JIFUNZE KUOMBA KIMASWALI (Part 1).

Waraka wa Octoba.

 Na: Sanga, P.S.  

Yeremia 29:13 “Nanyi mtanitafuta na kuiniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” Bada ya kuwa nimeliza kidato cha sita najiandaa kwenda chuo mwaka 2004, changamoto iliyokuwepo ni kitu gani nakwenda kusoma chuoni. Baba yangu alinitaka nikasomee uhasibu (Accountacy) na mimi nilipenda kwenda kusomea utawala wa biashara (Business Admnisration).

Sasa kati yangu na baba yangu kulikuwa na mvutano mkubwa sana, ikalazimu nishirikishe waombaji wengine katika hili. Wakati huo sikuwa na ufahamu mzuri kuhusu mapenzi ya Mungu, mimi nilijua kuishi katika mapenzi ya Mungu ni kutenda yale yaliyoandikwa kwenye Biblia tu,sikujua kwamba mapenzi ya Mungu ni katika kila nyanja ya maisha ikiwa ni pamoja na nitasoma nini,ninafanya nini (kusudi),nitaishi wapi,nitamuoa nani n.k.

Nilipoendelea kushirikisha waombaji wengine kuniombea ndipo nilipo fika kwa mama mmoja na kumshirikisha changamoto yangu ya nini natakiwa kwenda kusoma. Huyo mama kimsingi taaluma yake ni ya shule ya msingi,akaniambia nimtajie ‘course’ zote ambazo zipo kwenye chuo ninachoenda kusoma.Sasa chuo nilichotakiwa kwenda kusoma ni Chuo cha elimu ya biashara(CBE) na course walizokuwa wanatoa ni Accountacy (Uhasibu), Business Administratio (Utawala wa biashara),Procurement and Supplies Management (Ugavi na Manunuzi),Legal and Industrial Metrology (Mizani na Vipimo). Nilipomtajia course hizo akaniambia tulia nimuulize Mungu. Nakumbuka alianza kwa kumshukuru Mungu kwa ajili ya fursa hii ya kwenda kusoma na kisha akaomba akisema Mungu mtumishi mbele yako kuna course nne, je ni ipi kati ya hizi   (akazitaja) anayotakiwa kwenda kusoma sawasawa na kusudi lako juu yake.  Baada ya maombi hayo kwa dakika kadhaa alitulia kidogo kama anayesikiliza kitu fulani na kisha akasema “Ameni”.

Ndipo akaniambia Mungu anataka uende ukasomee “Ugavi na Manunuzi” na akanieleza kwanini natakiwa kusomea course hii. Kumbuka taaluma ya huyu mama ni ya shule ya msingi na lengo la kukueleza hili ni ili ujue si katika ‘interest’ yake alisema nikasomee ‘Ugavi’ kwani kwa jinsi ya kibinadamu katika course hizo zote yeye hana hata moja anayoijua. Japo awali ilikuwa ni vigumu kulipokea kwani ‘interest’ yangu ilikuwa ni Utawala wa biashara.

Hata hivyo baadae nikasomea mambo ya Ugavi na Manunuzi na sasa nimejua kwa nini Mungu alinitaka nikasomee na ninajua kama nikiendelea kudumu kuwa mwaminifu kwake wapi naelekea katika fani hii, hivyo ninajitahidi kuakikisha mapenzi yake yanatimia. Si hivyo tu lakini hata baba yangu amefurahia mimi kusomea taaluma hii.

Lengo la kukupa ushuhuda huu ni kukuonyesha mfumo (style) nyingine ya maombi ambayo najua si watu wengi waliozoea kuomba maombi ya namna hii, yaani maombi kwa njia ya maswali au maombi yaliyo kwenye mfumo wa kimaswali tegemeana na haja/hitaji ulilo nalo.

Mfumo huu wa maombi aliotumia yule mtumishi ulikuwa mgeni sana kwangu kwani nilikuwa sijafundishwa kuomba kwa style hii. Na yule mtumishi akanieleza hivi ndivyo wewe (Patrick) pia unavyo takiwa kuomba kama unataka kuona Mungu akiyaongoza maisha yako kwa maana ya kukufundisha na kukuonyesha njia utakayoienda (Zaburi 32:8). Kwenye kila changamoto unayokutana nayo ipeleke kwa Mungu kwa njia ya swali/maswali, ukitaka/kutafuta ufumbuzi kwake na Mungu atasikia na kukujibu.

