NAFASI YA MWANAMKE KIBIBLIA.

Na; Patrick samson Sanga.

Mwanzo 1:27 ‘Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba. Sikiliza mahali popote pale mwanamke ni mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya mambo kuliko hata mwanaume.Ikiwa ushawishi huu utatumiwa katika mpango wa Mungu basi kusudi la Mungu litatekelezwa.

Mungu hakumwumba mwanamke kwa bahati mbaya au makosa,kila ambacho Mungu alikifanya ,alikifanya kwa kusudi.kwa lugha nyingine kila ambacho Mungu alikifanya maana yake moja kina nafasi mbele zake na mbili kuna wajibu ambao Mungu aliweka ili utekelezwe na hicho kitu.

Lengo la ujumbe huu ni kukueleza nafasi ambayo Mungu amempa mwanamke katika kanisa,jamii,nchi,ndoa na nk na wajibu wa yeye kutekeleza katika nafasi hiyo:-

1.Mungu anamtazama mwanamke kama msaidizi wa mumewe . Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema si vyema huyo mtu awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”. Tangu kuumbwa kwa Adam,mpaka Mungu kumletea Eva inasemekana miaka mingi ilipita hapa katikati.Sasa tunajua katika ile sura ya kwanza na ya pili ya kitabu cha mwanzo,Mungu alikuwa amempa Adam wajibu wa kutekeleza.

Ikafika wakati Mungu akaona ule wajibu ni mkubwa sana kwa Adam kuutekelekeza ndipo akampa Eva.Kitu Mungu anataka tujue hapa ni hiki,wajibu aliopewa Adam peke yake asingeweza kuutekeleza bila Eva,maana yake nafasi ya Eva kwa Adam ilikuwa ni ya muhimu zaidi.Pasipo Eva,Adam angeshindwa kutekeleza wajibu.

Sasa hata leo katika ndoa,kanisa Mungu ameweka wanawake ili wawe wasaidizi katika majukumu ambayo Mungu amewapa na waume zao au wachungaji wao makanisani.
2. Mwanamke kama mlinzi wa agano na kusudi la Mungu. Mithali 14:1 “ Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake ; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe” , Mwanzo 3;13 “ Bwana Mungu akamwambia mwanamke ,nini hili ulilolifanya ? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya ,nikala”..

Ndoa ni agano la Mungu kwa wanadamu. Mlinzi wa agano kimsingi ni mwanamke. Mara nyingi shetani akitaka kuvuruga ndoa atatafuta mpenyo au nafasi hiyo kwa mwanamke ili asambaratishe ndoa hiyo.Sasa mwanamke yupo ili kulinda kusudi hilo.Asipokaa kwenye nafasi yake ya ulinzi basi ajue kwamba kusudi la Mungu la kuwaunganisha halitatimia.

Nisikilize ndoa yoyote inapovuruguka ujue mwanamke hakusimama vema kwenye nafasi yake ya ulinzi. Ngoja nikuonyeshe kitu hiki. Adam na Eva walipokula tunda ambalo Mungu aliwaambia wasile , kila mmoja wao aliulwiza swali lake. Adamu aliulizwa uko wapi? Mwanzo 3:9, na Eva alimwambia Mwanamke ni nini hili ulilolifanya , Mwanzo 3:13.Ipo tofauti kubwa sana katika haya maswali mawili.Swali la Adam lilimaanisha kwa nini haupo kwenye nafasi yako? Na swali la Eva lilivuka hapo na kumaanisha kwa nini hujafanya ulilotakiwa kufanya yaani kulinda agano.Mahali popote mwanamke ulipo ikiwa ni katika ndoa ,kanisa ,jamii,nchi, jifunze kulinda kusudi la Mungu ambalo unajua Mungu amekuagiza . jifunze kupitia mama yake Musa , yeye alilinda agano la wana wa wa Israeli kwa kumficha Musa na kuhakikisha hafi maana alijua Musa hakuzaliwa kwa bahati mbaya. Kutoka 2:1-10.


3.mwanamke kama muombolezaji.

Luka 23;27-28 “Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata na wanawake waliokuwa wakijipiga vifiua na kumuombolezea , Yesu akawageukia akasema ,Enyi binti za Yerusalemu ,msinillie mimi bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu”.Sikliliza , Mungu amweapa kinamama uwezo mkubwa wa kuomboleza kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ndani ya jamii ,ndoa, kanisa, nchi nk. Hivyo Mungu anamuhesabu mwanamke kama muombolezaji.

Hii ina maana kam kuna vitu havijakaa sawasawa kwenye ndoa,kanisa,nchi nk, Mungu anajua mwanamke atasimama kwenye nafasi yake na kuomba ili Mungu apate kuliponya taifa kupitia maombi .Ukiona maasi mengi yamezidi katika taifa mfano, vijana wa kike kutoa mimba, uasherati,uchafu na uzinzi basi ujue kina mama katika mji au taifa hawajasimama vizuri kwenye nafasi zao. Si kana kwamba nawalaaumu mama zangu na dada zangu kwa kusema hivyo,bali ninachotaka niwaonyeshe ni kwamba usalama na maendeleo mazuri ya vijana wa kike na kiume katika familia,kanisa na taifa kwa ujumla upo katika mikono yenu na ndio maana Yesu aliwaambia mjililie ninyi na hao vijana wenu.

