IMANI

Waraka wa Mei.

Na: Patrick Samson sanga.

 

Waebrania 11:1 ‘Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana’.

 

Ukisoma vema (Mathayo 17:14-21) V19,20 utagundua  wanafunzi wa Yesu walishindwa kumtoa pepo kwa sababu ya upungufu wa imani yao.

Sasa, tujiiulize maswali yafuatayo;

 

1. Je Kuna uhusiano gani kati ya imani yao na kutoa pepo?

2. Ni upungufu gani/ upi wa imani walikuwa nao?

3. Je ni kiwango gani cha imani walikihitaji ili kumtoa yule pepo?

4. Je walitakiwa kuongezaje imani yao?/imani inaongezekaje?/unawezaje kuongeza imani?.

 

Swali la kwanza ; Kuna uhusiano gani kati ya imani yao na kutoa pepo?

 

*Kwa mujibu wa Waebrania 11:6 ‘Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Si hivyo lakini Biblia pia inasema katika Marko 9:23 ‘Yote yawezekana kwake aaminiye’ Hivyo pepo asingeweza kutoka kama maombi hayakuwa connected na imani. Na kwa hiyo walihitaji imani pia ili waweze kumtoa pepo.

 

Swali la pili; Upungufu wa imani ya wanafunzi ulikuwa kwa namna mbili;

 

2.1. Wakati wanaomba ndani yao hawakujenga imani/hawakuwa na uhakika kwamba kwa maombi yao katika saa ile yule mgonjwa atapona. Hii ina maana maombi yao yalipungukiwa imani. Hivyo maombi peke yake bila imani hayatoshi kutengeneza jibu la mahitaji yako. Marko 9:14-29, v29. Hapa Waebrania 11:6 ilikuwa imepungua.

2.2 Kiwango cha ufahamu wao juu ya kutoa pepo kilikuwa ni kidogo sana  na ndio maana pepo hakutoka. Refer Marko 9:14-29, v17 – wanafunzi wajua pepo bubu tu. V25 – Yesu alimuona na pepo kiziwi.

 

Swali la tatu ; .Je ni kiwango gani cha imani walikihitaji ili kumtoa yule pepo?

3.1Wanafunzi walihitaji imani kiasi cha punje ya haradali ili waweze kumtoa yule pepo.  Je kiwango hicho ni kiasi gani?

Soma vizuri hii mistari kwanza; Luka 17:6 inasema ‘Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali ,mngeuambia mkuyu huu ng,oka ukapandwe baharini nao ungewatii na Marko 11:23 inasema ‘Amini, nawaambia, yoyote atayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia yatakuwa yake pamoja na Mathayo 14:31’…..Ewe mwenye imani haba mbona uliona shaka’.

 

Sasa kama ukiunganisha kwa kuyahusianisha  mawazo ya mistari hii mitatu utapata sentensi inayosomeka hivi, ‘Kama mngekuwa na imani pasina/bila kuona shaka ndani yenu, bali mkaamini hayo msemayo yametukia, basi mngeuambia mkuyu huu ng’oka ukapandwe baharini nao ungewatii’. Kilichomfanya Petro aanze kuzama ndani ya maji ni kuona shaka.

 

 Kwa lugha nyepesi wakati wanaomba wanafunzi walitakiwa kutokuwa na shaka ndani yao juu ya uhakika wa kutoka kwa pepo yule. Imani ya wanafunzi haikufika size ya punje ya haradali kwa sababu ndani yao walioona shaka na ndio maana walishindwa kumtoa pepo. Hivyo imani kiasi cha chembe ya haradali ni imani ambayo ndani haioni shaka/ina uhakika wa asilimia zote mia moja.   

 

Swali la nne, Wanafunzi walitakiwa waongezeje imani yao?/ imani inaongezekaje?/unawezaje kuongeza imani?.

 

Unaweza kuongeza imani yako juu ya kitu chochote kwa njia kubwa nne zifuatazo:

 

1.Kwa kusikia – warumi 10:17, Yohana 17:20, Mithali 2:29, Zab 42:5,11, 56:11.

Warumi 10:17 Biblia inasema chanzo cha imani ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Hivyo basi kumbe chanzo cha imani ni kusikia. Na hii ina maana kadri unavyozidi kusikia juu ya habari fulani/jambo fulani/mtu fulani ndivyo na imani yako juu ya hicho kitu inavyoongezeka.

