UPONYAJI WA NAFSI ILIYOINAMA.

 

Na: Patrick Sanga

 

Mithali 12:25a “Uzito katika moyo wa mtu huunamisha”

 

Mwanadamu anapita katika vipindi/mazingira tofauti tofauti kwenye maisha yake.Mazingira hayo yanaweza yakamsababishia nafsi yake kuinama au kufuarahi. Biblia inasema uzito wa moyo wa mtu huuinamisha , kwa lugha nyingine moyo wa mtu huinama kwa sababu ya uzito uliomo ndani yake.

Maana yake nini? Uzito kwenye moyo inawakilisha  hali ya mtu kuchoka moyoni, kukata tamaa moyoni, kuhuzunika, kufadhaika, kuugua, kukosa amani moyoni nk.

 

Chanzo chake nini?

 

* Kuchelewa kwa kilichotarajiwa, Mithali 13:12.

Kuwa na matarajio ya mambo mabalimbali kutoka kwa Mungu ni kawaida ya mwanadamu.Tarajio linapochelewa moyo wa mtu unainama, mfano kuchelewa kuolewa/kuoa, kuzaa, kupata kazi, kupoana nk.

* Hatari/hofu ya kifo, Matahyo 26:37-38.

Ukisoma habari hii utaona jinsi Yesu mwenyewe alivyougua na kusononeka kwa sababu ya kifo kilichokuwa kinamkabili. Hata leo watu wengi nafsi zao zimeinama kwa sababu ya hofu ya kifo kupitia magonjwa ukimwi na uchawi pia.

 

* Hali mbaya kiuchumi, dhiki nk 2Wafalme 4:1

Hii imekuwa ni changamoto kwa watu wengi sana na limepelekea watu wengi kuona kama wokovu ni mgumu sana.

 

* Dhambi

Mtu anapofanya dhambi anakuwa amempa Ibilisi nafasi kutawala maisha yake. Dhambi pia inaondoa furaha rohoni.

 

* Maneno ya kuvunja moyo toka kwa watu wengine. Zaburi 42:2-3

Katika hali ya kawaida maneno ya fitina, uzushi, kuaibisha nk yanaumiza sana watu wanapokusema. Huu ni mfano wa Onesmo katika Filemoni ule mstari wa kumi na moja.

 

Nini cha kufanya?

 

Jifunze kujitamkia maneno yanayolenga kuinua nafsi yako.

Neno jema/zuri ni uponyaji wa nafsi iliyoinama, linaleta furaha kwenye nafsi hiyo.

 

 Hebu tuangalie mfano wa mwimbaji wa zaburi ya 42.

 

Ukisoma hii Zaburi utagundua huyu mwimbaji wa Zaburi nafsi yake iliinama kwa sababu ya maneno ya kuumiza watu waliyokuwa wanayasema dhidi yake. Na chanzo cha kauli hizo hakijatajwa, lakini huenda ni kwa sababu alitenda dhambi. Lakini siri ya ushindi kutoka kwenye mazingira ya kifo ilikuwa ni kujitamkia maneno yenye kujenga na kurejesha afya ya nafsi yake. Mstari wa tano katika sura hii unasema ‘nafsi yangu kwa nini kuinama,na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu, aliye afya ya uso wangu, na Mungu wangu”

 

Ndani ya Biblia kuna ahadi na mistari mingi sana ambayo waweza kuitumia ili kuinua nafsi yako au hata ya mtu mwingine ikiwa imeinama kutokana na mazingira anayoyapitia kwa wakati huo. Mistari ifuatayo itakusaidia sana kurejesha nafsi mahali pake, hakikisha unaisoma yote na ukiweza kuiandika mahali ili kila wakati uwe unaitamkia nafsi yako.

 

Mithali 11:8, 26:2c, 28:20, 28:13b, 24:16a.

