NAMNA UNAVYOWAZA NI PICHA YA NAMNA UTAKAVYOISHI.

 

Na: Sanga P.S

Waraka wa Machi.

Zaburi 36:4

Huwaza maovu kitandani pake, hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii’.

Aina ya maisha/mapito anayoishi au kupita mtu ni matokeo ya mawazo yake. Mawazo ya mtu ndiyo yanayoamua maisha ya mtu yaweje.

 

Jifunze yafuatayo kutoka katika msatri huu wa Zaburi hii ya 36.

 

Ø      Kumbe kwa kuwaza maovu mtu anajiweka katika njia mbaya.

Ø      Hii ina maana mtu anatumia mawazo yake mwenyewe kujiweka kwenye njia mbaya.

Ø      Mtu huyu yuko katika njia mabaya kwa sababu anawaza maovu. Hii ina maana mtu huyuhuyu kama akiwaza mawazo mazuri/mema atajiweka katika njia bora/njema na nzuri.

Ø      Mtu huyu atafanikiwa ikiwa atawaza kufanikiwa na atafeli ikiwa atawaza kufeli.

Ø      Kwa hiyo mpaka hapa tunagundua kwamba kumbe mawazo yake yanatueleza hali au matokeo ya maisha yake yatakavyokuwa.

 

Je mpendwa wangu, kiroho, kihuduma, kijamii, kibiashara, kiuchumi , kikazi nk uko katika hali/njia/mfumo gani wa maisha, ni mzuri au ni mfumo mbaya. Kama ni mbaya angalia jinsi unavyowaza kuhusu hilo eneo. Ulivyo kwenye hilo eneo kibiblia ni matokeo ya ulivyowaza nafsini mwako. Kama huoni kufanikiwa kwenye biashara/kazi/kiuchumi ina maana umewaza au uliwaza kutokufanikiwa. Na hata kama unawaza kufanikiwa basi hauwazi sawasawa na ahadi za Mungu katika maisha yako.

 

Hasara ya kuwaza vibaya ni kujiweka katika njia mbaya, yaani unajitengenezea mazingira mbaya, mazingira ya kutokufanikiwa katika maisha yako kwa ujumla. Ili neno la Mungu liweze kutenda yale yote ambayo limetumwa na Mungu kuyatenda kwenye maisha yako kwa uaminifu ni lazima kwanza na wewe ujifunze kuwaza in a positive way.

 

Yaani kuwaza sawaswa na ahadi au na neno la Mungu kwenye maisha yako. Kinyume chake haliwezi kutimia na hivyo utakuwa umempa Ibilisi nafasi kutekeleza mapenzi yake juu yako.

 

Jifunze kuwa makini na unavyowaza juu ya mambo mbalimbali unayokutana nayo kila siku. Hakikisha hauwazi kinyume na ahadi za Mungu kwenye maisha yako.

 

Neema ya Kristo iwe nawe.

Advertisements

One comment

  1. Moja kati ya comments ninazokumbuka toka kwa Mchg wangu ni ile inayosema “:your mental picture will determine ytour actual future.” Wawazao mabaya huishi wakitenda mabaya na wale wawazao mema vivyo hivyo huenenda katika wema. Kuwaza ni kati ya hatua kuu tatu za binadamu kuishi nyingine zikiwa kunena na kutenda. Na mara nyingi kuwaza huja kabla ya mtu kunena ama kutenda. Kwa kifupi ni kuwa kuwaza ni kama mzizi wa maneno na matendo na kama tutajitahidi kujikomboa katika tuwazayo, basi hatutakuwa na shida sana katika kuratibu na kuhariri maneno na hata matendo yetu.
    Asante kwa somo hili.
    Blessings

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s