UFUNGUO WA BARAKA ZAKO KIFEDHA

Na: Patrick S. Sanga

Ukisoma fungu la  Malaki 3:1-12 ule mstari wa nne na wa tano unasema “wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zintakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu wa wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi”

Mpenzi msomaji sijui kama unajua kwamba neno la Mungu ni jumla ya mawazo na majibu ya Mungu kwa mwanadamu. Kuna siri nyingi sana ndani ya Biblia, ambazo si rahisi kuzielewa mpaka Roho wa Yesu akufunulie kwa utukufu wake utakapomtafuta.

Ilikuwa tarehe 31/08/2008, wakati naomba nilimuuliza Mungu maswali mawili ya kifedha.  Moja lilihusu ujenzi wa kanisa la mahali ninapoabudu na la pili lilihusu mahitaji yangu ya kifedha.  Baada ya maombi hayo ndipo Mungu aliponifunulia siri hii nami nataka nikushirikishe. Ukiweka kwenye matendo siri hii naamini maisha yako ya kiuchumi yatabadilika na kuwa bora zaidi.

Inawezekana maisha yako kiuchumi kwa sasa si mazuri, biashara zako pia hazijakaa vema, miradi yako pia haijakaa vema ni kama haisongi mbele, kuomba unaomba, yumkini na fungu la kumi unajitahidi kutoa, na sehemu ya mapato yako unapeleka kwa watumishi, bado kuna fungu jingine hata maskini unawasaidia.

Huenda pia kama ni mwajiriwa selikarini au taasisi binafsi n.k unaona hautendewi haki katika malipo mbalimbali na hata mshahara wako pia.  Huenda wewe ni yatima au mjane halafu kuna haki zako ambazo zimetekwa na yule adui, huenda ni sehemu ya mirathi yenu, huenda kama wewe ni mjane basi stahili na mali ulizotafuta na mume wako zimechukuliwa na maisha ni magumu, unaona kama Mungu amekusahau na umeenda kwenye vyombo vya sheria lakini ufumbuzi bado haujapatikana nk.

Leo nina habari njema kwako, usidhani Mungu amekusahau, isipokuwa wewe ndio umemsahau, “Naam umemsahau”.  Mungu anachotaka ni kukupigania katika haki zako.  Mungu hafurahii unayoyapitia anataka upate haki zako zote.  Sasa ili uweze kupata haki zako ni lazima ujifunze na uanze kutoa dhabihu/sadaka za haki na za kumpendeza yeye.

 Yawezekana pia baraka/haki zako  zimetekwa na wachawi, wazinzi, na watu waapao kwa uongo na wenye kukuonea. Wewe huna uwezo wa kuwashinda hawa watu kwa nguvu zako, naam  Mungu anao uwezo huo. Nguvu za Mungu za kukupigania na kurejesha baraka/haki zako zimo katika wewe kutoa sadaka za haki na za kumpendeza yeye.  i.e Kadri unavyotoa sadaka za haki ndivyo unavyomkaribisha  Mungu kukupigania na mbili ndivyo unavyowasogeza adui zako mbele za Mungu awashughulikie. Unamfanya Mungu asistarehe juu ya adui zako.

Mungu anposema  wachawi uwe na hakika anazungumzia watu ambao wanalenga kuharibu uchumi na mafanikio yako kwa ujumla katika kila nyanja  biashara,kikazi,kilimo, kiroho,kihuduma nk, na  anaposema wazinzi ana maana mbili moja ni hawa wazinzi/ makahaba wa kawaida ambao yumkini unatafuta fedha yako kwa jitihada lakini inaishia kwa hao na pili ni wale waganga wa kienyeji na watumishi/manabii wa uongo, wanaosema Bwana amesema toa hiki na kile utabarikiwa, huku mioyoni mwao wakijua hayo ni mawazo yao na si Bwana. Kibiblia huu ni  uzinifu wa rohoni. Yaani wamezini katika roho zao kwa kujifanya wana nena neno la Bwana kumbe ni mawazo yao.

