MATOKEO YA DHAMBI YA UZINZI/UASHERATI KWA MTU ALIYEOKOKA.

 

 

Na : Patrick Samson sanga.

Waraka wa Septemba.

 

Nakusalimu katika jina la Bwana mwezi huu wa tisa. Katika mwezi huu nimesukumwa ndani yangu tujiunze habari hii juu ya athari/matokeo ya dhambi ya zinaa/uasherati pale kwa mtu aliyeokoka. Yaani kitu gani kinatokea mtu aliyekwisha kuokoka anapoanguka katika dhambi hii.

 

Katika Mithali 6:32 Biblia inasema “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake” na pia katika  Mithali 6:26 inasema “Maana kwa Malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani”

 

Ni watu wengi sana ambao wamerudi nyuma na kuanguka katika dhambi hii, wapo ambao kwa hiari yao walikuja kwangu moja kwa moja niweze kusaidiana nao katika hili, wapo wengine ambao hata wao pasipo kuniambia walilofanya Mungu alifunulia na kunionyesha jinsi watu hao walivyoanguka katika dhambi hii na madhara yake. Hadi sasa bado kuna kundi kubwa la watu waliokoka ambao bado dhambi hii ina nguvu juu yao na bado wanafanya jambo hili kinyume na mapenzi ya Mungu katika maisha yao.

 

Si kana kwamba Mungu anafuga dhambi kwa kutokuwadhihirisha hao watu na uovu wao, isipokuwa hataki jina lake litukanwe, kwa kuwa ikijulikana huyo mtu au hao watu wameanguka huenda  kutokana na nafasi zao kiuongozi, kihuduma kiushuhuda nk jina la Mungu litatukanwa sana na mataifa lakini pia hata na wale waliokwisha kuokoka. Kwa lugha rahisi hao watu au huyo mtu atakuwa ametoa nafasi ya jina la Mungu kutukanwa.

 

Kwa bahati mbaya sehemu kubwa ya watumishi wa Mungu katika makanisa yao wanoona athari ya hili jambo katika upana wakekama Biblia inavyosema.   Inafika mahali baadhi yao wanawafariji wale walioanguka kwa kusema jipe moyo, tubu na Mungu ni wa rehema atakusamehe. Na wengine utasikia wanasema haukuanza wewe, Daudi naye yalimshinda sembuse wewe.

 

Wengine wanatumia maandiko kabisa wanasema mwenye haki huanguka mara saba, we mara moja tu wala isikusumbue sana tengeneza tu Mungu atakusamehe, na wengine wanasema mimi mwenyewe nilishindwa so, hata wewe isikusumbue sana kazana tu uoe wa kwako au omba upate mume. Ni kama vile watu wanatumia rehema/neema ya Mungu kuendelea kutenda dhambi (It seems as if people are taking the advantage of God’s mercy/grace to commit sin). 

 

Si kana kwamba napingana na neno au na mawzo ya hao watumishi wenzangu. Nakubali  kwamba Mungu husamehe dhambi na maovu  ikiwa ni pamoja na dhambi hii ya uasherati/uzinzi. Mungu husamehe kwa sababu moja hafurahii kifo cha mwenye dhambi na pili ni ili kukurejesha kwenye nafasi yako ili uweze kulitumikia kusudi lake. Lakini je, unajua madhara/matokeo ya dhambi hii kwa mtu aliyeokoka anapoifanya? Hata kama akikusamehe/amekusamehe, unajua nini kimetokea/kilitokea kwako pale ulipofanya dhambi hii? Au je unaijua gharama ya kurejea kwenye nafasi yako aliyoikusudia Mungu?

 

Katika miaka zaidi ya sita niliyomtumikia Mungu nimejifunza na kukutana na kesi nyingi sana za watu mbalimbali  katika suala hili. Kwa hiyo ninapoandika haya si tu maadamu naweza kuandika ila naandiaka vitu ninavyojua vinatokea kweli na athari yake ikoje. Na mwezi huu wa tisa ndio kitu ambacho nasikia rohoni tujifunze kwa pamoja.

 

Biblia inasema aziniye na mwanamke afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake? Huenda huwa unausoma tu huo msitari bila kujua uzito wa hayo maneno. Ni vizuri kwanza ukajua kwamba ndani ya nafsi ya mtu ndiko kwenye hisia, nia, akili, na maamuzi. 

