LAKINI NAMNA HII HAITOKI ILA KWA KUSALI NA KUFUNGA.

 Waraka wa Julai.

 

 

Na: Patrick Samson Sanga.

 

 

Mathayo 17:12 “lakini namna hii haitoki, ila kwa kusali na kufunga”.

 

Mpenzi msomaji naamini kwa sehemu huenda unaijua vizuri habari ya Mathayo 17:14-21 “Habari hii inahusu kijana mmoja aliyekuwa na pepo wa kifafa, wanafunzi wa Yesu wakamwombea wasiweze kumponya. Yesu alipokuja toka mlimani akamponya yule kijana. Baadae walipokuwa faragha wanafunzi walitaka kujua kwa nini wao walishindwa kumtoa pepo. Yesu aliwapa sababu 2, moja kwa sababu ya upungufu wa imani yao, na pili akawaambia namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.

 

Sasa mwezi huu nataka tutafakari swali hili kwa pamoja, Je, ni wakati gani/au kwa mahitaji gani unatakiwa kusali na kufunga? Hapa Yesu alimaanisha kuna mambo/maombi mengine hayawezi kujibiwa mpaka kwa maombi ya kufunga.. Sasa swali ni wangejuaje kwamba hitaji hili/namna hii inataka kusali na kufunga au kusali bila kufunga.

 

Nina amini hata msomaji wnagu una mahitaji mengi unayoombea, yapo ya kwako binafsi, familia, kanisa, nchi, kazi, mume, mke, mchumba, biashara, watoto nk.

 

Hii ina maana kuna baadhi ya maombi yako hayatajibiwa haraka au kabisa hadi uombe na kufunga. Swali ni Je, unajuaje kwamba sasa natakiwa kusali na kufunga au kusali bila kufunga.

 

Mambo matatu yafuatayo yatakusaidia;

 

a)         Kutokuona matokeo ya maombi ya bila kufunga.

Hii ina maana huenda kwa muda mrefu umekuwa ukiombea jambo fulani bila kuona matokeo yake. Usibakie kusema kwamba natakiwa kuwa mvumilivu. Huenda hiyo ni taarifa kwamba ndugu namna hiyo haitoki ila kwa kusali na kufunga. Hivyo ongeza kufunga kwenye maombi yako, utaona matokeo yake kwa kipindi kifupi.

 

b)        Uzito na uharaka wa suala unaloombea.

Uzito wa jambo unaloombea ni kwa mtu binafsi (too personal). Jambo ambalo kwako ni zito/mzigo kwa mwingine si zito. Mfano suala la binti anayetafuta mume/mtu anayetafuta kazi uzito wa hili suala hauwezi kulingana kati ya mtu na mtu. Huenda huyu dada ameomba miaka 3 na hajaona mtu akija kumsemesha, kwa mtu huyu tatizo hili ni zito sana. Hatua kama hii inamtaka afunge na kuomba.

 

Mfano mwingine ni hatari ya kifo kama mazingira yaliyowakuta kina Esta katika utawala wa mfalme Ahusuero, pindi ulipoandaliwa mpango wa kuua wayahudi wote, tunaona walifunga kwa siku tatu, au watu wa mji Ninawi walipoambia na Yona kwamba wasipotubu mji wao pamoja na wao wataangamizwa, nao walifunga. jifunze kwa Esta, Daniel, Yona, Nehemia, Yesu n.k

 

c)   Kwa uongozi wa Roho mtakatifu.

   Mathayo 4:1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani… akafunga siku arobaini …………”

Awali ya yote kumbuka Roho mtakatifu ni msaidizi  hata kuomba anatusaidia. Roho mtakatifu ndiye anayeleta au kuweka  mzigo wa kuomba ndani ya mtu. Roho mtakatifu ndiye anayejua habari ya mambo yajayo, kwa sababu hiyo huwa anamsukuma mtu kufanya maombi ya kawaida au ya kufunga tegemeana na hitaji husika na kile kilichopo mbele ya mtu husika. Kwa lugha nyepesi Roho mtakatifu humuongoza mtu katika maombi ya kawaida au ya kufunga pia.