Wakati huo nilikuwa natakiwa kwenda chuo, akaniambia hakikisha una anza sasa maana huko uendako mimi sitakuwepo na hata simu sina kwa hiyo utakuwa wewe mwenyewe na Mungu wako. Tangu siku hiyo nilianza kuweka kwenye matendo fundisho hili, jambo lolote liwe kubwa ama dogo kwenye kila nyanja ya maisha yangu nilianza kuiombea kimaswali, nikitafuta kujua kutoka kwa Mungu mtazamo/hoja zake dhidi ya hoja na haja zangu.

Mfumo huu wa maombi ulinisaidia kuomba huku kwenye ufahamu wangu naona kwamba Mungu ni rafiki yangu na ananisikia wakati naomba. Na uzuri wa maombi haya ni maombi yanayomtaka/yanayomlazimu Mungu kufanya jambo/kujibu, (prayers that demands God’s reactions).

Maombi haya ni namna ya kusemezana na Mungu ambayo unapeleka hoja zako na kisha unasubiri na yeye ajibu. Maana yake ukisha eleza kwa kuuliza mambo yako unakaa kimya kusikiliza yeye Mungu ana hoja gani juu ya za kwako. Kwa kweli ilinichukua muda zaidi ya miezi sita kufikia kiwango cha kuwa na mpenyo kwenye maombi ya namna hii.

Katika kujifunza maombi haya nilikosea mara nyingi na kutaka kukata tamaa. Lakini Roho Mtakatifu alinitia nguvu na kunihimiza kujifunza kwani aliniambia kukatishwa tamaa kunatokana na adui kwani kila Mkristo mwenye siri au ufahamu huu, maombi yake ni uharibifu mkubwa kwenye ufalme wa giza. Uvumilivu wangu katika kusubiri na kijifunza hata kwa makosa naufurahia kwa sasa tokana na mpenyo nilionao.

Zaidi katika kipindi hicho nimejifunza kwamba “mtu anahitaji kuwa na ufahamu mkubwa wa neno la Mungu ili aoene mpenyo katika maombi haya”. Maana mara nyingi Mungu husema kupitia neno lake anapojibu maombi yako uliyoyapeleka kwake kimaswali. Hivyo suala la neno la Kristo kuwa kwa wingi ndani yako ni lal lazima kama unataka kuwa na mabadiliko kwenye maombi yako. Maombi haya kwangu binafsi yamebadilisha mahusiano na mawasilano yangu na Mungu.

Baadhi ya watu wanaonishirikisha maombi yao huwa wanashangaa inapofikia mahali naanza kuwauliza vitu ambavyo wamefanya na wao hawakunijulisha waliponishirikisha mambo yao. Kwa sasa nina uhuru mkubwa sana wa kwenda mbele za Mungu na kuhojiana naye juu ya jambo lolote lile ambalo naona ndani linazaa maswali ambayo sina majibu yake na hata nikiwa na majibu bado sio mazuri. Kwa sababu hii nayachukua hayo maswali na kuyapeleka kwa ‘mzee wa siku’ ambaye hawezi kunyamaza hujifunua kwa njia mbalimbali kwangu, nampenda sana.

Anza sasa;

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa na muda wa utulivu. Sikuzote Mungu anajifunua/anafunua siri zake kwa wamchao wanapokuwa katika mazingira ya utulivu rohoni na hata kimwili. Kwa hiyo ili uone matokeo ya maombi haya hakikisha unakuwa na mazingira ya utulivu, ndipo uanze kuomba. Siku moja nikiwa katika kuomba nilisikia sauti kwenye ufahamu wangu ikisema “mimi Mungu napatikana kwenye utulivu, kama unataka kuniona jifunze kuwa na mazingira/muda wa utulivu kwa ajili ya kunitafuta mimi”.

Ngoja nikupe ushuhuda huu, mwaka 2007 kiongozi wa vijana kwenye kundi lake katika chuo chao alinijia akanishirikisha mahitaji ya vijana anaowaongoza na akaonyesha hakika anahitaji msaada msaada wa Mungu katika kundi lake. Nilianza kufanyia kazi mahitaji yake. Mengine niliyaombea kwa kawaida lakini yaliyonilazimu nimuulize Mungu maswali,niliyapeleka kimaswali.