 

Mambo matatu yafuatayo ndiyo yanayotokea mtu aliyeokoka anpofanya dhambi hii ya uasherati/zinaa ;

 

Moja, Kuharibika kwa mfumo wa mahusiano na mawasiliano kati yake na Mungu.

 

Katika  mfumo wa ufalme wa Ki – Mungu ni kawaida kwa mtu aliyeokoka na mwenye mahusiano mazuri na Mungu, kuona Mungu akiwasiliana naye kwa njia mbalimbali ili kumshirikisha mawazo na mipango yake ikiwa ni namna ya kumuongoza mtu huyo katika kusudi lake chi ya jua.  Hii ina maana suala la mawasiliano kati ya mtu na Mungu ni la kawaida kwa mtu mwenye mahusiano mazuri na Mungu wake.

 

Sasa mtu anapofanya dhambi hii, athari yake ni hii, dhambi inaharibu mfumo huu wa mahusiano kati ya mtu na Mungu. Na mahusiano kati ya mtu na Mungu yakiharibika  mawasilano kati ya Mungu na mtu yanakatika/kuharibika pia. Ninaposema yanakatika ina maana si rahisi kwa Mungu kusema tena na huyo mtu au huyo mtu kusema tena na Mungu wake kwa sababu asili/mazingira ya mfumo huu hayaruhusu na hili linapelekea mafunuo/sauti ya Bwana kuwa hadimu kwako, kwa kanisa, kwa jamii, kwa kampuni na hata nchi tegemeana na nafasi yako katika ufalme wa Mungu.

 

 

Pili, Kuharibika kwa mfumo wa kufanya maamuzi/kufikiri ndani yako.

 

Dhambi hii inaharibu mfumo wa kufanya maamuzi, shetani anapomuongoza mtu kufanya dhambi hii, lengo/interest yake ipo kwenye nafsi ya mtu huyo. Shetani akikamata nafsi ya mtu maana yake amekamata akili/nia ya mtu huyo, akikamata akili ya mtu huyo maana yake amekamata maamuzi yake pia.   Na akikamata maamuzi yako amekamata matokeo ya maisha yako ya sasa na ya baadae.

 

Hivyo mtu huyu hataweza tena  kufikiri mambo ya rohoni kama Paulo anavyoagiza kwa Warumi ile sura ya 8:5 “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Hivyo kufanya dhambi hii ni kuathiri mfumo wako wa kufanya maamuzi, na hii ina maana hata Mungu akileta wazo lake kwako huwezi kulipokea maana mfumo wa kuamua umeukabidhi kwa Shetani kwa njia ya zinaa/uasherati.

 

Tatu, Kuharibika kwa mfumo wa utiifu ndani yako.

 

Warumi 2:13 says ‘Kwa sababu sio wale wasikiao sheria walio  wenye kuhesabiwa haki, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki”. Kuharibika kwa mifumo huu huu, ni matokeo ya kuharibika kwa mifumo miwili hapo juu yaani ule wa mahusiano na ule wa kufanya maamuzi. Ubaya wa dhambi hii inaharibu mifumo hii ambaayo ndiyo misingi ya mwenye haki. Fuatili maisha ya watu wengi sana walioanguka kwenye dhambi hii angalia utiifu wao mbele za Mungu ukoje. Nakuhakikishia utagundua ni ngumu sana kwao kutii maagizo ya Mungu kwao. Mtu wa aina  hii hata Mungu akimpa maagizo ya kutekeleza hataweza kwa kuwa tayari mahusiano yamevunjika, mamuzi yametekwa .

 

Nini Mungu anataka tujifunze katika hili? 

 

Unapokuwa na mahusiano mazuri na Mungu  hii mifumo yote mitatu inafanya kazi vizuri. Dhambi hii inapoingia inasababisha kuharibka kwa mifumo hii mitatu. Kitu kibaya au kinacho muumiza Mungu ni kwamba  hata kama akikusamehe pale utakapotubu, kwa sababu hii ni mifumo itakugharimu sana kuirejesha mahali pake. “It will cost you taking the systems back to the ancient paths”. Na ndio maana neno linasema afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Hii ina maana kila kilichomo ndani ya nafsi pia kinaangamizwa. Ili kuirejesha mifumo hii maombi ya muda mrefu  ya rehema na kutengeza mahali palipobomoka ni ya lazima.  

