NJIA KUMI ZA KIBIBLIA ZA KUMPATA MWENZI WA MAISHA.

Na: Patrick Samson Sanga.

Mpenzi msomaji hizi ni dondoo tu zilizomo ndani ya kitabu hiki ndani ya kitabu cha kwanza, nimeona ni vema walau kwa sehemu nikueleze yaliyomo ndani.
Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa babaye bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana’.Nianze kwa kusema kuoa au kuolewa ni mpango kamili wa Mungu. Zipo sababu nyingi za kwa nini unahitaji mke au mume Moja unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana, mbili ni kwa sababu zinaa (1 Wakorintho 7:20) na tatu unapopata mke unakuwa umepata msaidizi na mlinzi.

Kibiblia mke /mme mwenye busara mtu hupata kutoka kwa Bwana, maana yake Mungu ndiye anayehusika na kumpa mtu mke/mme. Mungu pekee ndiye anayejua nani ana busara ya kukaa na fulani halafu ndiyo anayekupa huyo mtu. Suala la kumpata mwenzi ambaye hakika ni wa mapenzi ya Mungu kwa mtu husika, imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa vijana na pia wale ambao bado hawajaoa au kuolewa.

Lengo la kitabu hiki ni ;

*kuwasaidia vijana wengi ambao bado hawajaoa au kuolewa kufanya maamuzi sahihi.

*Kuwapa maarifa wale ambao wanafuatwa na vijana wengi kwa lengo la kutaka kuwaoa, nini wafanye pindi wanapofuatwa na vijana wengi.

*Kuwapa uhakika / uthibitisho wale ambao tayari wameshafanya maamuzi haya na tayari wana wachumba kwamba wachumba hao wanatokana na Mungu au la.

*Kuwafariji na kutoa mwongozo kwa wale ambao huenda hamna anayejitokeza kutaka kuwaoa, wanaokataliwa na wale ambao wamechelewa kuolewa halafu wao wanafikiri ni laana.

*Kutoa mwongozo kwa wazazi, wachungaji, walezi, viongozi wa makundi ya kidini kuwasaidia vijana wao katika kufanya maamuzi haya makubwa .

*Kukusaidia kuzipinga hila zote za shetani katika safari hii ya maamuzi.

Kabla ya kuzitaja njia, ndani ya kitabu hicho nimetaja kwanza misingi unayotakiwa kuijua kabla ya kuzijua hizo njia nayo ni;

*Kwa kila jambo kuna majira yake hivyo hata wewe kuoa au kuolewa kwako kuna wakati wako maalumu.

*Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wako.

*Mungu anavyo vigezo vya kwake ya kukupa mke au mme ambavyo si lazima viendane na vigezo vya kwako.

*Si kila mke au mme hutoka kwa Mungu.

*Mungu anapoamua kukupa wewe mke au mme anakuwa ameangalia mbali kuliko wewe unavyofikiria.

*Usimuombe Mungu akujulishe mke au mme wako wakati ndani yako umeshajichagulia wa kwako.

*Ni vema uwe umekomaa na umekua kiakili, kiufahamu, na kiroho kwanza kabla ya kufanya maamuzi kama haya na hujaokoka fanya maamuzi ya kuokoka maana ni kwa faida yako mwenyewe.

*Ni vema ukatambua ya kuwa mwenzi wako si lazima atoke kanisa lako, shule au chuo ulichosoma au kazini kwako nk.

Zifuatazo ni njia za kibiblia, ambazo hakika zimewasaidia wengi kuwajua na kuwapata wenzi wao wa maisha;

*Kwa kumcha Mungu, ( kumtii Mungu ).

*Kwa sauti ya Mungu mwenyewe.

*Amani ya Kristo.

*Upendo wa ki –Mungu ( wa Dhati ).

*Mafunuo ya ki-Mungu.

*Kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu.

*Kulijua kusudi la Mungu katika maisha yako.

*Kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.

*Wazazi /walezi/wachungaji/kiongozi wako katika kundi lenu.

*Dhamiri za watu wengine au ushuhuda wa watu wengine.

Mpenzi msomaji hapa nimetaja tu hiyo misingi na njia husika. Lakini ndani ya kitabu nimefafanua kila msingi na njia kimapana maana isingekuwa rahisi kuziweka kurasa zote za kitabu hiki humu ndani.

Kama huna kitabu na ungependa kupata kitabu au hata kumchukulia mtu mwingine nenda katika Category ya vitabu utapata maelekezo huko.

