Archive for December 2009

NAMSHUKURU MUNGU NIMEPATA MKE

December 21, 2009

Ilikuwa ni tarehe 06/12/2009 katika kanisa la EAG(T) Sinza Makaburini Dar ndipo Bwana alipotuunganisha mimi na Flora D. Mwakalago kuwa mume na mke.

                                                                  

Natumia fursa hii  kuleta shukrani zangu za dhati kwa wasomaji wa blog hii, rafiki na jamaa zangu wote kwa namna mlivyoshiriki pamoja nasi kwa maombi, michango na ushiriki wenu ili kufanikisha harusi hii.

Mnisamehe nilikuwa kimya kwa siku kadhaa bila kuandaa masomo na kuweka kwenye blog kwa sababu ya maandalizi ya shughri hii. Naam sasa tumerudi kazini na maisha yetu yanaendelea vema kabisa.  Ni imani yangu kwamba kusudi la Mungu la “kuinua misingi ya vizazi vingi (Isaya 58:12), litaendelea kutekelezwa”. Hakika namshukuru Mungu kwa kumpata msaidizi huyu.

 Bwana Mungu awabariki sana, tuzidi kuombeana.

Thanks

Mr&Mrs. Sanga.