 

Hivyo basi Roho mtakatifu akikuongoza kufunga wewe usimzimshe au usikwepe maana yeye anajua nini kinaenda kutokea mbele yako na kinahitaji nguvu kiasi gain ya maombi ili uweze kuvuka au ili namna hiyo iweze kutoka.

 

Ni imani yangu kuwa ujumbe huu mfupi utakusaidia kukujengea nidhamu katka maombi yako kwa ujumla na utakuwa makini na maombi unayoyafanya.

 

Barikiwa na Yesu kristo.

 

 

Advertisements

44 Comments »

 1. 1
  DORA Says:

  Nahitaji mniombee kuhusu maisha yangu Mungu aniongoze na kunisaidia kwa kila njia nipitayo. Naomba mniombee tena Mungu amguse mchumba wangu asidanganyike na ya dunia kwakua anapata vishawishi vingi sana nakuomba mchungaji umuombee ili Mungu amshindie kila anapopita na majaribu ya shetani yashindwe kabisa. Nahitaji msaada wako mchungaji Mungu akuongoze katika kuliombea jambo hili, Mungu akubariki.

 2. 2
  past.mukongo bahanda yohana Says:

  Tunawashukuru sana kwa maombi yenu mutusaidiye kuomba kwa ajiri ya kazi ya Bwana.

 3. 4
  Aneth Says:

  Bwana yesu asifiwe,

  Nimeguswa na hii website sikuwa naifahamu.

  1. Ila nina mmzigo mkubwa sana wa madeni natamani ninywe sumu nipotee humu duniani.Bwana Yesu naomba nifungue katika kifungo hiki kibaya.

  2. Nipo katika harakati za kutafuta kazi nimeshaitwa kwenye usahili zaidi ya mara tatu sehemu tofauti (wiki iliyopita) naomba Bwana Yesu akatende miujiza niweze kufanikiwa.

  Barikiwa.

  • 5
   sanga Says:

   Hello Anneth,
   nami pia nimeguswa sana na haja uliyo nayo. Nakuomba tafadhali usichukue maamuzi wala hata kufikiri kunywa sumu maana kwa kufanya hivyo unampa Ibilisi nafasi ya kukumaliza kabisa na kukupeleka kuzimu ukawe mali yake milele. Unisikilize madeni na kuto kupata kazi visiharibu mahusiano yako na Mungu na pia future nzuri ambayo Mungu amekuandalia. Mawazo ya Mungu juu yako ni mazuri sana hebu soma Yeremia 29:12 uone Mungu anakuwazia nini?

   Nafikiri unahitaji ushauri mzuri kwa sasa, hivyo nenda kanisani tafuta watu au mtu aliyeokoka vizuri na mwenye ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu naamini atakusaidia. Nami pia nitazidi kuwasilana nawe.
   Pili hakikisha unajenga nidhamu ya kusoma Biblia na kuitafakari sambamba na kuomba kila siku hakika utaona mabadiliko makubwa, maana neno la Bwana ni taa ya miguu yetu.

   Ndg waombaji na wasomaji wa blog hii naomba tushirikiane kuomba na kumtia moyo dada Aneth katika changamoto hizi zinzomkabili.

   • 6
    Aneth Says:

    Amen Kaka Sanga.

    Nimefurahi sana kwa kunipa moyo..nitatenda kama ulivyoniagiza. Na sitaacha kukushuhudia.
    Bwana mungu akubariki sana.

    Aneth

 4. 7
  Jackob I Kaaya Says:

  BWANA YESU ASIFIWE AMENISISIMUA DADA ANETH
  NAPENDA KUKUTIA MOYO NA PIA AONDOE MAWAZO
  YA KUNYWA SUMU KWANI UTAKUA UMEKIMBIA MADENI
  NA KUKIMBILIA MOTO WA JEHANAM .
  MUNGU AKUBARIKI ZIDI KUMWOMBA MUNGU.

 5. 8
  peter japron tem Says:

  Napenda kuwasalimu ninyi nyote kwa jina la Yesu kaka Sanga nimesoma sana mafundisho yako yamenibadilisha mambo mengi. Naomba Mungu azidi kukutia nguvu ili uzidi kufundisha kondoo wa Bwana pia ningeitaji unitumie mistari ya kunifundisha kupitia e.mail yangu asante sana kaka sanga.