Bwana Mungu akubariki na akutangulie katika safari hii ya maamuzi makubwa katika maisha yako.

Advertisements

89 comments

 1. Nimefurahi sana kusoma makala yako, kwa kweli nimejifunza mengi na namuomba sana Mungu anisaidie. Ningependa kama ungekuwa unanitumia kwenye mail yangu

  Mada mbalimbali za urafiki,uchumba hadi ndoa.

  Asante sana

  Like

 2. nashukuru kwa sana kwa msaada ambao nimeuoata katika kusoma makala hii.ila nina swali kuhusu jinsi ya kutafta mchumba.swali kama lifuatalo.mimi kama mkristo je kabla sijaanza kutafta mchumba yanipasa nimushilikishe mungu katika sala ua natafta mchumba huku niki muomba Mungu na mimi naendelea kutafta au namuomba mungu halafu mimi mwenyewe nakaa kimya paspo kujishughulisha kutafta?

  Like

 3. nashukuru kwa sana kwa msaada ambao nimeuoata katika kusoma makala hii.ila nina swali kuhusu jinsi ya kutafta mchumba.swali kama lifuatalo.mimi kama mkristo je kabla sijaanza kutafta mchumba yanipasa nimushilikishe mungu katika sala ua natafta mchumba huku niki muomba Mungu na mimi naendelea kutafta au namuomba mungu halafu mimi mwenyewe nakaa kimya paspo kujishughulisha kutafta? na pia ninaweza kumwambia mungu sifa za mchumba ninayemtaka/mhitaji?

  Like

 4. Asante sana kwa maoni na msaada wako kwa vijana,mimi binafisi nimefarijika sana kwa ushauri huo.ila nilikuwa na maswali kadhaa kulingana na maelezo uliyoyatoa kwamba mke mwema hutoka kwa Mungu,na mume mwema hutoka kwa Mungu pia,
  Je! utajuaje kuwa huyu niliyempata(mchumba) ndiye Mungu kanipa?
  Pili, inakuwaje mwanamke au mwanamume anakuwa namwenziwake mlevi?japo kuwa alimshirikisha Mungu ili kumpatia mke au mme mwema je huyo anakuwa ametoka kwa Mungu?

  Like

  • jamani ninacho amini ni kwamba ukimuomba mungu akupe mchumba unakuwa ujaomba sahihi unachotakiwa kuomba ni kuomba mume au mke moja kwa moja unaweza ukaomba mchumba akabaki kuwa mchumba msifikie kwenye lengo lenu kwa hiyo pindi uombapo jaribu kuomba mke aumme alafu ukimpata amani ya mungu huwa inaamua ndani yA mtu mwenyewe utakuwa na amani naye kama kweli ummemuomba mungu.barikiwa sana

   Like

 5. Nashukru kwa maoni yenu mazuri ya kuanzisha webset hii maana imenibariki sana. Ninaomba mniotumie kwenye email yangu masomo mengine mengi ya vijana
  Ahsante sana
  mbarikiwee.

  Like

 6. Nami nimefurai zaidi kwa kukutana na mada hii ila ningependa kuuliza kuwa kama kijana umefikia kumpenda mtu na katika maombi Mungu akakudhihirishia kuwa huyo ndiye nawe ukaridhika naye ila unapomshirikisha yeye anakuwa kama akuelewi ufanyeje wakati hupo kwa utani naye umeamua kumwambia ukweli kutoka moyoni si kama vijana wengine wanaopindisha maneno. Hii inamsumbua rafiki yangu ambaye amefikia hatua ya kukata tamaa….afanyeje?

  Like

 7. Nimefurahi sana kwa mafundisho haya ambayo mnatoa kwa jamii hasa kuwasaidia Vijana. Hivyo mimi kama mnavyoona address yangu ni Mchungaji. Hivyo natoa semina kwa vijana kabla ya ndoa. kama kuna uwezekano naomba mnitumie mafundisho ya URAFIKI, UCHUMBA NA NDOA, kwenye email address yangu.
  Natanguliza shukrani,
  Wenu Mchg. kagaruki.

  Like

 8. Ahsante mtumishi kwa masomo yako mazuri. Mimi nakiri kuwa yamenipa uamsho mkubwa.
  Naomba niulize, unatushauri nini sisi tulio wajane tena vijana? Mimi ni mjane tokea mwaka 2004, May. Nina miaka 39. Nina watoto wawili wakike, namba uniombee sana mtumishi.