 

 

Yamkini unaweza kusema la muhimu Mungu amenisamehe, hayo mengine sijali sana.Unaweza kusema hayo maneno kama hujui/ huelewi muda unathamani kiasi gani kwa Mungu, na pia mahusiano kati ya muda na Mungu. Ngoja nikuambie siri ya Mungu na muda japo kidogo. Muda na Mungu ni marafiki, na tena wote wana mahusiano mzuri sana.  Muda anaongoza maamuzi ya Mungu na Mungu anaongoza matumizi ya muda kwa kuiweka mipango katika ndani ya mtu na kumwagiza atekeleze ndani ya muda. Hivyo kwa Mungu muda ni muhimu sana.

 

Kitu gani namaanisha hapa;

 

Mungu hakutenga/kuweka muda wa mtu kurejesha mifumo hii kwa sababu umeanguka katika dhambi. Katika kipindi ambacho wewe unatubu na kutengeneza kwa Mungu wako ili kurejesha mifumo hii, basi uwe na uhakika upande wa pili umesha athiri kusudi la Mungu  duniani kupitia wewe. Sasa kama utatumia siku tano, mwezi mmoja, miezi sita, mwaka mzima nk, kurejesha hii mifumo basi kwa kipindi hichocho utakuwa umekwamisha kusudi la Mungu kupitia wewe. Na ndio maana biblia inasema Shetani anawinda nafsi yako iliyo ya thamani, maana anajua akikamata nafsi yako amekamata akili, nia, hisia na maamuzi yako na hivyo amefanikiwa kuharibu hiyo mifumo na kusababisha mipango ya Mungu isifanyike kwa muda aliokusudia kupitia wewe.

 

Labda tujifunze kwa mfano huu;

 

Fikiria umepangiwa na Mungu kusafiri umbali wa kilomita 500 ndani ya masaa saba (7).  Mungu amekupa gari ambalo ni kusudi lake kwako. Hivyo litazame   gari ulilopewa kama kusudi la Mungu kwako na wewe ni dereva. Sasa wewe ukaamua kuliendesha  gari bila kuweka maji kwenye injini. Baada ya kusafiri umbali wa kilomita 300 injini ya gari ikafa kwa kukosa maji na mbele yako zimebaki kilomita 200. Je unajua utakuwa umeathiri kwa kiwango gani kusudi la Mungu?. Kutokana na mfano huu unapotenda dhambi hii  je unajua ni kwa kiwango gani utakuwa umeathiri mipango ya Mungu kupitia wewe duniani kwa kipindi chote ambacho utakuwa unairejesha mifumo mahali pake?.

 

Kinacho muumiza/huzunisha Mungu kimsingi si kwa sababu umeanguka dhambini, lakini ni kwa sababu kuanguka kwako dhambini kunamzuia yeye kukutumia wewe mpaka hiyo mifumo yote irejee mahali pake. Hii ina maana interest ya Mungu ipo kwenye muda. Maana anajua itakugharimu wewe muda wa kutengeneza na itamgharimu yeye muda wa kukusubiri wewe utenegeze mifumo hii.

 

Nisikilize  Mungu hategemei wewe uanguke katika dhambi hii, maana kadri unavyoanguka ndivyo unavyokwamisha na kuchelewesha kazi ya Mungu duniani kupittia wewe? Je unajua hasara na matokeo ya kukwamisha na kuchelewesha kazi ya Mungu?.

 

Naamini ujumbe huu utakusaidia kuhakiksha unafanya maamuzi ya kutofanya tena dhambi hii si kwa sababu imeandikwa tu usizini bali ni kwa sababu unampenda Mungu na unataka kuhakikisha kusudi la Mungu linafanikiwa bila kukwamishwa kwa dhambi hii.

 

 

 

Barikiwa tuzidi kuombeana.

 

 

 

 

 

 

 

61 comments

  1. Amen, asante sana mtumishi kwakweli imenigusa na nimefanya tathmini nimepata mifano ya wengi tu walioadhirika na hili. Mungu akubariki na akuzidishie hekima na maarifa. Barikiwa

    Like

  2. Asante Mtumishi wa Bwana kwa kugusia jambo hili linalo tafuna baadhi ya wapendwa kama mchwa, pia mambo kama haya ni nadra kufundishwa makanisani kwa kuogopa kupoteza kondoo, wakaenda sehemu nyingine yenye malisho. Endelea kutufundisha ili kufikia ule utimilifu, kwani yeyote yule anaweza kuanguka katika jaribu. Roho aendelee kukutumia mafundisho yako yananibariki, yananiganga pia. UBARIKIWE MTUMISHI, Mungu akupe siku nyingi za kuishi ili uponye roho za watu wengi, tusije kujikuta tupo jehanamu, wakati duniani tulikuwa tunasema tumeokoka. Be Blessed again. Amein

