JIFUNZE KUMILIKI MAJIBU YA MAOMBI YAKO

 Waraka wa Septemba

 

Yoshua 13:1-7

Utangulizi,

Katika dunia ya leo  watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao mwingi ikiwa ni pamoja na kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuomba Mungu awabariki, awaponye, awalinde kwa kifupi awajibu mahitaji yao waliyonayo mbele zake siku zote. Wapo waliokuwa hawazai wamezaa, vipofu wameona, wasioajiliwa wameajiliwa, biashara za wengi zimefanikiwa, ndoa nyingi Mungu ameziponya, wapo waliotaka kuolewa au kuoa na Mungu amewapa waume na wake wazuri. 

 

   Sasa hao hao watu ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika kuomba Mungu awatendee miujiza katika maisha yao, imefika mahali wanaona yale ambayo yalikuwa ni majibu ya Moambi yao shetani ameyavamia na kuleta balaa zaidi na limekuwa pigo kubwa sana  kwa wana wa Mungu. Na kwa sababu hiyo wamejikuta wakimlalamikia Mungu kama vile wana wa Israeli na imefika mahali  pa wengine  kuona kama Mungu  hawezi na hivyo kumuacha.

Tatizo  la haya yote ni kwamba wakristo wengi hawana tabia ya au mazoea ya kumiliki mujibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Huenda ulikuwa huna mtoto na Mungu amekupa kuzaa mtoto, sasa  huyo mtoto ndiyo jibu lenyewe kutoka kwa Mungu. Sasa ni lazima ujifunze kumiliki  huo muujiza wa mtoto, sasa si mtoto tu bali ni pamoja na ajira, ndoa, uponyaji, kanisa, Nchi, Biashara nk. 

 

  Kusudi la waraka huu mfupi ni kukufundisha njia zitakazokusaidia kumiliki majibu ya maombi yako na kukupa maarifa yatakayokusaidia kuwa makini na majibu ya Mungu katika maisha yako.Tafsiri ya Kumiliki, Neno kumiliki linapozungumziwa kibiblia lina maana ya kukiweka kitu au jambo fulani chini ya utawala wako, maana yake unakuwa na nguvu au umri juu ya hicho kitu. Una hakikisha  hakiwezi kutoka kwako. Kumiliki siku zote kunahusisha mapambano makali Sasa mimi sijui Mungu amekutendea nini? Ila ninachojua kwa namna moja au nyingine lazima kuna mambo ulikuwa unamuomba Mungu  akufanyie na mengine tayari ameshakufanyia na mengine ndiyo anayafanya na bado kuna mengi atafanya.sasa katika hayo aliyokwisha kufanya huenda amekupa mke au mme mtarajiwa, huenda ameiponya ndoa yako, nafsi yako, mwili wako, Afya yako, Huenda amekupa mtaji, amekupandisha cheo, amekupa mtoto, amepanua  mipaka ya huduma yako  nk.

 

    Katika lolote ambalo amekufanyia unatakiwa kulimiliki kwa maombi. Kama shetani alikuwa hataki uzae usidhani atamfurahia mtoto uliyemzaa. Kama alishindwa kumzuia asizaliwe usidhani atakubali aendelee kuishi. Shetani atafanya kila  analoweza kuua huyo mtoto au kuharibu chochote kile ambacho Mungu amekutendea kama jibu. Sasa kwa sababu hiyo ni lazima uzijue njia za Kibiblia zitakazokusaidia kumiliki hayo majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu.

 

 Huenda zipo njia nyingi zifuatazo ni sehemu na ni za msingi kati ya hizo nyingi.

 

Njia ya kwanza, kumiliki kwa kuupigania na kuujenga huo muujiza au jibu lako toka kwa Mungu.

