KWA NINI UNATAKIWA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU USIKU NA MCHANA?

 

Vjana wakijadiliana. 

  Na; Patrck samson Sanga.

Yoshua 1:8 “kitabu hiki cha Torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo……..)

Hapa tunaona jinsi Mungu alivyomtisitiza Joshua kwa habari ya kulitafakari neno la Mungu usiku na mchana .

Lengo la waraka huu mfupi kwako mpendwa msomaji ni kukueleza sababu za msingi kwa nini ni lazima na sio ombi kwamba usome na kulitafakari Neno la Mungu usiku na mchana.Kabla sijakueleza sababu nikupe tafasiri ya Neno la Mungu kwa ufupi, neno la Mungu ni jumla ya mawazo ya Mungu juu ya mwanadamu.

Ndani ya Neno kuna maamuzi (hukumu), sheria, maagizo na njia za Mungu za kumtoa mwanadamu katika shida aliyonayo, kumfanikisha katika mambo yote na kumsaidia, kuishi kwa kulishika shauri (kusudi) la Bwana.

Sababu hizo ni ;

(a) uweze kuelewa nini mawazo ya Mungu juu yako .
Katika kitabu cha Yeremia 29:11 Mungu anasema nayajua mawazo ninayokuwazi si mawazo mabaya ………, sasa ili uweze kuelewa Mungu anakuwazia nini ni lazima usome kwa kulitafakari neno lake ili upate anachokueleza kuhusu maisha yako, huduma, kazi, biashara nk.

(b) upate kuifanikisha njia yako.
Yoshua 1:8b. Mungu anasema nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea ………….( Zaburi 32:8), kumbuka kila mmoja ana njia yake ya kupita ili kilitumikia shauri la Bwana. Sasa ili uweze kufanikiwa katika njia yako ni lazima usome na kulitafakari Neno la Mungu maana ni taa ya miguu yako. Zaburi 119:105.

(c) usimtende Mungu dhambi .
Zaburi 119:11. mwimbaji wa zaburi anasema, moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisikutende dhambi. Neno linawekwa moyoni kwa kulitafakari. Kadri unavyolitafakari kimapana ndivyo linavyokusaidia na kukulinda na dhambi. Litakuonyesha hila na mitego ya dhambi ya shetani, na litakupa ushindi kwa kila ushawishi wa adui.

(d)Ili uongezeke kiimani.
 warumi 10:17. Ikiwa chanzo cha Imani ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la kristo, maana yake kadri unavyolisoma na kulitafakari Neno la kristo mara kwa mara, kisha ukajitamkia mwenyewe ili ulisikie hii ina maana lazima imani yako itaongezeka tu.

(e)Neno limebeba jibu la mahitaji yako.
 Zaburi 107:20. kwa kuwa ndani ya neno kuna mawazo na njia (mikakati) ya kukufanikisha kimaisha, hii ina maana, unapolitafakari licha ya kuelewa mipango ya Mungu juu yako, pia utaelewa na njia za Mungu za kukuondoa katika shida uliyo nayo kiroho, kimwili, kindoa , kibiashara nk.

(f)uweze kustawi sana .
Yoshua 1:8b, Biblia inapozungumzia kustawi ina maana ya kutawala na kumiliki vema, kimapana yale ambayo Mungu ameyaweka chini yako .Mtu ambaye ndani yake amejaa Neno la Mungu kwa wingi huyo ana uwezo mkubwa sana wa kutawala na kuongoza watu pia.

(g)Litakupa miaka mingi duniani . Mithali 3:1. Ukilitafakari Neno la Mungu katika maisha yako.Neno litakupa miaka mingi ya amani (mafanikio) hapa duniani na kila ulifanyalo litafanikiwa.