  Like

 9. Bwana asfiwe Mtu wa Mungu,
  ubarikiwe kwa huduma hii ambayo Mungu amekupa, mie naona nikushirikishe kuniombea nipate mke mwema wa kufanana nami nitafurahi sana kama tutaendelea kushirikiana nawe mpaka pale Mungu atakapokuwa amefanya ubarikiwe sana.
  Jina la Mungu likuinue
  Josi

  Like

  • Amina Josiah, tumwamini Mungu kwamba atafanya jambo hili sawasawa na mapenzi yake na wewe jifunze kukaa mkao wa kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie kwako kwa kila jambo. Sanga

   Like

 10. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu ninahitaji maombi yako;nina mpango wa kuoa ila ninakutana na mlima ktk mpango huo kiasi najiuliza haya ni amepenzi ya Mungu au.
  ningepata tel ningeongea na wewe kwa undani zaidi.
  ubarikiwe

  Like

 11. Bwana Yesu asifiwe! hongera kwa somo lako zuri. ukweli nimejifunza mengi kutoka kwako. Nami naomba tushirikiane katika maombi niweze kumpata mume mwema. Nimepita mapito mengi kiasi nimefika mahali nikaona ni mpango wa Mungu. Mungu akubariki sana!

  Like

 12. NATAMANI KUPATA MENGIO KUTOKA KWAKO KWANI NAHITAJI MSAADA ZAIDI KATIKA SUALA LA MAHUSIANO HASA KIROHO ZAIDI NA SI KIDUNIA ZAIDI.
  nitafurahi kama nitapata ushauri zaidi juu ya hili kwani mimi ni kijana niliyemaliza elimu ya chuo kikuu lakini suala hili limekuwa likininyima raha siku hadi siku na linahitaji huruma toka kwa MUNGU NA MSAADA PIS

  Like

  • Ok, Mr. Nzagi nitafanya hivyo, wasiliana nami kuptia namba zangu za simu kwenye page ya Patrick, nipe muda nitakutumia mambo zaidi ya kukusaidia kwenye mail yako pia.

   Like

   • NI MUDA SASA TANGU UNIAMBIE NIKUPE MUDA UTANITUMIA UJUMBE KUPITIA KWENYE E MAIL YANGU LAKINI NAONA NI MUDA SASA NA SIJAPATA UJUMBE WOWOTE KHS MIMI WAKATI NI KWELI KWAMBA NAHITAJI MSAADA WAKO KIROHO ILI KUFANIKISHA SUALA HILI AMBALO NI TATIZO SANA KWA VIJANA WALIO WENGI NIKIWEMO MIMI PIA KAMA KIJANA, NATEGEMEA KUPATA MENGI KUTOKA KWAKO NA MUNGU AKUBARIKI KATIKA HUDUMA HII

    Like

   • Hello Ndugu Nzagi, nisamehe bure mpendwa wangu, na Bwana anisamehe pia. Kwa mujibu wa comment yako ya mwisho ulitaka msaada zaidi katika suala la mahusiano ingawa hukuwa specific kwenye eneo gani, maana mahusiano ni somo pana sana. Na kwa kuwa nimekuwa nikiendelea kuandika masomo mbalimbali ya mahusiano na kuyaweka kwenye blog hii naliamini na kwako pia naweza pia kuwa nimejibu suala lako. Labda kama una maeneo maalumu ambayo ungependa kujifunza nandikie, nitaandaa masomo hayo kwa ajili yako na kwa wengine pia, Mungu akubariki, niombee pia maana wajibu huu ni mkubwa sana.

    Like

 13. BWANA YESU ASIFIWE! NAMSHUKURU MUNGU KWA KUIPATA BLOG HII, KWA MUDA MFUPI NIMEGUNDUA NI MAHALA AMBAPO NITAJENGWA VIZURI KUTOKANA NA MAFUNDISHO YAKO, NI MAOMBI YANGU MUNGU AZIDI KUKUWEZESHA NA AKUPE MAONO ZAIDI KWA KUSUDI LA KUTIMIZA MAPENZI YAKE. MIMI NI BINTI AMBAYE BABO SIJAYAINGIA MAISHA YA NDOA.NINA MASWALI MENGI SANA KWA HABARI YA MAMBO YA MAHUSIANO,ILA KWA KUANZA NA SWALI LA KWANZA NINGEPENDA KUJUA, HIVI JAPOKUWA MUNGU AMESEMA SI VEMA MTU AWE PEKE YAKE,YAANI NI MAPENZI YA MUNGU BINADAMU TUYAINGIE MAISHA YA NDOA,JE MUNGU AMEWEKA WITO HUO KWA WATU WOTE AU WATU WENGINE MUNGU HAKUWAITIA HAYO MAISHA YA NDOA KABISA JAPOKUWA NI MAPENZI YAKE WATU WAYAINGIE?