Na anaposema waapao kwa uongo maana yake anazungumzia waongo kwa ujumla wanaweza kuwa washirika wako kibiashara, kikazi, kihuduma n.k watu wanaotumia uongo kukuibia pesa yako, muda wako, maendeleo yako wanaokopa wasilipe n.k Je kwa nini hayo yote yanakukuta wewe? . Ni kwa sababu bado hujatoa dhabihu za haki na za kumpendeza Mungu, naam bado hujatoa.

Je, Kutoa dhabihu za haki na za kumpendeza Mungu ndio kukoje?

Ni kutoa kwa muda na uongozi wa Mungu matoleo yako mbalimbali.  Si watu wengi wenye nidhamu hii. Pesa na utajiri ambao Mungu anakupa mkononi mwako ni kwa ajili ya kuimarisha agano lake pia.  Yaani kuhakikisha makusudi yake hapa duniani yanafanikiwa kwa kutumia watu anaowabariki.  Kumbuka kufanikiwa kwa makusudi ya Mungu duniani kunategemea utiifu wa watu wake duniani.  Sasa hii ni pamoja na wewe kama mtu wa Mungu kutoa fedha yako kwa ajili kazi ya Mungu hapa duniani.

Suala sio kutoa tu, bali ni kutoa kwa kufuata muongozo wa Roho Mtakatifu ndani yako kwa maana ya wapi upeleke sadaka yako na pili kutoa kwa muda unaotakiwa kutoa kwa maana ya lini/wakati gani unatakiwa kutoa.

Jambo hili linaweza kuonekana gumu kwa jinsi ya kibinadamu, lakini huku ndiko kuongozwa na Roho Mtakatifu katika utoaji.  Kama ukiweka mahusiano yako na Roho Mtakatifu kuwa mazuri ni rahisi sana kuona uongozi wake juu ya matoleo yako.  Fahamu kwamba baraka za mtaoaji zimefungwa katika muda na eneo/mahali anapotoa.  Hii ina maana kila sadaka unayotoa ina baraka zake.  Sasa baraka hizo zinategemeana na namna unavyotoa kwa maana ya muda na eneo.

Kwa hiyo jifunze kutoa kwa uongozi wa Mungu, kabla hujatoa sadaka yako, jifunze kumuuliza Mungu je sadaka hii napeleka wapi na kwa muda gani?     Kwa kufanya hivyo utakuwa umetengeneza mazingira ya Mungu kufungua baraza zako kifedha/kiuchumi n.k. Kama huoni baraka za Mungu kifedha kwako huenda ni kwa sababu umezizuia kwa kutotoa dhabihu (sadaka) za haki na za kumpendeza Mungu. Neno kumpendeza Mungu linawakilisha kiasi/kiwango na muda. Maana yake toa kwa kiwango anachotaka yeye kwa ajili ya kazi yake na si kwa kiwango unachotaka wewe na pili toa kwa muda anaotaka yeye na si wewe. Kinachosisitizwa hapa pia ni uaminifu katika kutoa na si kumuibia Mungu (Malaki 3:8).

Ikumbukwe kwamba hapa sizungumzii sadaka yako ya kawida uliyopanga kutoa kanisani wakati wa Ibada.  Bali nazungumzia sadaka maalumu ambayo unataka kutoa kwa ajili ya wahitaji, wajane, yatima, zaka/fungu la kumi, kwenye huduma mbalimbali, watumishi nje ya eneo unaloabudu nk. Hii ni sadaka ambayo Mungu anakubariki na ndani yako kabisa unasikia msukumo wa kutoa kwa ajili ya kazi yake.  Naam naamini huwa kuna nyakati unakutana hali kama hii.

Sasa unapotaka kutoa sadaka ya aina hii ndipo unapopaswa kumuliza Mungu vizuri juu ya wapi, lini na kwa kiwango gani utoe. Japo wakati mwingine Mungu huwa anasema na mtu au watu moja kwa moja kwamba pesa hii peleka mahali fulani. Sasa wengi wanapinga kwa kuwa huenda kanisani mwao mafundisho waliyopewa wameambiwa sadaka yoyote inapaswa kutolewa kanisani tena wanapoabudu tu kitu ambacho Kibiblia si kweli.

