KUOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU.

go-conference-166 

Waraka wa Novemba.

Na: Patrick Samson Sanga.

 

Biblia katika kile kitabu cha 1 Yohana 5:14 inasema “Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,atusikia’.  Tafsiri ya kiingereza inasema ‘And this is the confidence that we have toward him, that if we ask anything according to his will he hears us’.

 

Ndani ya msatari huu kuna nafasi mbili ambazo muombaji yoyote ni lazima azijue;

 

Nafasi ya kwanza ni kwa yule anayeomba (position ya muombaji).

 

Kipengele cha kwanza kinasema, na huu ndio ujasiri tulionao kwake. Sasa ukiiweka hii sentensi kwenye umoja itasomeka hivi, “na huu ndio ujasiri nilionao kwake”. Neno ujasiri nilionao linawakilisha nafasi ya muombaji mbele za Mungu. Je huyu muombaji yukoje, anaombaje, anaomba saa ngapi, anaombea wapi nk.

 

Ukisoma 1 Yohana 3:21 Biblia inasema “wapenzi mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu”. Hukumu ya moyo ndani ya mtu ndio taa. Wakati unaomba moyo wako usipokuhukumu maana yake taa yako inawaka na kati yako na Mungu kuna mawasilano. Yaani unakuwa jasiri kwenda mbele za Mungu kimaombi.  

 

Moyo wako ukikuhukumu maana yake taa yako haiwaki na kati yako na Mungu hakuna mawasilano mazuri na hivyo huwezi kuwa na ujasiri kwenda mbele za Mungu kimaombi bila kwanza kutengeneza na Mungu wako. Mara nyingi hukumu ya moyo inasababishwa na mtu kutokutii maagizo ya Bwana Mungu wake na hivyo kupelekea mahusiano kati yao kuwa mabaya.

 

Nafasi ya pili ni kwa yale anayoomba.

 

Kipengele cha pili cha andiko kuu la somo hili kinasema “ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia….” ukiweka hii sentensi pia kwenye umoja itasomeka “ya kuwa nikiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, anisikia. Maneno ‘nikiomba kitu sawasawa yanawakilisha mfumo wa maombi ambao muombaji anautumia wakati wa kuomba.

 

Je anaomba nini, kwa nani, na katika mamlaka gani? Haya ndiyo maswali yanayozaliwa kutokana na sehemu ya sentensi hii. Siri hii imeelezwa vema kwenye  Yeremia 29:12 inayosema “ikiwa mtaniita, mtakwenda na kuniomba ndipo nitwasikiliza”. Ili uweze kuielewa vizuri nafasi hii ya pili nakusihi rejea ujumbe wa “Namna ya kumuuita, kwenda na kumuomba Mungu ili akusikilize” ndani ya blog hii kwa kubonyeza category ya mafundisho ya Neno la Mungu.

 

 

Jifunze yafuatayo kutoka kwenye ujumbe huu;

 

ü      Wito wa Mungu kwako ni kuomba sawasawa na mapenzi yake.

ü      Unaweza ukaomba kitu sahihi lakini usiombe sawasawa na mapenzi yake.

ü      Unaweza ukaomba sawasawa na mapenzi yake  lakini usiombe kitu sahihi.

ü      Katika kila ombi unalopeleka kwa Mungu liwe la kwako, kanisa au nchi nk kuna mapenzi ya Mungu ndani yake. Hivyo kabla hujaomba taka/tafuta kujua nini mapenzi yake kwa hayo unayotaka kuyaombea.

ü      Nafasi yako kama muombaji na mfumo wa maombi unaoutumia ni muhimu sana kwa Mungu katika kujibu maombi yako.

ü      Mapenzi yake juu yako katika nyanja hii ya maombi yamefungwa kwenye nafasi yako kama muombaji na pia mfumo wa maombi unaoutumia wakati wa kuomba.

ü      Suala sio kuomba, bali ni kuomba sawasawa na mapenzi yake kwa maana ya kukaa kwenye mkao ambao una ujasiri kwamba anakusikia na pia unatumia mfumo/mkakati ambao yeye (Mungu) anataka uutumie.

 

Neema ya Kristo na iwe pamoja nawe.

Advertisements

One comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s