    Like

  3. Mungu akubariki sana Mtumishi wa Mungu, ujumbe huu ni muhimu sana hasa kwa wakati wetu huu wa mwisho ambao Yesu alisema kizazi hiki hakitapita. Watumishi wa Mungu wengi vijana wameanguka katika dhambi hii. Lakini pamoja na hayo yote tunamwamini Mungu kuwa wengi wachokapo yeye huwatia nguvu walio wake hasa wale wanaomtafuta (Mithali 8:17, Isaya 40:29, Warumi 7:25a).Tumwamini Mungu tu kuwa amejisazia watu waaminifu kwa ajili ya jina lake wasioanguka katika dhambi hii. Mungu akubariki na aendelee kuiinua huduma yako kwa ajili ya kanisa la leo (1Timotheo 1:12)

    Like

  4. mtumishi napenda kufahamu, je mtu anapoanguka katika dhambi hii inatakiwa afanyaje, na anatakiwa awambie watumishi ili wamwongoze sala ya toba au ni yeye na Mungu mpaka kieleweke???? maana biblia inasema ” Mungu hasikii maombi ya mwenye dhambi

    Like

    • Hello ndugu swali lako ni la msingi sana, jambo la muhimu ni toba ya kumaanisha ndani ya mtu husika, toba maana yake ni kujutia kosa ambalo mtu amefanya na kuamua kubadilika kwa kutorejea tena kufanya kosa lile lile. Ndani ya muhusika likijengeka wazo la aina hii na akalitekeleza huyo tunasema ameamua kutubu. Pia nashauri ni vema mhusika akamweleza Mchungaji wake au Mzee nk kwa lengo la kupata msaada zaidi katika kushinda dhambi hii. Hata hivyo ni muhimu sana ukawa makini na aina ya mtu unayemshirikisha suala hili, maana sio wote wanajua namna ya kuwasaidia waliofungwa na dhambi hii.
      Maana wengine unaweza kuwaeleza ukaongeza tatizo zaidi, ukweli ni kwamba hata sasa wako watu wengi sana ambao wameanguka katika dhambi hii na wanaendelea tu na masuala ya huduma as if hakuna kimetokea. Naam jambo muhimu ni kumaanisha kuachana na dhambi husika, kama mtu atalenga kushirikisha watumishi wengine basi atafute waliokua vizuri katika masuala ya imani na wenye ushuhuda mzuri pia ili wamsaidie namna ya kuwa na ushindi dhidi ya dhambi husika.

      Like

  5. BWANA YESU ASIFIWE, MUNGU AKUBARIKI SANA MTUMISHI. MUNGU ANISAMEHE KWANI NIMECHELEWESHA KUSUDI LAKE NAOMBA UNIOMBEE SANA NIRUDI KWENYE NAFASI YANGU ASANTE MUNGU KWA KUMTUMIA MTUMISHI WAKO

    Like

  6. Nimesumbuka sana kujua jinsi ya kufanya toba ya kweli umenisaidia sana. Nitatubu kwa muda mrefu kwa nia ya kuacha dhambi

    Like

  7. Amen,kwa utukufu wa Mungu Baba ubarikiwe sana mtumishi wa Bwana,Neno la Bwana tumelisikia
    Mungu awe nasi,safari ni ndefu na vikwazo ni vingi,tunahitaji rehema yake iliyokuu

    Like

  8. MUNGU ALIE JUU SANA HUKO MBINGUNI , KWA MACHACHE TUNASEMA ATUSAMEE SANA MAANA HATUJUWI KUOMBA IPASWAVYO . NAPIA ALIBALIKI NENO HILI LENYE UWEZO MKUBWA ILI LIPATE KUTENDA KAZI HASA KWA WOTE WALE WANAOHITAJI MSAADA ; AMEN.

