NINI CHA KUFANYA MUNGU ANAPOWEKA MSUKUMO/MZIGO WA KUOMBA NDANI YAKO? (Part 1)

 

 

Na: Patrick sanga.

 

Mpenzi msomaji wangu ni imani yangu kwamba unaendelea vema katika Bwana. Katika mwenzi huu wa tano nataka kujibu swali hili ambalo naamini limekuwa likiwasumbua wengi hasa wanpokuwa kwenye mazingira hayo.

Mwezi wa nne mwanzoni kiongozi wa kundi fulani la kiroho kutoka Lindi, alinijia akaniuliza akisema, mara nyingi Mungu huwa ananiwekea  msukumo wa kuomba ndani yangu .Je natakiwa kufanya nini pindi msukumo huo unapokuja?

 

Kwa sababu watu wengi pia wamekuwa wakiniuliza swali hili, ndiyo maana nimeona ni vema nilijibu pia kupitia blog hii ili kuwasaidi na wengine ambao wangependa kujua.

 

Yule mtumishi nilimjibu hivi;

 

Moja, nilimueleza kwamba ni kweli kabisa na ni kibiblia Mungu kuweka mzigo wa kuomba kwa watu wake mbalimbali hapa duniani kwa ajili ya ufalme wake.

Mbili, Unapokuwa kiongozi wa kundi la watu kwa maana ya mchungaji, mwalimu nk tegemea sehemu kubwa msukumo utakaokuja utalenga hao watu unaowaongoza. Na kama sivyo basi mapema kabisa Mungu atakuwa bayana juu ya hilo.

Tatu, matokeo ya kile unachokiombea ndiyo yanayoonyesha mwisho wa huo mzigo au msukumo ndani yako. Unachokiombea kikitokea ule mzigo unaondoka ndani yako kuashiria kuna kitu kimezaliwa au kufanyika.

Nne, mara nyingi Mungu anapokuwekea msukumo wa kuomba huwa anakuwa wazi juu ya nini anataka ukiombee au huo mzigo unahusu kitu gani?.Kuwa wazi haaimanishai kila anapoweka huo mzigo anakuuleza unahusu nini?

Tano, ni jukumu lako kila unpopata msukumo wa kuomba kumuuliza Mungu huo msukumo unahusu nini?

Isaya 40:6 inasema ‘ Sikia ni sauti ya mtu asemaye lia, nikasema nilie nini? Wote wenye mwili ni majani.

Sita, sio mara zote pia ukimuuliza Mungu huo mzigo ni wa nini atakujibu isipokuwa utashangaa ule msukumo bado upo tena kwa nguvu ya ajabu.

Saba, unachotakiwa kufanya endelea kuomba tu hasa kwa kunena kwa lugha mpya. Wakati huohuo maombi yako yalenge pia kutaka kujua nini unakiombea na kwa vyovyote vile lazima Mungu atakujulisha tu kabla au pindi matokeo ya maombi yakikamilika. Japo awali anaweza asiwe wazi kukutajia wahusika kama ni mzigo unaolenga mtu au watu, anaweza kukutajia tatizo, au shida ya huyo mtu pekee kwanza.

Nane, Mungu ana njia nyingi za kuweka msukumo au mzigo ndani yako. Kitu cha muhimu ni kujua jinsi Mungu alivyozoea kusema nawe mara kwa mara kupitia nafsi, roho au mwili wako. Hapa namaanisha je ni ishara (Signal) gani ikitokea kwenye nafsi, roho au mwili unajua kwamba huu ni uwepo wa Bwana au hapa Bwana anasema nami.

Zaidi ni muhimu kujua kwamba msukumo wowote ambao Mungu anauleta huwa unakuja kwa nguvu kisasi kwamba unaweza kushindwa kufanya hata jambo lolote lile japo hili linategemea na uharaka(urgency) ya jambo husika.

 

Tisa, Misukumo au mizigo ya kuomba ipo katika viwango mbalimbali.

*Muda mfupi– mtu anapopewa kuombea hitaji la mtu fulani

*Muda wa kati – unaombea jambo linalookaa kwa kipindi kifupi cha muda.

*Mzigo mkubwa/muda mrefu – Msukumo unodumu kwa mda mrefu..

 

Kumi, Mzigo au msukumo wowote ule una;

*Mfumo wake maalumu wa kuuombea – yaani aina ya maombi unayotakiwa kuomba. Hivyo ni vema ujifunze kumuliza Mungu ndiyo ninaombaje juu ya mzigo huu ulioweka ndani yangu.

*Maagizo yake – hii ina maana hakikisha neno la Kristo linakaa kwa wingi ndani yako ili iwe rahisi kuelewa maagizo anayokupa juu ya lile unaloombea tegemea na ngazi ya jambo lenyewe.

*Muda maalumu wa kuliombea hili jambo –  yaani  muda mfupi, muda wa kati au muda mrefu .

*Upako maalumu wa kukusaidia kuubeba huo mzigo – kitu cha muhimi ni kujua kushirikana na huo upako kwa maana ya kuhakiksha unomba kwa kadri ya ratiba ya Mungu ya kuliombea hilo jambo.

 

Naamini ujumbe huu utafanyika msaada kwako na utajusaidia kujua nini ufanye pindi Mungu anapokuletea msukumo au mzigo wa kuomba.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s