  Like

  • ASANTE DADA GRACE. BIBLIA INASEMA KAMA HUWEZI KUISHI MAISHA SAFI KATIKA MUNGU NA HUWEZI KUJIZUIA NI HERI UOE AU UOLEWE. MUNGU HAJALAZIMISHA NI LAZIMA WOTE WAOE AU KUOLEWA. KWA KUWA KUOLEWA KUNA SIFA ZAKE NA KUOA. KAMA HUNA HITAJI USIOLEWE WALA KUOA. UNAOA KWA SABABU UNA HITAJI. KAMA MAOMBI UNAPOKWENDA KUOMBA NI LAZIMA UWE NA MAOMBI NA UJUE CHA KUFANYA. NA NDOA NI MPANGO WA MUNGU KWA MTU MWENYE HITAJI. ASANTE KAMA UTAAMUA KUTOOLEWA NA KUISHI MAISHA BILA DHAMBI MUNGU ATAPENDEZWA SANA NA WEWE. BARIKIWA.

   Like

 14. UBARIKIWE SANA MTUMISHI WA MUNGU,KUJITOA KWAKOILI KUTUSAIDIA VIJANA MAANA UJANA NI NJIA PANDAINAYOHITAJI MAAMUZI SAHIHI KWA MTU ILI AJUE NI WAPI PA KUELEKEA KWA JIL YA MAISHA YAKE HAT KRISTO ATAKAPORUDI

  UBARIKIWE SANA amen!

  Like

 15. MUNGU AWABARIKI KWA KAZI YENU NZURI KWA KUTULISHA NENO ZURI LA KIMUNGU.NIMELIPEDA SANA SOMO LENU LAKINI JE MUNAWEZA KUNIPA NJIA AMBAZO ZINAWEZA KUPATA MUME MWEMA KWANI KWA SASA UNAWEZA KUSEMA NIMEPATA MUMEA MWEMA KUMBE SIVYO.JE UTANISAIDIA VIPI ILI KUJUA HUYU NI MUME MWEMA?

  Like

 16. Nimefurahishwa na mafundisho haya na ninapenda sana kuelewa kwamba je? kama mungu amekuonyesha mchumba na mkakubaliana naye kwa misingi mizuri tu ya kuishi pamoja kwa badae kama mke na mume,ni vitu gani ambavyo vinahitajika ambavyo vinaweza kuendeleza uchumba huo?

  Like

  • Hapana hiyo ni dhambi kubwa. Kumbuka mchumba sio mume au mke. Ili Mungu akusaidie katika safari yako hiyo ngumu ni lazima ukubali kuishi maisha matakatifu. Ndoa zote zilizosimama zilianza vizuri na Mungu.

   Like

 17. nimependa michango yenu wapendwa, naomba kuuliza kuwa, kwa kuwa mtu anapomtafuta mwenzi anakuwa anaficha makucha yake, je, yanipasa kuchukua muda gani ili kujua ukweli halisi juu ya maisha ya mwenzi ninayetarajia kuoa na wakati huo mkizingatia changamoto za dunia hii ya sasa?

  Like

 18. ujumbe ni mzuri mtumishi wa mungu yaani mungu akutie nguvu zaidi na zaidi, nami nakuahidi nitafundisha wenzangu japo bado sijaolewa niko kwenye changamoto kubwa sana za kimaisha,naomba unitumie kwenye email yangu mafundisho zaidi
  regy

  Like

 19. Kwa kuwa vijana wetu wengi hukurupuka tu katika kuwapata wenzi wa maisha yao, kuna haja ujumbe huu kuwafikia wengi. Naona mara nyingi kanisa limekosa muda wa kutosha kwa vijana ambao wanakumbana na changamoto nyingi maishani mwao.

