JE, MAAMUZI YA NANI ATAKUWA MWENZI WAKO WA MAISHA NI YA MUNGU AU YA KWAKO?

 Na: Patrick Samson Sanga.

 Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana”.

Ni matumaini yangu kwamba u-mzima kijana mwenzangu na una maendeleo mazuri kiroho na kimwili. Katika waraka huu mfupi kwa vijana nataka kujibu swali hili ambalo vijana wengi wamekuwa wakijiuliza. Wengine kutokana na kutojua ukweli wake wamejikuta wakifanya maamuzi ambayo hadi leo wanayajutia .

Kibiblia, tunajua kabisa ni mpango wa Mungu tuweze kuoa au kuolewa. Sasa swali linakuja, je ni lazima Mungu anionyeshe, anipe mke au mume wa maisha yangu? Kwani mimi kijana sina uwezo wa kuangalia mtu kisha nikaomba Mungu na mwisho nikajichagulia mwenyewe? Au kifupi maamuzi ya nani atakua mume/mke wangu ni ya nani?

Hili ni swali ambalo vijana wengi limekuwa likiwachanganya. Wengine wanaamini maamuzi hayo ni ya Mungu kunipa mke/mume na wengine wanaamini Mungu hahusiki, bali wao ndio wenye nafasi na wanaohusika. Sasa hayo ni mawazo yao wala mimi sitaki kuyapinga lakini ngoja nikuonyeshe Biblia inasema nini halafu utajua ukweli ni upi:-

Kwenye kitabu cha Mithali 19:14 , Mungu anasema suala la nyumba, mashamba, maduka na vyote vifafanavyo na hivi nimewapa uwezo na ruhusa wazazi wako baba & mama) wa mwili wakupe lakini suala la mke au mume mwenye busara mimi pekee ndiye ninaye wajibika kukupa .Sikiliza kama unataka mke/mume kwa ajili ya kulitumikia kusudi la Mungu alilokuumbia basi huna budi ni lazima upige goti kuomba na kisha ungoje Mungu akuonyeshe/ akupe mke/mume wa kusudi lake.

Vijana wengi wanafikiri eti kwa sababu wameokoka, na wamejzwa roho mtakatifu basi wanao – uwezo wa kujichagulia mke/mume wa kuishi nao. Sikiliza kama una amini umeumbwa kwa kusudi la Mungu na unataka kutembea katika njia yake basi mruhusu Mungu akupe mke/mume mwenye busara ya kukaa na wewe.

Mke au mume ana sehemu kubwa katika maisha yako. Anaweza akabadilisha maisha yako, ya kiroho, kiuchumi, kimwili, kihuduma na kima husiano na watu wengine.Hivyo kibiblia maamuzi ya nani atakuwa mkeo au mumeo ni ya Mungu na si ya kwako. Hii ina maana ukimuomba Mungu hakika atakuletea mtu halisi wa kukaa na wewe. Lakini maamuzi ya kumkubali au kumkataa ni ya kwako na si ya Mungu. Ukikubali shauri la Bwana litatumikiwa, ukimkataa, umejikaribishia laana.

Zifuatazo ni sababu za msingi zinazomfanya Mungu akuchagulie/akupe mke/mume na sio kukuruhusu wewe/wazazi/ukoo wako/mchungaji wako kukuchagulia mke.

(a)Kusudi la uumbaji (kuwaunganisha) .
Sikiliza hakuna mtu aliyeumbwa kwa bahati mbaya, Mungu ndiyo aliyekuchagua na siyo wewe uliyemchagua na akakuweka duniani ili umtumikie sasa yeye ndiye anayejua nikimuunganisha huyu kaka na yule dada watalitumikia kusudi langu.  Warumi 8:28-29.  Mungu anapofanya maamuzi anafanya kwa kuangalia kusudi lake na muda na wahusika wa hilo kusudi. Yeye ni Mungu na anafanya kwa utikufu jifunze kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie na si ya kwako.

(b) Mungu ndiye ana-fahamu nani mwenye busara ya kukaa na wewe.
Mithali 19:14b Busara ni uwezo uliomo ndani ya mtu (mke/mume) unaomsaidia kujizuia kufanya jambo ambalo liko nje ya mpango/mapenzi ya Mungu kwa kufanya lile lilio katika mapenzi ya Mungu.Hivyo Mungu pekee ndiye anaye mjua mke/mume mwenye busara ya kukaa na wewe, kamwe wewe hutaweza mjua bila uongozi wa Mungu.

(c) Sababu za ki-Agano.
Zaburi: 32:8 Siku uliyofanya maamuzi ya kuokoka maana yake uliyakabidhi maisha yako kwa Yesu, ukamwambia nafungua moyo wangu uingie uyatawale na kuyaongoza maisha yangu sasa hilo ni Agano lako kwa Mungu. Kwa sababu hiyo Yesu anawajibika kwako kukufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, hii ikiwa ni pamoja na kukupa mke/mume wa kukufaa.

(d)Mawazo yake, si mawazo yako.
Isaya 55:8 Sikiliza Mungu anayo mawazo (mipango) na njia (mikakati) ya kukufanikisha kimaisha. Sasa katika kutekeleza mipango yake kwako na kupitia wewe lazima atumie mikakati yake ili kutekeleza mawazo yake. Sasa moja ya mikakati yake ni kukupa mke au mume wa kusudi lake .
Sasa, sikatai huenda kwa jinsi ya mwili ni kweli huyo mtu anayekupa Mungu ana upungufu fulani. Huenda umbile lake, sura yake, kabila lake, rangi yake, dhehebu lake, haliko
 kama ulivyo kuwa unavyotaka wewe. Mungu anakupa mke au mume kutokana na sababu hizo ambazo nimekuekezea hapo juu na ninakuhakikishia ukimkubali atakupa neema ya kukaa naye huyo mtu na kukufanya uridhike naye na kumpenda huyo mwenzako .

Nakutakia uongozi wa Mungu katika eneo la maamuzi ya nani atakua mumeo au mkeo .

Advertisements

14 comments

 1. I thank God 4u & 4ur service, i received this website of urs bt real i was not awear if its you my fellow friend from CBE.
  Ok by the way nipo hapa Ukwata DIT, na nimefurahishwa sana na huduma hii nzito iliyoko ndani yako,zaidi sana kwa habari ya mafundisho ya VIJANA na hata kwa mwongozo mzima wa somo kuhusu ROHO MTKTF.
  4SURE BROTHER “MUNGU AKUBARIKI SANA”.

  Like

 2. mtumishi nimekuwa miongoni mwa watu wenye bahati kuiona tovuti yako maana mimi kama kijana nilie na changamoto nyingi itanisaidia sana kuenenda katika kusudi la Mungu.
  nimejaribu kwenda kwenye kipengele cha maswali na majibu ili niweze kuuliza swali langu ila nikakuta sehemu hio haina mahali napoweza kuuliza swali na kulituma.
  sasa ni hivi,mimi ni kijana wa umri wa kuoa sasa,wakati nasoma shule ya sekondari niliwahi kumwomba Mungu na nikamtajia jina la msichana niliemwomba aniruhusu aje kuwa wangu wa maisha,basi baada ya hapo maisha yameendelea wakati mimi sina hata uhusiano wa karibu na msichana husika,mwanzoni mwa mwaka huu huyo msichana alianza from no where kuwasiliana na mimi kupitia simu,tumeendelea baadae akaniambia………nahisi utanifaa sana kama mume wangu maishani!
  kuanzia hapo tumekuwa wapenzi kama ujuavyo ujana.
  sasa swali langu ni kutaka kujua kama ni Mungu amenijibu au ni hisia zake zimemtuma kwangu kwa namna ya kibinadamu? naomba mtumishi unijibu pamoja na wengine waliopo kwenye ndoa ambao walimwomba Mungu awapatie wenzi na wakapata,MAJIBU HUWA YANAKUJA KTK STYLE GANI HASA? kwa wengine nitaomba wanijibu kupitia email yangu jimlaki34@yahoo.com AU (+254 714 359 077) ,amani ya bwana na itawale mioyo yenu AMINA

