NINI MATARAJIO YA MUNGU KWAKO 2008?

Waraka wa Januari.

 Na:Patrick Samson Sanga

Mpenzi msomaji wangu, nakusalimu katika Jina la Bwana na kukutakia heri ya mwaka mpya .Katika waraka wa mwezi huu wa kwanza ninataka kukufikirisha juu ya Je nini matarajio ya Mungu kwako kwa mwaka 2008?. Sijui kama umeshajiuliza na kujijibu swali hili vizuri. Najua yapo mambo mengi ambayo Mungu anatarajia kutoka kwako katika mwaka huu. Lakini lengo langu ni kukupa changamoto juu ya kuukomboa wakati kama tarajio la Mungu kutoka kwako kwa mwaka huu 2008 .

Nianze kwa kusema Sehemu kubwa ya watu wameshaorodhesha orodha ya vitu vingi sana ambavyo wanatarajia Mungu awafanyie kwa mwaka huu. Nami natamani  ujifunze kuyatazama mambo kwa mtazamo wa Ki-Mungu, unapoweka matarajio kutoka kwa Mungu, jua na yeye ana matarajio yake kwako.

Hivyo kabla hujaandaa au kuurodhesha unayotaka akufanyie, jifunze kufikirii na kumuuliza akuelekeze ni vitu gani anatarajia kutoka kwako kihuduma, kimasomo, kikazi, kama kanisa, kama wanandoa, kama familia, kibiashara na kisha uweke malengo ya kutekeleza hayo kwanza .

Biblia inasema katika Wefeso 5:15-16 ‘Basi angalieni sana jinsi mnavyoonenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.’ Na pia ukisoma katika Mhubiri 3:1 ‘Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu’ Hii ina maana

*Mungu ameyafunga mambo kwenye majira.
*Mungu ameyaweka makusudi yake katika wakati.
* Na hii ina maana Mungu ameifunga mipango yake katika muda .
*Hivyo basi lolote analotaka kulifanya amelipangia muda maalumu wa hilo jambo kutekelezwa.
*Na kwa hiyo lolote analolifanya analifanya kwa kuongozwa na kuzingatia muda uliopo.

*Na kama anaongozwa na muda hii ina maana kwa Mungu muda ni wa muhimu sana .

Mtume Paulo kwa kujua haya yote, ndiyo maana akawaambia kanisa la Efeso waangalie sana jinsi wanvyoenenda, kwa maana zamani hizi ni za uovu. Je, ni kitu gani Mungu anataka ujifunze au anakizungumza kwako ?;

*Moja, anataka ujifunze kuutumia muda vizuri.

*Pili, lolote analokuagiza kulitekeleza ujue limewekwa kwenye muda, hivyo ni lazima likamilike kwa huo muda.

*Tatu, anataka utumie vizuri muda ili kuboresha mahusiano kati yako na yeye, maana Mungu huwapenda watu wanaojali muda.

*Nne, Shetani naye anatumia muda uliopo kufanikisha mipango yake. Na kwa sababu hiyo atakutengenezea mazingira ya kukuibia muda ili mipango ya Mungu kupitia wewe isitekelezwe kwa muda.

*Tano, kwa kila muda/dakika kuna ajenda inatakiwa kutekelzwa, huenda ni ya Mungu au ya shetani.

*Sita, kwa hiyo kwa muda huo ukishindwa kutekeleza agizo/ajenda ya Mungu jua kabisa umetoa fursa ya ajenda ya Shetani kutekelezwa

*Saba, uchukulie/utazame muda kama uhai wa mtu na hivyo usipoukomboa/usipoutumia vizuri maana yake huyo mtu atakufa.

Siku moja nilipokuwa chuoni naomba ilikuwa yapata  saa moja jioni, naliona katika maono ya wazi mkono wa kushoto umevaa saa inyong’aa sana na niliona mishale yake inakimbia kwa spidi ya ajabu. Nilipo uliza Mungu maana yake nini, akaniambia ‘ Muda uliobaki ni kidogo sana, Jifunze kuutumia vizuri, muda uliopita, umepita hauwezi kujirudia, Kwa hiyo usipofanya ulichotakiwa kufanya kwa muda huo maana yake umeupoteza muda huo’.

Huenda mfano huu utakufanya uelewe zaidi , fikiria watu wamepanda basi na ndani ya hilo basi kuna bomu limetegwa na litalipuka baada ya dakika kumi na tano (15) kutoka sasa. Mwenye ujuzi wa kulitegua hilo bomu ni wewe, na Mungu anakuagiza uende kulitegua ili kuzuia maafa kwa sababu hafurahii kifo cha mwenye dhambi.

Na kwa mazingira yaliyopo unaweza kulitegua hilo bomu ndani ya dakika tano tu na basi hilo lipo jirani na wewe.Sasa badala ya kuutumia muda vema, wewe unaingiza ratiba za kwako ambazo kimsingi ni halali lakini si zote zifaazo. Mpaka Mungu akakupa agizo ina maana kwa muda huo ajenda ya muhimu ni ya kwake.