 

Ikiwa imani chanzo chake ni kusikia hii ina maana kadri unavyooendelea kusikia habari za kitu fulani ndivyo imani yako juu ya hicho kitu inavyozidi kuongezeka. Soma 1Wakorinto 15:33 & Zaburi 1:1. Yohana 17:20 – imani inakuja kwa kusikia neno, hivyo ili imani yako ipate kuongezeka basi tafuta na lenga kusikia neno hilo kwa wingi zaidi.

 

Hebu tuangalie mfano huu katika Luka 17:5 Mitume walimwambia Bwana tuongezee imani? Je Bwana aliwaongezeaje imani?

*Kwanza alijenga msingi wa wanafunzi kuwa na imani kiasi cha punje ya haradali siku zote V6.

*Pili Kwa kuponya watu 10 wenye ukoma V11-19. Japo kwenye zoezi hili la kwanza wanafunzi hawakuelewa bado wakaja kuelewa kwenye mfano au zoezi la pili wa Marko 11:12-24. V12 – wanafunzi wake wakasikia, V20&21 – wanafunzi wakakumbuka kitu alichosema Yesu juu ya ule mtini.

 

2.Kwa njia ya mawazo/kubuni/kufikiri – Webrania 11:10,27,28, Mithali 23:7a, Ezekiel 38:10, Nehemia 6:8, Mathayo 15:9. Imani ni kuona, kutazamia na kuhesabu. Mfano Imani ya Ibrahimu – Waebrania 11:8,10,17,19. Imani ya Yakobo – Waebrania 11:20+21, Imani ya Musa     Waebrania 11:25,26,27.

Hawa ndugu imani zao zilijengeka/kuongezeka kutokana na nguvu ya kuona, kutazamia,kufikiri, kuwaza, kubuni, i.e power of positive thinking.

Kadri walivyotumia muda mwingi kufikiri juu ya matarajio yao na ahadi zao ndivyo imani ilivyoongezeka.

 

3.Kwa njia ya ufahamu – Webrania11:3 inasema  kwa imani twafahamu—–, na  hii ina maana imani inampa mtu kufahamu Mithali 2:2b,4,5, (11b relates to  Waebrania10:38), Mithali 8:14b, Mathayo 15:21-28, V27 (hii ni habari ya yule mwanamke Mkananayo ambaye binti yake alipagawa na pepo). Mathayo 8:5-10, V9 (hii ni habari ya akida aliyekuwa mna mtumishi ambaye amepooza).

Kwa lugha nyingine jitengenezee vyanzo vya mapato wa ufahamu juu ya Yesu (Mithali 4:7) ili imani yako juu ya Yesu iongezeke. Na hili lina maana wanafunzi walitakiwa kuongeza ufahamu wao zaidi juu ya kutoa mapepo ili wakati kwingine pepo wasiwasumbue tena. Hivyo unataka imani yako juu ya damu ya Yesu, kuponya wagonjwa, kufungua waliofungwa basi hakikisha unaongeza ufahamu wako kwa kusoma na kusikiliza kila mafundisho au mahubiri yanayolenga kile unachotaka imani yako iongezeke.

 

4.Kwa njia ya maombi – Luka 22:31, Luka 18:1, Waefeso 6:18,

Yohana 17:11,15,20. Katika Luka 22:31 alikuwa akijibu swali la Luka 18:8.

Hapa kwa kifupi Yesu alikuwa anamwambia Petro, najua jaribu linalokwenda kukupata na shetani anataka kukupeta kama ngano, sasa nimangalia imani yako nikaona haiwezi kushinda jaribu hilo, hivyo mimi nimekuombea ili imani yako isitindike.

 

Neema ya Kristo na iwe nawe.

 

Advertisements

One comment

  1. Aisee nimepata kuelewa zaidi juu ya Imani na ninaamin maombi yngu yatajibiwa coz ndani yke pia nimeweka imani ya kuamini kwmba Yesu anaweza, na nina imani mungu atatenda. Maana inaenda kuleta majibu mahali ambapo cna ndgu wala rafk isipokuwa Yesu peke yke. Nimefurahi sana kw somo la Imani

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s