MAMBO YA KUJUA MUNGU ANAPOKUITA UMTUMIKIE.

Waraka wa Februari.

Na;Patrick Samson Sanga.

Mpenzi msomaji wangu, ninajua unajua kwamba umeumbwa kwa kusudi fulani hapa duniani, haukuubwa kwa bahati mbaya, siku zote Mungu, hufanya kazi pamoja na wale wampendao ndio wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:27 Sasa kusudi la Mungu kwa kila mmoja linatofautiana. Huyu ameitwa hivi na yule kaitwa vile. Everyone is unique” ie. Every cailing is unique in nature.

Lengo la waraka huu mfupi kwa mwezi huu wa pili ni kukueleza mambo unayotakiwa kujua Mungu anapokuita umtumikie katika huduma yoyote ile katika huduma kuu tano yaani utume, unabii, uinjilisti, uchungaji na ualimu. Au kwa lungha nyingine haya ni mambo ambayo lazima Mungu atakuagiza na kukutaka uyafanyie kazi ili uweze kutumikia kwa kusudi.

Jambo la kwanza.Atakufundisha ahadi zake.
Mungu atahakikisha anakujulisha ahadi zake zote zinazohusiana na wito aliokuitia, na hataishia hapo bali atakufundisha kuishi kwa Imani yaani uziamani ahadi alizokupa. Isaya 54:17b.

Jambo la pili; Nidhamu kwa Roho mtakatifu.
 Wito ambao Mungu anakuitia hauwezi kuutekeleza bila kuwa na nidhamu kwa Roho mtakatifu. Mungu atakupa Roho mtakatifu msaidizi wako katika huduma uliyopewa. Kufanikiwa kwako katika huduma kunategemea kiwango chako cha nidhamu kwa Roho mtakatifu maana ni lazima ujifunze kutii kila ambacho Roho mtakatifu, anakuambia.

Jambo la tatu.Kujifunza kushirikiana na upako ambao Mungu anakupa.
Sikiliza, hiyo huduma au huo wito hauwezi kuufanya bila nguvu za Mungu. Hivyo Roho mtakatifu atakupa uwezo, nguvu za Mungu za kuutekeleza huo wajibu. Kuna upako unaokuja maalumu kwa kusudi fulani na ule uliobeba wito kwa ujumla unachotakiwa ni kushirikiana vema na huo upako ili kusudi litimie.

Jambo la nne. Atakufundisha ukuu wake jinsi ulivyo.
uweze kumtumikia Mungu katika wito aliokuitia, lazima ujue atakujengea wazo hili katika ufahamu wako, kwamba kwako yeye ni Bwana na kama yeye ni Bwana maana yake, wewe ni mtumwa, siku zote upo chini yake, ana sauti juu yako na hivyo lazima uwe tayari kutumika kadri atakavyo na siyo utakavyo. Ukisoma vizuri Biblia kila Mungu alipotaka kusema na watu wake, manabii na mitume alianza kwa kusema mimi ni Bwana Mungu wako.., Ili wajue Bwana mkubwa ndiye anayezungumza, bila yeye hatuwezi jambo lolote.

Naamini sehemu hii ndogo kuhusu wito itakusaidia na kukupanua kimawazo zaidi ili Mungu akikiuita Kwenye wito au huduma fulani uelewe nini mipaka yako kwake.

Neema ya kristo na iwe nawe.

Advertisements

2 comments

  1. thxs but viashilia vya kujua wito wako yaani nifanye nn je unaweza kufunga novena ili nijue wito wangu au niganye nn maan hapa Niko njia panda

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s