Ushuda wangu binafsi juu ya muda;

Uandishi na kufundisha ni sehemu ya vipawa ambavyo Mungu amenipa.Zaidi amenijalia kuwa  na blog/ tovuti mbili moja kwa lugha ya kiingereza ya kiingereza na nyingine kwa Kiswahili. Haya masomo unayoyasoma ukweli yananigharimu muda mwingi sana kuliko kawaida, ninapoandaa napiga picha kwenye ufahamu wangu kwamba hili somo kuna kijana, mama, baba, Mchungaji au mtu yoyote mahali fulani ambaye yamkini amekata tamaa au amekwama na nafsi imeinama anchohitaji ni somo hili ili avuke hapo , vinginevyo anaweza akapotea kabisa.

Hichi ni kitu ambacho Mungu ameniwekea ndani yangu. Ni kama mtu huwa ananiambia fanya haraka kuna mtu/watu mahali fulani wanasubiri hilo somo likamilike, usipoteze muda vinginevyo watanikosea.

Siku moja nilikuwa kwenye daladala mkoa fulani, nikasikia ndani kuwaambia wadada fulani wawili ndani ya hiyo daladala habari za Yesu. Kwa kuogopa watu na mazingira nilinyamza mpaka niliposhuka. Wakati nimelala nikaletewa picha ya vijana wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Yule wa kiume alikuwa akimshawishi yule wa kike wafanye uasherati na nami nilikuwa nawasikia vizuri.
Kisha nikasikia sauti ikiniuliza, Patrick unafurahia dhambi? Uko tayari huyu binti afe katika dhambi, kwa nini hukuwaambia wale wadada habari zangu?, Je unajua kitu gani kilikuwa kinaenda kuwatokea? . Nilishindwa cha kujibu nilibaki kulia na kutubu.

Hii ina maana gani? Ningeweza kusema nitawahubiri siku nyingine au watahubiriwa na watu wengine au kwenye mkutano wowote watahubiriwa.

Lakini ukweli ni huu, wale wadada walikuwa wanatakiwa kuhubiriwa injili kwa muda ule tena tukiwa ndani ya basi kabla mimi sijashuka na wao hawajashuka na  siyo kesho au baada ya saa moja.

Mpaka leo sijui nini kilwatokea wale wadada lakini jambo hili ilikuwa ni fundisho kwangu na sasa nimejifunza kuutazama muda kama uhai, nisipoukomboa na kuutumia vizuri nitaupoteza. Ndiyo maana nimeona ni vema nikushirikishe na wewe, usiseme nangoja Mungu anifundishe, jifunze kutoka kwangu pia itakusaidia .

Wewe pia ni shahidi wa matumizi ya muda wako. Mara ngapi Mungu anakuagiza ufunge, utoe, ukeshe, usome neno au uende ibadani, uende kumuombea mtu fulani, au uende kuhubiri eneo au kwa mtu fulani, au ugharamie huduma fulani nk,  lakini wewe unasema nitafanya siku nyingine au watafanya wengine .

Mungu anajua kuna hiyo siku nyingine na pia kuna hao watu wengine ambao nao amewapa maagizo yao. Hivyo alichokagiza leo ni lazima kifanyike leo na sio kesho, ni mfano wa mtu mwenye kutegua bomu kwenye basi, akisema ataenda baada ya dakika 20 litakuwa limeshalipuka na wote wamekufa .

Jifunze kufanya vitu kwa muda, lolote analokuagiza Mungu, kufanya lione kwamba ni mfano wa watu kwenye basi/ kwa maana ya uhai wao na kwamba usipolifanya kwa wakati wake basi kuna roho zitakzopotea.

Nakuambia ukijifunza kuyachukulia maagizo ya Mungu kwa nidhamu hii ndipo utakapoona akizungumza vitu vingi na wewe maana anajua unanidhamu ya kutumia muda vizuri.

Mpenzi msomaji sina lugha ya kukusisitiza katika hili, kwa sehemu naamini Mungu amesema na wewe juu ya muda na utaanza kuujali muda .

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe nawe.

Advertisements

One comment

  1. sasa hapa umeniokoa ndugu mtumishi mimi nilikuwa saa zote ninasoma bibilia kwa ajili ya hofu kumbe shetani alikuwa ananibana ili nisijue kifaransa maana nitawahubiria wazungu,naishi suiss lakini siku moja mungu akaniambia kuwa wewe unatakiwa kusoma hiyo lugha kwa bidii mpaka mwezi wa 7 mwaka huu 08 nianze kuongea mtumishi nimepangiwa na muda katika ndoto maana niliota,kutokana na somo hili nimefunuliwa mambo mengi sana,asante sana kwa mahubiri mazuri ,

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s