 6. 9
  peter japron tem Says:

  Bwana apewe sifa napenda kumtia moyo Dada Aneth aondoe hilo wazo la kunywa sumu bali asimame kwenye neno atayashinda majaribu yote ubarikiwe Dada na Bwana amen..

 7. 10
  mary budili Says:

  Bwana Yesu apewe sifa. Napenda kutoa shukurani zangu kwa kazi nzuri ya mtumishi. Somo lake hapo juu, limefunulia upeo wa juu sana katika kuendelea kukua kiroho.
  Bwana akubariki sana mtumishi.Akupiganie katika kazi yako.
  Na usichoke kutuombea na kunitumia masomo mengine yatakayonisaidia kukua kiroho. AMEN

 8. 11
  kwezi y. Mwakapala Says:

  kwa kweli nami sikuwa nafahamu web hii ni nzuri nitakuwa mwanachama ubarikiwe kaka sanga

  Kwezi

 9. 13
  Mamlimbo Says:

  Shalom!

  Asante kwa somo hili, binafsi nimekua natafuta info abt fasting bila mafanikio, napenda kupendekeza ikiwezekana utuwekee maelezo zaidi on how to go abt it (fasting). Kwa mfano Kufunga mlo mmoja, miwili ama milo yote. Ama kufunga chakula ukipendacho zaidi, kufunga kufanya vitu uvipendavyo kama vile kuangalia tv. Hope that makes sense.

 10. 14
  Pendo Says:

  Bwana Yesu asifiwe!

  nashukuru sana kwa mafundisho yako mazuri. Naomba mniombee kwani nimechoka kuwa hekalu la mapepo na majini nahitaji kuokolewa sasa. Nitashukuru sana pindi yatakapokimbia

 11. 15
  noel chitanda Says:

  sijui niseme nini, Mungu awabariki. Naahidi kuiweka blog hii kwenye maombi yangu leo, na wote watakaogusa tu kwa maana ya kuifungua na kujifunza chochote basi Mungu akutane na haja ya moyo wake.

  • 16
   sanga Says:

   Amina Mungu akubariki, naomba maombi yako yawe endelevu kwa blog hii na nyingine nyingi zenye kufundisha neno la Mungu, ubarikiwe sana.

   • 17
    ruth Says:

    Bwana Yesu asifiwe, mimi napenda kumtia moyo dada Anneth kwamba aachane na mawazo ya kunywa sumu kwani kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu. Neno la Mungu linasema Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu chini ya jua. Tena Mungu anafanya njia pasipo na njia.

    Usiache kuomba dada yangu.

    Mungu akubariki.

    Ruth.

 12. Mungu akubariki Mr. Sanga kwa huduma yako.

 13. 20

  Ukifunga na kuomba,unaongeza siginal za kiroho.hivyo unakuwa mwepesi wa kusikia sauti ya ROHO MTAKATIFU.unakuwa mwepesi

 14. 22
  ALPHONCE MICHAEL Says:

  Mtumishi, Bwana Yesu apewe sifa sana, umekuwa baraka na unazidi kufanyika baraka katika maisha yetu ya wokovu, hakika unatujenga nakutuimarisha kiroho, binafsi tangu nilipo anza kufuatilia masomo yako kwa sehemu misuri yangu ya imani ninaiona ikikua.

  • 23
   sanga Says:

   Amina Ndg. Alphonce, tuzidi kuombeana, endelea kuongeza jitihada yako katika kumjua Mungu, utazifahamu siri nyingi za ufalme wa Mungu.

 15. 24
  Elisante Tasseni Says:

  1.kuna baadhi ya watu wanaosema kufunga sio kws chakula,bali kwa imani
  2.utajuaje suala unaloliombea linahitaji mfungo wa siku ngapi?

 16. 25
  jahet kanywa Says:

  wanamao naitaji maombi yenu mimi mwana maobi mwenzenu nina kikundi cha maombi ambacho sasa ivi kinaitaji msaa wa vitendea kazi kwaajili ya huamsho wa vijana makanisani kinaitwa sinai naitaji maombi yenu na michango kwaajiri ya kununu vyombo vya mzik

 17. 27
  ester Says:

  naomba mniombee nipate kazi

 18. 29
  DEVIS RWEYONGEZA Says:

  ubarikwe sana, kaka ninaloloombi juu mchumba nisaidie.