Yoshua 13:1-7, 2 Samwel 2:1-7.Ule mstari wa kwanza wa kitabu cha Yoshua katika kitabu Yoshua 13 unasema “Basi Yoshua alipokuwa mzee na kuendelea sana miaka yake BWANA akamwambia wewe umekuwa mzee na kuendelea sana miaka yako, kisha inasalia nchi  nyingi sana bado kumilikiwa” Kumbuka katika ile sura ya kwanza  ya kitabu cha Yoshua Mungu anamwambia Yoshua uwe Hodari na moyo wa ushujaa maana ni wewe utakayewarithisha watu wa nchi hii. Na ukisoma vizuri kitabu chote cha Yoshua unaona kabisa Yoshua alitekeleza agizo la kuwarithisha wana wa Israel nchi ya ahadi.

 

 Wakati Mungu anamwambia Yoshua bado inabaki nchi yaani maeneo mengi sana ambayo bado hayajamilikiwa tayari Yoshua alikuwa ameshapiga zaidi ya wafalme 32 na kuiteka miji yao, lakini bado Mungu anamwambia bado nchi nyingi inasalia. Kitu gani Mungu anataka tujifunze hapa? Sikiliza Yoshua alipewa kuwarithisha wana wa Israel nchi hii lakini sio kuwamilikisha. Suala la kumiliki lilikuwa kwa yule aliyekabidhiwa nchi  au mji lakini sio kwa Yoshua. Sasa ndiyo maana Mungu akamwambia Yoshua kwa sababu wewe  ni mzee igawanye  hiyo nchi kwa wana wa Israeli kwa kufuata kabila zao ili waweze kumiliki. Maana yake waingie kwenye mapambano ya kile ambacho Mungu amewapa kupitia Yoshua.

 Niseme hivi chochote unachokipata kwa njia ya maombi kinamilikiwa kwa njia ya maombi, jifunze kukipigania na kukijenga yaani kuendelea kukiri uwepo wa hicho kitu siku zote. Mfano kama uliomba mke au mme na Mungu amekupa usipunguze kuomba maana shetani usidhani anafurahia ndoa au uhusiano wenu. Ukiendelea  kusoma zile  sura zinazofuata za kitabu cha Yoshua ndipo utakapoona makabila yalivyopambana ili kumiliki jibu lao toka kwa Mungu la nchi. 

 

Njia ya Pili; Miliki majibu yako kwa kutafuta maarifa zaidi ya kutunza huo muujiza.

 Hosea 4:6a inasema “Watu wangu wanaangamizwa  kwa kukosa maarifa”.Sikiliza  muujiza au jibu lolote lile ambalo Mungu amekujibu au amekutendea una maarifa yake ya kuutunza. Maarifa hayo yanaweza kuwa ndani ya Biblia na hata katika vitabu vingine nje ya Biblia. Mfano umemwomba Mungu akupe mtaji uanze biashara na Mungu amekupa, sasa huo mtaji una namna zake za kuuendesha ili uweze kuzaa kwa faida. Kuna namna fulani ambayo ukiwekeza utapata faida nzuri. Sasa maarifa hayo ya kuwekeza yapo mengine kwenye Biblia lakini mengine ni kupitia watu wenye uzoefu katika hilo eneo, vyombo vya habari, kuna semina za kiserikali kuhusu biashara nenda huko ufuatilie ili  ujue zaidi, maana apendaye mafundisho hupenda maarifa. Huenda ulikuwa hujaoa au kuolewa na sasa uko kwenye ndoa. Hudhuria semina za ndoa na kusoma vitabu husika ili upate maarifa yatakauokusaidia kuishi katika ndoa vizuri.

Umezaa watoto wengi wanakufa kwa malaria halafu watu wanasema ni shetani tu wakati mwingine si shetani  ila ni wewe ulimweka mwanao katika mazingira  ya  kuumwa  na mbu vizuri ndio maana akafa. Soma habari za matumizi ya ngao, chandarua yanayotolewa na serikali hujui kwamba serikali yoyote ile imewekwa na Mungu. Kwa kifupi muujiza wowote amabo Mungu amekutendea una maarifa yake ya kuutunza na chanzo kikubwa cha maarifa ni neno la Mungu. Hivyo lisome likae kwa wingi ndani yako.