  Like

 3. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI WA MUNGU SANGA.
  AWALI YA YOTE NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YENU KWA HUDUMA MNAYOITOA AMBAYO IMEKUWA MSAADA KATIKA MAISHA YANGU KAMA MKRISTO NA KAMA MWANAJAMII.MUNGU AWABARIKI SANA.
  PILI NAOMBA MSAADA WA MAARIFA JUU YA NAMNA YA KUMTAMBUA MKE AMBAYE MUNGU AMENIANDALIA.NIMEFANYA MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU MKE MWEMA TANGU SEPTEMBA 2008 HADI SASA LAKINI BADO SIJAPOKEA MAJIBU YA MAOMBI YANGU.NINAAMINI NINASUMBULIWA NA TATIZO LA UPOKEAJI WA MAJIBU YA MAOMBI YANGU JAMBO AMBALO LINAHATARISHA USTAWI WANGU KIROHO.NAOMBA KWA MANUFAA YA WENGINE PIA AMBAO WANA TATIZO KAMA LANGU UTUPATIE MAJIBU HAYO KWENYE KIPENGELE CHA MASWALI NA MAJIBU.NINAOMBA PIA KWA AJILI YANGU NA WENGINE AMBAO NINAWEZA KUWAFIKIA UNISAIDIE MAJIBU HAYO KUPITIA EMAIL ADDRESS YANGU HAPO JUU.
  ASANTE SANA NA MUNGU AWATIMIZIENI HAJA ZA MIOYO YENU NA KUIMARISHA HUDUMA YENU ILI WATU WENGI ZAIDI WAIMARIKE KIROHO.

  Like

  • Mimi ninakutia moyo wa bidii ya kuendelea kuomba,tia bidii na mkumbushe Mungu ahadi zake kupitia neno lake atakujibu tu, wakati wako utafika na utapokea majibu yako…Miujiza mingi inatendeka katika kuomba kwa bidii.

   Like

 4. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI WA MUNGU SANGA.
  AWALI YA YOTE NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YENU KWA HUDUMA MNAYOITOA AMBAYO IMEKUWA MSAADA KATIKA MAISHA YANGU KAMA MKRISTO NA KAMA MWANAJAMII.MUNGU AWABARIKI SANA.
  PILI NAOMBA MSAADA WA MAARIFA JUU YA NAMNA YA KUMTAMBUA MKE AMBAYE MUNGU AMENIANDALIA.NIMEFANYA MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU MKE MWEMA TANGU SEPTEMBA 2008 HADI SASA LAKINI BADO SIJAPOKEA MAJIBU YA MAOMBI YANGU.NINAAMINI NINASUMBULIWA NA TATIZO LA UPOKEAJI WA MAJIBU YA MAOMBI YANGU JAMBO AMBALO LINAHATARISHA USTAWI WANGU KIROHO.NAOMBA KWA MANUFAA YA WENGINE PIA AMBAO WANA TATIZO KAMA LANGU UTUPATIE MAJIBU HAYO KWENYE KIPENGELE CHA MASWALI NA MAJIBU.NINAOMBA PIA KWA AJILI YANGU NA WENGINE AMBAO NINAWEZA KUWAFIKIA UNISAIDIE MAJIBU HAYO KUPITIA EMAIL ADDRESS YANGU HAPO JUU
  lucas.maro@yahoo.com
  ASANTE SANA NA MUNGU AWATIMIZIENI HAJA ZA MIOYO YENU NA KUIMARISHA HUDUMA YENU ILI WATU WENGI ZAIDI WAIMARIKE KIROHO.

  Like

 5. God is gud all the tym and i believe that!Ithank God for sababu amewachagua ninyi kwa makusudi ya kumtumikia yeye,nimekuwa nikimuomba Mungu for so long to provide me a capable husband,nimefunga na kuomba sana about that,i cant blame God coz he knows why it is like that,on ma side nahisi labda nakosea kuomba,kiasi kwamba imeniathiri hata kihuduma kanisan!it gives ma mind to be upset!stay blecd!

  Like

  • Amen, as you have said indeed God is good all the time, never be upset because he has good plan for you. Smith in his book says just hold on to your faith, because at the moment you think God doesn’t make sense he really makes sense. Currently I’m preparing another module on relationship, once I’m done with it I will send it you, I know it will be of great help.

   Like

 6. Naamini ni Mungu tu aliyenisaidia kuijua website hii sina namna ya kusema Mungu atukuzwe pekee ,sifa na heshima ni za Mungu ,Mungu asante kwa kuumba watu wanaoweza kusimama kwenye kusudi lako kama Patrick mpe wingi wa siku na maisha ya ushindi daima.Amen

  Like

 7. thanks man of God for the way you are using by God for healing many marriegies,is true your teachings are giong to make great revolution to the church, May God use you as well as needed

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s