  • 30
   sanga Says:

   BWANA Mungu akufanikishe kwa kadri ya mapenzi yake, kadri nipatavyo nafasi kuna masomo nitakutumia ambayo naamini yatakusaidia zaidi, nikisahau nikumbushe tafadhali.

 19. 31

  upo. vizuri nafulahi sana ninapo sikia neno la. mungu ila nahitaji pia. kujua kuomba na kusoma bublia na kuweza kuichanganua

 20. 33
  IRENE Says:

  Ubarikiwe sana kwaajili ya huduma yako mungu aendelee kukutia nguvu katika hili

 21. 35
  FELICIAN Says:

  Kweli mtumishi umenena kitu kilicho harisi.
  Kuna siku nilisikia kiashiria moyoni kinanielekeza kufunga ila sikujali na kesho yake jirani yangu alianza kuvukiza udi kwake na ile harufu ilinisumbua sana maana ilikuwa inaishia chumbani kwangu.Baada ya hapo nilianza kujisikia vibaya..Nilipoona hivyo nikakumbushwa kuwa nilipewa taarifa moyoni kabla haya mambo kutokea..Naliomba toba kwa kutomsikiliza Roho Mtakatifu na kisha nikafunga siku2.Wala sikusikia hiyo harufu ikivukizwa tena,na niliskia kuendelea kufunga

 22. 36
  Beda Modest Levira Says:

  Tumsifu Yesu Kristo!
  Mimi ni muajiriwa katika masuala ya miradi maendeleo ya jamii hususani maji na mazingira, kazi ambayo hunipasa kuishi maeneo husika ya utakelezaji wa mradi.
  Nilibahatika kufunga ndoa miaka mitatu iliyopita na kwakipindi chote hiki maisha yangu yamekuwa nikuishi na familia kwa kipindi kifupi kifupi yaani kipindi cha likizo tu kitu ambacho kwakweli kwa maisha ya sasa inatuwia vigumu mimi pamoja na mwenzangu.
  Kusudi la kuandia ujumbe huu ni kuwaomba ndugu zangu mnisaidie hususani katika sala zenu ili niweze kutatua suala hili kwa namna ambayo mwenyezi mungu anaona inatupasa.
  nawatakia maisha mema,
  Kristo….

 23. 38

  Ubarikiwesana Mchungaji Ilanaombauniombee Nipatemtoto Bwanaakubariki

 24. 40
  judith Says:

  jamini blog nzuri sana pianahitaji maombi maan nnamizigo mizito nahitaji kuitoa

  • 41
   Flavious Says:

   Muite MUNGU kwa toba, kwa kufunga na kusali. Mimi nimeona miujiza mikubwa kupitia Mungu na hakika nimuweza wa yote. Kikubwa ni kuisikiliza sauti ya Bwana Mungu bila kwenda mkono wa kushoto wala wa kulia soma Kumb.la Torati 28:1-14 uone baraka alizokuandalia Mungu na vile vile katika Isaya 54:7. hakika fadhili na Ahadi za Bwana ni za kweli. Katika Injiri ya Yohana 14:13 Yuse anaahidi kutupa chochote tuombacho kwa jina Lake

 25. 42
  Anny Says:

  Naomba mniombee mambo yafuatayo; 1. nitapate mwenzi wa maisha maana nimeshaomba sana lakini bado sijafanikiwa. 2. mniombee Mungu anibariki nipate pesa kwa ajili ya mahubiri kanisa letu limepanga kila familia wafanye mahubiri. 3. Mungu anisaidie kushinda majaribu maana tuko katika kipindi cha mwisho na Mungu anipe uamsho wa kiroho ili nifanye kazi yake maana watu ni wengi hawajamfahamu.

 26. BWANA apewe sifa sana wapendwa Wa mungu, naomba mniombee sana Mungu anipe kibari kwaajiri ya safari yangu ya kwenda nje ya nchi kufanya kazi,amen


RSS Feed for this entry

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: