KWA NINI UNATAKIWA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU USIKU NA MCHANA?

 

Vjana wakijadiliana. 

  Na; Patrck samson Sanga.

Yoshua 1:8 “kitabu hiki cha Torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo……..)

Hapa tunaona jinsi Mungu alivyomtisitiza Joshua kwa habari ya kulitafakari neno la Mungu usiku na mchana .

Lengo la waraka huu mfupi kwako mpendwa msomaji ni kukueleza sababu za msingi kwa nini ni lazima na sio ombi kwamba usome na kulitafakari Neno la Mungu usiku na mchana.Kabla sijakueleza sababu nikupe tafasiri ya Neno la Mungu kwa ufupi, neno la Mungu ni jumla ya mawazo ya Mungu juu ya mwanadamu.

Ndani ya Neno kuna maamuzi (hukumu), sheria, maagizo na njia za Mungu za kumtoa mwanadamu katika shida aliyonayo, kumfanikisha katika mambo yote na kumsaidia, kuishi kwa kulishika shauri (kusudi) la Bwana.

Sababu hizo ni ;

(a) uweze kuelewa nini mawazo ya Mungu juu yako .
Katika kitabu cha Yeremia 29:11 Mungu anasema nayajua mawazo ninayokuwazi si mawazo mabaya ………, sasa ili uweze kuelewa Mungu anakuwazia nini ni lazima usome kwa kulitafakari neno lake ili upate anachokueleza kuhusu maisha yako, huduma, kazi, biashara nk.

(b) upate kuifanikisha njia yako.
Yoshua 1:8b. Mungu anasema nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea ………….( Zaburi 32:8), kumbuka kila mmoja ana njia yake ya kupita ili kilitumikia shauri la Bwana. Sasa ili uweze kufanikiwa katika njia yako ni lazima usome na kulitafakari Neno la Mungu maana ni taa ya miguu yako. Zaburi 119:105.

(c) usimtende Mungu dhambi .
Zaburi 119:11. mwimbaji wa zaburi anasema, moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisikutende dhambi. Neno linawekwa moyoni kwa kulitafakari. Kadri unavyolitafakari kimapana ndivyo linavyokusaidia na kukulinda na dhambi. Litakuonyesha hila na mitego ya dhambi ya shetani, na litakupa ushindi kwa kila ushawishi wa adui.

(d)Ili uongezeke kiimani.
 warumi 10:17. Ikiwa chanzo cha Imani ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la kristo, maana yake kadri unavyolisoma na kulitafakari Neno la kristo mara kwa mara, kisha ukajitamkia mwenyewe ili ulisikie hii ina maana lazima imani yako itaongezeka tu.

(e)Neno limebeba jibu la mahitaji yako.
 Zaburi 107:20. kwa kuwa ndani ya neno kuna mawazo na njia (mikakati) ya kukufanikisha kimaisha, hii ina maana, unapolitafakari licha ya kuelewa mipango ya Mungu juu yako, pia utaelewa na njia za Mungu za kukuondoa katika shida uliyo nayo kiroho, kimwili, kindoa , kibiashara nk.

(f)uweze kustawi sana .
Yoshua 1:8b, Biblia inapozungumzia kustawi ina maana ya kutawala na kumiliki vema, kimapana yale ambayo Mungu ameyaweka chini yako .Mtu ambaye ndani yake amejaa Neno la Mungu kwa wingi huyo ana uwezo mkubwa sana wa kutawala na kuongoza watu pia.

(g)Litakupa miaka mingi duniani . Mithali 3:1. Ukilitafakari Neno la Mungu katika maisha yako.Neno litakupa miaka mingi ya amani (mafanikio) hapa duniani na kila ulifanyalo litafanikiwa.

(h)uwafundishe wengine kumjua Mungu.
 kumbukumbu 6:1-10. Mungu anataka watu wamjue yeye, kwa hiyo pindi unapotafakari anajifunua kwako, akajifunua kwako anataka uwaambie na wengine jinsi alivyo na ukuu wake ili wasimsahau yeye

Naamini baada ya kuwa umejua umuhimu wa kusoma na kutafakari Neno la Mungu usiku na mchana, utaamua kuanza pia kulisoma na kulitafakari usiku na mchana.

Advertisements

50 Comments »

 1. 1
  Bryceson G Mangesho Says:

  Shukrani nyingi zikufikie mtumishi kwa kazi kubwa ya Mungu unayoifanya,
  Mungu akubariki sana.
  usichoke kutuombea.
  Kazi njema na wakati mwema.Tumsifu Yesu Kristo.

 2. 3
  Mshauri na mwalimu Says:

  KWA KWELI NIMEBARIKIWA,
  NAWE UBARIKIWE

 3. 4
  Gloria Says:

  nimebarikiwa kweli ni muhimu kusoma neno la Mungu kila wakati

 4. 5
  whitney Says:

  nimebarikiwa sana mtumishi…Mungu akubariki nawe.

 5. 8
  Cleotilda Says:

  Kweli Mungu anapolituma neno huwa halirudi bure,nimebarikiwa na umenigusa sana ubarikiwe mtumishi na Mungu azidi kukutumia asante.

 6. 9
  Peter Says:

  Nimebarikiwa sana Mungu azid kukutia nguvu za mwilini ni rohoni

 7. Nimebalikiwa sana mawazo yangu naona Yesu ni neno mfano amri usiibe au usiseme uongo ukiweza kuzishika amri hizo na kuzitenda hizo hapo tunasema Yesu au neno limekaa ndani yako kwa hiyo Yesu ni hali nzuri na siyo object tusifikiri yesu ni kiumbe kinachoweza kukaa ndani yetu ni roho hayo ni mawazo yangu.

 8. 11
  mussa mwakatobe Says:

  Mwenyezi MUngu akubariki

 9. 12
  Janeth Maina Says:

  Mungu azidi kukubariki mtumishi wa Mungu unatutia nguvu ya kulisomaneno la mungu mwanzo nilisoma tu bila kutafakari kwa sasa nimepata muongozo kamili wa kujua neno la Mungu.

  Mungu akubariki sana

 10. 14
  Tumaini john Says:

  Mungu akubariki kwa maana neno lake ni taa inayo tuongoza maishani mwetu.

 11. 16
  Anna Says:

  neno la Mungu ni taa ya miguu yangu. ni vema kulitafakari kila wakat

 12. 18

  Ubarikiwe sana Mtumishi,
  binafsi nimetiwa nguvu, tumaini lenye baraka na nimenoti mistari michache kwa ajili ya wengine.

 13. 20
  mkumbo Says:

  bwana asifiwe kaka , mm ni mkumbo. ubarikiwe kwa kazi njema, na mungu azidi kukutumia katika huduma hii.

 14. 21

  Nimependa somo lako. Mungu akubaliki ili uendelee kutangaza neno lake ili wasiofahamu waweze kufunuliwa na kufuata neno lake kwa usahihi, maana watu wengi wanashindwa kutafakari neno la Mungu, wanasubili kutafsiliwa na mtu mwingine hata kama ni cha uongo atafuata kutokana na uwelewa wa aliyemtafsilia

 15. 23
  nurueli Says:

  Bwana Yesu asifiwe mtumishi, Mungu akubariki kwa mafundisho mazuri

 16. 24
  Philbert Kamugumya Says:

  NENO LA BWANA NI NGUVU UBARIKIWE MTUMISHI WA MUNGU

 17. 26
  Rose Mpembo Says:

  Amìna.

 18. 27
  mayala kimotoli Says:

  mtumishi Bwana akubariki sana maana umenitoa katika sehemu niliyokuwa na kuniweka mahali salama

 19. 29
  HOSEA MWASUNDA Says:

  nimebarikiwa mtumishi

 20. 31
  Bizzo simiko Says:

  Mmmh! somo tamu sana! Mungu akubariki mtumishi aendelee kukufunulia mafundisho ya Neno lake..

 21. 33
  LEONARD FELICIAN Says:

  Mungu akuzidishie hekima,ili nasi tuzidi kuvuna matunda kwako na kuwajuvisha wengine..zab1:1-3.heri mtu yile asiekwenda ktk shauri la wasio haki,wala hakusimama ktk njia ya wakosaji;wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
  Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo
  Na sheria yake huitafakari usiku na mchana
  Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji uzaao matunda yake kwa majira yake;
  Wala jani lake halinyauki na kila alitendalo litafanikwa

 22. 35
  Martha Says:

  Mungu akubariki sana Patrick kwa mafundusho mazuri. Nimekuwa nikiwashirikisha wanakikundi wenzangu kujifunza masomo haya na yamefanyika baraka sana katika maisha yetu na mwongozo mkubwa katika kulitumikia kusudi la Mungu katika nafasi mbalimbali. Binafsi kiwango changu cha imani kimekua kupitia mafundisho yako. Ninamwomba Roho Mtakatifu aniwezeshe kukuombea wewe na huduma hii bila kukoma. Roho Mtakatifu azidi kukupa mafunuo ili uendelee kulisha na kunywesha roho zetu. Mungu akubariki sana wewe na huduma yako.

  • 36
   sanga Says:

   Amina dada Martha ahsante sana kwa ushuhuda wako, naam nashukuru sana pia kwa maombi yako maana kwa haikia nayahitaji sana hasa kipindi hiki cha sasa, tuzidi kuombeana na BWANA aendelee kukuza imani zenu na kuwafanya kumjua yeye zaidi na zaidi.

 23. 37
  Imani Swillah Says:

  Mungu wa mbinguni akubariki sana kaka kwa mafundisho mazuri, umeniongezea hatua kubwa sana katika kutumika. Na kwa nafasi hii nilopewa na kupata kibali namwomba Mungu kwa jina la Yesu azidi kuifunua akili yako kuyaelewa maandiko ili uendelee kuwaleta watu katika kusudi la Kristo. Mungu akubariki na kuiponya kila hatua ya huduma yako.

 24. 39
  NUHU J. MAKAYA Says:

  Jihadhari na manabii wa uongo.

 25. 40
  Edson paul Says:

  Mungu ni nimkubwa

 26. 41
  GODWIN MGENI Says:

  barikiwa mtumishi kwa kutupatia chakula cha uzma

 27. 42
  Rehema Says:

  Asante sana mtumishi kwa mafundisho yako mazuri, Mungua akubariki sana
  kwakweli nimebarikiwa saanaa

 28. 44
  Deogratius emmanuel Says:

  Amen, nimebarikiwa na kujifunza kupitia neno hili. Mbarikiwe na kristo.

 29. 45
  obeid Says:

  Mtumishi umenena kweli mungu akuzidishie zaidi

 30. 46
  ANTHONY GAUDENCE Says:

  Thanks, and God gonna bless u

 31. 47
  Mrs. Elly Says:

  Mtumishi barikiwa sana …nimejifunza mengiii

 32. 48
  Dave Says:

  Ni kweli kabisa lazima tuishi kwa kutafakari neno ili tuweze kuyaishi mapenzi yake.Mungu akubariki brother.

 33. 49
  John Kifaru Says:

  Fundisho zuri sana…ahsante ubarikiwe.

 34. 50
  RUNGU LA YESU Says:

  MUNGU AKUBARIKI SANA


RSS Feed for this entry

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: