JIANDAE KUFA KIFO KIZURI.

Waraka wa Aprili. 

Na: Patrick Sanga.

 

‘Maadam unaishi, lazima utakufa pia, hata kama hupendi kufa, kifo ni sehemu ya maisha na kinakungoja. Kifo chako ni mwanzo wa aina nyingine ya maisha ya umilele. Maisha hayo ni huenda  uzima wa milele au mateso ya milele katika Jehanum ya moto. Maamuzi ya wapi unataka kwenda yanafanyika kabla hujafa. Kwa hiyo ni afadhali ufanye   maandalizi mazuri sasa, maana unakokwenda baada ya kufa kunategemea sana maamuzi yako ya sasa kabla hujafa na baada ya kufa hakuna uhuru wa kuamua wala nafasi ya kujaandaa tena’.

 

Mpenzi msomaji, katika mwezi huu wa nne, nahitimisha ujumbe nilioanza nao mwezi machi unosema ‘USIKUBALI KUFA KIFO CHA KIPUMBAVU’. Nyaraka hizi mbili  nimeziandika kwa mujibu wa Bibblia au kutoka na Biblia. Lengo la nyaraka hizi 2 kwako sio kukutisha au kukuogopesha bali ni kukumbusha tu kile amabcho Neno la Mungu linasema. Na zaidi ni kukutahadharisha juu ya maisha yako baada ya kufa.  

 

Kuzimu (Isaya 14:9-11) ni mahali ambapo watu ambao wamekufa katika dhambi wanahifadhiwa wakisubiri hukumu ya mwisho na kisha watupwe Jehanamu ya moto kwa hukumu ya moto wa milele. Huko kuzimu kuna mateso yasiyo ya kawaida ambayo hakuna mfano wake.  

 

Kwa taarifa yako kuna nyakati Yesu huwa anashuka kule kuzimu kwa maksudi maalumu. Akiwa huko huwa anawaona watu wanavyoteseka na kupata taabu sana. Moyo wake huwa unaumia sana kwa sababu hakutaka wale watu waende kule, lakini maamuzi na maandalizi yao ya kufa  wakiwa duniani hayakuwa mazuri na hivyo wakajikuta wakitupwa kuzimu baada ya kifo chao.

Yafuatayo ni mambo ya msingi yatakayokusaidia kufanya maandalizi mazuri ya kifo chako ili kujitengenezea mazingira mazuri ya maisha yako baada ya kufa;

 

*Kufanya maamuzi ya kuokoka sasa kabla hujafa.

 Yohana 3:16 ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Biblia inaposema asipotee inazungumzia kwa habari ya mtu huyo kufa katika dhambi zake na hivyo kuukosa uzima wa milele. Hivyo basi kama haujaokoka nakushauri chukua hatua ya kufanya maamuzi ya kuokoka. Kama unataka kuokoka bonyeza category ya wokovu utapata maelekezo zaidi.

 

*Kulitumikia kusudi la Mungu.

Matendo 13:36 ‘ kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala akawekwa pamoja na baba zake,akaona uharibifu’.Kulitumikia shauri la Bwana maana yake ni kutekeleza au kukamilisha wajibu ambao ulimfanya Mungu akuumbe. Kila mtu chini ya jua ameumbwa kwa kusudi maalumu. Hivyo ni vema ukajua kwa nini uliumbwa na kisha kila unalofanya lilenge kutekeleza wajibu wako. Kibiblia Mungu huruhusu kifo kwa mtu wake anapokuwa amemaliza wajibu wake duniani.

 

*Kuyafanya mapenzi ya Mungu.

Mathayo 7:22  Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni’. Mpenzi msomaji suala si kuokoka tu, bali zaidi unatakiwa kuyafanya mapenzi ya Mungu. Mapenzi ya Mungu yamefungwa kwenye  Neno lake na Roho mtakatifu. Kwa ufafanuzi zaidi hapa nenda bonyeza Category ya ‘Maswali na Majibu’ na kisha fungua ujumbe unaosema nini maana ya mapenzi ya Mungu.

 

*Kuishi kwa imani.

Waebrania 11:6 ‘Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima amini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao’. Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo tena bayana ya yale yasiyoonekana. Sote tunatarajia kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo kuja kulichukua kanisa lake au watakatifu.

 

Sasa hili ni suala la imani na hii ina maana endelea kuamini hivyo mpaka siku ya kufa kwako, isifike mahala ukasema huyu Yesu harudi bora niishi maisha ya dhambi. Uwe na imani na siku moja utamwona. Usiruhusu mtu, jambo au kitu chochote kikuondolee imani yako kwa huyu Yesu Kristo maana hakuna mtu atakayemwona baba (Mungu) bila kupitia kwake (Yesu) kwa maana ya kumwamini yaani kuwa na imani kwake (Yohana 14:6).

 

*Kuishi kwa amani na watu wote na maisha ya utakataifu.

Webrania 12:14 ’Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao’.

 

Zaidi unatakiwa pia ujitahidi kuhakikisha kwamba siku zote unaishi maisha ya utakatifu na pia unakuwa na amani na watu wote. Biblia imeshasema kukosa mambo haya ni kukosa kumwoana Bwana, hivyo ukifa wakati huna utakatifu na huna amani na watu pia maana yake tegemea kutupwa kuzimu.

 

Kutekeleza mambo hayo manne hapo juu na kisha kuhakiksha jambo la 2,3 na la 4 yanakuwa sehemu ya maisha yako nakuambia ndiko kufanya maandalizi ya kifo chako.  

 

Hivyo basi kama hutaki kufa kifo cha kipumbavu sawasawa na ujumbe wa machi basi ni vema ufanye maandalizi ya kufa kifo kizuri ili uweze kuurithi uzima wa milele pamoja na Kristo (Yohana 14:1-3), kwa sababu maamuzi ya wapi unataka kwenda ukifa yanafanyika kabla hujafa.

 

Neema ya Bwana wangu Yesu Kristo ikufunike.

Advertisements

8 comments

  1. Mungu azidi kupewa sifa milele na milele kwa kutuletea mafundisho ya uzima wa milele kupitia kwa mtumishi wake BWANA MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI. AMINA

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s