KUFANIKIWA KWA MAKUSUDI YA MUNGU DUNIANI KUNATEGEMEA UTIIFU WA WATU WAKE DUNIANI.

picture-264

Waraka wa Desemba.

 

To my dear sister Sara,

 

Salam  katika Jina la Yesu aliye hai.

 

Huu ni waraka maalumu kwako, ambao imenilazimu kukuandika ili kukumbusha nafasi yako ndani ya  Kristo nikilenga kukujengea nidhamu itakayokusaidia  kushirikiana na upako/nguvu za  Mungu juu yako ili kusudi lake  kupitia wewe liweze kufanikiwa hapa chini ya jua .

 

Kufanikiwa kwa maksudi ya Mungu duniani kunategemea utiifu wa watu duniani. Kufanikiwa kwa kusudi la Mungu duniani kupitia (Sara) kunategemea utiifu wa Sara hapa duniani. Hii ni kwa sababu Mungu alijifunga kumtumia mtu kwa mambo au kazi au maksudi yake chini ya jua. Ukisoma mafungu yafuatayo ya maandiko utaona ni kwa namna gani Mungu amejifunga kumtumia mtu chini ya jua.

 

Mwanzo 1:26, Kutoka 32;9, Yeremia 1:4-7, Warumi 8:28-30, Waefeso 4:11, Ezelkiel 22:30, Yeremia 5:1, 2 Nyakati 16;9, Mathayo 28:18-20.

 

Kumbuka siku zote Mungu anaposema naenda kufanya, au nitafanya, au nataka kufanya kitu fulani jua kabisa maana yake anatafuta mtu aliye tayari amtumie kufanya alilolikusudia. Hivyo jifunze kukaa mkao wa kutumiwa na Mungu siku zote.

 

Ukisoma Yohana 1:12 Biblia inasema wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Hii ni siri kubwa sana ambayo ni lazima uielewe. Mungu kwa kujua kuwa kufanikiwa kwa maksudi yake kunategemea utiifu wako na yeye pia anawajibika kukupa upako, nguvu au kukupaka mafuta ya kukusaidia kutekeleza maagizo yake.

 

Jifunze kwa Yesu mwenyewe. Ukisoma  Luka 4:18 utaona Yesu anaweka wazi kusudi la kuja kwake duniani kwamba ni kuutangaza ufalme wa Mungu, kufungua vipofu, kufungua waliofungwa, kuwaacha huru walionewa nk. Lakini kabla ya hayo yote ameanza kwa kusema kwamba Roho ya Bwana i juu yake naye amemtia mafuta kwa ajili ya mambo hayo anayoyataka ayafanye duniani.

 

Nini maana yake ? hii ina maana kwa nyakati tofauti tofauti Mungu alikuwa akiachilia upako tofauti tofauti kwa mwanawe tegemeana na kusudi au wajibu wa Yesu kwa wakati huo.

 

That is, kuna wakati upako wa uponyaji ulikuwa juu yake, kuna wakati upako wa kufundisha ulukuwa juu yake, kuna wakati upako wa kuomba ulikuwa juu yake nk. Sasa maksudi haya yalifanikiwa kwa sababu Yesu alikuwa ana utii kwenye upako unaokuwa juu yake kwa wakati huo. Hii ina maana hakchanganya mambo. Upako wa kuomba ulipokuja hakwenda kupiga stori bali aliomba, upako wa kuhubiri ulipokuja hakwenda kuomba na ndio maana alikuwa  na ujasiri wa kusema katika Yohana 17 kwa baba yake kwamaba kazi uliyonituma nimeimaliza.

 

Sasa hiki ndicho kitu ambacho Mungu ana kitafuta na kukitaka kutoka  kwako.

Nidhamu yako kwenye upako/nguvu/mafuta amabayo huwa anaachilia juu yako kwa ajili ya kusudi lake. Jifunze kuwa mtiifu kwenye upako unaokuwa juu yako kwa ajili ya kufanikisha kusudi la Mungu hapa duniani kupitia wewe.

 

Na kwa kuwa wewe ungali mwanafunzi basi nidhamu ya hali ya juu inahitajika. Uwe na uhakika licha ya kuwa mwanafunzi bado Mungu ana kusudi la ki – Ufalme la kukupeleka kwenye hiyo Shule maana ninajua nini Mungu ameweka ndani yako kwa habari ya huduma. Na hii ina maana kuna wakati atataka kukutumia kueneza ufalme wake, kufungua waliofungwa na kuwaeleza watu habari zake na Jina lake.

 

Na hii ina maana utatakiwa kuwa na muda wa kuomba kwa ajili ya mambo hayo, kuwa na muda wa kusoma Neno la Mungu, kuwa na muda wa kusoma masomo yako, kuwa na muda wa kupumzika, kuwa na muda wa kuwaambia wengiene habari za Yesu na uzuri wake nk. Katika mambo hayo yote yeye (Mungu) atahakikisha kwa kila jukumu anakupaka mafuta ya kukusaidia kutekeleza wajibu huo. So kinachotakiwa ni kuhakiksha unatumia vizuri upako huo kwa kutokuchanganya mambo ili uweze kufanikisha mambo yote na hivyo kufanikiwa katika mambo yote.

 

Kukosa nidhamu katika hili kunaweza kusababisha Mungu aondoe upako huo juu yako na kuupeleka kwa mtu mwingine aliye tatari kutii. Soma Mathayo 21:28-32 utaelewa kitu nasema hapa. Huu ni mfano wa vijana wawili ambao bwana wao aliwaagiza kwenda kwenye shamba lake kumchukulia zabibu.

 

Matokeo yake wa kwanza alipokataa licha ya kupewa uwezo, bwana wake alihamishia upako kwa kijana wa pili aliyetii agizo la bwana wake. Kitu hiki utakachokiona hapa ndicho  kilichotokea kwa Sauli na Daudi. Kwa sababu ya Sauli kukosa utiifu Mungu alihamisha upako kuoka kwake na kuupeleka kwa Daudi. Soma 1 Samweli sura ya  15 &16.

 

Tahadhari, angalia jambo hili lisitokee kwako kwa kutokutii maagizo ya Mungu. Mungu hawezi kukubali kazi yake ikakawma.  Na kwa sababu alishajifunga kumtumia mtu then uwe na uhakika atamtafuta mtu mwingine kwa kazi hiyo maadamu yuko tayari kutii na kushirikiana vizuri na upako wake.

 

Je, ndani yako kuna utiifu kiasi gani? Na unautumiaje upako wa Mungu juu yako.

 

Naomba ufanikiwe katika mambo yote na zaidi Roho wa Yesu akufundishe kujua namna ya kushirikiana na upako wake juu yako ili kuhakikasha kwamba shauri la Bwna linafanikiwa katika kizazi chako.

 

 

Yours in Christ

 

 Patrick.

Advertisements

One comment

  1. Asante sana kwa ujumbe huu mzuri ambao unaendelea kunitia nguvu na kunifanya nianze kujua ninalopaswa kufanya.

    Nimekuwa nikioteshwa kuwa ninafanya huduma ya kuombea watu wengi ambao wanaonekana kuwa ni wagonjwa na wanashida mbalimbali. Ndoto hii nimeletewa kama mara 5 hivi siku na miezi tofauti. Je, hii ina maanisha kuwa hii ndiyo karama yangu? Je, nifanye nini ili niweze kutii sauti ya Bwana na kufanya sawasawa na mapenzi yake.

    Ubarikiwe sana.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s