JIONYESHE KUWA UMEKUBALIWA NA BWANA.

 Na :Sanga, P.S

 Waraka wa Septemba

Nawasalimu kwa jina la Bwanakatika mwezi huu wa Septemba, 2009. Katika mwezi huu nakuja na changamoto fupi, inayohusu mwenendo wetu katika Kristo kama vijana tuliokoka. Biblia katika 2Timotheo 2;15a Paulo alimwambia Timotheo akisema “jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Bwana

Kama unafuatilia mwenendo wa sasa wa watu nitumie wanaosema wameokoka utagundua kwamba matendo yao ni tofauti na ukiri wao. Ndugu zangu nimeshuhudia watu wengi sana wanaosema wameokoka lakini kupitia wao Mungu wetu na wokovu kwa ujumla umekuwa ukitukanwa na imepelekea watu wengine kusema hakuna kuokoka duniani. Hebu tujiulize kwa nini wafikie mahali waseme kauli hizi kama si kwa sababu ya matendo yetu kufanana na ya kwao.Je si kwa sababu wanaona tunapokea na kutoa rushwa kama wao,je si kwa sababu na sisi tunakunywa pombe,kutoa mimba, zinaa,uasherati nk. kama wao?

 Ndugu zangu wokovu ni mfumo wa maisha ambao una taratibu zake za kuishi Endapo ulifanya maamuzi ya kuokoka basi sharti uishi kwa mfumo wa wokovu. Naamini haukulazimishwa kuokoka lakini uliamua kwa hiari yako.Unapoamua kuokoka unatangaza vita katika ufalme wa shetani. Hii ni kwa kuwa awali ulikuwa haki yake. Kuokoka ni kuleta nuru ulimwenguni,  yaani ni kuwasha taa mahali penye giza.

   Mungu anasema mtakuwa watakatifu kama mimi nilivyo mtakatifu,Waebrania 12;14 anasema “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo UTAKATIFU kwa maana hakuna mtu atakaye muona Mungu asipokuwa nao”. Zaburi 16: 3 anasema “Watakatifu walioko duniani ndio walio bora, na hao ndio   ninao pendezwa nao”.Nimekupa hii mistari ili uone kuwa INAWEZEKANA mtu kuishi maisha ya utakatifu akiwa hapa duniani.

   Mungu anatutaka tuwe watakatifu kwa kuwa yeye ni mtakatifu. Mungu hawezi kutoa agizo ambalo anajua halitekelezeki. Yeye angekuwa mzinzi tulikuwa na haki ya kuwa wazinzi,walevi,wachawi nk, lakini kwa kuwa yeye ni mtakatifu LAZIMA na sisi watoto wake tuwe watakatifu.

    Paulo alimweleza Timotheo ajitahidi kujionyesha kuwa amekubaliwa na Bwana. Kwani alijua kwamba inawezekana kuishi maisha ya utakatifu tungalipo vijana. Paulo anataka ujana wetu usitukanwe kwa namna yoyote ile bali tuwe kielelezo. Ndugu zangu kama umeamua kuokoka lazima uazimie kuishi maisha ya mfumo wa wokovu. Kila kambi inapigania upande wake ufanikiwe, sasa kama upo kambi ya Yesu unatakiwa kuishi kama yeye anavyo taka uishi ili tuwe na ushindi dhidi ya kambi ya Shetani na mapepo yake. Suala ni kujizuia katika yale mambo ambayo hayampendezi Mungu wetu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

 Pengine nitumie fursa hii pia kukualika wewe Mkristo ambaye unapenda na unataka kwenda mbinguni kwamba tafuta kitabu kilichoandikwa “Kweli mbingu ipo” cha Choo Thomas usome. Ni kitabu cha kweli na cha muhimu kwa kila Mkristo kukisoma. Nukuu mojawapo kwenye ile sura ya 24 ukurasa wa 211 inasema “ kuzaliwa mara ya pili kunamaanisha ni kuachana na mambo yasiyo ya Kimungu ambayo hapo awali uliyatamani na unachohitaji ni kumpendeza Mungu tu”. Zaidi unaweza kusoma mengi zaidi kuhusu kitabu hiki na mwandishi huyo kupitia anuani hii ya website yake http://www.choothomas.com

       Maadam tupo katka dunia hii vikwazo/changamoto za kututoa kwa  Yesu ni nyingi, lakini tunatakiwa kujua nafasi zetu kwenye ufalme wa Mungu, na kuishi maisha ya kifalme.Vitu vyote ni halali lakini kumbuka kwetu sisi tulio okoka si vyote vifaavyo. Kwa hiyo suala la kujizuia katika yale mambo ambayo hayaleti utukufu kwa Mungu wetu ni la LAZIMA. “Tunawajibika kuishi maisha matakatifu kwani inawezekana kwake yeye aaminiye

 

Neema ya Kristo iwe nawe.

Advertisements

4 comments

 1. Shalom,

  Ni mafundisho ya msingi.

  Neema ya Mungu ile iliyotupa wokovu bado inaweza / inatosha kutusaidia kusimama imara katika wokovu kwa imani iliyo ndani ya jina la Yesu. Si kwa kuwa sisi ni wajanja, tuna akili sana bali kwa kuwa tunaye Yesu ndani yetu Yeye Aliye ushinda ulimwengu basi tuna ujasiri wa kukikaribia kiti cha neema ili tupate rehema, kuweza kupata neema inayotusaidia kushinda siku za changamoto , majaribu ndani ya ulimwengu huu uliojaa uovu.

  Tito 2:11-12
  Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
  nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa

  Yuda 1;24
  Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s