    Like

  9. Dhambi hii iliyo zungumzwa na Mtumishi wa Mungu Sanga ni mbaya kweli. Inatesa, inakokota watu bila kujali watumishi na wasio watumishi. Mungu atusaidie Watanzania na kwingineko tuweze kujua kusudi lake kwetu kuwapo hapa ulimwenguni. Nimetafakari sana habari za toba na nimeona dhambi hii yaweza kukufanya uende kwenye toba na hata ulie nakusema tangu leo sintarudia tena. Ubaya wa dhambi hii ukutoka hapo kwakuwa mifumo ilikwisha vurugwa kama tulivyo fundishwa utaona mdada anapita mbele yako na kwa ghafla nikama siyo wewe uliyekuwa unalia kwa uchungu ukiomba kusamehewa na kutorudia tena. Kwa kweli ni jambola kusikitisha sana. Ni mbinu ya kututenga na Mungu milele. Na hata tukitubu kweli na kusamehewa tukapata siku moja nafasi ya kumwona Bwana bado tuna hasara kwani tutaonyeshwa mengi tuliyotarajiwa kufanya katika kulikamilisha kusudila Mungu ambayo sasa kwa ajili ya kuchagua ujinga hatukukamilisha. Walio simama wata julikana nakuvaa taji zao kama mashujaa ilihali wengine kuambulia aibu. Kwakweli ni fadheha. Kimsingi namshukuru mtumishi wa Mungu Sanga na nimeona akisistiza sana kuwa tuzidi kuombeana. Hilo nikweli kwani dhambi hii haimwachi mtu kuwa huru bali mtumwa akitenda lile asilolipenda. Tuzidi kuombeana kwakweli.

    Like

    • Ndg. Kelvine ahsante sana kwa mchango wako muhimu kwenye eneo hili lenye changamoto kubwa. Ulichokiema ndicho hakika kinachowakuta vijana au wapendwa wengi leo ambao walianguka kwenye dhambi hii. Kwa sababu ya changamoto ya kuvuka na kuwa huru kabisa ilivyo kubwa ndiyo maana tunajitahidi kufundisha vijana na wapendwa wajilinde wasianguke kwenye dhambi maana madhara yake ni makubwa sana.Naam na tuzidi kuombeana.

      Like

  10. Amen mtumishi wa Mungu kwa kweli tupo wengi sana tunaoanguka katika hii dhambi jaman ebu tuombe kugeuka jaman ilo andiko linatisha,,,azinie na mwanamke hana hakili kabisa… leo nimepona naanza kujenga kwa upya na Mungu wangu.

    Like

  11. ASHUKURIWE MUNGU ALIYENIPITISHA KATIKA KURASA/BLOG HII.

    Kwanza kabisa nikupongeze kaka Yangu Patrick S. Sanga kwa huduma nzuri unayofanya.

    Dhambi ya uzinzi ni kweli haimuachi mtu kuwa huru, na katika jambo hili nadhibitisha mimi mwenyewe kuwa kuna wakati najihukumu mimi dhamiri yangu mwenyewe, na ninajihisi nisiyestahili kusemezana na Mungu, na hata kama nikiwaza maombi au sadaka nahisi kabisa kuwa haviwezi kupokelewa na Mungu.

    Hali hii hupelekea uzito ktk nafsi na kunifanya kuacha vyote, kwani naona nafanya kazi bure.

    Aidha dhambi hii imekuwa ni msingi wa kulalamika katika maisha yangu, pamoja na ukweli kuwa si kosa pekee kulitenda lakin limekuwa na matokeo mazito katika mfumo wa hisia zangu maana nahisi ndilo mwanzo wa kuporomoka kwa maisha yangu.

    Sichelei kusema, vijana wengi sana tena sana wamebunguliwa na uovu huu, pamoja na somo hili zuri na thabiti,
    Niweke wazi kuwa
    vijana wameanguka katika kipindi cha kutafuta wenzi wao wa maisha.
    Katika kipindi hiki huonja/onjwa na kuacha.

    Ubarikiwe Sanga.

    Like

    • Mungu akubariki sana kwa ushuhuda wako wenye kujenga na kuwasaidia wengine, ndio maana tunajitahidi kuandika masomo haya ili kuwasaidia vijana wasiingie kwenye mtego huo maana utaharibu future yao.

      Like

    • Mungu akubariki sana kwa ushuhuda wako wenye kujenga na kuwasaidia wengine, ndio maana tunajitahidi kuandika masomo haya ili kuwasaidia vijana wasiingie kwenye mtego huo maana utaharibu future yao.

      Like

  12. Barikiwa Kwa Ujumbe Ambao Roho Ayaambia Makanisa(watu), Nimejifunza Mengi Sana. Jina La Mungu Libarikiwe

    Like

Leave a reply to Ashery Mahenge Cancel reply