 Kwa hiyo ukikuta ndani yako msukumo wa Mungu unakuongoza kutoa eneo tofauti na lile ulilozoea usiogpe. Jambo la kufanya ni kuuliza tu vizuri kwa Mungu tena ili kuthibitisha maana huo ni utaratibu wa Mungu ili kufanikisha kazi yake , kuwatunza watumishi wake na wahitaji kupitia baraka anazoachilia kwa watu wake.

Ni vizuri nikatoa angalizo hili, kwenye masuala ya fedha makanisa mengi yameweka utaratibu wao na sheria zao kuhusu matoleo mbalimbali ikiwemo  sadaka na mafungu ya kumi. Na mara nyingi makanisa yanataka utaratibu huo ufuatwe na uheshimiwe. Zipo taratibu ambazo hakika hata Mungu zinambariki lakini pia zipo taratibu ambazo kweli si za Kibiblia. Kama wewe ni msomaji wa Biblia naamini bila shaka utakubaliana na kile nimeandika kwenye ujumbe huu kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Yesu alisema ninyi mkikaa katika neno langu mmekuwa wanafunzi wangu kwelilkweli, tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru  (Yohana 8 :31-32). Mfano kanisani ni mojawapo ya maeneo ambayo mtu anaweza kutoa fungu la kumi. Yapo na maeneo mengine mengi kama wahitaji, watumishi/watakatifu,  huduma mbalimbali nk. Kwa hiyo ni suala la kumsikiliza Mungu anakuongoza kutoa wapi na kwa kiwango gani. Unaweza pia kuwa na sadaka au fungu la kumi na Bwana akakuongoza kuligawa kwenye mafungu kadhaa tegemeana na maeneo na kiasi anachotaka upeleke.

 Siku hiyo 31/08/2008 Mungu alinifundisha kama nataka kuona mabadiliko kwenye masuala ya kifedha katika maisha yangu basi nifanye hayo niliyoandika hapa. Naam mwaka umepita tangu aliponijulisha hili na nimelifanyia kazi na kuthibitisha kuwa Mungu si mtu hata aseme uongo, maneno yake na ahadi zake ni kweli na amina.

 Maana haki zangu na baraka zangu ambazo Shetani aliziiba zimerejeshwa. Lakini nimegundua kwa kutendea kazi neno hili kumbe hata baraka zangu za mbele ambazo Bwana Mungu amekusudia nizipate nazo zinakuja kwa wakati na kwa kiwango kilichokusudia nizipate. Na hivyo nimejifunza kwamba kutoa sadaka kwa nidhamu ya eneo, muda na kiwango ni kinga dhidi ya baraka zangu za kiuchumi katika siku za mbele/zijazo.

 Lengo langu ni kufundisha kweli ya neno la Mungu ili watu wabadilike katika maisha yao ya kiuchumi. Naam anza sasa kwa kuwa na nidhamu katika matoleo yako. Hakika utaona baraka za Mungu katika kila nyanja ya maisha yako. Hata kama kuna haki/baraka zako ziliibiwa zitarejeshwa. Vitarejeshwa maana Mungu si mtu aseme uongo na  analiangalia neno lake apate kulitimiza.

Asomaye na afahamu.

Advertisements

20 comments

 1. Amen, mtumishi yaani unasema kweli kabisa.Ni wiki hii tu ninaomba kwa ajili ya hili, umenibariki sana.
  Ukitaka mafanikio mwahidi Mungu kwanza utamfanyia nini, na sio wewe ufanyiwe tu. Mfano nitakutolea mshahara wa mwezi mzima, nitajitoa kuhudumu mwaka mzima (ukimaanisha utasamehe vitu kama overtime, harusi, sendoff nk) na kuwa nyumbani mwake ukihudumu kwa muda huo. Daudi alimwahidi kumjengea Mungu nyumba ingawa alikataa lakini alimbariki na kumwahidi baraka za milele kupitia uzao wake. Suleimani alipotoa dhabihu nyingi kuliko mfalme yeyote Mungu alimtokea usiku na kumwambia “omba chochote utakacho na nitakupa” 1 Wafalme 3: 4 – 5.
  Sio kwamba sadaka bila kuliishia neno inatosha lakini, kama tunataka baraka kweli basi tuwe pia na moyo wa kumtolea Mungu. Na iwe kweli ni Roho Mtakatifu anakuongoza kutoa hapo, maana kuna hizi roho zidanganyazo ukizitolea ni kama umetupa halafu hupokei ulinzi wowote kutoka kwa Mungu, hivyo omba ujue Mungu anakutaka utoe wapi na nini(imeishanitokea hii)
  Asante Mtumishi kwa kutukumbusha hili,
  Ubarikiwe sana

