KUSANYA NGUVU ZAKO.

Kusanya nguvu.

Ujumbe wa 2008. 

Na: Patrick Samson Sanga .

Heri ya mwaka mpya mpenzi msomaji wangu, ni furaha iliyoje Mungu kutupa fursa nyingine tena kwa mwaka huu wa 2008, ambao mimi nauhesabu kuwa ni ni mwaka wa kutengeneza mahali palipomoka, kupajenga mahali pa ukiwa na mwaka wa kurejesha vyote alivovinyang’anya shetani.

Namshukuru Mungu kwa kuwa ametulinda na kutupa neema ya kuingia 2008. Tunapoingia 2008, Mungu anakupa ujumbe/taarifa hii, ni jukumu lako kuifanyia kazi 1Wafalme 20:22 inasema “Akamwambia kusanya nguvu zako, ujue na kuangalia ufanyavyo , kwa maana mwakani mfalme wa shamu atakuja juu yako’.

Hii ni habari ya mfalme Ahabu wa Israeli. Ben-hadadi mfalme wa Shamu alikuwa amepigana na Ahabu na matokeo yake Ahabu na Israeli wote wakashinda vita ile. Lakini safari hii Ben- hadadi hakufa aliweza kukimbia na baadhi ya watu wake .

Sasa huenda baada ya ushindi huo Ahabu alijisahau akafikiri vita imekwisha, lakini Mungu kwa kujua yaliyoko mbele na mipango aliyonayo mfalme wa Shamu ndipo akatuma nabii kumwambia kusanya nguvu zako, ujue na kuangalia ufanyavyo, kwa maana mwakani mfalme wa shamu atakuja juu yako .

Nabii alimtaka Ahabu akusanye nguvu, ila wakati anakusanya nguvu;

(a) Basi akusanye huku akijua kuwa mwakani kuna vita inamkabili.

(b) Pili aangalie namna anavyokusanya hizo nguvu

(c) Tatu nabii alimpa Ahabu muda ambao vita itakwakutokea, japo hakuwa haukuwa wazi sana kwa sababu hakumtajia mwezi wala siku.
Hebu tufikiri kwa pamoja juu ya haya yafuatayo;
*Kwa nini nabii alimtaka Ahabu ajue kwamba mwakani kuna vita?
*Kwa nini pia alimtajia na muda wa vita?
*Kwa nini pia alimtaka aangalie namna ananvyo kusanya nguvu zake?.

Yamkini yapo majibu mengi, lakini zifuatazo na sbabu chache za msingi kwa haya maswali;

* Moja ni kumpa taarifa, ili azitumie  kufanya maamuzi . *Ajiandae kukabiliana na vita
* Alipewa muda ili autumie kimaandalizi.
* Pia alimtaka aangalie namna anavyo kusanya nguvu ili akusanye nguvu za kutosheleza  kuikabili vita mbele yake kwa kutumia mikakati bora na inayotakiwa kwa kuzingatia muda ni mfupi sana.

Hii ina maana gani kwetu leo hii?


Ni kweli umevuka mwaka 2007 salama, unapaswa kumshukuru Mungu kwa jambo hili. Ninachotaka kukuambia usidhanie vita imekwisha, Shetani naye anajua kwamba mwaka jana hakuweza kukushinda, hivyo amepajipanga kwa upya mwaka huu kuhakikisha ankuangamiza kiuchumi, kiroho, kihuduma, kibiashara, kindoa , kifamili, kimasomo, kikazi nk.

Nami nakutaarrifu kwa jina la Bwana kwamba kusanya nguvu za kutosha za kiroho huku ukiwa makini na mikakati (strategies) unazotumia kukusanya hizo nguvu kwa sababu mwaka huu shetani amepanga kukujia tena.

Mwombe Mungu akupe mikakati mipya ya kumshinda shetani, usitegemee mikakati ya mwaka jana kwa kuwa mwaka huu shetani naye amebadilisha mikakati (strategies) yake ya kukumaliza .

Kumbuka Mwivi haji ila kwa lengo la kuiba na kuchinja na kuharibu, usiweke silaha chini mpaka ushindi utakapopatikana, muda wote kaa mkao wa vita maana wewe ni askari wa Kristo. Kumbuka tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu.

Mungu wangu akubariki, nakutakia mwaka wa mafanikio.

Advertisements

2 comments

  1. Nashukuru kwa mafundisho yako ,naomba sana tu neema ya mungu inisaindie kufanyia kazi mafundusho . kama nitapata mafundisho mengine kwa njia ya mail nitashukuru .Mungu akubariki.

    Like

  2. Ndugu yangu ama kweli haya mahubiri yamenigusa. Bwana asifiwe sana mtumishi wa kirsto umenipa picha ya vita niliokuwa nao mwaka elfu 2006 kumbe mimi natakiwa kukaa sawa sio kuwa imekwisha.ooo!yesu asante sana umenifungua macho kwa hili somo barikiwa mtumishi na Bwana.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s