 

 Njia ya Tatu; Miliki majibu yako kupitia shukrani, sadaka au utoaji wa aina  yoyote ile.

 2Wafalme 5:17”Naamani akasema kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili, kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa BWANA. 

Hizi  ni  habari za Namani Jemedari  wa jeshi la shamu alikuwa na Ukoma. Alipokwenda Istraeli  kwa nabii Elisha ili aombewe kuhusu tatizo la ugonjwa wake Elisha alimpa maagizo ya kutekeleza kuwa akajichovye / akajizamishe ndani ya mto Yordani mara saba na ndipo atapona. Baada ya Namani kutii maagizo Biblia inasema alipona na ngozi yake ikatakasika ikawa kama ya mtoto mchanga.Baada ya jibu  hilo kwanza Namani alimshukuru Mungu wa Elisha na kisha akasema tangu siku ile hatatoa tena sadaka kwa miungu yao kule shamu isipokuwa kwa Mungu wa Elisha pekee.

Unapomshukuru Mungu kwa lile alilokutendea ni ishara ya kupokea kwa kuonyesha kujua nani aliyekutendea hilo jambo na  hivyo kumrudishia yeye utukufu. Pia unaweza kumiliki majibu ya maombi yako kwa njia ya kutoa sadaka kwa yatima, wajane na pia unaweza kumshukuru Mungu kwa kushuhudia kwa wengine nini Mungu kakutendea au kutoa sadaka ya shukrani au utoaji kwa makundi mengine yasiyojiweza  katika jamii.

 

 Njia ya nne: Kumiliki muujiza kwa kuwatunza watumishi wa Mungu na kuchangia huduma mbalimbali.

Yoshua 12:1-3 kwenye ule mstari wa pili Biblia inasema “Basi wakamwandalia karamu huko naye Martha akamtumikia na Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi chakulani pamoja nao. 

Hii pia ni habari nyingine inamhusu Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua baada ya kuwa amekufa kwa siku nne. Sasa Lazaro aliumiliki muujiza wake wa kufufuliwa kwa kumtunza Yesu pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Hii ina maana Lazaro pamoja  na dada zake waliingia gharama kwa ajili ya kuwatunza Yesu pamoja na  wanafunzi wake, Kwa siku zote ambazo Yesu alikaa kwa Lazaro, Lazaro alihakikisha hawalali njaa, anawapa mahali pa kulala nk.

Sasa unaweza kumiliki muujiza wako kwa kuruhusu watumishi wa Mungu wakae nyumbani kwako. Huenda wamekuja kwenye mkutano au semina kwa wiki moja au mbili itoe nyumba yako itumike, kufanya hivyo ni kumfanya Mungu aendelee kukulinda wewe na yale aliyokupa maana anajua hutamnyima siku moja atakapohitaji kuvitumia. Wapo wengine wanaomiliki kwa kutoa magari yatumike kipindi chote cha mikutano, unaweza pia  kumiliki kwa kuchangia gharama za mikutano  si lazima pesa lakini hata kufanya kazi mbalimbali katika mkutano huo, huenda  ni  usafi,  kubeba vyombo, kufanya usafi walikofika watumishi, kuombea huo mkutano au semina nk. Nakuambia unaweza ukaona kama ni vitu vidogo lakini ndivyo mujibu ya maombi yanavyomilikiwa bila kujali Mungu amekutendea nini.

 

 

 Nija ya tano: Kumiliki muujiza kwa kufanya  maamuzi ya kuokoka endapo Mungu alikufanyia huo muujiza kabla hujaokoka, na kuwaambia wengine habari ya Yesu aliyekuponya. 

 Ukisoma ile sura nzima ya 9 ya kitabu cha Yohana utakutana na habari ya kipofu mmoja tangu kuzaliwa kwake  ambaye Yesu alikuwa amemponya. Ule mstari wa 39 unasema “akasema,Naamini, Bwana akamsujudia” Ukisoma vizuri habari hii utagundua baada ya mahojiano marefu kati ya mafarisayo na yule kijana kuhusu uponyaji wake ndipo Yesu akamwuuliza je unamwamini mwana wa Mungu? Yule kijana akamwuliza ni nani huyo nipate kumwamini? Kwa kifupi Yesu akamjibu unayezungumza naye. Ndipo yule kijana  akasema, naamini Bwana akamsujudia.

