji alikuwa nayo moyoni mwake. Na ukitaka kujua ukweli soma sura ya 58 na 59 kwa pamoja utaelewa vema.

Katika andiko hili la Isaya 59 tunaona, Kilichoufica uso wa Mungu kwa watu wake ni dhambi zao. Tatizo lilikuwa kwa watu na si Mungu amejificha bali ni kwa sababu mtu amefanya dhambi. Uovu na dhambi yao ilikuwa kizuizi kati yao na Mungu. Kwa hiyo tunajifunza kwamba mtu anapofanya dhambi anajenga ukuta kati yake na uso wa Mungu. Ukuta huo utakata mawasilano kati yake na Mungu na hivyo hawezi kuona tena uso wa Mungu mpaka atengeneze kwanza njia zake. Mungu akijibu maswali yao alimaanisha, ndugu zangu hamnioni kama kwanza kwa kuwa dhambi zenu ndizo zilizo kata mawasilano kati yenu na mimi, na kwa sababu hiyo hakuna wokovu tena  kwani nilipotaka  kunyosha mkono wangu kuwakoa dhambi zenu zikanizuia.

 Tunajifunza nini?

 Hata leo kwako mwombaji inapofika unaona  Mungu yupo kimya lazima ufikirie kwanza njia zako zipoje mbele za Mungu, je kuna uovu au dhambi ndani yako au mazingira uliyopo. Vinginevyo ni ngumu sana kumsikia Mungu akijifunua hata kama ukiomba maombi kwa mfumo huu wa maswali. Na Mungu hawezi kukujibu/kujifuna kama ndani yako au katikati yako kuna uovu na dhambi. Nafikiri nawe unajua jinsi Mungu alivyokuwa kimya kipindi cha kuhani Eli kwa sababu ya dhambi za watoto wake. Biblia inasema ‘… Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri” (1Samweli 3:1)

 

Nini kifanyike?

 Ni jukumu lako kuhakikisha unaishi maisha ya utakatifu ndipo utaona mpenyo kwenye maombi haya. Wakati mwingine kiroho kwa mwombaji hata mazingira, majirani au wale ambao katika ulimwengu wa roho umepewa kuwasimamia/kuwaongoza kama kuna dhambi ndani yao inaweza ikasababisha maombi yako yasisikilizwe. Kwa hiyo ni lazima mwombaji ujifunze kuwa makini na hali yako na ya mazingira yako kabla hujaanza kufanya maombi haya.

 Tahadhari;

Kama utaendelea kuomba kimaswali wakati ndani yako kuna uovu na dhambi basi kuna hatari ya kupata mafunuo ya kipepo na wewe ukadhani ni Mungu. Na hapa ndipo penye hatari kubwa juu ya maombi haya. Kitu kisichotakiwa ni mazoea, unatakiwa kuhakikisha siku zote unaishi maisha ya utakatifu na kujitakasa kwa damu ya Yesu ili uwe tayari wakati wowote kufanya maombi haya. Wengi wamezoea kujitakasa wanapoanza kuomba, lakini maombi haya yanataka uwe mtu wa kuhakiksha siku zote unaliishi neno la Mungu.

 Ni imani yangu kwamba kama ukiweka kwenye matendo ujumbe huu hakika maisha yako ya kiroho hasa kimaombi yatabadilika. Hutaona Mungu yuko mbali na wewe. Dhambi ndicho kizuizi kikubwa kwenye maombi ya mtu kwa Mungu wake. Hata kama vipo vizuizi vingine havina uwezo juu ya maombi ya mfumo wa maswali lakini dhambi na uovu wa mtu vina uwezo wa kuzuia.

 Narudia tena kusema haijatokea na haitatokea, kama mtu akizingatia kanuni hii ya utakatifu, na akaenda mbele za Mungu kuomba kimaswali kwa lengo la kupata majibu ya maswali yake, haitatokea Mungu anyamaze bila kujibu. Hii ni kwa sababu ‘mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia’.

 Tuzidi kuombeana

Advertisements

7 comments

  1. Mungu akubariki kwa somo zuri nashukuru hata mimi leo nimepata majibu maana lilikuwa linanisumbua swala hili la kuomba muda mrefu na sijaona mabadiliko yoyote.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s