MWANAMKE, JIFUNZE KUSIMAMA KWENYE NAFASI YAKO KAMA MLINZI.

 

Na : Mwalimu Sanga P.S

 

Yeremia 31:22” hata lini utatanga tanga , Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume”.

Soma pia habari hii yote katika Isaya 32:9-17

 

Ule mstari wa tisa unasema “Inukeni enyi wanawake wenye raha, sikieni sauti yangu; enyi binti za watu wasiokuwa na uangalifu,tegeni masikio yenu msikie sauti yangu”.

 

Moja ya majukumu makubwa ambayo Mungu amemkabdihi mwanamke ni jukumu la ulinzi kwa mwamamumue yoyote na si mumewe tu kama wengi wanavodhani au kufikiri. Kwa maana hili andiko linawahusu wanwake haijalishi wameolewa au la, ni binti au mjane linamhusu.

 

Si wanawake wengi wanaoifahamu siri hii juu yao. Imeandikwa ya kwamba Mungu ameumba jambo jipya, mwanamke atamlinda mwanaume. Hii ina maana ulinzi wa mwanaume uko kwa mwanamke. Hii inaashiria kumbe Mungu ameweka neno la ulinzi wa mwanaume kwa mwanamke.

 

Hebu tuangalie mifano kadhaa ndani ya Biblia;

 

*      Kuzaliwa kwa Musa, Kutoka 2;1-10.

Tunaona wazi kabisa mama wa Musa alivyomlinda mwanae akijua ndani yake kuna kusudi limebebwa.

*      Kuzaliwa, kukua na ndoa ya yakobo, Mwanzo 25:21-28, 27:1-4, 5, 6, 11-13, 17, 46.

Siri ya kusudi la Mungu hapa duniani kupitia Yakobo aliiweka kwa mamaye. Alimweleza maana ya vita iliyokuwa ikiendelea tumboni mwake alipokuwa mjamzito. Rebeka alihakikisha kusudi la Mungu juu ya watoto atakaowazaa linatimia, kwa sababu alijua Yakobo ndiye taifa kuu alihakikisha hilo linatimia na pia alihakikisha Yakobo haoi nje ya mpango wa Mungu kwa maana ya kuoa mataifa.

*      Kuzaliwa na maisha ya Samson, waamuzi 13:2-5, 12-15.

Siri ya nini Mungu amekiweka kwa Samson na kwa nini anamleta duniani, pamoja na namna mtoto huyo anavyotakiwa kulelewa aliiweka kwa mamaye Samson na si baba yake, Mzee Manoa. Sasa ukisoma utaona jinsi huyu mama alivyosimama kwenye nafasi yake ki ulinzi mpaka Samson alipoanza wajibu wake uliomleta duniani.

*      Zaidi unaweza ukajifunza pia kupitia kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Siri ya kitu gani kitazaliwa, Malaika aliileta kwa Mariam, akijua ni jukumu lake kulinda hiyo siri mpaka utimilifu wake. Soma Mathayo 1:18-25.

 

Hata leo wanawake wanatakiwa kusimama kwenye nafasi zao za ulinzi kwa ajili ya watoto wao, vijana wao, waume zao, ndugu zao waume nk. Kwa lugha nyepesi ni shauri la Bwana kwamba kila mwanamke amlinde mwanamume anayetoka katika tumbo lake, mumuwe kama ameolewa nk ili kuhakikisha kusudi la Mungu linatimia.

 

Kosa la hawa wanawake/mabinti katika siku za nabii Isaya ni kujisahau, kufurahia starehe na kutokuwa waangalifu katika kufuatilia maagizo ya Mungu kuhusu ulinzi wa watoto, vijana, na waume zao nk.

 

Kibiblia ni utaratibu wa Mungu kumpa kila mwanamke taarifa juu ya mtoto atayemzaa, juu ya mume ambaye atamuoa lengo ikiwa ni kumsaidia ajipange ki-ulinzi.

 

Mwanamke hakikisha unasimama vema kwenye nafasi yako ya ulinzi kwa mwanamume. Kama utasiamama vizuri kwenye nafasi yako ya ulinzi basi uwe na uhakika umeubariki moyo wa Mungu na kwa sababu hiyo umepelekea uponyaji kwenye familia yako, jamii yako, taifa lako na uchumi wako binafsi lakini na ule wa taifa pia.

 

Kazi kubwa ya Shetani ni kuwafanya wanawake waliokoka  duniani wajisahau, wasiwe waangalifu na hivyo wasifuatilie maagizo ambayo Bwana Mungu ameweka ndani yao kuhusu waume zao, vijana, watoto na ndugu zao wa kiume ili  kusudi la Mungu lisifanikiwe. Sasa wewe usikubali shetani akuzidi maarifa, weka neno hili kwenye matendo utaona wazo la Mungu linatimia kwa kuwa MWANAMKE AMESIMAMA KWENYE NAFASI YAKE YA ULINZI.

 

Bwana na akubariki.

 

Advertisements

25 comments

 1. Ndg,umenibariki sana kwani karibu masomo uliyofundisha
  Mungu amekuwa akinifundisha na nimekuwa nikiwamegea
  vijana ambao kwa kweli wako katika harakati za kutaka kuoa
  na kuolewa.Wengi wanafikiri kuoa na kuolewa tu LAKINI
  Wanasahau Nafasi ZAO NA WITO WAO waliopewa na Mungu,
  Na hili ni kosa kubwa sana maaana ukivurunda hapo
  utakiona cha moto mbele ya safari.

  Like

  • Glory to our ‘Redeemer who lives’, tuzidi kuombeana na kusimama katika nafasi zetu ili kulitumikia shauri la Bwana katika zama hizi.