Mtu mwingine ni Naamani ambaye tumekwisha ona habari zake, kitendo cha yeye kusema toka leo sitatoa sadaka kwa miungu  ya shamu ila kwa Bwana  ni dalili  ya kuonyesha kumwamini Mungu wa Israel. Hivyo hata leo wapo ambao Mungu anawatendea mambo mengi hata kabla hawajaokoka sasa ili kumiliki  hayo ambayo Mungu amekufanyia mwamini Yesu ndio huo muujiza utadumu. Wapo watu leo wanafunguliwa kwenye nguvu za mapepo huo ni  uponyaji. Sasa badala ya kuwasaidia watu wamwamini Yesu tunawaacha, nakuambia pepo watarudi kwa huyo mtu wenye nguvu zaidi kuliko yule wa kwanza. 

 

  Pia ukisoma vizuri habari hiyo hiyo utagundua kwamba huyu jamaa alimiliki uponyaji wake kwa kuwaambia wengine habari za Yesu na kukiri kwamba  mponyaji ni Yesu na si mtu mwingine, nakuambia  kufanya  hivyo ni kujihakikishia kudumu kwa huo muujiza na Mungu ataendelea kuutunza huo muujiza  maana wewe ni chombo chake. Mungu akikuponya au kukubariki usinyamaze kimya waambie wengine habari za Yesu aliyekuponya. Jifunze kutoka kwa mwanamke msamaria. Uponyaji wa nafsi yake ulipelekea watu wengi wa mji wa Samaria kuokoka. Soma kile kitabu cha Yohana sura ya nne mistari 30 ya kwanza utaiona habari hii. 

 

Mpenzi msomaji wangu mpaka hapa naamini utakuwa umepata kitu cha kukusaidia labda nikuambie hivi  siri kubwa ya mafanikio ni kuliweka neno la Mungu kwenye matendo, si unajua imani pasipo matendo imekwisha kufa katika nafsi ya huyo mtu mwenye imani hiyo. Nimeamua  kuandika ujumbe  huu baada ya kuona wana wa Mungu wengi imefika mahali  wanakuta yale ambayo Mungu aliwapa kama majibu ya maombi yao yameshaharibiwa na shetani, wapo waliozaa watoto wao wakafa na walimuomba sana Mungu kuhusu hao watoto nk. Sasa  ni imani  yangu kwamba tangu sasa jambo lolote ambalo Mungu atakupa kama jibu la maombi yako utalimiliki.

 

 Ndimi katika huduma

Patrick Samson  Sanga

Tuendelee kuombeana.

Advertisements

42 comments

 1. Nimeokoka natamani sana kukua kiroho na kuishi maisha matakatifu ndani ya Kristo.
  Natamani kupokea karama nilizonazo, kupokea muujiza wa Imani kubwa sana, Kupokea karama ya uponyaji, Unabii na kuwa mfundishaji wa neno kama mwalimu

  Like

 2. Naitwa John Mushi, Nimeokoka, Namshukuru Mungu aliyeniwezesha kusoma habari njema kama hii. Ndugu uliyeandika Mungu akuzidishie, hatimaye na sisi tufuate nyayo zako katika Kristo Yesu.Amina.

  Like

 3. Praise God Brother!
  Thax God for your ministry, actuary this is my first time to visit ua web and i really like it.

  I just wish to know a little bit about you especially which church do u worship, where are u and much more Is it allowed to share some of ua teachings with my fellow youths here where i am? to assure you, the teaching will be presented as they are or just few additions through HOLY SPIRIT guidance.

