NAMNA AMANI INAVYOWEZA KUAMUA KWA AJILI YAKO.

Waraka wa Februari. 

Na; Patrick Samson sanga.
Wafilipi 4:7 inasema ‘Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote , itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu’.

Wakolosai 3:15″ Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja tena iweni watu wa shukrani “.

Yohana 14: 27 ‘Amani yangu nawaachieni; amani yangu nawapa;niwapavyo mimi si kama ulimwengu utoavyo.Msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwe na woga’

Ule mstari wa 6 wa kitabu cha Wafilipi sura ya nne unasema “Msijisumbue kwa neno lolote ;bali katika kila neno kwa kusali na kuomba , pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu’’ Kimsingi mstari huu unazungumza suala la mahitaji/maombi ambayo watu wanakuwa nayo siku zote na wanayapeleka mbele za Mungu. Katika haya mahitaji mhusika anakuwa anahitaji kujua/kupata jibu kwa kuwa linamsaidia au litamsaidia katika kufanya maamuzi fulani.

Haya ni maombi ambayo mhusika anasubiri kwa hamu jibu ili afanye maamuzi. Mfano, Binti anayeomba kujua je, kijana aliyemfuata kutaka kumuoa ni wa mpango wa Mungu au kijana anayetaka kujua ni binti gani katika wengi waliopo ambaye hakika ni mapenzi ya Mungu waoane, au pia mtu anayeomba kujua je ni mpango wa Mungu aache kazi na kuanza huduma n.k au tuseme mwanafunzi ambaye anenada kuanza mwaka wa kwanza chouni na anataka kujua ni kozi gani Mungu anataka asomee? Nk.

Sasa, Kibiblia amani imewekwa au unapewa amani ili ikusaidie kufanya hayo maamuzi. Maana imeandikwa katika Wakolosai 3:15 “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu…………’.Sasa hii ina maana ni lazima amani iamue kwanza na kisha wewe ufuate uongozi wa amani yaani amani ya Kristo ikuongoze wewe kufanya mamuzi, ikuelekeze upi ni uamuzi sahihi na mzuri.
Je, amani inaamuaje ?

Kwa kuuhifadhi moyo wako na nia yako katika Kristo Yesu.

Ezekieli 38:10 inasema Bwana Mungu asema hivi; itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya; na pia Nehemia 6:8 kwenye kipengele cha mwisho inasema ‘Lakini kwa moyo wako wewe mwenyewe umeyabuni’, ukisoma pia ‘Mathayo 15:19 inasema ‘kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati,wivi,ushuhuda wa uongo na matukano’. Hivyo basi ukiiunganisha hiyo mistari mitatu utajua kwamba kumbe mawazo huingia moyoni, mawazo hubuniwa moyoni na kisha mawazo hutoka moyoni.

Moyo wa mtu ni uwanja wa mapambano ambao ndani yake kuna mawazo mengi sana ambayo humwingia mtu na kubuniwa yakisubiri kutoka. Yapo mawazo ya kutoka kwa Mungu,shetani au ya mtu binafsi. Na mara zote yale ya shetani ni ya kupinga kusudi la Mungu kwa huyo mtu na pia mara nyingi ya kutoka kwa mtu pia huwa hayalingani na ya Mungu.

Sasa kwa kujua hilo Yesu alituachia amani, kinachotokea wakati unaomba ni hiki , amani inaukamata moyo wako ili kuhakikisha kwamba mawazo mengine ya Shetani yanayoweza ingia ndani yako yasiweze kuuondoa moyo wako kwenye nafasi ya wewe kukaa ndani ya kusudi la Bwana ili kulinda nia ya Kristo ndani yako isiharibiwe.

Hii ina maana kazi ya amani ni ya ulinzi. Kwa hiyo tunaweza kusema licha ya amani kuwa mwamuzi, amani pia ni mlinzi. Amani anafanya kazi ya kuulinda moyo wako na nia yako isiharibiwe na mawazo ya kutoka kwa shetani kwa kuwa mawazo hayo yamebeba kusudi baya.
Kwa hiyo amani inapigana kuhakikisha moyo wako hauharibiwi na mawazo mengine yaliyoko kinyume na mapenzi ya Mungu juu ya ombi au hitaji ulilonalo mbele za Mungu. Sasa ikishaulinda moyo wako dhidi ya mawazo mengine kuhakikisha kwamba hayaharibu mpango wa Mungu juu yako ndio inakuongoza katika uamuzi ambao ni sahihi.