   2009/5/23 Patrick Sanga

   > >

   Like

 2. hello Pastor Sanga nafurahishwa sana na mada zako kwa kweli zinatia moyo encourage katika safari hii tuliyonayo hakika imejaa vikwazo na majaribu mengi sana ila kama neno la Mungu linavyosema avumiliaye mpaka mwisho atashinda. Hakika majaribu ni mengi sana kaka Sanga ha

  Like

 3. Am happy to state that the message was dedicated to me.Am single with a fiencee for four years have being thinking of getting marriage but whenever i think of all the task behind me was to decide to stay single forever in mylife.The scripture teach me i should have my own husband to care of,to have sons to take care of them because onces i care blessings wil fall on me and mycountry will be blessed and also iwil be healed . Glory to God for wonderful work that i have ahead of me .My brothers and sisters pray for me because i will inform my fiancee to wed next year.May God bless you as spread the work of GOd.

  Like

 4. Mungu azidi kukufunulia kaka Sanga.nimefarijika sana na hili somo lako kwa kweli nimejigundua sikuwa kwenye zamu yangu ya ulinzi,mimi nimeolewa nina mtoto mmoja lakini kwa sasa mume wangu ameondoka nyumbani na yuko na mwanamke mwingine wanaishi kwa kweli baada ya kusoma hili somo nimegundua nililala, mwizi akaingia kwenye lindo langu na kuiba mume wangu.
  kaka sanga yani sasa hivi wako wa mama wengi wanalia kuhusu swala hili kama langu tupo wengi maskini kwa matajiri utazani kuna upepo umetuvamia,naomba tuelekeze jinsi ya kufanya kuwarudisha waume zetu nyumbani na tusimame kwenye malindo sasa bila kulala.
  Asante sana Mungu akulinde.

  Like

  • Nashukuru kwa comment yako dada Veronica, usemalo ni kweli akina mama wengi kwa kutokuwa kwenye nafasi zao wamempa Ibilisi nafasi na limekuwa teso kwenye ndoa zao. Naomba maombi yako sana, kwani kazi ya kuandaa masomo ina changamoto nyingi sana na upinzani mkubwa. Kuna masomo nayaandaa naamini yatafanyika msaada kwako na kwa wengine wenye changamoto kama yako.
   Mungu wetu ni mwaminifu, tuamini kwamba atamrejesha mume wako.
   Barikiwa.

   Like

  • Veronica, nimeguswa kwa hakika na ujumbe wako huu, lakini tumwamini Mungu maana YOTE YAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE. Anza kwa kuyafanyia kazi hayo niliyaainisha kwenye ujumbe huu, omba kwa ajili yangu ninapoandaa masomo haya yalenge kujibu maswali ambayo watu wamekuwa nayo kwa muda mrefu, maana mafundisho ya neno la Mungu ni njia mojawapo ambayo Mungu anatumia kujibu maombi na maswali ya watoto wake.
   Kwa hiyo kwa maombi yako juu yangu na huduma hii nitaandaa masomo ambayo na hakika yatakusaidia wewe na wamama wengine wanaokabili tatizo linalofanana na la kwako.

   Like

 5. BWANA YESU ASIFIWE! KAKA SANGA KWA KWELI HUDUMA YAKO INANIBARIKI SANA.HII BLOG NIMEIPATA WKT NAPITAPITA TU KWENYE MTANDAO SIKUWA NAIFAHAMU.NAONA SI VIBAYA KAMA UKIANDAA HATA VIPEPERUSHI RAHISI VYA KUITANGAZA ILI WATU WENGI WAJENGWE KUPITIA MAFUNDISHO YAKO.MUNGU AWAPIGANIE WEWE NA MRS WAKO HUDUMA HII ISONGE MBELE ZAIDI. MBARIKIWE SANA.

  Like

  • Amina dada Grace, tunashukuru kwa comment zako, maombi na ushauri wako pia. Naamini huu ni wakati wa Mungu kufanya hivi kwani ni watu wengi sasa wametoa ushauri a kuitangaza blog hii. Ubarikiwe sana.

   Like

 6. UMENIBARIKI SANA, MUNGU AKUZIDISHIE UPEO WA WA KUFIKIRI ILI UZIDI KUYABARIKI MAISHA YETU coz yamenipamwangaza wa maisha yanayoitajika katika ndoa though sijafika huko bt nimebarikiwa xanaxana

  Like

 7. Akika Nami Nishapitia Kwa Mtego Namajuto Hayo ,muke Nilio Naye Ajawaitaka Kusimama Kwa Jukumu Wake ,mimi Ni Pastor Kama Angenipata Kama Sina Wokovu Ninge Muacha Nikaowa Mke Mwingine Ila Nishaa Vumilia Nakusimama Maalipangu ,yeye Ameishi Akikosa Kuridhika ,nikimwelekeza Ajawai Kubali Amefanya Nimepitia Magumu Sana \HAYA UJUMBE WAKO NABII TUMESOMA PAMOJA NAE ,NIOMBEE SANA ASIMAME MALI PAKE ILI ATA MIMI NIPOKEE BARA?

  Like

  • Pole kwa changamoto zote Mchungaji wangu, neema ya BWANA Yesu ikusaidie kushinda ili kutoathiri kusudi na huduma ambayo Mungu ameweka ndani yako kwa ajili ya jina lake, tunaendelea kukuombea pia.

   Like

 8. NAOMBA MUNGU ANISAIDIE NIPATE NGUVU YA MAOMBI NA UJASIRI NA USHINDI KIBALI POPOTE NITAKAPOKUWA FAMILIA YANGU IFANIKIWE KATIKA JINA LA YESU KRISTO AMEN

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s