  Like

  • Thanks brother Kidenya, for your interest towards what God is doing through me, in fact I’m a member of an Evangelistic Assemblies of God Tanzania(EAGT) under Bishop Moses Kulola, Currently I’m at Dodoma and I worship at an EAGT Centarl Church. Iam a born again Christian, writing is one of my gifts from God, and I have decided to use this gift to write for my Lord. Sure be free to use my teachings to teach others, u have my blessings. May God be with you. I would also like to know about you. We can even contact via our emails.

   Like

 4. Bwana Yesu asifiwe!
  Kwanza na mshukuru Mungu aliyeweka wapakwa mafuta wa Bwana wanaojitolea kwa moyo wao wote ili kuokoa watu wa Mungu. Naomba Roho Mtakatifu ajifunue ndani yangu ili nipate maarifa na niweze kuishi katika neno.
  Ubarikiwe sana Mtumishi wa Bwana.

  Like

 5. Bwana Yesu Asifiwe Mtumishi wa Mungu.
  Asante sana kwa Mafundisho ya Neno la Mungu,hakika nimejifunza vitu vipya kabisa. Bwana akuzidishie nguvu za ROHO MTAKATIFU ili uwe na mafunuo mengi zaidi kwa ajili ya mwili wa KRISTO.
  Ubarikiwe sana!
  “nimeokoka na nampenda sana Bwana Yesu’

  Like

 6. Ndugu Sanga nashukuru sana kwa mafundisho yako kwani jana nilikuwa kwenye semina na Mwl. Mwakasege nilipokuja kusoma msg hii leo naona nimefunguliwa sana Mungu akubari ila usiache kutuombea pia.

  Like

 7. Bwana Yesu asifiwe mtumishi,asante sana kwa mafundisho mazuri ambayo yanaujenga mwili wa kristo Yesu.Mungu akubariki sana ,azidi kukuzidishia karama mbalimbali za roho mtakatifu.Amen

  Like

  • Nashukuru kwa ujumbe mzuri, nimekuwa mdau wa masomo yako hata kuprint na kufundisha wengine. Mungu akubariki sana. naomba ujumbe UNAOHUSU SADAKA YA SHUKRANI

   Like

   • Thanks Teddy, ahsante kwa kuwa na muda wa kupitia masomo haya na hata kuwafundisha wengine. Kwa habari yaujumbe unaohitaji naomba nipe muda naamini mpaka Januarui 2013 kwa neema ya Mungu kwani Desemba nina mambo mengi ya kufanya, Barikiwa.

    Like

 8. “”””Hakika MUNGU na ahimidiwe na watu wote,ninashukuru sana kwa ujumbe,kweli umetupa jambo jema sana ktk maisha yetu,wakati mwingne tukifanikiwa ktk maombi yetu tunasahau tulipotoka,hata MUNGU tunamweka pembeni. MUNGU nisaidie kumiliki majibu ya muujiza wako,zidisha majibu ktk maombi yangu kwako. AAMINAA!!

  Like

  • “”Thamani Ya Mwanadamu ni kubwa sana,na uhai ni bora kuliko maisha”” hakuna awezaye kuutambua na kuwa na juhudi kupata Utakatifu wala kuukaribia,majibu ya sala na maombi si pekee kigezo cha Utakatifu ila juhudi za kutendea kazi majibu hukaribia kufikia lengo la Utakatifu,ndio maana pasaka sio ufufuko tu bali ni kazi ya majibu katika fumbo la ufufuko. kupata jibu si fursa ya kuishi ila kazi ya jibu ndio maisha,kwani uhai ni bora kuliko maisha. hakuna aliyekamili ila kukamilishwa. MUNGU ndiye.””

   Like

 9. “””kilicho Ndani Ya Roho Huiponya Na Kuiponza,wokovu Unamfaidia Nini Asiye Hai Japo Ana Nafasi Kubwa Katika Kuishi. Kuishi Ni Muhimu Katika Maisha Japo Si Kila Mtu Ana Mpango Wa Uhai Wake, Wito Wangu Ni Kumwomba MUNGU atujalie neema zaidi ili kutamani kuuishi uhai kwa IMANI na MATENDO”””

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s