Na ili kujua uamuzi huo ni sahihi amani itakupa raha nafsini mwako, utajisikia furaha na nafsi yako kufunguka juu ya kufanya jambo fulani. Ukiona hayo mazingira ndani yako fuata amani inakokuelekeza kumbuka amani ni mwamuzi na mlinzi. Sasa siku zote mlinzi huwa hampeleki bwana wake kwenye hatari na hii ina maana amani itakuongoza kufanya uamuzi ambao ni bora na ulio katika mpango wa Mungu.

Uzuri wa amani ya Kristo ni huu inakuonyesha uamuzi ambao ni wa hatari/mbaya kwako na pia inakuonyesha na kukuongoza katika uamuzi ambao ni mzuri kwako. Inakuonyesha kwamba huo uamuzi ni mbaya kwa kukosesha raha, furaha na uhuru juu ya uamuzi unaotaka kuufanya. Na pia inakuonyesha kwamba huo ni uamuzi bora kwa kukupa raha na furaha na uhuru juu ya huo uamuzi.Kwa kifupi niseme unapoomba maombi ya namna hii halafu ukakosa amani ndani ya moyo wako jua kwamba huo uamuzi huenda ni wazo la shetani au huenda ni la Mungu lakini, huo sio muda muafaka wa kutekeleza hilo wazo japo hili linategemeana na aina ya hitaji ulilonalo.

Hivyo ukikosa amani usitekeleze hayo mawazo yanayokujia kama jibu, endelea kuomba na kama hali hiyo ikiendelea basi usifanye huo uamuzi maana mlinzi hayuko na wewe. Sasa kama ni la Mungu lakini muda wake bado, Mungu ni waminifu atakujulisha na kukufunilia hilo pia.

Lakini unapoomba ukiiona amani katika mawazo yanayokuja kama majibu jua kabisa hilo ni wazo la Mungu na ndani yake limebeba mpango na njia za Mungu za jibu la ombi lako. Lakini pia pima kwanza hayo mawazo kwa njia ya neno la Mungu uone kama viko sawa maana Shetani hujigeuza ajifanye malaika wa Nuru. Hata siku moja shetani hawezi kukuletea wazo ambalo linaendana na neon la Mungu.

Soma huu mstari utaelewa ninchosema zaidi Zaburi 34:14 ‘Uache mabaya ukatende mema, utafute amani ukaifate’.Maana yake achana na maamuzi mabaya tulia sikiliza amani iankuongoza wpi na kisha ifuate maana yeye ndiye mlinzi wa moyo wako.
Ni imani yangu kwamba ujumbe huu utakusaidia kujibu mawali mengi uliyokuwa nayo mbele za Mungu.

Amani ya Kristo na iwe pamoja nawe.

Advertisements

5 comments

 1. nifanyeje ninapokosa amani mara kwa mara? na ni njia ipi iliyosahihi kwa mkristo kujua kama maombi yake yamejibiwa au bado?

  Like

  • Hello ndg. Kibiki

   Swali lako ni pana sana, kwani kukosa amani huweza kusababishwa na mambo mengi na kila sababu ina namna yake ya kushughulika nayo. Kama kukosa kwako amani kunatokana na sababu ya wewe kutenda dhambi dawa ni kutubu na kutengeneza vinginevyo hutakuwa na amni kama Roho wa YESU YU HAI NDANI YAKO.

   Na kama si dhambi basi dawa yake ni wewe kulisoma na kulitafakari neno la Bwana kwa wingi ili umjue Mungu, maana kataika Zaburi 119:165 imeandikwa ‘Wana amani nyingi walishikao neno la Bwana wala hapana la kuwakwaza’ na pia Ayubu anasema mjue sana Mungu ili uwe na amani. Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu, siku zote maadam unalo kwa wingi ndani yako litakupa uamuzi sahihi katika kila mazingira unayokutana nayo.

   Ubarikiwe, naamini nimejitahidi kujibu lakini kama unafikiri utahitaji msaada zaidi basi tuwasiliane kwa email yangu.

   Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s