Nikiwa katika kuomba na kutafakari ndipo nikapata ufahamu kuwa Roho wa Yesu ana wajibu wa kuwafundisha na kuwaonyesha watu njia wanayopaswa kuiendea. Kamwe hawezi kumuacha mtu anaye kwenda mbele zake na shida au changamoto inayotaka ufumbuzi halafu akanyamaza. Kama akinyamaza kwa vyovyote vile atampoteza mtu huyo.

Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu kwa hiyo maadam ukipeleka kwake haja zako kwa kutafuta kujua/ufumbuzi uwe na uhakika atajifunua kwako ili kuhakikisha makusudi ya Mungu kwako yanafanikiwa. Sina shaka juu ya hili nimeshuhudia mara nyingi. Nini maana yake kwako mpendwa wangu, Mungu yuko tayari kukusikiliza, anza sasa kuomba kimaswali na utaona mabadiliko.

Katika hatua za mwanzo unaweza kuona Mungu hajibu au usione kitu chochote, endelea kuomba taratibu utaanza kuona kwanza Mungu akileta alama/signal za mawasiliano kati yake na wewe kama njia rahisi ya kukufanya uelewe namna yeye atakavyokuwa anawasiliana na wewe tegemeana na kiwango chako mahusiano yenu.

Kumbuka MUDA WA UTULIVU ndio kiungo cha maombi haya, kama huna muda huwezi kuomba, haya sio maombi ya kienyeji. Ni maombi yanayotaka ujenge NIDHAMU YA KUWA NA MUDA WA KUOMBA KIMASWALI. Kwa hiyo kama ni kila siku au kwa wiki tafuta/tenga MUDA ambao utakuwa unatulia kufanya maombi ya aina hii. Ukifanikiwa kwenye hili utamuona Mungu. Shetani atahakikisha siku zote ana kunyima muda kwa kukuletea shughuri na ratiba nyingi ambazo nyingine wewe utadhani ni za Ki Mungu kumbe Shetani analenga kukunyima muda huu wa maombi maana ni pigo kubwa kwenye ufalme wake. Lakini kwa msaada wa Mungu na wewe kuwa na nidhamu utafanikiwa.

Mungu wangu akubariki,wakati mwingine nitaendelea kutoka hapa katika sehemu ya pili ya maombi haya.

Advertisements

13 comments

 1. SHALLOM,NAKUSALIMU KATIKA JINA LA BWANA,NAANDIKA E MAIL HII KUTOKANA NA MAKALA YAKO YA MWEZI WA SEPTEMBA,nimesoma na kuna jambo tafadhali nahitaji kuzungumza nawe, tafadhali naomba nitumie namba zako za simu ili niweze kuwasiliana nawe,mimi niko Mwanza na ninafanya kazi na banki ya Azania.

  Like

 2. Mtumishi hiki kitu kimenipa shida muda mrefu, hadi ijafikia kushuka kiutumishi, kwani maswali nauliza mengi then naona kama hamna jibu hata moja. Ukipata nafasi nifundishe zaidi hata kama ni kwa simu ntakuwa nakupigia ninapokuwa na nafasi au baada ya kazi.

  Like

  • Amina Peter, nafikiri tunahitaji kuwasiliana kupitia email zetu ili tuongee kwa upana. Uhakika nilionao ni kwamba Mungu hawezi asijibu kabisa maambi ya watoto wake, kwani kufanya hivyo ni kuwaacha wapotee. Naamini kuna namna amejibu ila huenda hujajua kwamba amejibu, au pengine ni muhimu kuangalia namna unavyouliza maswali yako kwake. Tumia email hii paxifari@gmail.com ili tuweze kuwasiliana vema, uwe na amani kwa Mungu hakuna lisilowezekana.

   Like

 3. MTUMISHI WA MUNGU SANGA NAKUSHUKURU MNO KWA MAFUNDISHO YAKO NA KIKUNDI CHAKO CHA MAOMBI MUNGU WA MBINGU NA NCHI AWABARIKI WOTE NAAMINI NIMESHAPOKEA MAHITAJI YANGU YOTE ASANTE KWA KUNIOMBEA KWA MZIGO AMEN

  Like

 4. Bwana yesu asifiwe wapendwa naomba mnisaidie kuomba mimi nasumbuliwa sana naroho chafu ambazo ndani yake zina mtukana mungu kwaiyo hii hali ikianza napatwa na mauchungu sana ndani ya moyo ikitulia basi mimi maumivu makubwa sana napatwa naomba maombi yenu mnisaidie kuomba nami naomba harufu mimi mwenyewe siipendi hata kidogo jama ni

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s