(h)uwafundishe wengine kumjua Mungu.
 kumbukumbu 6:1-10. Mungu anataka watu wamjue yeye, kwa hiyo pindi unapotafakari anajifunua kwako, akajifunua kwako anataka uwaambie na wengine jinsi alivyo na ukuu wake ili wasimsahau yeye

Naamini baada ya kuwa umejua umuhimu wa kusoma na kutafakari Neno la Mungu usiku na mchana, utaamua kuanza pia kulisoma na kulitafakari usiku na mchana.

50 comments

  1. Shukrani nyingi zikufikie mtumishi kwa kazi kubwa ya Mungu unayoifanya,
    Mungu akubariki sana.
    usichoke kutuombea.
    Kazi njema na wakati mwema.Tumsifu Yesu Kristo.

    Like

  2. Kweli Mungu anapolituma neno huwa halirudi bure,nimebarikiwa na umenigusa sana ubarikiwe mtumishi na Mungu azidi kukutumia asante.

    Like

  3. Nimebalikiwa sana mawazo yangu naona Yesu ni neno mfano amri usiibe au usiseme uongo ukiweza kuzishika amri hizo na kuzitenda hizo hapo tunasema Yesu au neno limekaa ndani yako kwa hiyo Yesu ni hali nzuri na siyo object tusifikiri yesu ni kiumbe kinachoweza kukaa ndani yetu ni roho hayo ni mawazo yangu.

    Like

  4. Mungu azidi kukubariki mtumishi wa Mungu unatutia nguvu ya kulisomaneno la mungu mwanzo nilisoma tu bila kutafakari kwa sasa nimepata muongozo kamili wa kujua neno la Mungu.

    Mungu akubariki sana

    Like

  5. Nimependa somo lako. Mungu akubaliki ili uendelee kutangaza neno lake ili wasiofahamu waweze kufunuliwa na kufuata neno lake kwa usahihi, maana watu wengi wanashindwa kutafakari neno la Mungu, wanasubili kutafsiliwa na mtu mwingine hata kama ni cha uongo atafuata kutokana na uwelewa wa aliyemtafsilia

    Like

  6. Mungu akuzidishie hekima,ili nasi tuzidi kuvuna matunda kwako na kuwajuvisha wengine..zab1:1-3.heri mtu yile asiekwenda ktk shauri la wasio haki,wala hakusimama ktk njia ya wakosaji;wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
    Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo
    Na sheria yake huitafakari usiku na mchana
    Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji uzaao matunda yake kwa majira yake;
    Wala jani lake halinyauki na kila alitendalo litafanikwa

    Like

  7. Mungu akubariki sana Patrick kwa mafundusho mazuri. Nimekuwa nikiwashirikisha wanakikundi wenzangu kujifunza masomo haya na yamefanyika baraka sana katika maisha yetu na mwongozo mkubwa katika kulitumikia kusudi la Mungu katika nafasi mbalimbali. Binafsi kiwango changu cha imani kimekua kupitia mafundisho yako. Ninamwomba Roho Mtakatifu aniwezeshe kukuombea wewe na huduma hii bila kukoma. Roho Mtakatifu azidi kukupa mafunuo ili uendelee kulisha na kunywesha roho zetu. Mungu akubariki sana wewe na huduma yako.

    Like

    • Amina dada Martha ahsante sana kwa ushuhuda wako, naam nashukuru sana pia kwa maombi yako maana kwa haikia nayahitaji sana hasa kipindi hiki cha sasa, tuzidi kuombeana na BWANA aendelee kukuza imani zenu na kuwafanya kumjua yeye zaidi na zaidi.

      Like

  8. Mungu wa mbinguni akubariki sana kaka kwa mafundisho mazuri, umeniongezea hatua kubwa sana katika kutumika. Na kwa nafasi hii nilopewa na kupata kibali namwomba Mungu kwa jina la Yesu azidi kuifunua akili yako kuyaelewa maandiko ili uendelee kuwaleta watu katika kusudi la Kristo. Mungu akubariki na kuiponya kila hatua ya huduma yako.

    Like

Leave a reply to ANTHONY GAUDENCE Cancel reply