Isaya49:15-16, 24-26, 43:25, 50:8, 54:7-10

Zaburi 34:4, 19, 89:33-34

Mhubiri 3:8

 

Baada ya kusoma anza kuiambia nafsi yako kama mwimbaji wa zaburi alivyiambia nafsi yake akisema nafsi yangu usiiname kwa sababu….., sasa tegemeana na kilichosababisha nafsi yako iiname tamka neno ambalo linavunja ile fikra iliyopelekea nafsi yako kuinama. Mfano kama ni hatari ya kifo, Iambie nafsi yangu usiiname kwa kuwa  Kila silaha itayofanyika juu yangu haitafanikiwa…. Isaya 54;17 nk. Weka neno hili kwenye matendo utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.

 

Mungu wangu akulinde na kukuponya nafsi yako.

 

 

 

 

 

 

Advertisements

14 comments

 1. Ubarikiwe mpendwa Sanga,
  Ndiyo mara yangu ya kwanza kuingia kwenye hii blog yako,nimebarikiwa na mafundisho ya Neno la Mungu.Nafsi yangu imeinama kwa mambo ninayopitia ila namshukuru Roho Mtakatifu kwa kuniongoza kusoma juu ya maandiko uliyoyaweka kwenye hili somo.Nimeyaandika na nimeanza kuyafanyia kazi.
  Nakushukuru sana!

  Like

  • Hello Aika,

   Mungu wetu ni mwaminifu, tena ni mtetezi aliye hai (the redeemer who lives). Mimi ni shahidi wa jambo hili nililoandika hapa, weka kwenye matendo ujumbe huu na utaona Mungu akikushindia na kuirejesha nafsi yako mahala pake. Nguvu za Mungu na ulinzi wake vikuongoze.

   Like

 2. Asante ndugu kwa ujumbe wako kuhusu nafsi uliyoinama. Nimebarikiwa sana na fundisho ili. Sikuelewa vizuri kwa mistari uliyotoa katika kitabu cha Methali 1811:8, naomba mafasirio kwa hiyo.

  Salamu katika Kristo Yesu .

  Ndugu Honore

  Like

 3. Ndugu Honore, kwanza nashukuru kwa kutembelea blog hii, kuniombea na kwa swali lako pia. Huo mstari ulipaswa usomeke Mithali 11:8, ni katika kuzidiwa na kazi wakati mwingine umakini unapungua, nashukuru nitaparekebisha. Barikiwa

  Like

 4. Mpendwa katika Kristo,Hakika mafundisho haya ya nafsi iliyoinama yamenipa changamoto ya hali juu kwangu mwenyewe na familia yangu, lakini zaidi sana kwa jamii au familia ninazozifahamu ambazo zinapita sasa kwenye mapito magumu ambazo mara nyingi zimetushirikisha katika kuomba pamoja kwa ajili ya mapito hayo.Na baadhi ya mapito hayo ni kama kuondokewa na wapendwa wao (mume au mke,wazazi,watoto n.k),magonjwa au kuugua kwa muda mrefu kukosa kazi hata baada ya mtu kuhitimu elimu nzuri tu n.k. Sasa nimepata kitu cha ziada ambacho kwa pamoja tutakiweka kwenye matendo ili kuinua nafsi hizi na biblia inasema changamko la moyo ni dawa nzuri(Methali 17:22)
  Ubarikiwe sana mtumishi wa Bwana na Mungu aendelee kukupa afya njema ya kimwili na kiroho pia.

  Like

  • Amina, u heri wewe ukiyatenda haya maana naamini nafsi za hao ndugu zitarejeshwa mahala panapofaa. Ahsante kwa maombi yako. Hakika nayahitaji kulingana na upinzani ninao uona kila ninapoandaa haya masomo, lakini Bwana kwa maombi yenu ananiwezesha.

   Like

 5. Ubarikiwe sana Sanga.Nimebarikiwa sana na somo hili…Nafsi yangu imeinuka na itainuka milele kwa kuwa Mkombozi wangu anaishi na alishanikomboa.Niko huru sasa…

  Like

 6. Lucy

  Shalom,

  This year 2015 am going to Love God through out of the year.

  God Bless you in your Business, Employment.

  AMEN.

  Lucy

  Like

 7. Nimebarikiwa Sana Mungu Akuinue Zaid Tena Zaid Nataman Nami Nimtumikie Mungu Kama Ulivyo Wewe.Mungu Akupeleke Ktk Viwango Vingine

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s