  Like

 2. Ndg Bwana Yesu asifiwe, Mbarikiwe sana watu wa Mungu kwa kuifanya kazi hii kwa Moyo,kwani tunabarikiwa kupitia mafundisho haya,Pia wengine sio wazoefu kuomba mda mrefu tunaomba mtusaidie la kufanya,”mbarikiwe sana.”

  Like

 3. Bwana apewe sifa nimebarikiwa sana. Sasa najua siri ya mafanikio sababu mimi ni mmoja niliye mjaribu Mungu kwa njia hiyo nika muona…Mbarikiwe sana.

  Like

 4. amina mtumishi.ubarikiwe.nina fungu la kumi nimekusanya kwa muda sasa huwa nina tabia ya kumuuliza Mungu nipeleke wapi.mpaka sasa hivi sijapata jibu,naendelea kuuliza.niombee ili anijulishe hilo fungu nipeleke wapi kwasababu nimezificha mahali kwa miezi kama minne sasa. bado sijajua kusudi la Mungu.
  ubarikiwe

  Like

  • Hello mama, Mungu akubariki kwa kuwa na nidhamu ya kutafuta uongozi wa Mungu juu ya namna unavyopaswa kutoa zaka, ukweli si wengi wanaoijua nidhamu hii na kuitenda. Hata hivyo si rahisi kwamba ukae zaidi ya miezi minne bila kupata uongozi wa wapi uipeleke, naamini lazima Mungu alikusemesha wapi uipeleke ila wewe hukuelewa. Naam hii ni kwa sababu licha ya zaka kutolewa kwa uaminifu unapaswa kuitoa kwa wakati, kutokana na mahitaji ya zaka katika mwili wa Kristo kule anapokuongoza kupeleka. Binafsi sidhani kama unapaswa kuendelea kuomba sana angalia watu wenye uhitaji mfano Yatima, Wajane, Watumishi, kanisani kwako nk then peleka. Na uzuri mwingine ni kwamba waweza pia kugawanya zaka yako kwa maeneo tofauti kadri unavyosikia rohoni kufanya. Naam chukua muda, tulia omba kwa kutaka kujua upeleke wapi, Roho Mtakatifu atasema nawe instantly.Ni muhimu kuitoa kwa wakati ili usiingie kwenye mtego wa kuitumia kwa mambo yako. Barikiwa endelea kuwa na nidhamu hii.

   Like

  • Amina, namba yangu ni 0755 816 800 ingawa nie si Mchungaji kwa jinsi ya kibinadamu kwa maana ya kuwa na kanisa, mimi ni Mwalimu na Mwandishi wa mafundisho ya neon la Mungu

   Like

 5. Asante mtumishi kwa kutuondoa kwenye shida. Lakini mimi nina swali moja mtumishi, hivi kama una kipato cha kukuwezesha kupata mahitaji yako muhimu tu na wakati mwingine ukipunguza hela hiyo kunakuwa na uwezekano hata wa kukosa chakula. Je sadaka hiyo niitoe tu bila kujali kukosa mahitaji yangu naomba unisaidie kwa hili.

  Like

  • Ndiyo unapaswa kutoa zaka na sadaka kwa kila fedha unayopata. Ni lazima ujifunze kutazama suala la zaka kama hitaji muhimu zaidi kuliko kununua chakula. Ukiwa mwaminifu kutoa zaka Mungu atafungua milango kwa mahitaji yako mengine.

   Like

 6. Nashukuru kusoma somo hili juu ya mafanikio, nahitaji tuwe na mawasiliano ndugu mwalimu kwa msaada wa Neno La Mungu.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s