  Like

 20. Asante kaka Sanga kwa ujumbe wako mimi natamani sana kama ningeweza kukipata kitabu ili nikisome na nipate uelewa vizuri Ubarikiwe kaka kwa huduma ambayo Mungu amekujalia ili utusaidie tujui ni nini makusudi ya Mungu katika maisha yetu

  Like

 21. namshukuru Mungu kwa mafundisho yako, ni muda nilipitia blog yako, Namshukuru Mungu kwa kuipitia tena leo, kwa kweli nahitaji hiki kitabu kwa sasa, nipo Arusha, naomba unipe process ya kukipata. ubarikiwe sana.

  Like

 22. Nimefurahi sana kusoma ukura huu kwani umenifungua kiasi ,kwakuwa nilikuwa sielewi vzr ,kumpata mchumba kutoka kwa bwana naomba mungu anisadie ilinifahamu vema na kuomba kwa bidii ,naomba kupata muongozo zaidi ,nitumie kwenye emila adrress yangu williabrdsiah@yahoo.com

  Like

 23. Bwana yesu asifiwe mtumishi sanga nashukuru kwa ushauri wako kupitia maoni unayotuandikia ubarikiwe sana mtumishi ombi langu naomba uniombee nipate kazi na mke mwema maana anatoka kwa bwana

  Like

  • BWANA Mungu akusaidie, daima tunaomba kwa ajili ya wale wanaohitaji kuoa na kuolewa katika kusudi la Mungu, neema ya BWANA Yesu na hekima yake iwaongoze katika mapenzi timilifu ya ufalme wake

   Like

  • Ni kweli unachokisema, mfumo wa dunia unataka watu wafanye hivyo, lakini kimaandiko suala la tendo la ndoa ni kwa wana ndoa tu na si vinginevyo (Rejea 1Wakorinto 7)

   Like

 24. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Bwana…?? ubarikiwe kwa somo zuri la kutukomboa vijana hasa kwa somo la kumpata mwenzi wa maisha naamini umetuponya vijana wengi.Namshukuru Mungu kwa kunifikisha hatua niliyopo yakuingia kwenye ndoa.ningependa Mtumishi tushirikiane ktk maombi ktk kufanikisha ndoa yangu.ubarikiwe na Bwana.mm ni msichana

  Like

 25. Mwingiliano wa maisha, wazazi kuwa “busy”, Kazi za wazazi/walezi kuwa tofauti na za vijana hivyo kumepelekea kuwa na mpasuko wa kukuza na kuendeleza maadili mema kisha kupelekea vijana kuwa na maamzi yanayochochewa na misukumo ya tamaa za mwili na si ya misingi ya kimaisha.
  mfano. mtoto ni shule, wazazi/walezi ni ofisini wengine shambani kwamtindo wa sasawa chakula wa ‘self-service’ umepelekea wazazi kukosa fursa ya kuonana na watoto.
  Hii pia iliendelea kuchochewa na malezi kutoka kwenye mfumo wa kijamii na kubaki kuwa wa kifamilia moja. Mfano mtu mzima hayupo tayari kukemea au kuonya mtoto wa jirani; vijana nao wameichukulia kama faida, wako tayari kumuamkia mtu wanayemuona ni mkubwa wa kiumri hata kama hawamjui lakini hawako tayari kuyapokea maonyo ya mtu huyo!
  Kanisa na jamii tujipange kwa upya.

  Like

 26. nimefurahi sana na kitabu chako na ubarikiwe sana…vp kama nataka kuomba mke/mume mwema kutoka kwa bwana kwa njia ya maswali nitafanyaje…make nahisi nakosea kuomba kama nikufung nafunga sana na naomba sana but kujibiwa bado vp nisaidie mtumishiii..

  ubarikiwe ww na mkeo kwa kazi nzuri mungu awarinde mzidi kutufundisha ss.

  Like

 27. Nasema asante sana kwa mafundisho yenu hakika nimejinza mengi Mungu awabariki sana kwa kazi ya kutoa hii elimu kweli vijana tunapotea kwa kukosa maarifa, Mungu awabaliki sana

  Like

   • Amina mtumish Mungu akubariki xn kwa huduma hii nzur kwan maswala ya uhusiano imekuwa ni changamoto kwa vijana walio wengi especially walio okoka… Mungu aendelee kukufunilia zaidi na zaid ili kulinusulu kundi kubwa la vijana amina

    Like

 28. Ahsante sana . kwani nimejifunza na kupata elimu kubwa jinsi ya kummpata mchumba mwema . MUNGU akubariki sana unapoendelea kutoa elimu hii kwa sisi vijana . nimeipenda sana makala hii coz na mimi ni vijana wanaotafuta mchumba !,.!! @

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s