MOYO WAKO UNASEMA NINI?

 

 

 

 

Na: Sanga P.S

 

Zaburi ya 14:1 “Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, hakuna atendaye mema”.

 

Zaburi 14:1 b,c ni matokeo ya kauli ya kipengele a. Kwa sababu mtu huyu ambaye ni mpumbavu ameshasema moyoni mwake kwamba hakuna Mungu, hivyo suala la kutenda dhambi kwake  ni kawaida.

 

Ukisoma pia  Zaburi 36:1 Biblia inasema  Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake’. Sikiliza mtu huyu hawezi kuwa na hofu ya Mungu kwa sababu tayari moyoni mwake ameshasema hakuna Mungu.

Kwa nini inakuwa hivi? Ni kwa sababu awazavyo nafsini mwake ndivyo alivyo na pia ni kwa sababu maamuzi yake ndiyo yanaamua maisha yake. Soma Zaburi 36:4 na Mithali 23:7a.

 

Mpumbavu ni mtu anayejua kitu au kweli halafu anafanya maksudi kuvunja hiyo sheria au kukiuka hiyo kweli.

Je, nawe msomaji wangu unapopita kwenye hali ngumu kiuchumi, moyo wako unaema nini?

Unapojaribiwa, unapoachwa, unapochelewa kuoa/kuolewa, kuzaa, kupata kazi moyo wako unasema nini?, unapowekwa na Mungu kwenye nafasi ya uongozi, unapobarikiwa, unapokosewa na ndugu yako, je moyo wako unasema nini?.

 

Katika mazingira yoyote unayopita lolote utakalolisema moyoni lina matokeo yake, yanaweza kuwa ni mazuri au mabaya tegemeana na ulivyosema.

 

Lolote utakalolinena moyoni mwako kinyume na ahadi za Mungu juu yako, hii ina maana na wewe umesema hakuna Mungu katika hilo. Kwa lugha nyepesi umekataa wazo au msaada wa Mungu kwenye hilo unalolipitia hadi ukasema hakuna Mungu. Na ukisema hakuna Mungu tegemea kutopata msaada wa Mungu bali kuonewa zaidi na utawala wa Shetani.

 

Tuangalie mifano kadhaa kwenye Biblia;

*      Mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka 12, Mathayo 9:20-22

*      Anania na safira , Matendo 5:1-4.

*      Yuda Iskariote, Yohana 13:2

*      Mikali binti Sauli, mke wa Daudi, 2samweli 6; 16, 20-23.

Katika hii mifano yote hawa watu hawakusema kwa vinywa vyao, bali ni mawazo/kusema kwa mioyo yao.

Na ndiyo maana Yeremia 17:9 inasema;

 

Moyo huwa mdanganyifu sana kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha, nani awezaye kuujua? Mimi Bwana , nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.

 

Jifunze kuwa makini na namna unavyosema moyoni mwako, ukihakikisha unasema sawasawa na ahadi/mapenzi ya Mungu kwenye maisha yako.

 

Bwana Mungu akubariki.

Advertisements

10 comments

 1. Yesu apewe sifa, naitwa David kutoka Moshi Kilimanjaro. Hakika nimebarikiwa sana na mafundisho hayo, siko tena kama nilivyo awali mafundisho yako yamenibadilisha mtumishi wa Mungu. Mungu akubariki sana ili wakati mwingine uweze kuandaa masomo mengine kwa ajili ya wengine. Ubarikiwe sana

  Like

  • Amina David, nashukuru kwa comment yako pia, ukweli comment zenu ndizo zinazonifanya nione kile ninachofanya ni chema na tena kinambariki na Bwana Yesu, kwa hiyo sitaacha lakini naomba maombi yako sana maana upinzani ni mkubwa katika ulimwengu wa roho. Barikiwa na Bwana

   Like

 2. Mimi naitwa Malipo Lukandamiza Mbalanga kutoka Port Elizabeth South Africa, muzaliwa wa Uvira DR Congo. Nashukuru sana mtumishi wa Mungu Nimepata ujumbe wako Mungu akubariki mpaka ushangae kwa injili unayo itangaza,usini ache na mimi uwe na nitumiya ujumbe.

  Like

 3. Shalom Mtumishi. Barikiwa na kazi ya Bwana. Mimi ni mmoja Wa kupata baraka za Mungu kupitia we we. Neema ya Mungu iendelee kukupa ufunuo.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s