Nikuulize swali , jiulize una weatoto wangapi? Tabia na mwenendo wao ukoje? Je ni mzuri? Unambariki Mungu? sivyo jiulize chanzo cha tabia hizo kwa mwananao ni nini au ni nani aliyehusika na tabia hiyo? Najua unaweza kwa haraka kusema ni shetani au kumtupia lawama mmeo. Sikiliza Shatani huwa hafanyi chochote isipokuwa pale anapokuwa  amepewa nafasi na mtu au watu fulani , kwa kifupi mtu anaposhindwa kusimama kwenye nafasi yake. Sasa ukisoma vizuri Biblia utagundua nafasi ambayo Mungu amempa  mwanamke kwa habari ya watoto wake, ndoa yake, kanisa lake kwa ujumla.

Jifunze kusimama kwenye nafasi yako, funga na kuomba kwa ajili ya taifa hili ili Bwana Mungu apate kuliponya . maombi yako yatasababisha kutengenezwa kwa mahali palipobomoka na krejeshwa kwa njia za kukalia. 
4.Mwanamke kama mlinzi wa nafsi ya mtoto wake wa kiume .

Katika hii sura ya 31 ya kitabu cha Mithali tunaona habari za mama mmoja ambaye alikuwa na mtoto wa kiume na huyu mtoto alikuwa ni mfalme. Ule mstari wa pili unasema “ Ni nini mwanangu ?, tena ,nini mwana wa tumbo langu? Tena nini mwana wa nadhiri zangu ? Usiwape wanawake nguvu zako; wala moyo wako usiwape wale waharibuo wafalme”. kinamama wakijua namna ya kuzikamata nafsi za watoto wao wa kiume ,nakuambia kuna uwezekano mkubwa kabisa hawa watoto wasifanye tendo la ndoa mpaka watakapo kuja kuoa.

Hili litawezekana pale tu kinamama watapofanikiwa kuzikamata na kukaa kwenye nafsi za watoto wao wa kiume.Huyu mama alimuuliza maswali mengi mwanawe kwa sababu aliona nafasi yake mama kwenye nafsi ya mwanawe inanyang’anywa na wanawake wengine.

Naamini waraka huu mfupi na wa kwanza utafanyika kuwa msaada kwa wamama wengi mahala popote pale.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.

32 comments

  1. mimi ni mwinjilisti mnyarwanda na nimebalikiwa sana na mafundisho yenu.kwa bahati nimeiona website yenu na ninataka tuwe na ushirikiano
    ili ni we mwanafunzi wenu katioka neno la Mungu.Uso wenu unajaa upako wa Mungui na ninawatakia kuendelea na upako huo ili mpate kuponya moyo iliyopotea.
    wako Seneza.

    Like

  2. Wanawake tuwe makini kwani hata Mungu ameandika ya kwamba mwanamke mpumbavu atabomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe na yule mwerevu atajenga kwa mikonoyake mwenyewe.
    Hivyo wanawake tuwe na msimamokatika maisha yetu kwani hata shetani anapenda kututumia sisi wanawake kwa sababu anajua udhaifu wetu hivyo basi tusimpe shetani nafasi. wanawake tunaweza.

    Like

    • veronika, unakosea mwanamke si dhaifu, mwanamke ana nguvu sana ktk ulmiwengu wa roho, ndo Mungu anamwita mlinzi, mjenzi, msaidizi, n.k
      veronika kataa wewe sio dhaifu, shetani anajua mwanamke ana nguvu ndo maana anavizia mwanamke akijisahau tu anamwangushe na nyumba yake yote
      mimi huwa nasema hata mume kutoka nje ya ndoa ni kutowajibika kikamilifu kwa mwanamke ktk nafasi Mungu alizompa ikiwemo ya ulinzi, mwanamke funga mumeo kwa tabia njema ya damu ya YESU asiende kwa kahaba

      Like

    • Mungu akubariki dada Veronika kwa mchango wako juu ya wanawake kusimama kwenye nafasi zenu. Jambo la msingi analowinda Shetani kwa mwanamke ni umuhimu wa nafasi yake, maana anajua akifanikiwa kumpata mwanamke basi kupitia huyo ataleta uharibifu mkubwa. Naam akina mama ni Jeshi kubwa, simameni kwenye nafasi zenu.

      Like

  3. Kwakweli Mungu akubariki sana Mtumishi wa Mungu kwa kutufanya wamama tuzione ndoa zetu zirudi bustanini maana asili ya ndoa ni bustanini na asili ya mateso ni msalabani. TUCHANGAMKE WAMAMA KUZIPALILIA NDOA ZETU KWA MAOMBI YA ULINZI NA ULIMI MLAINI.

    Like

  4. mungu akubariki mpakwa mafuta umenifundisha,vitu vizito na nimefunguliwa ningependa jumbe kama hizi unitumie kwenye email yangu

    Like

  5. Kwakweli Somo hili Limenibariki na Kunifunza mengi.
    Mungu akuongoze katika nia yako na utume wako.
    Emmanuel Mwakabana

    Like

  6. Mungu akubariki sana mtumishi wa Bwana, umetukumbusha jambo jema maana wanawake wengi tumejisahau na kuacha lile kusudi la Mungu ambalo aliweka ndani yetu na matokeo yake tunatumika jinsi tunavyotaka sisi wenyewe.Asante kwani binafsi umenifundisha, na mwongozo huu utanisaidia kuwasaidia wanawake wengine pia. Roho Mtakatifu azidi kukupa ufunuo.

    Like

Leave a comment